UFANYAJE UNAPOKUWA KATIKA JANGWA MDA MREFU?

Somo fupi: ufanyaje unapokuwa katika jangwa mda mrefu?

Yohana 5:2-8

2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.

3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.

4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]

5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.

6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?

7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.

8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.

*Angalia huyu mwanamke amekaa katika pito miaka 34
ila hajawahi kukata tamaa.

*Ibrahimi naye alikaa katika pito la kumsubiri Mungu miaka 25, alihaidiwa mtoto akiwa na miaka 75, kuja kupata mtoto ana karibia miaka 100

*Ugumu wa jaribu si jaribu lenyewe bali ugumu wake upo katika mda! jinsi jaribu linavyokaa na mtu mda mrefu ndivyo jinsi jaribu ilo linavyomtawala kila kitu chake!

*Majaribu huleta uchungu, majaribu hukatisha tamaa, majaribu hupoteza matumaini, jaribu linapokuwa na mda mrefu sana hukaa mbele ya kila kitu kiasi cha kwamba hakuna kingine kinachoja akilini  zaidi ya hilo jaribu, manake jaribu mara ingine humtawala mtu.

*Jaribu hujeruhi nafsi! ushawahi kuona mama mtu anapiga mtoto hata kwa kosa la kawaida tuu, mwanawe akimwita tuu yani atatoa tusi kubwa kila mtu atashangaa, ni kawaida mtu ambaye nafsi yake imejehuriwa huwa ana hasira mda wote, hana amani, na hii hutokana na kutokusa
mehe! wanawake wengi wamejeruhi

wa nafsi , na wengi si wepesi wa kusamehe, na hii hutokana na nature yao na sheria ya Mungu toka mwanzo, kutokusamehe si rahisi, na kuachia uchungu si rahisi kibinadamu sababu hivi vitu ni roho kabisa za ibilisi wala haviko ndani ya mtu. kwa iyo unaporuusu Roho ya Mungu ya kusamehe inakuja juu yako basi

roho ya uchungu, na kutokusa
mehe ndipo roho hii humwondo
ka mtu na kumwacha hapo ndo utasikia anasema nimemwachia nimemsamehe kabisa wala sina kinyongo naye tena.

Jaribu huleta uchungu sababu shetani huongea kupitia jaribu na kiukweli hamna kitu kama hiko shetani anachoongea! shetani anatabia ya kuongea na nafsi yako kwa kukuonyesha kuwa mtu aliyehusika na wewe kupitia magumu hayo! aidha atakuonyesha Mungu ndo anayehusika, au mtu fulani ndo anayehusika! sasa sababu huwezi kulaumu maana ni sauti

uliyoisikia ipo ndani yako! ile lawama ndo inageuka kuwa uchungu, uchungu huleta hasira jazba, na kutokusamehe! na vyote hivyo ni roho za ibilisi, kilichosababisha ni yale maongezi ya ibilisi uliyokuwa unayasikia kwenye nafsi yako.

ndo mana mtu yoyote asiyejua hili aliyepitia kwenye pito la mda mrefu na hajapata msaada wa ki Mungu ana tabia ya kulaumu, ana hasira zisizo za kawaida, ni mkatili saa ingine, ana jazba, si mwepesi wa kusamehe, haridhiki katika lolote, anapenda kulipisha kisasi, hupenda kulumbana, au kupenda kuchafua hali ya hewa,

moja kati ya hizo utakuta anazo sana,au tabia yoyote ambayo si ya kawaida! kujitenga na watu, kutokujiamini, nazungumzia vitu ambavyo vinaweza mpata mtu kwa kupitia mapito ya mda ya mrefu,  lakini zote izo ni roho za ibilisi na leo Mungu atakufungua!

SASA TUNAFANYAJE KIBIBLIA!

luka 5-4-6
4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.

5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.

6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika;

1. Tafuta neno linalohusika na situation yako

*Umeona hapo Petro ameambiwa nenda mpaka vilindini utapata samaki Petro  kulalamika Bwana Mkubwa tumefanya kazi ya

kuchosha usiku kucha. baadae akagundua ya kuwa yule anayeongea naye ni Yesu na si mtu wa kawaida ndipo akasema KWA NENO LAKO NITASHUSHA NYAVU!

√Kitu cha kwanza kabisa lazima ujue kuwa Yesu situation yako anaifahamu na anaijua! Ndo mana hakutaka maelekezo mengi kwa Petro, Kitu cha kwanza kabisa ni kujua neno lako kwenye biblia la situation yako. Unajua maneno yote kwenye biblia ni program iliyokuwa tayari kusolve tatizo lako lolote. linafanya kazi kwa wewe kulikiri kwa jina la Yesu. unapolikiri unalazimisha wale Roho wa Mungu katika iyo program watoke katika neno waingie katika ulimwengu wako  wa roho waje kusolve!

√majaribu ya Mungu kama Mungu kataka uyapitie utayapitia tuu, ila kama jaribu linakushinda basi ujue ndani yake amejificha ibilisi, sababu majaribu yote ya Mungu yana mlango wa kutokea. kwa iyo usimwombe Mungu kutoka kwenye jaribu mwombe Mungu nguvu za Rohoni. nguvu za rohoni sio faraja, sio kutiwa moyo hapana! zipo nguvu kabisa ambazo Mungu

huongezea watu ili waweze kuvuka na kumaliza jaribu, na jaribu lolote la Mungu ni kwa utukufu wa Mungu ivyo usilaani au usifyonze, wala usiombe kutoka! nitakukumbusha kitu wana wa Israeli waliahidiwa baraka kupitia Ibrahimu si unakubali? lakini walipitishwa kwenye jaribu sio ndio kule misri? ila walivyotoka huko walitoka matajiri wakubwa kweli si kweli? je ile ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu ilitimia au haikutimia? nikukumbushe tena Yakobo alikuwa mtumwa wa labani miaka mingi sana

akaenda kujaribiwa lakini alivyotoka huko si alitoka na utajiri mkubwa wa mifugo na wake wawili, Yusuph pia alijaribiwa alipata mateso makubwa sana alivyotoka huko akawa waziri mkuu wa misri, Danieli alijaribiwa lile lilikuwa jaribu la kufa, lakini alipotoka hapo Mungu alimfanya mkuu wa nchi ivyo usilalamike bali, taka kujua hawa watu

kwenye biblia walivukaje vukaje, ilikuwaje Yesu akavuka pale gatesmane, ilikuwaje Ibrahim akaweza kusubiri miaka 25, inakuwaje nabii Eliya akaendelea na kazi ya Mungu wakati alifika sehemu alishamuomba Mungu afe?

2. Omba kutiwa nguvu na Mungu

1 Wafalme 19-4-8
4 Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee Bwana, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.

5 Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule.

6 Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.

7 Malaika wa Bwana akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako.

8 Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.

* Stori hii tunaifahamu! baada ya nabii Eliya kuwauwa manabii baali akapata vitisho kwa mke wa Ahabu Yezebeli, kuwa atauwawa kama alivyowauwa manabii wa baali, haya ni majaribu biblia inasema akaenda akajilaza chini ya mti akamwomba Mungu afe kwa akamwambia Mungu aitoe roho yake! Mungu alichofanya akamtuma malaika yule malaika akaja akamletea chakula manake nini mtu wa ndani alikuwa na njaa! akatiwa nguvu akala mara ya kwanza akala mara ya pili. kwa kile chakula alichokula kikamwezesha kutembea mwendo wa siku 40!

√ Mungu akikutia nguvu ndani ya jaribu lako nakwambia hutakata tamaa, hutasinzia kiroho, hutachoka! hutaona uchungu wala maumivu, na maombi ya kutiwa nguvu fanya maombi special siyo unasema Bwana nitie nguvu Bwana nitie nguvu no unaomba kabisa kama unavyoomba kazi, kwani ukimuomba Mungu kazi unaomba dakika 5? si zaidi! sasa ufanye ivyo.

Luka 22-41-43
41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,
42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka

chini.

√ Yesu alikuwa binadamu kabisa kama wewe na mimi na alimshinda ibilisi katika ubinadamu ili wewe pia umshinde.

√ Yesu pia alipata majaribu, akifikiria c.v kubwa aliyokuwa nayo amemfufua lazaro alafu ndo ilikuwa habari mpya ya mjini, ameponya viziwi, viwete, mabubu wameongea, kafanya maajabu makubwa kutuliza pepo, kulaani mti ukanyauka, akawa anafundisha maelfu kwa hekima na  maarifa ya juu sana

watu wanamuamini alafu embu fikiri leo hii unaambiwa ukasulubiwe, ukatundikwe juu ya mti uchi?! daah! kibinadamu ni ngumu maana akiwaza heshima tayari aliyojijengea watu wanavyomuamini kuwa hashindwi kitu, alafu alivyokuwa anawajibu wale mafarisayo na masadukayo! watu wanawacheka! dunia yote

imeanza kumwamini alafu gafla akapigwe alafu atundikwe uchi msalabani ilikuwa ngumu kwa Yesu, kama binadamu wengine akamwambia Mungu mmh! ikiwezekana jaribu hili linipite! liniepuke! Mungu akamtuma malaika tena akaja akamgusa akamtia nguvu ya Mungu. unaambiwa ile nguvu aliyoipata ilimfanya aombe mpaka atoke damu. Mungu hakughairisha lile jaribu

la Yesu bali alitiwa nguvu. Omba Yesu akutie nguvu! na zawadi yake yeye ni mfalme wa falme huwezi enda kwa Mungu bila yeye, huweza pata chochote bila yeye! kila kitu kipo mikononi mwake. Yesu alivipata hivi vyote baada ya kutiwa nguvu. Halleluyah Halleluyah, najua imani yako imeinuka na Yesu amekuponya. mrudishie Mungu utukufu.

jina la Bwana libarikiwe

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA