TAMAA ZA MWILI ZIPIGANAZO NA ROHO
Somo: "Tamaa za mwili zipiganazo na Roho"
Bwana Yesu asifiwe!
Asilimia 99% ya kutokufanikiwa kwa binadamu husababishwa na kutoisikia sauti ya Mungu, kutokutii sheria ya Mungu, na kutokufuata
Maagizo yake, au maelekezo yake! zipo sababu nyingi sababu ya kwanza zipo hata kwenye Yohana 1, kiburi cha uzima, kukataa maono
ya Mungu ambayo yameletwa na mtumishi, kushindana na Mungu kwa kubishana na watumishi, kutokuchukua hatua, baada ya
kupata maelekezo ya Mungu, kujihesabia haki! huko ni kupi ni kama hivi unaona neno unasema moyoni ili mimi haliniuusu linamfaa.
fulani, Bwana Yesu asifiwe sana. Sababu kubwa ambayo imejificha ndani ya watu ni TAMAA, tatizo linakuja hapa mwenye tamaa
hawezi kukubali ana tamaa, ni mpaka umuonyeshe umfunulie kwa maandiko, najua hata hapa unavyosoma tayari kuna ushindani
ndani yako, sauti ingine inakuambia haikuhusu, sauti ingine inakuambia wewe huna tamaa umeokoka utakuwaje na tamaa! lakini
Biblia inasema neno la Mungu ni upanga wa roho linauwezo wa kugawanya nafsi na roho! mafuta na nyama ndani ya mwili na si kwa
maneno kabisa bali ni dhahiri kabisa! neno linapochoma nafsi na roho vinaachana kwa Muda mafuta na mwili vinaachana kwa mda!
Halleluyah! Bwana Yesu asifiwe sana. Tuangalie neno sasa!
Petro (1) 2-11
11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
*Tamaa ya mwili ni sheria ya mwili inayopinga Roho, unaweza kuwa umeokoka lakini tamaa zikakutesa, Mwili hutamani vitu vingi sana
tena hutamani dhambi, mwili hata siku moja hauwezi kutamani mambo ya Mungu, ni sababu ya asili ya dhambi ya mwanadamu,
Mengi tunayopitia ni sababu ya kuondoa tamaa za mwili! unapopitia majaribu zile tamaa zinachomwa na moto na majaribu, kuna kitu
Kinaitwa moto wa majaribu, yani uposhuka huo moto, kiburi kitakaa kimya, jeuri itakaa kimya, kujinua kutakaa kimya, utabaki kimya tuu
huna la kufanya sana sana utasukumwa umtafute Mungu, Bwana Yesu asifiwe! Ndo mana ya lile neno Ezakiel 36:26:27, linasema
nami nitatoa jiwe mioyoni mwenu, nami nitaweka moyo wa nyama, nami nitatia roho yangu, nanyi mtaongozwa kwa sheria zangu
Bwana Yesu asifiwe, ziko tamaa ambazo zimejificha ndani ya mtu za siri na hata yeye hawezi jua kuwa anatamaa na ibilisi amefanya hilo
ndilo geti kuu la mapepo, wakitaka kuingia wanatafuta your weekness hapo hapo wanakuletea tamaa wanajua kwa vyovyote jinsi inavyo
kuja huwezi kataa, tayari unajikuta katika mazingira ya kushindwa kukataa na kuondoka kurudi nyuma unajikuta umefanya dhambi maana
tayari umeshaingia, mfano mtu mwenye tamaa sana ya pesa, kiasi kwamba yeye maisha yake moyo wake kaokoka lakini unaendeshwa
na pesa si Yesu, shetani hawezi kuja kitoto ataleta mazingira kabisa ya wewe kupata hizo pesa lakini si kwa njia ya Mungu, na anakuletea
na neno kabisa alafu anakuletea na ndoto anajidai yeye ni malaika wa nuru kumbe ni ibilisi anakuambia imeandikwa hivi, na wewe sababu
moyo wako umejaa tamaa, unashindwa kuipima roho unaingia katika mtego kwa moyo wa tamaa, si sababu huna neno no! moyo
wako unaendeshwa na tamaa ya pesa, baadae unakuta ni mtego unajikuta katika madeni, au unajikuta polisi au gerezani, au
unajikuta unakimbia kujificha, au unajikuta katika vishwawishi vya dhambi, sasa sababu uliingia kwa siri na unataka kutoka kwa siri
unajikuta katika dhambi kuu zaidi, wengine wanachanganyikiwa wanajikuta kwa waganga wa kienyeji, wanajikuta
Wameambukizwa HIV, wanajikuta kwenye majuto makubwa, wanajikuta wameuwa, wanajikuta wameiba, coz ulingia kwa siri sasa
unataka utoke kwa siri, inakugharimu sasa, shetani anazidi kukuwekea mazingira ya kumuudhi Mungu wako, lakini chanzo chake ni
nini tamaa,Huo ni mfano mmoja tuu Sasa Mungu hufanyaje kuondoa tamaa ndani ya mtu ili mabaya yasimkute, twende tuangalie neno :
Petro (1) 1-6
6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
*unajua Mungu yupo ili kuabudiwa kusifiwa kufanyiwa ibada sio KULAUMIWA, MUNGU huwa anaona mbele anaona yanayokuja kwa iyo
ili kuyaepusha wewe usianguke anaruusu majaribu sasa, ili uko mbele majaribu yasije kukukumba na kukuangusha! ndio maana
anasema ikiwa ni lazima mmehuzunishwa na majaribu ya namna mbalimbali! Mungu hapendi lawama za binadamu hata yeye
hafurahi wewe ukihuzunishwa na nayayokukuta lakini sasa atafanyaje kukusaidia na wewe tamaa inakuwaka ndani yako? huridhiki na
ulicho nacho? unataka more and more and more? yani tamaa inakutesa ila wewe hujui kuwa ni tamaa mbaya inakutesa! Moyo
uambatane na Mungu yeye ni Mungu pekee wa kufariji moyo wako ukaridhika, ukimpa nafasi Roho Mtakatifu akutawale 100% tamaa
ndani yako haitafanya kazi, na ndani yako hakuna tamaa basi hakuna maanguko, Bwana Yesu asifiwe sana, Mungu ndo mana kasema
Petro (1) 1-13-14-16
13 Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.
14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
* Bwana Yesu asifiwe unaposoma hapo unagundua moja kwa moja tamaa ni ya ibilisi si Roho ya Mungu. Kinyume cha tamaa ni
kutoshelezeka. Halleluyah watu wa Mungu! Sasa tuangalie hizi point Mungu alizonipa jinsi tamaa inavyopelekea kuanguka na baada
ya mifano hapo chini utajipima katika roho na kujitambua. Mwingine anatamaa ya kuwa na familia bora, kiasi cha kuona wivu
katika mazingira hayo hayo ibilisi anatengeneza mazingira ambayo bila roho wa Mungu huwezi chomoka, sababu unaongozwa na
roho ya tamaa na sio neno la Mungu unajikuta umeingia na badala kuwa na familia bora, unajikuta umetekeza familia na kurudi kumla
umu Mungu, na Mungu alishakuonya usifanye iyo biashara au uyo rafiki sio mzuri lakini umewekwa nta na tamaa iliyo ndani
yako, vitu vinavyotegaga watu ni vitu vidogo sana na ibilisi hutumia izo izo tamaa kutengeneza mazingira ambayo yatakuangusha
mfano mtu anatamani sana mme wake apendeze kama mme wa flani au mke wake avae gold kama wa flani, matokeo yake ibilisi anaweka
mtego alafu anakukumbusha na neno kabisa unasema huyu ni Mungu unaingia mtegoni unajikuta kwenye matatizo, mwingine ana
tamaa na nguo za gharama, ana tamaa ya kula vyakula vizuri kama familia flani, tamaa ya kutoka out kama familia flani, tamaa ya
kwenda nje ya nchi mapumzikoni kama familia flani, tamaa ya kuvaa nguo mpya kama mtu flani, tamaa ya kuwa na vitu vya gharama kama
simu za bei, tamaa ya kuwa na jiko la kisasa kama familia flani, tamaa ya kuwa kama watu flani! kuwa kama flani, bila kujua jinsi
alivyofanikiwa je Mungu Jehovah au ni miungu ya baali? ndo imemfanikisha, tamaa hupelekea watu kukopa pesa bila kujua
madhara yake, tamaa hupelekea watu kulazimisha kutembelea tax ya 50000 kwa siku wakati hali hairuusu, tamaa ya kuonekana bora
mbele za watu na kujikuta unafanya mataumizi yasiyo ya lazima au kuonekana mbele ya familia au mbele ya ndugu au mbele mtu flani
pasipo kujua madhara yake nini! tamaa ya watu wengi inayotusumbua ni kutamani vitu vizuri, kutamani maisha ya watu,
bila kujua chanzo cha baraka, au gharama gani kalipa, mazingira hayo hayo ibilisi hufanya mazingira ya kweli kabisa na wewe huingia na
kujikuta kila mara unaanguka, kila mara unarudi nyuma, ibilisi akishajua unakaribia kuinuliwa na Mungu hukutengenezea tamaa, ili
uingie, ukishaingia manake umeingia dhambini, ivyo baraka inapokuja inakupita inaenda kwingine maana baraka ya Mungu
haikai juu ya dhambi, giza halichangamani na dhambi! Halleluyah! kwa iyo tunasema Tamaa huwa inaipinga roho
sababu inaipinga roho tamaa ni roho ya ibilisi ni urgent wa ibilisi wa siri ambaye hufanya kazi kwa siri kazi yake ni kuharibu baraka kwa
siri kama nilivyokuelezea hapo jinsi ibilisi anavyofanya kazi saa ingine ibilisi atakupa pesa kabisa, mchumba, au chochote unacholilia
kumbe its fake, nia ni kuharibu, yeye anatafuta mashitaka ya kukushitaki, atakushawishi kwa hali ya juu, kuanguka kwako si sababu huna
Mungu no si sababu wewe unatamaa iliyopitiza ndani yako yako kwa iyo hupelekea yafuatayo:
√ Tamaa humfanya mtu kutomsikia Mungu akiongea
√Tamaa hufanya mtu kufanya maanuzi mabaya
√ Tamaa inamfanya mtu kutoka Rohoni, kwenda mwilini
√Tamaa inafungua milango kwa ibilisi ni malango ya mapepo
√Tamaa inaharibu miujiza na baraka
√Tamaa ni lango la ibilisi la uharibifu
√ Tamaa ni lango la hasira, hasa mtu anapokosa anachotamani
√Tamaa ni lango la mtu kukata tamaa
√ Tamaa ni lango la kuleta uvivu.
√ Tamaa ilimponza Daudi akazini na mke wa Mtu na alimuuwa mme wa yule mke ivyo kupelekea mtoto wa Daudi naye kufa ingawa aliomba rehema
√Tamaa ilimponza mfalme Suleimani akajikuta akiabudu miungu sababu ya kuoa wa mataifa
√Tamaa inauwa ndoa huduma biashara kazi familia ukoo
√ Tamaa ilianza na ibilisi mwenyewe alitamani kiti cha Mungu akapigwa na kufukuzwa mbinguni.
√Mwenye tamaa hafanikiwi
√Majaribu mengi tunayoyapata ni ili kuondoa tamaa ndani yetu
√ Tamaa ni malango wa shortcut, na unajikuta katika dhambi
√ Tamaa husababisha kuomba vibaya kwa Mungu Baba maana maombi yako huongozwa na tamaa
√Vitu vingi Mungu huvizuia sababu ya tamaa iliyopitiliza ndani yao! akikupa kakupoteza.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
This is powerful ahsante kwa neno Mtumishi. Mungu akazidi kukutumia kwa utukufu wake
ReplyDeleteUbarikiwe jaribu kuunganisha maneno uandishi unasumbua kusoma
ReplyDelete