MAOMBI YA KUVUNJA MITEGO NA TANZI KATIKA MAISHA YAKO
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
Ayubu 18:10
Zaburi 141:9
10 Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.
9 Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu.
Leo tushughulikie Tanzi na mitego! Niliwahi kusema kuokoka ni hatua ya kwenda kaanani! ukiokoka haina maana utafika tuu kaanani, hapana lazima upite jangwani, au nyikani Bwana Yesu asifiwe!
kwanini leo nataka tushughulikie Tanzi na mitego siku hizi ibilisi amegundua njia mpya ndo maana unaweza kuwa umefungwa na ukaenda kuomba na wenzako ibadani! pale kanisani ukawa huru lakini,ukitoka nje tuu matatizo yapo
palepale!? na hii ni sababu ibilisi hujenga ukuta kwa nje anakuzungushia ukuta, kupitia huo ukuta anatuma mishale ya kukubomoa.
√Tanzi ni vifungo vya kichawi vya kukuzuia usifanikiwe! Tanzi linaweza kuwa ndani ya mtu au nje ya mtu. nilishawahi kusema ukitaka uepuke hayo yote kuwa uweponi mwa Mungu 24/7 , pili neno la Mungu lisikose kwenye ulimi wako
yani ulikiri usiku na mchana ! unatakapo neno kwa lugha sana na kusoma biblia au kufunga basi kila mara mtu wa ndani anachajiwa! ni kama vile simu, ukiitumia lazima betri ipungue, kila mara inapopu
ngua lazima uichaji! mtu wa ndani anapokuwa full mishale ikija au majaribu unadunda tuu! sasa inafika sehemu ndani yako nguvu za kiungu zinapungua sababu ya
√kutumika. ndio lazima uricharge sasa! kwa kufunga, kusifu kuabudu katika roho, kula neno, na kuomba kwa kukiri neno ukifanya moja kati ya hayo wewe january to December
utapita tuu. sio kwamba majaribu yatakuwa hayaji yatakuwa yanakuja but kila yakija hayakutikisa hata kidogo ni kama vile ukipoteza sh 100! huwa unahangaika kuitafuta!?
√ Mitego ni kama ilivyo unategwa uingie mapepo wapate mlango wa kupita.wakupige kwa nje au kwa ndani. Ndo Biblia kwenye kitabu cha Mathayo 10:16 anasema angalia nawatuma kondoo katikati ya mbwa
mwitu. yani manake tunawindwa kila siku. njia pekee ni kuingia kuzama vilindini mwa Yesu! unapokuwa ndani ya Yesu wewe ni kondoo, na ni simba wa Yuda. Mbwa mwitu wanapokuja unageuka simba wa Yuda unawararua, unapotaka
kuiponya nchi au kumrudisha Mungu mahali kwa damu ya Yesu unavaa sura ya kondoo kwa kuachilia damu ya Yesu. Sasa yapo matanzi ambayo yamewashikilia watu na wamekwama kiuchumi, wamekwama katika ndoa,
√wamekwama kwenye kupata ajira, wamekwama kwenye kupiga hatua, wamekwama katika kazi zao, wamekwama katika afya, wamewekewa vifungo vya washirikina. kujinasua lazima uvae
sura ya simba wa yuda uvirarue ili upite, wengine wamewekewa tego ili wasivuke. ashukuriwe Yesu baada ya kuomba hapa wewe mwenyewe utaenda shuhudia nini Yesu kafanya. kama kuna tanzi lolote au
mitego yotote basi kwa jina la Yesu litaharibiwa kabisa. Halleluyah! wangapi wanakubaliana na Yesu kuwa aondoe tanzi zao, na mitego yao. Maana biblia inasema watakapo kubaliana wawili watatu duniani......... malizia mwenyewe.
Tukaombe sasa!
Ayubu 18:10
Zaburi 141:9
10 Amefichiwa tanzi chini, Na mtego amewekewa njiani.
9 Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu.
√Baba Mungu wa mbinguni asante kwa ufunuo huu! maana leo nimejua ya kuwa yapo matanzi na mtego ambao hutegwa njiani ili kumzuia
mtu kupita njiani. njia ya mafanikio, njia ya ndoa, njia ya kiuchumi, njia ya kupata kazi, njia ya kazi,biashara,huduma, njia ya
√kupata afya, njia ya kupiga hatua, njia za kujenga, njia kuanzisha miradi, njia za kusoma, njia za kupata mitaji, njia za kuzuia amani
na furaha, njia za familia kuwa na umoja na upendo, na vitu kama hivi Bwana! ee Bwana Mungu wa majeshi na vinavyofanana na hivyo! Ee
√Mungu mtakatifu wa Israeli, wewe ni mweupe kuliko weupe, na ni mtakatifu zaidi ya huo utakatifu kwako hakuna mawaa, hakuna
konakona, hakuna uchafu, hakuna ubatili, hakuna uwongo, hakuna fitina, hakuna wivu, hakuna kijicho, kwako hakuna uchafu wowote Baba. Ndio maana nikijiangalia
√naona sitoshi mbele zako! naona sina haki kusimama mbele zako, maana ukinimulika na tochi yako huwezi kosa uchafu au doa, Baba
ninakuja mbele kwa utakaso kamili. Ee Mungu naomba unisamehe naomba unirehemu katika jambo lolote Mungu nililokutenda! kila
√mashataka mbele yangu ya dhambi naomba unirehemu unitakase kwa damu ya Yesu! unitakase kwa damu ya Yesu! kila
kiambaza mbele yangu kilichojengwa sababu ya dhambi naomba unirehemu kwa damu ya Yesu! nami nakivunja kwa damu ya Yesu,
√Baba neno lako katika kitabu cha Ayubu18:10, Zaburi 141:9 ni sululisho ya pale nilipokwama katika maisha yangu, leo nakiri kwa
neno hili Baba unaenda kunivusha kwa nguvu na uweza wako Baba, asante kwa neno hili maana ni mkombozi wangu leo hii pale
√nilipokwama, maana neno lako Mungu ni moto unaokula nami huo moto uko katika ulimi wangu sasa kwa jina la Yesu, neno lako ni panga hatari, na shoka hatari sana
linalofyeka la Mungu, neno lako ni Roho! nami sasa ninakiri hao roho wa Bwana wa kupasua na kuvunja matanzi na tego katika hatua zangu sasa wako juu yangu sasa kwa
√jina la Yesu! Nami sasa kwa neno hili, kwa mamlaka ya jina la Yesu, kwa damu ya Yesu, na moto wa roho mtakatifu ninaenda kuteketeza kila mitego na tanzi ndani yangu au vilivyoniwekea ukuta nje yangu katika jina la Yesu.
√Ewe tanzi na mitego katika ndoa unasubiri nini kufa kwa jina la Yesu nakukamata ewe tanzi uliyekaa katika ndoa yangu kwa damu ya Yesu, nakukamata ewe mtego uliokaa kwenye ndoa yangu nakusambaratisha kwa moto,
√nakupasua kwa moto kwa jina la Yesu, Kwa damu ya Yesu! nawafyeka kwa upanga wa roho, toka katika ndoa yangu sasa kwa jina la Yesu, ewe tanzi ulietegwa katika biashara yangu, katika elimu yangu, katika hatua zangu, katika kazi yangu, katika huduma yangu,
√katika familia yangu, katika mafanikio yangu, katika kujenga kwangu, tanzi katika afya yangu nakumugia damu Yesu itika sasa kwa jina la Yesu! nakuamrisha uitike sasa kwa jina la Yesu, ewe mtego wa kichawi popote ulipo! itika sasa kwa jina la Yesu, ninawashika
√kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu, lazima udhihirike sasa kwa jina la Yesu! ninawafuata roho za kuzimu mlionifunga tanzi, ninawafuata roho za kuzimu mlionifunga tego ninawadaka wote kwa damu ya Yesu, kwa moto wa Mungu, Moto wa
√kuwayeyusha wa roho Mtakatifu uko juu Yenu sasa !nawateketeza kwa jina la Yesu, nakamata shoka nafyeka mizimu ya ukoo , nafyeka uchawi, nafyeka mapepo yote, nafyeka wachawi wote, nafyeka majini yote, nafyeka roho zote, nafyeka kila adui aliyenifunga tanzi na kuniwekea tego kwa jina la Yesu, Kwa damu Ya Yesu! awe ametoka ardhini, angani, baharini, chini ya bahari ewe tanzi uko hatarini nakufyeka kwa jina la Yesu! nasambaratishe kwa damu ya Yesu.
√Katika jina la Yesu Kristo aliye hai! Baba wa mbinguni kila ukuta wa kipepo ulionizunguka nje yangu naamuru kuporomoshwa chini kwa jina la Yesu kwa damu ya Yesu, nyie mlionizungushia ukuta wa tanzi na tego ili nisipite, nyie mlioniwekea mtego wa ili nisivuke naamuru nyote mkamatwe mpigwe pingu za moto kwa moto kwa jina la Yesu, kisha ninachukua shoka kutoka mbinguni wote wanaohusika
√kuniwekea ukuta ninawafyeka kwa jina la Yesu, nawakata kata kwa jina la Yesu! ulinzi wa kipepo wa ukuta kunizunguka naulipua kwa moto kwa jina la Yesu, Naangusha huo ukuta kwa jina la Yesu, nangoa mpaka msingi wake kwa jina la Yesu! wewe ukuta lazima uanguke kwa jina la Yesu! leo ni mwisho nawalipua kwa bomu la moto kwa jina la Yesu, nawateketeza kwa jina la Yesu Kristo! nawaangusha wote chini kwa jina la Yesu Kristo! asante Bwana Yesu maana utaenda fanya zaidi niombavyo na nifikiriavyo katika kija la Yesu Kristo Ameen
rudia mara 7*
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment