JINSI YA KUTUMIA DAMU YA YESU IPASAVYO ILI IKUFANIKISHE MAENEO YAKO YOTE.
Somo: JINSI YA KUTUMIA DAMU YA YESU IPASAVYO ILI IKUFANIKISHE MAENEO YAKO YOTE. PART A
Bwana Yesu asifiwe!
USHUHUDA:
Miaka ya nyuma kidogo kama uliwahi kusikia watu wanaitwa wapiga nondo, kule mbeya watu walikuwa wanakufa kwa kupigwa nondo! Ila kulikuwa na siri kubwa sana watu wengi hawajaifahamu iyo siri ya wapiga nondo mbeya Ila stori wanaifahamu. Walikuwa wakikukuta usiku au mchana wanakugonga kwa nyuma na watu wakawa wanakufa kweli. Ikawa imeenea
stori "wagonga nondo" hata Leo hii ukifika mbeya stori hizo utazipata ili siri ya watu kupigwa na nondo hawaijui! Najua wapo watu wa mbeya watakuwa wanajua jua kidogo stori hii! Ilitokea mtu mmoja alikuwa na biashara ya bucha, sasa biashara yake ilikuwa haiendi vizuri, akamwona mwenzake mwenye biashara tofauti si ya bucha anauza Sana. Akamtafuta pembeni ikabidi amuulize nini siri ya kufanikiwa? Kama ujuavyo njia ya
shetani ni pana na Ina watu wengi! Akamwelekeza kwa Fundi au mganga! Alipofika akaambiwa kusudi uuze inatakiwa damu, Damu ya kitu chenye uhai! Iyo Damu itakapomwagiga ndipo pepo la kuvuvia watu kuwavutia watu kwenye biashara litakapo kufanikisha. Akamuuliza mganga sasa nifanyaje! Yule mganga akamwambia kalete Nondo, alivyoleta ile nondo ikaja ikafanyiwa dawa za kienyeji na nguvu ya kipepo kiasi kwamba hata ikigonga kiti chochote tuu
lazima kife, akaambiwa ukishagonga iyo nondo iweke pembeni mwa bucha kwenye Kona. Yule Bwana akatoka anaenda nyumbani pale kwake kukawa na Mbwa anamsumbua sasa ile katika kumfukuza akamrushia ile nondo kichwani ile nondo ikamgonga kichwani yule Mbwa akafa! Asubuhi akaamka kwenda kufungua duka! ile nondo akawa nayo kwenye mfuko kachanganya na vifaa vingine vya kazi, gafla wakaja mbwa
wengi Sana pale kwake hee! Akahamaki ikabidi afunge akamfuata yule Fundi, akamweleze yaliyotokea akamwambia umekosea wewe umemwaga damu ya Mbwa ndo mana mbwa wamekuja. Sasa Kama unataka watu lazima umwage damu ya mtu! Kwa iyo! Yule Bwana akavizia mtu akamgonga na nondo yule mtu akaanguka akafa baada ya hapo bucha lake ikawa
haifiki saa 4 saa 5 asubuhi nyama imeisha wengine wenye mabucha wakamhoji nini siri, akawaelekeza tokea hapo sasa ndo kukawa na matukio ya kutisha ya watu kugongwa na nondo kufa. Nachotaka kukuonyesha hapa, uhusiano na damu iliyomwagiga na wateja kujaa dukani. Iyo siri ukiielewa kwa upande wa MUNGU basi wewe ni mshindi kila mahali.
MATUKIO MENGINE KIBIBLIA:
2 Wafalme 3:26
. Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki.
2 Wafalme 3:27
. Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.
* Tunaona Mfalme Moabu alimtoa mwanawe akamchinja kama kafara ili ashinde vita! Na Baada ya kumtoa mzaliwa wa Kwanza waisraeli wakawa na hasira ambayo hata Wao wenyewe ukiwauliza hawezi kujua hawana majibu kisha wanaacha kupigana naye wakarudi nyuma. Swali la msingi.
*Kuna uhusiano gani Kati ya damu ya mzaliwa wa kwanza wa Moabu na Hasira waliyoiona wana wa Israeli?
*Kuna uhusiano gani katika Damu iliyomwagiga na Wana wa Israeli kurudi nyuma?
JEE UNAJUA NI MARA NGAPI UMEKUWA UKIFANYA MAOMBI MAKALI GAFLA UNASIKIA KUCHANGANYIKIWA NA GAFLA UNARUDI NYUMA? AU UNAACHA KUOMBA MAOMBI?
JEE USHAWAHI KUJIULIZA KWANINI VIKUNDI VYA MAOMBI VINGI VINAVYOANZISHWA AU VINAVYOANZA VIKIANZA KUPATA MOTO GAFLA VINATAWANYIKA! USHAWAHI JIULIZA IYO NGUVU INATOKA WAPI? Wakati wanamuomba Mungu aliyehai?
USHAWAHI JIULIZA kwanini Mara ingine tatizo unalijua chanzo unakijua lakini huwezi kuomba! Ukijaribu tuu kuomba unaacha. Unafanya shughuli nyingine. Ushawahi jiuliza ni kwanini! Na inakuwaje kuwaje? JE NINI KINAKUZUIA USIOMBE?
UNAJUA SHETANI HUTUMIA DAMU KULIKO WEWE MKRISTO? UNAJUA SIRI HIZI SHETANI ALIZITOA WAP? HAIJALISHI UNAOMBA KIASI GANI? HAIJALISHI UNANENA KWA LUGHA SIKU NZIMA ILA KAMA HUJUI KUITUMIA DAMU YA YESU UTAOMBA UTAMALIZA AKIJA ANATOA KAFARA KUBWA YA DAMU. anakuvuruga.
Anakufunga usiombe tena.wakija kukushambulia huwezi omba.
USHAWAHI SIKIA GARI LA KAMPUNI FLANI LIMEANGUKA LIMEUWA WATU, ALAFU GAFLA BAADA YA MIEZI 3 AU 6 UNAKUTA
Amenunu magari zaidi ya 50, unajua uhusiano wa damu? Na nguvu ya utajiri? KAMA UNAJUA KWANINI HATUTUMII DAMU YA YESU IPASAVYO? KUVURUGA WANACHOFANYA?
USHAWAHI JIULIZA INAKUWAJE MTU ANAOMBEWA PEPO LINATOKA BAADA YA WIKI TUU LILE PEPO HUJA TENA LINAOMBEWA LINATOKA LINAKUJA TENA! NA SI KWAMBA hakuna uwepo wa MUNGU BALI PEPO LINAKUWA NA KIBURI. Kiburi huwa kinatoka wap?
Angalia hapo juu shetani unapomshinda lazima amwage damu! Unapoonza kuomba Ku catch fire 🔥 Kwa bidii anapoona unamzidi huwa wanamwaga damu! Ivyo unajikuta unaacha kuomba au unaacha kufanya vita.
*SASA UNATAKIWA KUFANYA NINI KUMSHINDA IBILISI HATA ANAPOMWAGA DAMU? UNASHINDAJE KUMSHINDA MTU ANAYETUMIA DAMU KUKUVURUGA? NA WEWE NI MKRISTO HUWEZI KWENDA KWA WAGANGA?
* AU KWANINI WEWE UKIAPPLY DAMU YA YESU HUONI MATOKEO MAKUBWA KAMA UNAYOYATEGEMEA? KWANINI UPANDE WA IBILISI WATUMIE DAMU ZA WANYAMA , NDEGE, BINADAMU,
KUTUONEA NA KUTUFUNGA?KWANINI SISI TUNA DAMU YA YESU NA BADO TUNAONEWA NA TUNAPAMBANA KILA SIKU? TUNAKOSEA WAPI? NINI KIFANYIKE?
*Endelea na introduction kwa Leo somo letu kuhusu damu ya Yesu linaendelea kidogo kidogo safari hii hatuna haraka! Bwana Yesu asifiwe Sana! Tutaenda hatua kwa hatua.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE!
PART B
Bwana Yesu asifiwe!
Muendelezo....
Kwanini damu?
Kwanini Shetani atumie damu ili afanikishe mambo yake?
Kwanini Mungu naye atake damu? Kwani maombi peke yake hayatoshi?
Kwani kufunga kwangu hakutoshi?
Kwani Roho Mtakatifu niliyenaye hatoshi mpaka nimwage damu?
Damu inapomwagiga inakuwa na maana gani?
Why should I use blood? Especially blood of Jesus?
AU KWANINI DAMU YA YESU? KWANI MTU ASIPOTUMIA DAMU ITAKUWAJE?
Damu ni nini? Kibiblia!
Kumbukumbu la Torati 12:16
. Lakini msiile damu; imwageni juu ya nchi kama maji.
Mwanzo 9:4
. Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.
Mwanzo 9:5
. Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.
DAMU NI UHAI. Unapoila basi unakula uhai ndo biblia imekataza. Pepo anapewa damu manake anaongezewa uhai na nguvu! Sasa inategemea damu iliyomwagiga! Ndio maana Kuna vifungo vingine vinajitaji more annoiting sababu it depends na damu iliyomwagiga! Mfano kifungo cha
damu ya kuku ivyo ni vipepo vidogo! Vidogo! Kifungo cha damu ya mbuzi au kondoo ni tofauti na kifungo cha damu ya Mtu hivi ndivyo vifungo vinasumbua watu. Sasa usipokuwa na maarifa ya kutosha. Mtu aliyefungwa na damu ya mtu iliyomwagiga aidha ya mtoto au ya
mtu mzima kifungo chake hakiwezi kuwa sawa na kifungo cha damu ya kuku. Hii ndo sababu watakuja watu wawili wanaombewa mmoja atafunguliwa mwingine ataendelea kufunguliwa. Na hapa ukipata Mtumishi ambaye anaenda
kwa mazoea na siyo Kumsikiza roho Mtakatifu basi kufunguliwa kwa mtu huchukua mda mrefu.
NANI ALIANZISHA MAAGANO YA DAMU?
au mikataba ya damu!?
Mwanzo 15:8
. Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi?
Mwanzo 15:9
. Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.
Mwanzo 15:10
. Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.
Mwanzo 15:17
. Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.
Mwanzo 15:18
. Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
* Mungu mwenyewe ndo mwanzilishi wa maagano ya damu. Shetani Hana jipya anachofanya anachukua Yale makatazo yote ya Mungu ndiyo anayoyafanya kipepo au anageuza neno la Mungu. Kulitumia against binadamu. But Hana aliloligundua au Hana alilolianzisha. Kila
kitu huchukua katika biblia kumbuka alikuwa makarubi kule mbinguni alikuwa karibu Sana na Mungu ivyo lazima anajua vitu vingi Sana vya Kimungu. Mungu alichosema usifanye yeye ndo anakifanya. Hapa tunamwona Mungu akidhibitisha ahadi yake kwa Ibrahim kwa Damu.
Ibrahim aliahidiwa mtoto akamwambia nitajuaje kama unayayaongea utayatimiza? Maana ushaniahidi vitu vingi huko nyuma nitajuaje kama kweli wewe Mungu unachoniambia kitatimia. Akamwambia Ibrahimu usiogope ilo tuu.
Lisikusumbue! Kaleta ngombe kondoo na njiwa kisha utamwaga damu Yao! Utanijengea madhabahu! BAADA YA KUFANYA VILE BIBLIA INASEMA KWENYE ILE MADHABAHU KULIANZA KUFUKA MOSHI MANAKE KULIWAKA MOTO. Kwa iyo katika ulimwengu wa roho shahidi wa agano la Mungu na Ibrahimu ni uhai wa
Damu. Manake ni hii ile Damu ya yule ndama, ile Damu ya kondoo, ile Damu ya njiwa zitakuwa zinaongea katika ulimwengu wa roho kumkumbusha Mungu kuhusu lile agano. Kwa iyo katika damu ipo roho! Na iyo roho ndiyo itakuwa inapiga kelele katika ulimwengu mpaka
kile kilichofunga agano kitimie! Bwana Yesu asifiwe! Ile Damu inapokuwa inapiga kelele malaika hufanya kazi kupitia damu. Kazi Yao ni kufuatilia damu inaongea nini katika ulimwengu wa roho.Au ni malaika wa shetani au ni malaika wa Mungu. Wapo malaika wako attention kufuatilia damu katika ulimwengu wa roho
inapomwagiga tuu hutokea sehemu ya tukio sasa wanasubiri maelekezo ya iyo damu. Ndio maana shetani alipogundua siri hii na yeye kupitia waganga wa kienyeji na wachawi huwa wanamwaga damu! Damu iyo inapomwagiga tayari malaika wa ibilisi wanafuatilia ile Damu, wanasubiri maelekezo. Ndio maana
ikimwagiga damu kwa mganga wa kienyeji atanuiza mfano "awe kichaa" awe kichaa! Lile pepo lililopewa uhai kupitia ile damu sasa kazi yake ni kutekeleza maagizo! Maana damu ile iyomwagwa huwa inaongea katika ulimwengu wa roho. Tuangalie maandiko ili tuelewe mambo haya ya ndani na muhimu sana kuyajua.
Mwanzo 4:10
. Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
*angalia hapo anasema sauti ya ndugu yako inanililia toka kwenye ardhi. Hii moja kwa moja inatupa picha damu ina sauti, Na damu ya Habili ilikuwa inanena malipizi, ilikuwa inanena laana! Kwa iyo damu inaweza kunena kwa ubaya au kwa uzuri! Kwa iyo wakati damu ya Habili
ilikuwa inanena laana juu ardhi, inanena malipizi na kisasi. Damu ya Yesu hunena ukombozi hunena kusamehewa dhambi, ushawahi jiuliza kwanini Mungu alimwadhibu kaini kwa kumlaania ardhi, kumfanya kutokuwa na maeneo maalumu kutangatanga? Na kizazi chake kuendelea na laana ya kuuana, visasi na malipizi,
wivu ni sababu damu ile ilikuwa inamsumbua Mungu masikioni ivyo ilikuwa lazima atimize kile damu inachosema! Kwa mapepo nayo hufanya kazi ivyo ivyo ndo mana huweza mfuatilia Mtu maisha yake yote ni sababu ya damu iyo iliyomwagiga! Inanena nini? BWANA YESU ASIFIWE!
JE DAMU INAPOMWAGIGA HUWA INAFANYA NINI?
1. Inaleta uwepo wa Mungu
*Katika agano la kale lote mahali Mungu alipotaka kushuka ilikuwa ni lazima damu imwagige! Kwa iyo damu ikimwaga ki Mungu huleta uwepo wa Mungu. Hii tunaiona kwa mara ya kwanza kabisa Ibrahim kumjenge Mungu madhabahu Mungu alishuka. Na madhabahu ilikuwa haikamiliki bila damu.
Mwanzo 12:8
. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana
*Soma mwenyewe hapo, akamjengea Mungu madhabahu kisha akaliitia jina la Bwana.
NUHU NAYE ALIFANYA IVYOIVYO...
Mwanzo 8:20
. Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Mwanzo 8:21
. Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
MFALME SULEMANI NAYE ALIFANYA IVYO IVYO ALIPOMWAGA DAMU YA NGOMBE 1000.
1 Wafalme 3:4
. Basi mfalme akaenda Gibeoni, ili atoe dhabihu huko; kwa kuwa ndipo mahali pa juu palipo pakuu. Sulemani akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu ya madhabahu ile.
1 Wafalme 3:5
. Na huko Gibeoni Bwana akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe.
2. Damu inapotolewa kwa Mungu inaleta kukubalika angalia mifano hapo juu.
3. Damu inapotolewa kwa Mungu inaleta inaleta kufunguka kwa milango ya baraka
*Angalia jinsi baraka ilivyofunguka tokea kwa Ibrahimu, kwenda kwa akina Isaka, kwenda kwa Jacob iyo trasition ilifanyika kwa damu wote walimjengea Mungu madhabahu. Hata wana wa Israeli ahadi zile za Mungu tokea kwa Ibrahimu walizipokea kwa damu iliyotolewa kwa Mungu.
*Kwa iyo damu ni kitu kikubwa sana kama damu inaleta kukubalika mbele ya Mungu, kama damu inaleta uwepo wa Mungu, kama damu inaleta mlango wa baraka basi usicheze kabisa na damu inayotolewa kwa Mungu. Shetani kawafunga sana watu . Kwa iyo damu inakuwa na nguvu mikononi mwa mwombaji sababu damu inaleta
1. Kukubalika(acceptance)
2. Uwepo wa Mungu (His presence)
3. Ufunguo wa baraka ya Ibrahimu(Blessing)
* Sasa jinsi damu iyo inavyofanya kazi kwa upande wa Mungu kumbuka shetani huiga ivyoivyo. Sasa anaiga kisha anafunga fikra zetu zisipate kujua siri hizi.au hata ukijua udharau! Au ushindwe kufanyia kazi hivi ndivyo adui anavyokuzibiti.
Tutaendelea PART C tukiangalia Damu ya Ki Mungu Kama ufunguo wa baraka, endelea kufuatilia ruusu moyo wako ujifunze tunakoenda ni kuzuri zaidi tunaenda hatua kwa hatua! .....
JINA LA BWANA LIBARIKIWE
PART C
Bwana Yesu asifiwe!
Tutaenda kuangalia damu ya Yesu Kama ufunguo wa Baraka za Ibrahimu. Au kujibu Yale maswali ya part A kwanini Damu ya Yesu?Nataka nikuonyeshe kibiblia kilichotokea katika agano la kale na kikaja kutokutokea agano jipya! Kwanini nitumie damu ya Yesu? Ina umuhimu gani? Yale maswali yote ya part A utapata majibu yake hapa katika part C na ndo ya mwisho.
AGANO LA KALE
Mwanzo 22:5
. Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.
Mwanzo 22:7
. Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, LAKINI YUKO WAPI MWANA-KONDOO KWA SADAKA YA KUTEKETEZWA?
Mwanzo 22:8
. Ibrahimu akasema, MUNGU ATAJIPATIA MWANA-KONDOO KWA HIYO SADAKA, MWANANGU. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.
SASA NATAKA UANGALIE AGANO JIPYA
Yohana 1:29
. Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
*Hapo juu inajibu lile swali la Isaka katika Mwanzo 22:7 LAKINI YUKO WAPI MWANA-KONDOO KWA SADAKA YA KUTEKETEZWA. agano la kale lile lilikuwa ni swali la kinabii na jibu lake akaja kulitoa Yohana Mbatizaji. Ambaye pia ukisoma Biblia Yohana Mbatizaji alikuja kumsafishia njia Bwana Yesu. Bwana Yesu asifiwe!
* ANGALIA ILO JIBU LA IBRAHIM ANASEMA MUNGU ATAJIPATIA MWANA-KONDOO YA SADAKA YA KUTEKETEZWA. Wote tunajua kipindi kile ukiangalia katika kitabu cha mambo ya Walawi ilikuwa kusudi mtu aondolewe dhambi ilikuwa
lazima imwagige damu ya mnyama.Iyo damu ya mwanakondoo katika madhabahu ya Bwana. Na uyo mwanakondoo ilikuwa ni lazima ataketezwe na moto. Ndivyo Haroon kuhani Mkuu alivyowatakasa wana wa Israeli. Kipindi kile alipokuwa na Musa.
Yohana 3:16
. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata AKAMTOA MWANAWE PEKEE, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
* Angalia kule juu MUNGU ALIONGEA NA NINI IBRAHIM? mwanzo 22:2 alisema hivi MWANA WAKO WA PEKEE, UMPENDAYE, ISAKA, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, UKAMTOE
*Najaribu kukuonyesha mambo ambayo Mungu aliyafanya katika agano la kale lakini yalikuwa ni kitendo cha imani cha maandalizi ya damu kumwagiga mwanakondoo wa Mungu. Yani mwana wa Mungu.kile kitakacho kuja katika agano jipya. Kile kitendo cha Isaka kutolewa kafara hakikukufungua tuu
baraka kwa ibrahim na uzao wake, au hakikuamisha baraka kwa Ibrahimu kwenda kwa Isaka! Bali lilikuwa ni tendo kivuli ya lile jambo ambalo litakuja kutokea. Kwa iyo ili kumiliki baraka hizi ilikuwa ni lazima uwe myahudi. Kwa iyo wewe kama si kizazi cha Ibrahimu ulikuwa huna haki ya kumiliki anachomiliki Ibrahimu! Kwa iyo wamiliki halali ni taifa teule yani zile baraka za Ibrahimu zilizopita kwa maagano ya damu. IBRAHIM>ISAKA>JACOB>ISRAELI
ADAMU NA EVA walibarikiwa kwa mdomo waliambiwa mkatawale ndege wa angani, viumbe wa baharini na vyote viendavyo juu ya nchi, lakini ili Mungu ku keep real agano lake alihitaji damu. Chunguza kila mahali Mungu alipotaka kufanya magano
na binadamu lazima alihitaji damu. Kwa iyo lile agano ya mwanakondoo pale Moria katika ulimwengu wa Roho ile damu ilikuwa inapiga kelele kwa iyo ilimlazimu Mungu kutimiliza agano ndio maana ikabidi amshushe mwana wake wa kipekee. Sababu kazi ya damu ni
kukumbusha katika ulimwengu wa roho.Kumbuka damu ya Habili ilivyomlilia Mungu. Inaongea katika ulimwengu wa roho! Ni kulazimisha watendaji kazi kuingia kazini hata kama hawataki. Agano ni agano linambana Mungu kwa upande wa Mungu
linambana shetani kwa upande wa shetani. Maagano ya Mungu yalihusisha damu sababu it was real. Yani siyo maneno matupu ni maneno yenye uhai. Ndo mana yalidhibitishwa na uhai. Yani damu.
1 Korintho 15:4
. na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;
*Angalia hapo juu ilo neno SIKU YA TATU, alafu angalia mwanzo 22:4, utaona SIKU YA TATU! yote yanazungumzia siku ya Tatu. Scenerio iyoiyo. Ya mwana pekee kuchinjwa. Kwa Ibrahimu ilikuwa ni ISAKA. Kwa Mungu ilikuwa ni YESU, sijui kama unaona ninachoona? Bwana Yesu asifiwe! inasema siku YA TATU AKAFUFUKA NA KULE JUU mwanzo 22:4 inasema siku ya TATU Ibrahim akayainua macho yake,
Kwa iyo ilikuwa ni ishara ya yatakayokuja.
Sasa ukichunguza hizi baraka zilianza kwa Ibrahim kwa agano la damu, baraka zikaenda kwa Isaka kwa agano la damu, kwa Yakobo alipata kwa agano la damu pale BETHEL, Kwa wana wa Israeli
walitolewa Israeli kwa agano la Damu kutoka 12:12 Ndivyo vilivyoendelea mda wote ilikuwa lazima ukitaka Mungu ashuke lazima utoe damu uchinje mnyama kwanza maana ilikuwa hatari sana Mungu akishuka bila damu unaweza
kufa! Wana wa Israeli baada tuu ya kuvuka bahari ya Shamu kuanza safari ya jangwani ilikuwa ni lazima Musa aende mlimani kuongea na Mungu. Ndipo awaletee ujumbe! Mungu akamwambia haina haja sasa utachinja sadaka ya
kuteketezwa na mtajitakasa kwa damu sadaka ya kutakaswa, amani katika madhabahu hemani kwa Bwana. Soma mwenyewe mambo ya walawi ndipo nitashuka.biblia inasema utukufu wa Bwana ulikuwa unashuka lilikuwa
linashuka wingu kisha Mungu anaongea kupitia lile wingu. Kwa iyo hakuna kumkaribia Mungu bila damu, hakuna uwepo wa Mungu bila damu, ukimshukuru Mungu lazima imwagige damu, baraka za Ibrahimu zilitolewa kwa
njia ya damu. Kwa iyo unaweza ukaona kinachomsukuma Mungu atende kitu kwa binadamu ni agano pekee sio sababu unapiga sana kelele! Yani kile Mungu alichosema ndicho anakifuatilia akitekeleze Yeremia 1:12 inasema huyaangalia maneno yangu nipate kuyatimiza!
Mungu akataka kupandisha mahusiano yake na binadamu. Maana sababu mojawapo kumtoa mwana wake wa pekee ilikuwa ni changamoto ya dhambi. Kipindi kile
ulikuwa ukifanya dhambi Mungu akisema unakufa unakufa kweli! Ama sivyo lazima wachinje mnyama au ndege wafanye upatanisho na Mungu. Soma mwenyewe mambo ya walawi utaona. Kosa kidogo madhabahuni kwa kuhani mkuu
akutakase kwa damu usije ukafa. Kingine ilikuwa huwezi nenda kwa Mungu bila kuhani mkuu kukuconnect na Mungu bila damu. Just imagine mmeenda kanisani hamwazi ibada kwanza mnatoka nje ya kanisa zinachinjwa kondoo kwanza mnatakaswa na kupatanishwa na Mungu na kuhani mkuu baada ya
hapo ndio muende kanisa mkafanye ibada. Kila kitu ilikuwa lazima upatanishwe na Mungu kupitia damu. Kusudi la tatu Mungu akaona uyu binadamu nataka nipandishe kiwango cha mahusiano naye! Kumbuka damu
Hii ilipokuwa inamwaga katika ardhi ndipo ilikuwa inafanya zile kazi tatu na nne nishazungumza 1. Ina leta kukubalika mbele ya Mungu 2. Inashusha uwepo wa Mungu 3. Inafungua baraka za Ibrahimu na kutembelea katika maagano yote Mungu aliyoingia na Ibrahimu.
Kumbuka Kaini ardhi ililaaniwa kwa ajili yake, kwa iyo sababu ardhi original yake ina laana! Unapomwaga damu juu ya ardhi Ki Mungu manake unaibatiza unaitakasa ndipo Mungu sasa anaweza kushuka na kufanya kazi na binadamu Mungu ni Mtakatifu hakai mahali penye laana. Na hii ndo sababu kuu ya kumwaga damu katika ardhi.
Mungu hatakuwatoa wana wa Israeli Misri ilikuwa ni sababu ya agano lake na Ibrahimu. Kwa iyo Mungu tokea dunia hii kuumbwa ni Mungu anayeangalia maagano yake yeye ili apate kuyatimiza ukishaijua hii siri nakamwambia hutatikisika.
Mungu akataka kupandisha kiwango cha mahusiano na binadamu pamoja na kuleta uwepo wake, pamoja na kumpa kibali binadamu mbele ya macho yake, pamoja na kumilikisha lango la baraka la Ibrahimu. Mungu aliona umuhimu wa kumpatia binadamu uhuru! Maana kumbuka Adamu na Eva walinyanganywa uhuru na shetani kule Bustanini kwa ajili ya dhambi.
Kwa iyo Mungu akaona kusudi kukata mzizi wa fitina kama ile damu ya kondoo tuu ilimwangusha farao, ile damu ya wanyama tuu mimi Mungu nilishuka kwa binadamu nikaa katikati yao, na nikawalinda, nikawashindia vita, niliwasamehe binadamu kwa damu ya wanyama, kama nilimkubali binadamu kwa damu tuu ya ngombe njiwa na
kondoo. Kama nilimlinda Ayubu na mali zake tuu kwa damu ya wanyama! Kama nilimbariki Suleimani mpaka mali zikamzidi nikamstarehesha kwa damu tuu za ngombe sasa mimi Mungu nataka wanadamu wote niwasamehe dhambi kila wanapokosea Niondoe mipaka yangu mimi na wao wawe wanaweza kuja kwangu mojakwamoja bila kufa, niwape uhuru wao walioupoteza kule bustanini! Niwape ule Ufalme wote wa duniani, chini
ya Nchi, yani hata kuzimu waweze kutawala na hata mbinguni wakiwa duniani. Niwape kutawala zile falme nne za shetani ziwe chini ya miguu yao yani wafalme wa giza wakuu wa giza wakuu wa anga na jeshi la pepo wabaya wawe chini ya binadamu, Lakini sasa iki kiwango kipya nataka nimpe binadamu nimpe yale maisha niliyowapa Adamu na Eva wakayaharibu lakini nitafanya agano. Sasa nitampa
nani? Nitafanya agano na nani?Mungu akafikiria!!!!! akakumbuka ADAMU ni Mtoto wangu mimi nilimtengeneza nikamwamini nikampa damu yangu hata DNA ungempima ingesema ni damu yangu mimi MUNGU! Mungu akaona hapana ngoja nishuke mimi mwenyewe. Kumbuka HAPA UWE MAKINI NDIO PENYE UFUNUO MKUBWA. katika kitabu cha
Yohana 1:1
. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Mwanzo 1:2
. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mwanzo 1:3
. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
*Twende taratibu ukisoma Hapo ivo vitabu viwili utagundua hapo mwanzo alikuwapo MUNGU, ROHO MTAKATIFU NA MAJI. Biblia inasema Roho ilipotua juu ya maji kukakuwepo Nuru. Kwa iyo sasa Mungu alijigeuza binadamu akawa mwanadamu. Kwa iyo ile mimba ya Mariam hata ungepima ungejua kuwa ilikuwa ya Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Halleluyah!
Biblia inasema Roho alipotua juu ya maji Mungu aliposema iwe nuru Roho Mtakatifu akafyatua Nuru. Kwenye case ya Mariam. Mungu aliposema mimba itungwe ya Mungu Mariam akakubali kwa iyo ikaja nuru ya ulimwengu duniani. Twende taratibu ukielewa hapa hutakaa uje udharau damu ya Yesu au uichukulie
kirahisihisi. Tuondoe maji. Tumweke Mariam . Biblia yetu tutaisoma hivi hapo mwanzo alikuwepo Mungu, Roho Mtakatifu na Mariam. Mungu akasema iwe nuru kwa iyo Roho Mtakatifu akafyatua nuru juu ya mariam(mimba sasa ya Yesu) kwa iyo Nuru ya ulimwengu ni mimba ya Mariam. Yani Yesu.
Kwa iyo sasa ni Tayari Yesu ni nuru ya ulimwengu cha pili kabeba damu ya Mungu si ya ngombe! Si ya mbuzi! Si ya kondoo wala si ya njiwa. Kwa iyo kama kawaida kusudi Mungu aweze kushuka duniani lazima iyo sehemu anayoshuka lazima imwagige damu! Kwanini imwagige damu ni sababu tayari ardhi hii ililaaniwa kupitia mikono ya kaini. Pamoja na
kulaaniwa bado Mungu hajasahau agano lake na Ibrahimu. Hatua sasa inayobaki ni Yesu kuimwaga damu yake katika ardhi kwa iyo atakapoimwaga damu yake katika ardhi ndipo sasa yale masharti na laana kule nyuma Mungu atayasahau! Kwa iyo Mungu yeye anaangalia agano lake na mtu mmoja tuu "YESU" Kama akikupenda wewe ni sababu ya agano la damu na
Yesu, akikusikiza wewe ni sababu ya Yesu, akikubariki ni sababu ya Yesu, wala si kwamba anakupenda sana no! Yeye anampenda Yesu! Sababu wameingia agano damu ilimwagiga. Na hii damu usichukulie ni damu ya kawaida hii ni damu ya MUNGU mwenyewe. Damu ya MUNGU Mwenyewe! HII SI DAMU YA KAWAIDA! Ina DNA ya Mungu mwenyewe! Lile ambalo shetani
aliliharibu Mungu amelifix kwa damu yake mwenyewe! Watu huwa wana mlaumu Mungu saa ingine kwanini Mungu kama alijua ndivyo itakavyokuwa kwanini alimruusu ibilisi basi? Kumbuka Mungu ni Mungu wa maagano hawezi vunja maagano yake mwenyewe maana atapoteza sifa ya u Mungu wake. Ivyo ni bora afanye agano jipya kubwa zaidi. Na hakuna agano kubwa kama la kujitoa uhai wako mwenyewe kwa ajili ya watu
wengine. Ndio maana basi huwezi fanya kitu chochote bila ya Yesu. Yesu kabeba nuru ya ulimwengu, Yesu kabeba baraka ya Ibrahimu, Yesu kabeba uwepo wa Mungu, Yesu kabeba vibali vya Mungu. Sasa kwa kutambua kwa upana huu nini maana ya damu ya Yesu na nini hii damu ilifanya huku ndiko kunakomnyima shetani usingizi. Hii damu ya Kimungu inapoingia mahali inapokuwa applied
sawasawa hakuna pepo wala ngazi yoyote linaweza kukaa si wakuu wa giza au wafalme wa giza, jeshi la pepo wabaya au wakuu wa anga. Hii damu ndo iliyomnyanganya ibilisi funguo za mauti na kuzimu. Hii damu ya Mungu ndio funguo kanisa lilipopewa na Yesu. Hii damu inatakiwa kuwa applied kila mahali mahali umekwama sema "kwa damu ya Yesu ninaachilia damu ya Yesu ya kukufua
biashara katika jina la Yesu" Huna haja ya kelele nyingi unapoijua kwa kiasi hiki hakuna ambacho kitakaa. Ukiapply katika cancer itatoweka apply katika uchawi utafutika! Apply katika kitu chochote! Hii ni funguo wa Yesu. wachawi wanatembea na hirizi sisi tunatembea na hii damu ya Mungu. Nilist mambo yangu yaliyokwama nikasema kwa damu ya Yesu ninayaamsha aya mambo yaanze kutembea sasa na
kukimbia na kila mikwamo ifutike" katika jina la Yesu. nakwambia gafla nikaanza kuona nuru hii si damu ya kawaida. HATA ILIPOMWAGIGA KWA MARA YA KWANZA HII DAMU YA MUNGU ILIFANYIKA KWA MAAGANO YA SIRI ILIKUWA KATI YA MUNGU NA YESU NGOJA NIKUONYESHE!
Luka 22:42
. akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.
Luka 22:43
. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Luka 22:44
. Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.
*nataka nikufungue macho uone angalia hayo maneno "WALAKINI SI MAPENZI YANGU, BALI YAKO YATENDEKE" rudia na kurudia hayo maneno hayo hii manake nini? Kuwa nimekubali mapenzi yako yatimie.YESU alikuwa anamfungulia Mungu gate la kumwaga damu yake juu
ya ardhi. Unasema nimejuaje baada ya kuomba vile malaika alishuka Mungu hakumjibu lakini malaika alishuka na kumgusa manake nini agano lilipigwa mhuri sasa safari hii halikupigwa mhuri na damu ya mnyama no! Na damu yake MUNGU mwenyewe. halleluyah!
Halleluyah! Mungu akusaidie uone nachoona. Bwana Yesu asifiwe sana! Biblia inasema tone la Damu likadondoka juu ardhi na hii ndo ilikuwa mara ya kwanza DAMU YA MUNGU kuigusa ardhi ya dunia hii. Bwana Yesu asifiwe sana.
SASA turudi kule part A Kwanini damu ya Yesu ndivyo jinsi ilivyo kwanini haina matokeo makubwa kama hapa navyoongea nisababu lazima moyoni mwako utambue Yesu ni Nuru ya ulimwengu huu and how. Pia utambue lango alilobeba Yesu, au agano alilobeba Yesu kupitia damu ya Yesu. Utambue
alichobebeshwa Yesu sio kwa kukremishwa no kama hivi sasa unajua. Ujue thamani ya damu ya Yesu unajua hii si damu ya kawaida ni damu ya Mungu mwenyewe. Pia ujue pia lango lako la kuingia mahali au kutoka mahali lipo katika hii damu ya Yesu. Pia ujue Yesu ndo lango pekee la Ibrahimu kwako, ndo lango
pekee kwa Mungu. Ndo kila kitu katika maisha yako sababu ya agano kubwa alilolobeba Yesu. Lazima umtambue Yesu kwa mapana yake. Leo umejua kidogo kuhusu damu ya Yesu endelea kujifunza. Na kujifunza. Sasa jinsi ya kutumia si vigumu unatakiwa uimwage tuu itafanya kazi wewe ni kuhani na kazi yako ni kuimwaga damu ya Yesu. Tatizo
hatuitumii. Sema kwa damu ya Yesu ninaachilia damu ya Yesu katika(.......) sema unachotaka ifanye(.........) then unaweka mhuri wa Bwana mkubwa Katika jina la Yesu. Hili ni zoezi la kila siku. Na la kiimani. Zaidi.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Da asante sana mungu akubariki
ReplyDeleteAhimidiwe MUNGU daima na milele. Abarikiwe sana mwandishi wa makala hii. Najua kuna sababu ya ujumbe huu kunifikia.
ReplyDeleteNimebarikiwa sana. Akili yangu imefunguka, fikra zangu zimebadilika for the better.
Asante YESU
Huyu Mungu aliyekupa ufunuo wa somo hili atukuzwe sasa na hata milele,Roho wa Mungu alinileta kuja kusoma hapa na nimeona akinifundisha sana..
ReplyDeleteBARAKA ZA BWANA ZIWE JUU YA YAKO
Haleluya ufahamu wangu wa kiroho umefunguka sana, Mungu akuimarishe mtumishi wake katika huduma aliyokupa. Ameen
ReplyDeletehakika neno lina ladha ya damu ya yesu.ubarikiwe sana mwandishi
ReplyDeleteAmen Mungu akubariki mtumishi masomo yako na maombi yamekuwa msaada kwangu hasa Hili somo ,Yesu akubariki
ReplyDeleteBwana Yesu asifiwe Mtumishi. Nimebarikiwa sana ni mambo mengi nimeyajua kuhusu damu ya YESU asante sana
ReplyDeleteBe blessed
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteVizuri sana, umeelezea vyema sana ni lazima watu wajue umuhimu wa damu ya Yesu ili iwasaidie na itusaidie sisi wote. Barikiwa sana!
DeleteUmenifungua sana nashukuru kwa hilo mungu akubariki uendele kufungua wengine kulielewa neno la mungu na kazi zake amen.
ReplyDeleteKiukweli umenifundisha mtumishi Mungu wa mbingu na nchi aendelee kukunyanyua mno, nimependa sana mifano yako ambayo inapanua ufahamu zais
ReplyDeleteamen shukrani kwa MUNGU BABA WA MBINGUNI somo ni tamu linafurahisha na kuchangamsha roho na moyo DAMU YA YESU ni ufunguo wa maisha yetu ya rohon na mwilini , MUNGU akuinue na akubariki matumish Joseph uzidi kutufunilia zaidi ya sirini
ReplyDeleteUmenifungua kwenye hili mtumishi asante sanaa kwa andiko ila ninajambo ningehitaji msaada wako
ReplyDelete