SABABU ZA KUKOSA MOYO WA KUFANIKIWA/UHODARI WA MOYO

somo: Sababu za kukosa moyo wa kufanikiwa/ Uhodari wa Moyo

Kumbukumbu 31:6,8

6 Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.

8 Naye Bwana, yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope wala usifadhaike.

* Uhodari wa moyo au ushajaa wa moyo ni ile hali ya kuwa na moyo wa kufanikiwa, Hali ya kutokutaa

tamaa, ile hali  ya kuwa na ujasiri  au uhakika wa kufanikiwa moyoni. Tuangalie Katika ilo neno kuna

mambo makuu mangapi.

1. Msiogope wala msihofu
2. Bwana Mungu wako ndiye anayekwenda pamoja na wewe
3. Hatakupungukia wala kukuacha
4. Ndiye atakayekutangulia
5.Atakuwa pamoja na wewe
6. Hatakupungia wala kukuacha
7. Usiogope wala usifadhahike

√ Biblia inaelezea sababu za mtu kuogopa na kuwa na hofu. Au sababu za Mtu kutokuwa na hodari

wa moyo, kinyume cha uhodari ni unyonge wa moyo katika kufanikiwa. Bwana Yesu asifiwe!

1.USIOGOPE WALA USIHOFU

*Asilimia ya watu wengi wanaogopa! ingawa hofu zinaweza kutofautiana mfano mtu ambaye ameokoka kweli kweli huwa hanaga

hofu ya mauti. Wala hana hofu kama leo ikiwa mwisho wa dunia, Ni sababu Yesu ni uzima wa milele ivyo anapoingia ndani yako basi

roho ya hofu inakuondoka inabaki roho ya uzima na milele. sasa tujiulize Woga na Hofu unatoka wapi? ukijua hii siri na kuelewa

Basi tokea leo hofu na woga ndani yako vitakuachia kwa jina la Yesu. Hofu na woga husababishwa na taarifa za uwongo! kutoka kwa ibilisi

Kwenye Biblia wanaita elimu ijiinuayo kinyume na Elimu ya  Mungu, ibilisi ana attack kupitia fikra, kupitia mawazo ya uongo!

sasa sababu yanakuta hakuna kizuizi,  cha mishale hii inapopiga basi huenda kukita katika moyo! ile sumu husambaa kidogo kidogo

katika mawazo na fikra na kuuwa kila ambacho unakiamini! na baada ya kuondoa kila unachokiamini ndipo sasa roho ya hofu na woga

tokea kwa ibilisi wanaanza kuja na kufanya kazi ndani yako kwa iyo ni roho za ibilisi kabisa roho ya hofu roho ya woga roho ya mashaka ni

kazi za adui ni wakala wa Yohana 10:10 kuuwa kuchinja na kuiba, Bwana Yesu asifiwe sana, Kwa iyo taarifa zenyewe zinazokuja ni zile

za kukutisha alafu hazina majibu kwa kuwa hauna neno, mfano utasikisikia sauti inakuambia wewe utakufa tuu na ajali, inajirudia na

kujirudia, utasikia inakuambia umekaa mda mrefu huna kazi hutakaa uje upate kazi, inakuambia itakuwaje kama ukigundua mme

wako anakusaliti, au  mke wako anakusaliti, au inakuambia hii biashara itakufa, au inakuambia unalogwa saizi kuna watu

wanakufanyia uchawi, au inakuambia mtoto wako ataja pata mimba akiwa shuleni, au inakuambia itakuwaje siku ukija

kukosa kazi familia utaiendeshaje? au sauti inakuambia maombi yako hakuna mahali yanaenda, hujui kuomba! Sasa sauti hizi

zinaendana  na kuonyeshwa mifano! mfano unaona picha ya ajali! kisha sauti inakuambia umeona iyo ajali? iyo ni kazi ya

uchawi! wewe huwezi

pambana na uchawi kwa maombi angalia jinsi watu walivyokufa? zipo sauti za uongo tunazozisikia kupitia sikio shetani anakunongoneza

sikioni na sauti zinazojirudia rudia katika nafsi usiku kucha mchana kutwa zikikuonyesha matukio ya zamani ulivyofaili, na macho yako

yakiona matukio ya kufaili, Baada ya mda inakutengenezea woga yani unasurrender kuwa huwezi baada ya kusurrender inakuletea kutojiamini

yani hofu ndani yako. wakati huo umesahau ahadi za Mungu zinasema nini katika biblia katika maisha yako, matokeo yake!

unaanza kwenda sawasawa na akili yako jinsi ionavyo badala ya neno la Mungu linasema nini? kwa iyo hata msaada wa neno unapokuja

kukutoa hapo ulipo tayari fikra zako na akili yako imefungwa! kwa iyo zipo taarifa za uongo za ibilisi kupitia nafsi, macho, fikra, ufahamu,

masikio, tafsiri potofu vinavyokuja kukupiga kwa sababu hakuna ulinzi izo sumu husambaa katika mawazo na fikra na baadaye roho wa hofu,

woga, mashaka huja kuanza kufanya kazi ndani yako na unakuwa tayari ni victim wa hayo mambo. Mungu alijua haya yote.

2.BWANA MUNGU WAKO NDIYE ANAYEKWENDA PAMOJA NA WEWE

*sasa nini hutokea katika akili yako kwanza unajiona uko mwenyewe na hakuna wa kukutetea? unafikiri kwa nini watu wanakuwa wanyonge

wakimya? unakuta mtu ni muongeaji gafla anakuwa mkimya? Ni sababu moyoni mwake haoni msaada wa mtu wa kutembea naye

katika hiyo taarifa ya uongo ya shetani iliyokuja. Isaya 41:10 imeandikaje nitakushika mkono wangu kuume nitakuwa na wewe! kila tatizo

duniani lina mtu wa kusolve aidha ni wewe au mtu mwingine. Yani kila tatizo duniani yupo mtu alishaandaliwa anajibu nalo.

Manake ni hivi majibu ya mtu huwekwa na Mungu kwa mtu.  sasa kama huyu mtu humuoni manake fikra zako zitafika mwisho wa

kufikiri zikishafika mwisho wa kufikiri manake hazina tena njia ingine kile kitendo cha kutambua akili yangu imefika mwisho na sina

jinsi au sina njia ingine basi inakutengenezea Woga na hofu. Hii ndo inaondoaga ujasiri wa moyo! au uhodari wa moyo. Halleluyah!

3.HATAKUPUNGUKIA WALA KUKUACHA

*Mungu anaeleze kuelezea hapa inakuwaje mtu anapata woga na hofu, siyo point zangu hizi ni za Mungu mwenyewe, kingine

kinacholeta woga ni kutokuwa na akika ya kama iko ulichonacho aidha ni ndoa au chanzo cha mapato kama kitakuacha au

kitapungua, nitoe mfano wa biashara yale mawazo ya uongo ya ibilisi kuwa hii biashara itakufa na hukuwa na neno la Kristo ndani

mwako, na unaanza kupima kwa elimu yako ya duniani, unaanza kufikiri hii biashara ndo ninayoitegemea, hii kazi ndo

ninayoitegemea, uyo mwanaume ndiyo ninayemtegemea uyu mama ndo ninaye mtegemea vip kama huduma ikikatika? au ikipungua

nitaishi vip? vip kama huu mradi ukikata au ukaondoka itakuwaje? vip kama kilimo nachokifanya hiki kikiondoka au nisivune

inavyotakiwa? itakuwaje? sasa maswali kama hayo majibu yake yapo katika biblia! kwa kuwa hakuna neno kwa wingi ndani yako!

maswali kama haya hukutengezea woga na hofu. Bwana Yesu asifiwe! Akili ya mwanadamu na fikra ya mwanadamu haikuimbwa

kujitegemea yenyewe! kama iliumbwa kujitegemea yenyewe nikuulize swali kwanini baadhi ya majibu huna? Kwanini baathi ya maswali

ukiyapata tuu yanakutengenezea kuchanganyikiwa yani hutaki hata kuwaza ilo jambo kuwa itakuwaje? ni sababu ili akili yako, na fikra zako

zijitosheleze lazima zisaidiwe na neno la Mungu na roho Mtakatifu !Halleluyah!

4.NDIYE ATAKAYEKUTANGULIA

*Kingine kinacholeta woga na hofu ni kutokuwa na hakika na safari yako, kutokujua mbele yako kunakuja nini? na Mungu hajaongea

na wewe akakufunulia kupitia neno! basi huwa inaleta shida sana. ni kama mwanajeshi anayeenda vitani hana hakika kama atarudi salama

au hatauwawa vitani! mkewe na watoto hawajui kama Baba atarudi akiwa hai au watapokea sanduku! ila biblia imesemaje kuwa atakapo

kuja uyo roho atawaelezea mambo yatakayo kuja, na kuwaweka katika kweli yote manake nini? ukijaa neno la Mungu kwa wingi ndani yako basi

Mungu atakapo kuwa anaongea utadaka mawimbi kwa msaada wa Roho Mtakatifu, Ndo mana Mungu hapa anasema mimi ndo

nitakayekutangulia katika safari ya maisha ya ndoa, maisha ya kustaafu, maisha ya kilimo, biashara au kazi mpya mimi ndo nitakaye

kutangulia. ilo kujua nani atanianzishia hii kitu. kweli nina ela za kuanza biashara lakini nani ataniongoza unajua ukiongozwa

ujasiri unaongezeka, uhakika unaongezeka, tena na  mtu ambaye unajua kabisa ana uhakika wa kuniongoza Bwana Yesu asifiwe sana.

5.ATAKUWA PAMOJA NA WEWE

* Ile hali ya kujua kuwa sina mtu wa
kunicompany katika safari yangu hii huwa inaleta woga na hofu. Sina mtu wa kunitia moyo, hakuna kitu

kikubwa kama kutiwa moyo! mtoto aliyezaliwa katika umasikini wa mwisho anaweza kulelewa kwa upendo na kutiwa moyo mpaka

akaja kuwa Raisi wa nchi. Kutiwa moyo hupunguza sana woga na hofu, na ndio maana viongozi wa Kiroho wanatia moyo sana na

kuwaganga watu mioyo yao. Bwana Yesu asifiwe sana! hivi vyote ukivikosa lazima chembecheme za woga na hofu zitakuwa ndani yako.

Lakini Yesu yupo kwa ajili ya kukucompany tena asiyebadilika, rafiki wa kweli na ndugu wa kweli, ukimshika na kulishika neno lake

atakuwa pamoja na wewe, atakutia moyo na nguvu, ukianguka atakupa mkono, shida ni kwamba inafika sehemu tunaacha Muangalia Yesu

tunaangalia tatizo. Wakati Mungu ameahidi na kuahidi. Amesema zaidi ya mara 365 kuwa mwanangu usiogope! usiogope! usihofu!

usitayarike! Sababu vitu vyote hivi humzuia mtu asiwe na mawasiliano mazuri na Mungu. ana hofu za maisha yake kila mara, ana

wasiwasi wa biashara yake kila mara, ana hofu ya ndoa, ana hofu ya biashara, na hofu ya kuolewa, anaogopa kuanza kufuga, kilimo ana

hofu ya kupata hasara, na hofu kama mke wake,mme wako akitoka nje ya ndoa, ana hofu na watoto wake halali usiku, na inampeleka nje

ya ahadi ya Mungu. Ana hofu na mashaka je Mungu atatimiza kweli alichoandika katika biblia mbona mda unaenda huu ni mwaka wa 4,

kwenye wokovu ana hofu na kila kitu, lakini zote hizi ni taarifa za uwongo za ibilisi, ana hofu nikipanda mbegu Mungu

ananibariki au nitapoteza sadaka, ana hofu ya kutoa fungu la 10 na hali yake inazidi kuwa mbaya, ana hofu ya kumkabithi Mungu chanzo

cha mapato kwa malimbuko Mungu atanibariki kweli au nitapoteza. Shetani kawapiga kwenye fikra na hali zetu zinazidi kuwa mbaya

sababu ya hofu na woga wa kutimiza maandiko! na Unajua kabisa imeandikwa usiposikia sauti na kufuata maagizo ya Bwana

Mungu wako laana itakupata. ukichunguza zile laana kuanzia kumb 28:15 ndizo wengi tunaziishi.Yesu atusaidie.

6.HATAKUPUNGUKIA WALA KUKUACHA

*Hapa karudia tena sitakupungukia wala kukuacha. Huyo ni Mungu Mwenyewe.

7.USIOGOPE WALA USIFADHAIKE

* Hapa anasisitizia usiogope wala usifadhaike? kwanini unafadhaika nakuogopa? kwa uwongo wa ibilisi! Mungu anasema wewe angalia

ahadi zake pekee! angalia neno lake  pekee, maana unavyofadhaika na kuhangaika shetani ndo anafurahi maana huo ni mlango wa mapepo!

kinachofanya mtu kufadhaika na kuhangaika ni sababu hana njia. Njia yako ni Yesu. Maswali uliyonayo majibu yake yapo katika

biblia hayapo kichwani mwa watu! hayapo katika masikio yako, hayako katika kiwango cha macho yako, hayapo jinsi unavyojisikia nafsini

mwako, hayako katika kiwango cha mtu flani alivyofanikiwa, hayako kwa boss wako anayekupa mshahara, yapo katika biblia. Acha

kuangalia ukubwa wa tatizo na kumfananisha na Yesu kama atakusaidia au vip? acha kumuwekea Mungu kiwango kwa

kumlinganisha na tatizo au mda wa tatizo ulilokaa, usimfungie Mungu nje ya fikra zako, usimfungie Mungu nje ya moyo wako, acha kujiuliza

maswali magumu yanayokuletea pressure na msongo wa mawazo yanayokusababishia kukonda kwa mawazo. Yesu anaweza yote.

Anachotaka umuamini mojakwamoja si nusunusu, si huku umemuomba huku umerudi kwa binadamu kutaka utatuzi.

ukishamkabithi Mungu mtegemee yeye pekee atakuvusha hapo ulipokwama, hapo palipokosa majibu, hapo kwenye giza, hapo gari
ilipoishiwa mafuta alafu mbele kuna kilima. mwamini Mungu. mtegemee Mungu acha kukengeuka kwa mawazo, acha kufuta maombi yako

mwenyewe, acha kutegemea akili zako mwenyewe, hazikuumbwa ivyo. zimeumbwa ziongozwe na Mungu. Shetani asikudanganye eti

litaisha au utasolve unajidanganya jitoe kwa Mungu. mtegemee Mungu pekee yeye ni mwaminifu kizazi hata kizazi. Usifadhaike wala

usiogope Mungu ndiye ngome yako. hutaanguka wala kudodondoka yeye atakutangulia, atakuongoza, atajaza palipopungua. wala hutatayarika.

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA