MAOMBI YA KUVUNJA ROHO YA KUKWAZIKA

*Maombi haya yana uvuvio wa Roho Mtakatifu. Wengi yamewafungua kwa kuwa ni Roho mwenyewe anafanya kazi kupitia neno la ukiri.

ivyo sina shaka na wewe utawekwa huru. Ni maombi niliyopewa na Mungu mwenyewe Ivyo unapoomba omba kwa kumaanisha kufunguliwa

Luka
MLANGO 17
1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!

√ kuna milango ya siri ya ibilisi ambayo hutumia kufunga vibali vya mtu. mojawapo ni KUKWAZIKA.

Tahadhari:  ujumbe huu si mwepesi ni wa mtu wa ndani ivyo ukijisikia tofauti ujue Mungu anaanza kudili na wewe!

Bwana Yesu asifiwe!

√ Mungu akitaka kukupa mambo makubwa au kukupeleka viwango vikubwa sana lazima utakutana na makwazo tuu. ili kuandaa moyo wako. Kukwazwa si tatizo! bali

√kukwazika kwenyewe ndiyo
mlango wa ibilisi. Hata Yesu mwenyewe walikuwa wanajaribu Kumkwaza, lakini hakukwazika alilinda sana moyo wake! Makwazo yapo kila mahali,

√yapo katika ndoa! yapo kwenye biashara! yapo kazini, yapo katika familia, yapo, yako katika ukoo, yapo kwenye daladala! yapo hospitalini, atakuja mtu kukukwaza makusudi

√sehemu yoyote kwenye huduma, hata ndani ya kanisa makwazo yapo na hayana budi kuja ila cha msingi! kulinda sana moyo hutakiwi ukwazike!

√kuna tofauti kati ya kukwazwa na kukwazika UNAPOKWAZIKA tuu ibilisi hupata njia. sasa tatizo lipo kwa wale watu wanaokwazika ovyo, yani akifungulia kuongea ataongea mpaka kifua

√kimuume, Mungu amezuia vitu vyako vingi vya msingi sababu kila akikuangalia anaona wewe huwezi sitahimili! hujafiti!  maana baraka inapokuja kubwa na

√walaji wanakuwa wengi kwa hiyo sababu kama unakwazika kirahisi itakupelekea wewe kutoka uweponi mwa Mungu na atakupoteza ndio maana

√Mungu anakuacha kwanza, kama unalilia mme, au mke alafu Mungu anakuona wewe ni  mtu wa kukwazika ovyo Mungu hukuacha kwanza mpaka

√ukomae! leo Mungu kuna vitu Mungu amevinyamazia kwa makusudi sio sababu hataki kukupa bali anaogopa kukupoteza, unajua alikununua kwa gharama ya damu ya Yesu kwa sababu iyo bado anakuona hujafiti akikupa utapotea maana kitu kidogo

√unakwazika, yani wewe ni mwepesi wa kukwazika, hata mambo ya kawaida kabisa wewe ni mtu wa kukwazika kwazika! hili ni somo la mtu wa ndani linamponya mtu wa ndani. ivyo ukiona wewe unakwazika ovyo tatizo halipo kwa

√wanaokukwaza, bali wewe unayekwazika ovyo. ni kitu ambacho humfanya pia Mungu kukupa wewe miujiza kidogodogo anaogopa kukupoteza kutokana na tabia ya kukwazika ovyo ivyo atakucheki kama utastahimili.

√na miujiza au baraka ndogo ndogo anazileta kisha anaruusu makwazo.kuna mtu Mungu akimfanyia baraka akapata kampuni, au biashara kubwa yenye mtaji wa
100m+ basi ndo Mungu kampoteza maana walaji

√watakuwa wengi sababu ya wewe ni mwepesi wa kukwazika mwisho unakuta hata ibada yake haifanyi katika roho na kweli. nia ya Mungu kukubariki ni ili wewe usiwe na kizuizi cha kumfanyia Mungu

√ibada katika roho na Kweli kukwazika huleta jazba, huleta kususa, huleta kuzira, hupelekea mtu kufanya maamuzi mabaya. Na hii ni roho kabisa ya ibilisi.inakaa ndani ya mtu. Embu twende leo

√tukaikemee kwa jina
la Yesu, alafu tumuombe Mungu yale mambo ambayo aliyazuia sababu ya tabia kukwazika ovyo sasa ayaachilie Bwana Yesu asifiwe sana.

√Natumai Roho Mtakatifu ataongea na wewe jumbe kama hizi mtu akipata au kusoma huwa hujitoa atasema mimi mbona sikwaziki! mpendwa tii

√sauti ya Mungu nyenyekea na uombe huwezi jua udhaifu wako uko wapi? jina la Bwana libarikiwe sana.

tukaombe sasa!

Luka
MLANGO 17
1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!

Baba katika jina la Yesu asante kwa kuwa nimefahamu na nimejua ya kuwa kukwazika ovyo kwa mtu kunakuzuia wewe kufanya baraka kubwa

katika maisha yangu,
pia kukwazika ni mlango wa ibilisi kupita ni mlango wa mamuzi mabaya, ni mlango kunikosesha taarifa nzuri,

mlango wa kuniharibia mahusiano na watu.
Ni mlango wa hasira, ni mlango wa kususa, ni mlango wa kuzira, hii hupelekea kufanya

maamuzi mabaya, ni mlango pia wa kuharibu mahusiano katika ndoa.Ni mlango wa  kuharibu mahusiano na watu, mahusiano katika biashara, ni

mlango pia unaopelekea ibilisi kufunga mambo mengine. Na sababu ya milango hii kufunguka pasipo mimi kujua, wewe Mungu unajua ndo mana

baraka zingine unasubiri kwanza hali kukwazika kwangu ovyo iniache. unanisubiri nikue kiroho. na kupelekea kuchelewa kufika. Mungu nimegundua

udhaifu wangu leo! pia nimejua na kugundua kukwazika nyuma yake kuna pepo la kukwazika au Roho ya kukwazika na ni lango la siri la adui hupita kufunga

malago yangu, leo Bwana katika jina la Yesu, ninaomba unirehemu ninaomba unisamehe! dhambi yoyote iliyofungulia mlango wa roho

ya hasira ninaomba rehema unitakase Mungu wa kweli. ninatubu dhambi zangu zote ovu mbele zako Mungu wa kweli, ninaomba unisamehe

unitakase katika jina la Yesu! nakuja kwako Baba kwa utakaso kamili, wakati mwingine umekuwa ukinionya lakini sikio langu limekuwa zito

leo nakugeukia wewe kwa damu ya Yesu! unitakase Mungu wangu kwa damu ya Yesu, Biblia imesema 1Yohana 3:8, tokea mwanzo atendaye

dhambi ni ibilisi na kwa kusudi
hili mwana wa Mungu alidhihirishwa kwetu ili kuzivunja kazi za ibilisi, Baba hii ni kazi mojawapo ya adui.

Ibilisi leo nimekugundua na leo kwa jina la Yesu na kwa damu ya Yesu ninaenda kukusambaratisha kwa damu ya Yesu, kwa moto wa Roho

Mtakatifu, wewe unayenifanya mimi kukwazika, wewe unayenitengenezea hasira ndani yangu, wewe unayenifanya mimi kuzira na

kususa, leo katika jina la Yesu Kristo, umekamatika leo katika jina la Yesu. malango uliyoingilia au yalikupa nafasi nayamwagia damu ya Yesu

nayatakasa wa damu ya Yesu, Bwana Mungu wa majeshi huo msingi wa pepo la kukwazika, huo msingi wote na hiyo sheria ninauteketeza kwa moto kwa

jina la Yesu, nafuta iyo sheria ya kukwazika kwa damu ya Yesu, naifuta katika ulimwengu wa roho, naifuta katika ardhi, naifuta katika anga, naifuta

katika bahari, hata kule chini ya bahari kule kuzimu iko kitabu kilichoandika jina langu kikakabithiwa pepo la kukwazika nafuta jina langu

kwa damu ya Yesu, nachoma makaratasi yote yenye huo mchoro wa kimkakati, wenye iyo master plan, ya mimi kukwazika nateketeza kwa

damu ya Yesu kwa moto wa Roho mtakatifu kwa jina la Yesu
Baba wote wanaohusika kusimamia na kutekeleza iyo sheria juu yangu mimi nina wa

mwagia damu ya Yesu ya hukumu juu yao sasa! katika jina la Yesu, juu ya wasimamizi na watekelezaji wa iyo sheria ya mimi kukwazika! ninawahuk

umu kwa damu ya Yesu, ninahukumu kwa damu ya Yesu. ewe adui sawasawa na na luka 10:19 saa imekwisha kufika wewe adui huna chako

tena kwandu maagano yako yamefutwa kwa damu ya Yesu, lango ulilokuwa unaingia limetakaswa kwa damu ya Yesu, na dhambi yangu imesa

mehewa na Mungu, ivyo wewe ni mhamiaji haramu katika mwili wangu, katika nafsi yangu, katika roho yangu! wewe na mawakala wako wote amba

o mmeharibu mahusiano yangu, mmeharibu ndoa yangu, umeharibu uchumi wangu, umenipotezea fursa, wewe pepo la kukwazika naongea na

wewe, wewe unayesababisha nipoteze baraka zangu, ninaharibu mahusiano na watu wazuri, wewe uliyekaa katika ndoa yangu, wewe uliyekaa

katika uchumba wangu, na umekaa katika uchumi wangu, ukafunga vibali vyangu, ukafunga hatua zangu, mafanikio yangu, ukanichelew

wesha kufika leo katika jina la Yesu, leo kwa damu ya Yesu, umekamatika huna pa kujificha, msingi wako umebomoka, nguzo zako zote zimeangushwa

tokaaa katika nafasi yangu, tokaaa katika akili yanguu,

tokaaa katika moyo wangu
tokaaa katika mawazo yanguu
tokaaa katika ulimwengu wangu wa roho! tokaa katika roho yangu, toka ibilisi,

mapando yako yote ndani yangu nayachoma moto wa roho Mtakatifu, nakuangamiza kwa moto! kama umepitia ardhi nakufuata hukohuko nakulipua

kwa moto, umepitia anga nakufuata hukohuko nakulipua kwa moto, umepitia baharini nakufuata hukohuko nakulipua kwa moto, umetokea kuzimu

chini ya bahari nakufuata hukohuko nakulipua kwa moto kwa jina la Yesu Kristo, ninakuamuru vitu vyangu vyote vizuri ulivyovimeza lazima

uvitapike, umemeza ndoa yangu, umemeza uchumi wangu, umemeza mahusiano yangu, umemeza huduma yangu, umemeza kazi yangu,

umemeza biashara yangu, nakuamuru tapika sasa! tapika mafanikio yangu, tapika vibali vyangu wewe pepo la kukwazika wewe wakala wa

ibilisi leo nakumiminia risasi za moto kwa jina la Yesu Kristo, kwa damu ya Yesu Kristo! tumbo lako lililomeza vitu vyangu lazima litapitishwe!

sawasawa na Ayubu 20:15, tapika sasa kwa jina la Yesu, achia ndoa yangu, achia hatua zangu, achia vibali vyangu, achia mafanikio yangu, achia

ndoa yangu adui, achia uchumi wangu adui, achia kazi yangu adui, achia biashara yangu adui, achia ufahamu wangu adui, achia nafsi yangu adui,

achia mawazo,akili yangu adui, achia mwili wangu adui, ukuta ulionizungushia naupasua kwa moto kwa jina la Yesu, naunyunyizi damu ya Yesu,

magereza uliyofungia baraka zangu na mpenyo nazilipua kwa moto katika jina la Yesu, vifungo vyako, vizuizi vyako, mipaka yako, ukuta wako,

misitu mbele yangu, jangwa mbele yangu, milima mbele yangu, na hilo jitu mbele yangu, mawe makubwa uliyonifungia, mawe katika miguu, mikono

shingo, vitanzi vyovyote katika
miguu, katika mikono ninaamuru futika! futika! futika! potea! potea! potea! katika jina la Yesu, kwa jina la Yesu Kristo!
wewe na watenda kazi wako walionijia kwa sura za wafalme wa giza, wakuu wa giza, mamlaka za giza, jeshi la pepo wabaya, roho chafu, pepo

wabaya, mizimu, majoka, majini ya aina yote, ikiwepo jini mahaba, wachawi, waganga wa kienyeji, na ma urgent wote wa ibilisi wowote wale, ninaamuru

kukamatwa sasa kwa jina la Yesu, ninaachilia mvua ya acid ya Mungu juu yenu, ninaachilia mvua ya damu ya Yesu juu yenu, ninaachilia mvua ya moto
wa Roho Mtakatifu juu yenu, ninaachilia mawe ya moto kutoka mbinguni yawapige na kuwaangamiza kwa jina la Yesu, popote mlipo au

mlipojificha nawafichua kwa moto kwa jina la Yesu, adui huna pa kukimbilia nakuachilia mishale ya moto kifuani, kichwani, nakuteketeza kwa

jina la Yesu, leo nakusambaratisha pepo la kukwazika, roho ya kukwazika, naamuru ukamatwe ufungwe katika shimo lenye moto na

usirudi tena dunia katika jina la Yesu. Mungu Baba naomba sasa kwa neema yako na Rehema zako yale mambo yote uliyoyazuia sababu ya

kukwazika kwa kuwa adui hayupo tena na ameangushwa ninaomba sasa uyaruusu yaje kwangu tena kwa utukufu wa jina lako ameen.Ameen

Rudia mara 7*

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA