"NGUVU YA YESU KATIKA KUFUMUWA MAKABURI YALIYOZIKA VITU VYAKO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
SOMO: "NGUVU YA YESU KATIKA KUFUMUWA MAKABURI YALIYOZIKA VITU VYAKO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO"
Bwana Yesu asifiwe!
unapofanya vita na ibilisi ni maisha haya wengine wanaomba kidogo wakipata mpenyo mwanga kidogo
tuu wanaacha kuomba wanaacha kumtafuta Mungu. kumbe umemgusa shetani kaachilia
mambo kidogo yani kaachilia nukta tuu baada ya wewe kuanza kuona dalili unahema unasema afadhali
mlango ushafunga! kumbe unasahau kwa Mkristo Vita ni maisha! Yesu alijiweka wakfu kwa
ajili yako ili afanye vita na wewe ili wewe ushinde! wengine wanaridhika haraka sana na matokeo madogo!
madogo! yanawapumbaza kumbe Mungu alidhamiria mambo makubwa sana katika maisha yako.
yani unaweza fika mbinguni kisha Yesu akamtuma malaika Gabriel embu fungua file la Joseph mfano
anakuonyesha jinsi shetani alivyokuhujumu, jinsi Mungu alivyokuwa amekupangia na jinsi
mpaka unakufa hujafikia hata robo
ya maisha Mungu aliyokuwa amekupangia! mbinguni umeenda
lakini kile Mungu alichokikusudia
kukupa ukiwa duniani hujakipata sababu ya uzembe na uvivu wa
kuomba! sababu ya kuridhika na
matokeo madogo! na kila unapofanya maombi ya aina flani
jifunze kumuuliza Mungu what next
niko hapa mtumishi wako nasubiri maelekezo yako! ukikaa kimya
ukitegemea Mungu atende Mungu
naye anakaa kimya! wengi hii sheria wanaisahau Mungu alikuambia
ujitawale na kakupa choice na uhuru wa kufanya kila kitu ivyo kama hauombi basi usimlaumu Mungu!
kazi ya Mungu kukupigania! Yesu
naye kukutia nguvu! Roho Mtakatifu kukusaidia kuomba kwa iyo acha
kuridhika na matokeo ya nukta tuu
ya maombi! au kumpima Mungu kwa mambo yanayoonekana!
endelea kuwa na Roho ya
unyenyekevu na moyo ya kutubu Isaya 57: 15-19!
ufunuo 3-1
1 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa
Bwana Yesu asifiwe! anasema "unajina la kuwa hai lakini umekufa" hii manake ni nini?
Tuangalie Ezakiel 37 ! huu mstari wengi wameusikia na wanaujua sana lakini sikiza tena leo Mungu
atakuvusha hapa wala usimzoee Mungu. elewa kwanza vizuri usikimbilie kuomba kitu usichokijua
Halleluyah! Soma neno taratibu hata kama ni refu hapa ndipo penye baraka zako.
MLANGO 37
1 Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa;
2 akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana.
3 Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
4 Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana.
5 Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi.
6 Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.
7 Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.
8 Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. 9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi.
10 Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.
*MAELEZO
Mungu aliongea hapa kipindi kile wana wa Israeli wako utumwani, wanamuomba Mungu usiku na
mchana wanapata matokeo kidogo! kipindi agano la kale Mungu alikuwa kama kawaida yake huongea kupitia
kuhani wake! Ezekiel alikuwa nabii siku iyo wakati kalala! Mungu kupitia Roho wake akamchukua
kumwonyesha kitu nia ni kusaidia wanawa Israeli! Mungu akampeleka kwa juu ya bonde lililojaa mifupa
mikavu, kule kwenye ndoto Mungu akawa anazungumza na Roho ya Ezakiel nabii akawa anahojiana na
Ezekiel anamuuuliza vip mifupa hii inaweza kuishi? Ezekiel akamwambia Bwana Mkubwa kwa
kweli mimi sijui ila wewe sababu ni muumbaji lazima utakuwa unajua tuu, unajua Mungu hawezi fanya kitu
hapa duniani lazima Binadamu aruusu ivyo swali la Mungu lilitaka Ezakiel aruusu Mungu kutenda, basi
Mungu akawa anampa maelekezo! jinsi ya kufanya akamwambia itabirie iyo mifupa mikavu! soma
mwenyewe hapo juu! Ezakiel akaanza kuitabiria ile mifupa mikavu! mara akaanza kuona ile
mifupa inakusanyika inatafutana, inakuwa fuvu la Mtu mara inaota nyama, ile mifupa mara ngozi juu
yake, na mishipa ya kupitisha damu! Hee gafla akili ya Ezekiel akashanga akaona hee kumbe hawa ni watu?
sasa ile mifupa ya kwanza imekuwa maiti sasa isiyokuwa na pumzi! Mungu hakuishia hapo na Ezekiel
akamwambia endelea Ezekiel na unabii, akamwambia uambie upepo pande nne uje uwapulizie hao watu
wapate pumzi ili waishi! upepo ukaja baada ya Ezekiel kutabiri kwa iyo wale watu wakawa hai
WAKASIMAMA KWA MIGUU YAO WENYEWE, anasema ilikuwa jeshi kubwa mno! Kwa iyo Mungu katika
ulimwengu wa Roho akiwaangalia wengi anaona ni mifupa mikavu ilitupiwa katika bonde! ingawa wewe
huku duniani unajiona uko sawa ila sivyo Mungu anavyokuona! wengi hawajasimama kwa miguu yao
wenyewe kama ni afya basi mtu anasimamia kwa dawa, kama ni gari anasimamia mkopo, kama ni
nyumba anasimamia mkopo, kama ni biashara zote zinasimamia mkopo! hivi sivyo Mungu
alivyokudesign wewe, Mungu kakudesign wewe usimame mwenyewe, kama ni ndoa basi
imesimamishwa na mashemeji au wakwe! Bwana Yesu asifiwe! kumbe kile alichoonyeshwa Ezekiel
yalikuwa ni maisha ya Wana wa Israeli! ndo lile neno kule juu linakuja sasa Ufunuo 3:1 unajina
lililohai lakini umekufa, manake umebeba jina la Yesu lakini, uchumi wako umekufa, ndoa yako iko
mahututi, vibali vyako vimekufa, afya yako imekufa, biashara yako imekufa hakuna kitu ambacho
unacho ambacho umesimama kwa miguu yako mwenyewe aidha kinategemea watu wa nje au
umekisimamisha na mkopo! Mungu akiangalia katika ulimwengu wa roho anaona mifupa yako katika
ulimwengu wa Roho! Mungu angemuambia Ezekiel ninaona makaburi katika ulimwengu wa
Roho Ezekiel asingeelewa! Ndo mana maisha ya watu wengi sana yameuwawa yapo kaburini na
uchawi 98% unafanyika makaburini, huko ndiko wanatamka biashara yake ife, ndoa yake ife, figo yake ife,
huko wananuiza kisha wanazika makaburi na kulia kabisa wachawi watu wabaya sana, sio swala la
kusema Mungu nisaidie ni swala la kuamka usiku kurudisha wanachokinuiza kirudi kwao,
Mungu atakusaidia kama unaomba si umelala usiku huku wachawi wakizika kazi yako biashara yako
ndoa yako afya yako vibali vyako kampuni yako wakitaka uhai wako kumbuka Yohana 10:10 kuuwa
kuchinja kuiba hii ndo kazi ya ibilisi, uchawi mkubwa huwa unafanyika makaburini. Mungu akiangalia
Katika ulimwengu wa roho anaona makuburi katika ulimwengu wa Roho, anaona vitu vyako vingi
zimezikwa ndo Mana Mungu hakumwachia katika ndoto! akaendelea kuongea naye sasa!
11 Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.
12 Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli.
13 Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu.
14 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana.
*anasema nami mtajua mimi ndimi BWANA NITAKAPOFUNUA MAKABURI YENU! Anasema nami
nitatia roho yangu ndani yangu nanyi mtaishi tena, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana nimesema hayo,
na kuyatimiza, Halleluyah! Halleluyah! Bwana Yesu asifiwe sana!
Tuangalie tena Mathayo 27- (45-46), 50-51
Mistari hii pia unaijua lakini leo nataka nikufungue jicho la Tatu uone ndani zaidi. Bwana Yesu asifiwe sana!
45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.
46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
50 Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
*Nataka uone hayo matukio, pakawa na giza nchi yote masaa 3 biblia inasema ilikuwa saa 6-9
Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini, nchi ikatetemeka na miamba ikapasuka.
Yes hapo kwenye nchi kutetemeka na miamba kupasuka ushawahi jiuliza ni kwanini nchi ilitetemeka
na miamba kupasuka? hii ni sababu kwenye nchi ndiko kwenye makaburi, makaburi hayo si katika
ardhi tuu yapo katika ulimwengu wa Roho miamba manake zipo roho za watu zimezuiwa mapangoni, kwa
iyo huku duniani mtu anaonekana, yupo sawa lakini katika ilimwengu wa roho yake imezuia katika
miamba ipo chini ya ardhi katika madhabahu ukiendelea kusoma iyo Mathayo biblia inasema baada ya
Yesu kufa tuu makaburi yalipasuka, yalifumuka sasa kufumuka huku kulikuwa na maana kufumuka
katika ulimwengu wa roho! kumbuka mambo ya madhabahu! uchawi haukuanza kwetu umeanza toka
zamani upo! kwa iyo wako watu ni kweli wameokoka lakini wamefungwa mambo yao hayako
Huru na vitu vyao vingi viko makaburini, elimu zao zipo makaburini, ndoa zao zipo
makaburini, vibali vyao vipo makaburini, kibali cha kuoa au kuolewa kipo makaburini, kibali cha
biashara kipo makaburini, wamefanikiwa lakini chunguza kama wamesimama kwa miguu yao
wenyewe? wewe ni kabila la Yesu, wewe ni Muisraeli Baba zako walitoka na mali nyingi sana misri,
je mali ziko wapi? mbona huna? zimeenda wap wakati Mungu alikupa? nakwambia ibilisi kafanya
njama, ibilisi kafanya hila na mambo yako yalikamatwa tuu aidha ulipokuwa tumboni mwa mama
yako, au ulipokuwa mtoto, angalia vipaji ulivyokuwa navyo ukiwa mtoto angalia siku hizi huvioni?
hujiulizi vimeenda wap? Shetani amezika mambo yetu makaburini, Mungu akiangalia anaona makuburi
mengi katika ulimwengu wa roho, ndio vilio vyetu kumbe vimezikwa na ushirikina vitu vilivyozikwa haina
jinsi lazima Yesu afumue haya makaburi kisha uamuru huo ushuhuda wako, sifa yako, haki yako
urudi sasa katika jina la Yesu kwa neno hili ukalielewa vizuri tutakapofanya maombi ni lazima
vitu vyote vilivyopo makaburini virudi kwa jina la Yesu, si sababu nimesema bali neno limesema!
Na MUNGU KASEMA NDIPO UTAKAPOJUA MIMI NI BWANA! saa ingine huwezi jua kama kuna kaburi
katika maisha yako! ni mpaka ufanye maombi ya namna hii! ndipo utajua kuwa Mungu huliangalia
neno lake. Lakini basi! kwanini tunamakaburi na tumeokoka ? ushawi jiuliza? tuangalie neno
Ufunuo 1-17
10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
* Unajua ukipata kuijua picha ya Yesu kwa picha ya Rohoni! basi utajua na kuamini anaposema
nitayafunua makaburi yako lazima ujue uyu ambaye unamwomba ni Mungu wa aina gani! tatizo la watu
wanamchukulia Yesu kama yule kwenye filamu! yule anayevaa viatu vya kimasai Yesu tunayemtizama
hapa ambaye utaenda kumuona utakapofanikiwa kufika mbinguni basi ni uyu hapa! si yule wa kwenye
filamu! si mdogo kama unavyofikiria kama malaika wa Mungu ni mkubwa kiasi hiko vip kuhusu Yesu!
uyu Yesu wa hapa ambaye tunamwomba uyu yupo zaidi ya umbo la malaika yupo umbo la U
Mungu. unajua usimfananishe Yesu aliyekuja duniani na uyu wa ulimwengu wa Roho! Sodoma na
Gomora ile miji ilichomwa na malaika wawili tuu, Daudi alipokosea akafanya dhambi ya
kuhesabu majeshi ya Mungu Alitumwa malaika mmoja tuu kuangamiza mji wote! kitabu cha
ufunuo kinaelezea Baragumu la Tano lilipopigwa alishuka malaika mmoja akaweka mguu wake mmoja
baharini mwingine kwenye ardhi mikono mingine juu angani akiapa kwa Mungu aliyehai! akiwa tayari
kuangamiza! Danieli aliwahi kuona malaika akaanguka akafa malaika akamgusa Daniel akapata uhai tena
sababu ya utukufu wa Mungu. Sauli aliwahi tokewa na Yesu yule aliye muuwa Stephano ule mwanga tuu
Sauli alipofuka macho! Hata Yohana mwenyewe Alipopelekwa mbingu ya Tatu Yohana alikufa Yesu
akamgusa naye akaishi, sasa Yesu ni zaidi ya malaika! na hakuna mtu ambaye atamwona Mungu akabaki
mzima! Sababu ya ule utukufu sababu ya ule mwanga huwezi stahimili wala kuvumilia, Musa
aliomba kumuona Mungu, Mungu akamwambia huwezi niona mimi ukiwa hai! Musa baada ya
kungangania sana ndipo Mungu akampa kisogo kwa nyuma, kule mlimani ndipo Musa akashuka chini
uso ungaaa mpaka wana wa Israeli wakashindwa kumuangalia! Yohana anasema aliona vinara saba vya
dhababu katikati ya ivo vinara akaona mtu mfano wa binadamu, kavaa nguo nyeupe mfano wa sufi
yani anaposema mfano manake anafananisha na vitu vya duniani, nguo iyo ilikuwa nyeupe zaidi ya sufi
nafikiri hata kuingalia inakuwa shida kwa ajili ya mngao wake! kisha akaona kichwani pake nywele
nyeupeee! kisha uso wa Yesu ulikuwa unangaaa zaidi ya jua! yani hautazamiki! huo ni utukufu alionao
Yesu, embu fikiria jua la saa saba unaweza liangalia? sasa Uso wa Yesu ni mfano wa Jua manake si
kama jua! anasema anapoongea ni kama mwangi ya maji mengi sana yanamwagika! wangap washaona
sehemu inapoingiliana mto na bahari huwa kuna sauti kuu na tetemeko kiasi kwamba ndege
ikipita juu lazima itetemeshwe, kwa iyo, sauti ya Yesu ni mfano wa iyo kitu! alafu mkono wake wa kuume
ameshika panga kali lenye kukata kuwili, miguu yake inangaaa kama shaba iliyosuguliwa sana! na macho
yake yanatoa miali ya moto! kisha ameelezea hapo juu akiongea ulimi wake kunatoka upanga ukitoka kulia
kwenda kushoto unaweza piga picha Yohana alikuwa katika condition gani? biblia inasema
Yohana alikufa, anasema nalikuwa mfano wa mtu aliyekufa, ndo mana huwezi muona Mungu katika huu
mwili sababu ya utukufu wa Mungu lazima utakufa tuu.ilibidi Yesu amwamshe! akamwambia
usiogope! AKAMWAMBIA MIMI NI WA KWANZA NA MWISHO, ANAKAMWAMBIA NALIKUWA
NIMEKUFA NIMEFUFUKA NAMI NINAZOFUNGUO ZA MAUTI NA UZIMA, Yesu ndo mtu wa kwanza
kushuka chini sana kuliko mtu yoyote alishuka mpaka kuzimu ya saba kule anapokaa lusifa
mwenyewe kwenye giza totoro! wachawi wengi wanaosumbua wameishia kuzimu ya 1 au ya tatu!
huko ndiko Yesu alishuka akamnyanganya funguo hizo ibilisi akawapa kanisa! kwa iyo uyo ndo
Yesu unayemwabudu kila siku, ndo uyo anayekupigania, ndo uyo unayemwita! ndo uyo aliyeketi
mkono wa kuume wa Mungu Baba si yule wa kwenye filamu! sasa unaweza jiuliza kama Yesu ndivyo
alivyo kwa nini nina makaburi katika ulimwengu wa roho!? JIBU NI RAHISI LAZIMA UKUBALI YESU
NDIVYO ALIVYO NA UKUBALI KUKETI NAYE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO! ndo mtu pia aliyewahi
kwenda juu sana kuliko binadamu yoyote baada ya kufufuka. hiki unachokiona duniani ni malaika
zake tuu! Halleluyah Halleluyah Halleluyah! kwa iyo lazima ukabali kuwa uyu Yesu kwa picha iyo
uliyoiona ndiyo atakaye yafumua hayo makuburi ukiwa na picha iyo! natangaza katika Roho Mtakatifu
lazima uje na shuhuda mahali hapa.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
endelea kutafakari wakati maombi yakija...
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment