MUNGU ATAKULETEA MTU SAHIHI WA KUKUTOA ULIPO

Somo fupi: "Mungu atakuletea mtu sahihi wa kukutoa ulipo"

Bwana Yesu asifiwe!

tuchukue dk. 3 tuu tayari utapata kitu kikubwa sana katika maisha yako! nataka kukuambia kitu kimoja cha ukweli na kitakushangaza,
" Muujiza mana yake ni Mungu kuvunja taratibu au majira yake kwa binadamu"

Mungu ameweka majira na nyakati ya kila kitu, kwenye muuhubiri Mungu amezungumza majira na nyakati zote! iyo ndo program ya kimungu kwa binadamu, inapotokea muujiza basi Mungu kaamua kuvunja utaratibu wake Mwenyewe na huwa haitokei mara zote hutokea mara moja

moja moja sana, na kwa watu aliowachagua! ivyo usiishi kwa miujiza! ukiishi kwa miujiza utavunjika moyo! na unaweza choka sana kumsubiri Mungu,ishi kwa majira na nyakati za Mungu. Mungu akitaka kukutoa lazima atamtuma mtu katika hayo majira na nyakati uliyopo! nitakupa mifano! Yesu alipokuja duniani Yohana Mbatizaji alitumwa kumsafishia njia Yesu, na msomaji mzuri wa

Biblia ukifuatilia vizuri hakuna mtu Yohana Mbatizaji hata ukienda mbinguni leo  hutamkuta Yohana utamkuta Eliya nabii, Ndo mana tabia za Yohana mbatizaji na Nabii Eliya zimefanana kila kitu! roho ya Nabii Eliya ndio ilitungwa tena kama mimba tumboni kwa Elizabeth, naye akamzaa Yohana Mbatizaji ambaye ndio uyo uyo aliyekuwa Eliya.

Mungu akitaka kukutoa sehemu atamtuma mtu sahihi! jina la Bwana libarikiwe uyo mtu akija nakwambia hutapata shida. Tuangalie neno;

Waamuzi 1
22 Nyumba ya Yusufu nayo, wao nao walikwea kwenda juu ya Betheli; naye Bwana alikuwa pamoja nao.

23 Kisha mbari ya Yusufu wakatuma watu waende kuupeleleza Betheli. (Jina la mji huo hapo kwanza ulikuwa ukiitwa Luzu.)

24 Hao wapelelezi walimwona mtu atoka katika huo mji, wakamwambia, Tafadhali, utuonyeshe maingilio ya mji huu, nasi tutakutendea mema.

25 Basi akawaonyesha maingilio ya mji, nao wakaupiga huo mji kwa makali ya upanga; lakini huyo mtu walimwacha aende zake, na watu wote wa jamaa yake.

26 Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo.

Bwana Yesu asifiwe! ukisoma stori hii utaona kuwa hawa wadadisi waliotumwa kwenda kuchunguza huu mji walikuwa wazunguka sana mda mrefu pale walipochoka kuzunguka, ndipo akaja mtu wakamuuliza hujui malango ya mji huu? nasi tutakutendea wema? yule mtu akawaonyesha na wakayaona malango wakapita! manake ni hii!

yule mtu alitumwa na Mungu, Na walipochokea kuzunguka kumbe ndipo kulikuwa na malango ya ule mji! ilipaswa tuu mtu wa kuwaonyesha njia. Basi maisha ya binadamu ndiyo yalivyo unahangaika sababu huijui njia na njia anayo Mungu, siku Mungu akikurudishia macho yako uliyonyanganywa sababu ya dhambi utaona kila kitu clear, Mungu huwa hutuma

watu wa kuja kukuvusha katika maisha yako, hakuna muujiza, muujiza ni 1% ya 100%, hivyo wewe uliyeokoka na kukomaa sisi tunamuomba Mungu amtume mtu sahihi!siyo miujiza ni chakula cha watoto, uyo mtu sahihi anaweza kuwa mtu sahihi kwa maana unampenda au humpendi lakini ndio Mungu kamtuma, shetani ni mjanja sana mara nyingi yule mtu wa kukuonyesha njia ndio shetani anakugombanisha naye mnakuwa chui na paka ili

ukose huo msaada! haijalishi atakuja malaika au mtu kabisa, jifunze kuwa na unyenyekevu, jifunze kueshimu kila mtu, maana hujui Mungu atamtuma nani wengine watu wao ni watumishi wasio na majina, ambao hata level yako haingii,yani ukimkusanya hata dhamani yake ya nje ni kama houseboy wako. wengine ni mtu unakutana naye barabarani, au njiani you will

never know nakuambia. Vita kati ya Daudi na Sauli Mungu alimuinulia Nathan mtoto wa Sauli kuwa ndiyo mtu wa kumfikisha katika ufalme.kwa kumpa siri! can you imagine Baba mtu anataka kumuuwa Daudi, mtoto wa Baba mtu anaenda kutoa siri zote,  leo anza kumuomba

Mungu uyo mtu sahihi wa kukufisha ambaye jibu lako limewekwa kwake aanze kuachiliwa katika jina la Yesu. pia mtu hufanikiwa kwa kusikia maelekezo ya Mungu na kuyatekeleza weka kichwani iyo. jina la Bwana libarikiwe! jina la Bwana libarikiwe! Halleluyah! Halleluyuh!

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

  1. i am blessed.. nabarikiwan sana na mafundisho yako na yananivusha.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA