OMBEA MALANGO YAKO YA ROHONI VIBALI VYAKO VIPATE KUWA HURU
*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.
*ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa.
Twende kwenye neno moja kwa moja na tukakiri na kuomba
Ufunuo 3:8
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
Waamuzi 5:8
8 Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli?
Isaya 60:11
11 Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.
1 Wakor 16:9
9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
√ wachawi wanaponuiza manuizo yao au laana zao za kichawi pepo linapotumwa huja moja kwa moja malangoni kufanya uharibifu.
√ Huja kupitisha vitu visivyofaa ndio maana binadamu hapata maaribifu. unajua siku moja nilikuwa nasikiza wachawi aliyeokoka akitoa shuhuda washirikina wanavyofanya
√ Ndipo nikasema Mungu nisaidie ili kila saa 6 - 9 usiku niombe nisilalale mfano mtu anataka amkuchukue mme wa mtu anaenda kwa mganga wa.
√kienyeji au mchawi anaelezea shida yake mimi flani nimekuja kumfunga flani nataka ndoa yao ivunjike, kisha yule mganga atachukua maelekezo au mashitaka
√ ataulizwa huyu mwanaume ukishamchukua je uyu mkewe tumfanyaje pengine atasema auugue cancer miezi 3 afe! yale maelekezo yake na sadaka
√vinachukuliwa, ikifika saa 6-9 usiku wanaanza kunuiza sasa wanaamka wanaanza kufanya kazi zao. anasema eeh anayefuatia! anayefuatia labla ni Juliana, Eeh mbaya wake
√anasemaje atasema mbaya wake anataka ndoa yake ivunjike kisha mke wake auugue afe! sadaka yake, sadaka mbuzi, kuku, bata, ngombe! watamchinja yule
√ mnyama wakitaja ewe jini flanipokea sadaka hii! ukatenge ndoa ya flani, ukamuuwe flani, na kutamka maneno ya laana usiku mzima kuanzia saa 6-9
√wanaloga tuu nakutambika, wakimaliza wanafanya tendo la imani la kutenga ndoa, na kuleta jeneza kufanya msiba na wanalia kabisa wachawi kama wapo msibani, wakisha
√kumaliza tuu wanajibizana
tawire! wanajibu tawire! mambo yao huku wakristo tumelala, wakimaliza kazi sasa !unasikia mtu kapata ajali kafa, au kaumwa kichwa gafla kafa! sasa vitu vinavyoruusu aya
√mashambulizi ni malango katika ulimwengu wa roho. wako watu wanaokuzunguka wanakuchekea lakini hawakup endi,solution sio kutengana nao no! wapo ndugu, jamaa
√marafiki kila tatizo katika maisha yako asilimia kubwa limesababishwa na uchawi! hawa wachawi kila siku wanalani watu,wananuiza kila siku
√ wanafunga watu hawachoki huku wewe umelala tuu unakoroma, sasa usipojifunza kulinda malango yako utakuwa mateka kila siku. maombi ya kwenye malango ni ya kila siku.
√ili kila jini au pepo linapokuja linakutana na damu ya Yesu linafunga break za hatari na kurudi spidi kwa aliyetumwa ndo unasikia wachawi wamekufa gafla ni sababu ya
√ damu ya Yesu iliwashambulia mapepo wakaenda kuwashambulia waliowatuma. sasa ni muhimu maombi haya utafanye kila siku. vita vya
√vyovyote katika ulimwengu wa roho hufanyika malangoni, ukifanikiwa kumiliki malango shetani hakuwezi kamwe! ukicontrol malango yako umefanikiwa hapa duniani na hata mbinguni.
Bwana Yesu asifiwe sana!
twende tukapambane sasa katika malango! yapiganie malango yako!
Baba asante kwa kunikumbusha ya kuwa vita vyote katika ulimwengu wa roho hufanyika katika malango! asante kwa kunijulisha na leo
ninaenda kufanya vita malangoni pangu katika jina la Yesu Kristo na kwa damu ya Yesu, Roho Mtakatifu ninaomba unisadie kuomba kama vile
utakavyo wewe! Bwana Yesu ninaomba uniunge vita katika mapambano haya katika jina la Yesu. Eee Mungu Baba ninakuja kwako kwa ajili ya utakaso
kamili katika jina la Yesu, ninaomba unirehemu katika jambo lolote Mungu lililo mbele yangu kama mashtaka ya dhambi naomba unirehemu
Mungu, ninaomba unisamehe unitakase kwa damu yako, unitakase kwa damu yako katika jina la Yesu, Naomba damu ya Yesu inioshe na
kunitakasa kwa jina la Yesu Kristo. Mungu uliye hai naomba uyafute makosa yangu yote niliyoyatenda! natangaza kuwasamehe watu wote
niliowaweka moyoni! watu walioniudhi, kunikwaza Baba Mungu ninatangaza wote kuwasamehe ni kuwasahau! Ee Mungu Baba nimezingatia
sheria ya kusamehewa dhambi sasa Baba yangu uliye mbinguni ninaomba unisamehe sasa na usahau uovu wangu wote ninaukiri mbele zako na
ninaomba unirehemu na kunitakasa katika jina la Yesu, Unitakase kwa damu ya Yesu Baba, nitakase roho yangu, mwili wangu, nafsi yangu Baba
Ee Mungu Baba ninaenda kuachilia damu ya Yesu ya utakaso Baba ili kumiliki malango yangu! sawasawa na neno lako 1 wakor 16:9
kwamba nimepewa malango mengi ila wanipingao ni wengi ni kweli Baba wanaonipinga ni wengi! Ni kweli Baba katika ulimwengu wa roho wanatafuta
malago yangu Baba ni wengi! Baba kwa namna moja au nyingine nimehusika kufanya maagano na ibilisi ivyo yakasababisha milango hii
kuwa wazi kwa mapepo, leo ninaomba unirehemu katika jina la Yesu, maagano yote niliyoyafanya na miungu, niliyoyafanya katika ndoto
maagano yote kwa njia ya kula na kunywa, maagano yote kwa njia ya kuona kusikia, kwa njia ya kuona, maagano yote kwa njia ya kukiri, maagano yote
kupitia rafiki zangu, kupitia ndugu zangu, kupitia watu wanaonizunguka, kupitia matendo yangu! maana imeandikwa umetegwa katika
maneno ya kinywa chako ninaomba leo unirehemu katika jina la Yesu.Baba ninaomba sasa rehema kwako unisamehe katika source ya dhambi, asili
yoyote ya dhambi ya iliyoingiza magaano hata kama ilikuwa ni majibizano, au kitu chochote nachokumbuka au nisichokumbuka ninaomba
rehema Mungu ninaomba unisamehe ninatubu kwa ajili ya uovu huo katika jina la Yesu Kristo. Baba kwa kutumia damu ya Yesu Kristo ninaenda sasa
kutakasa malango yangu yote, na kwa msaada wa damu ya Yesu Kristo! Ewe malango yangu ya ndoa, biashara, kazi, marafiki, vibali, kumiliki,akili
malango yangu ya kutawala, mahusiano, uchumi, huduma, mikono, miguu, afya, familia, uzazi/uzao, watoto, Fursa, kuongezeka, kupiga hatua,
kupanua hema, wafanyakazi wa ndani, Heshima, Maarifa , Hekima, Makazi, Ndoto, Mme, mke, Wasaidizi wa kiungu (JEHOVAH) Lango la nafasi ya
kazi, malango ya nafsi, malango ya mwili, malango ya roho, malango ya ulimwengu wa roho, malango yangu yaliyopo katika ardhi, katika mbingu,
katika anga, baharini, lango la amani, lango la furaha, lango la kumwabudu Bwana katika roho na kweli.kila mahali sasa katika jina la Yesu! inueni vichwa
vyenu sasa! inueni shingo zenu sasa, nawatakasa damu ya Yesu, nawanyunyizia damu ya Yesu, ya utakaso, chochote kinachopita, au kilichopita,
katika malango hayo nakitakasa kwa damu ya Yesu! eee Mungu Baba ninaomba utakase malango yangu, nanyunyizia damu ya Yesu ya
utakaso katika malango yangu katika jina la Yesu. kila sheria iliyo katika malango hayo ya ibilisi ninaivunja kwa damu ya Yesu sheria inayotawala
malango yangu kupitia ardhi, kupitia anga, kupitia bahari, hata chini ya bahari izo sheria za ibilisi nazifuta kwa damu ya Yesu, sheria ya mitandao ya ..
giza katika malango yangu, izo sheria za ibilisi katika malango yangu nazipasua kwa moto, nazifuta kwa moto wa roho Mtakatifu kwa jina la Yesu Kwa
damu ya Yesu, nateketeza, michoro ya giza, master plan ya kukandamiza malango yangu kutoka kwa ibilisi nakulipua kwa moto kwa jina la Yesu
ninafunika malango yangu kwa moto wa roho mtakatifu! ninayawekea ukuta aa damu ya Yesu, ukuta wa moto kwa jina la Yesu Kristo.
wazimamizi haramu na walinzi haramu kutoka kwa ibilisi nawalipua kwa moto , nawateketeza kwa damu ya Yesu, Enyi wasimamizi wa
sheria wa kipepo katika malango yangu, watekelezaji wa sheria hizo nawalipua kwa moto kwa jina la Yesu, ninaamuru wote wanaotumwa
kuja kupandikiza mambo mabaya ya ibilisi, kupitisha mambo mabaya toka kwa ibilisi ninaamuru kuharibiwa kwa moto kwa jina la Yesu Kristo
Ewe adui katika malango yangu unafanya nini hapo nakuzungushia moto wa Roho Mtakatifu hapo ulipo nakuyeyusha sasa na moto wa
Yesu, nakulipua kwa damu ya Yesu, nawatakamkia ya kwamba mipango yote ibilisi katika malango yangu kutokufanikiwa kwa jina la Yesu
Baba ninaweka mlinzi katika malango yote ambao ni malaika wako wa vita, malaika wako wa ulinzi katika jina la Yesu. Nikimwaga damu ya Yesu ya
hukumu ya haki katika malango yangu yote. katika jina la Yesu nimeomba Amen.
rudia mara 3*
omba kila siku mpaka ufanikishe njia yako!
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Be blessed pastor Iam so excited with your lesson
ReplyDeleteUbarkkiwe Mtumishi wa Bwana Yesu. Nimejifunza kitu kuhusu malango.
ReplyDeleteRev. Mtinege. A. K
TANGA, Tz