MADHARA YA KUTOKUOMBEA FIKRA
Tuanze kuangalia kwanini tuombee fikra? Kwani tusipoombea Kuna matatizo gani? Kwani ni lazima kuombea fikra?
Fikra imekaaje kaaje kibiblia?
Kuna uhusiano gani Kati ya fikra za mtu na kufanikiwa? Najua wapo watu ambao tayari wana ABC kuhusu fikra, hapa najenga msingi wa maombi, sababu nimejifunza kitu chochote chenye msukumo kwa mtu ni sababu kina majibu ya why? Au kwanini? BWANA Yesu asifiwe!
zifuatazo ni dalili za fikra zilizofungwa, kutokuona njia ya kwenda! Yani kuona giza, Kulalamika, kunungunika, kutokujua cha kufanya, akili kufikia mwisho, kuishi kwa kutegemea akili ya mtu! Kotokutaka kuwaza kuhusu ilo
jambo! Utasikia mtu alisema "ilo sitaki hata kulisikia" utasikia akisema wala sisumbui akili yangu, kukata tamaa ni dalili ya fikra kupigwa, mtu kukaa idle tuu kuanzia asubuhi hata jioni. Akili kuwa nzito,
kutokuona fursa mpya, kuwa na maisha Yale Yale tarehe 1 mpaka tarehe 1. Kushindwa kupanga matumizi ya pesa ni fikra zimepigwa, kushindwa kuelewa neno, kuelewa kushindwa kufuata neno la Mungu, au maagizo ya
Mungu, kuhairisha mambo muhimu, kuamua kuacha mambo muhimu bila sababu ya msingi, kungangania kitu kimoja, au kuanzisha ugomvi sababu ya kitu kimoja ni dalili ya kufilisika kifrika, kuwa na pesa
kushindwa kuizungusha pesa hapo fikra zimepigwa, kushindwa kuwa na displine na pesa fikra zimepigwa, kushindwa kukaa nafasi yako kama mke, Mme, Baba, mama, au kiongozi! Kuishi kwa kuiga watu
fikra zimepigwa, kuishi kwa kufanyiwa maamuzi hizo ni fikra zimepigwa, kuishi kwa hofu izo ni fikra zimepigwa, wasiwasi mashaka ni dalili ya fikra kupigwa, kutokujiamini, kutokuwa na maamuzi hizo ni fikra zimepigwa,
kuishi kwa sheria ya mtu mwingine izo ni fikra zimepigwa! Kumuona huwezi izo ni fikra zimepigwa! Iko mifano mingi Sana lakini mpaka hapo roho wa Mungu atakuwa ameanza kuzungumza na wewe. HALLELUYAH
Natamani nisiingie sana ili twende kwenye maombi ili maombi na somo linalokuja liweze kukuvisha. usipange kulikosa ni somo nyeti sana na pia limefanya kazi kwangu. Chochote kinachokuja hapa kichukue kifanyie kazi, kimepita maabara ya Roho Mtakatifu. Halleluyah!
Roho wa Mungu anasema andika zaidi ili Mimi Roho nizamishe ndani Yao? Swali la kujiuliza sasa matatizo ya fikra yalianzia wap? Kwanini mtu anakuwa na matatizo huko juu? Inakuwaje au inatokeaje tokeaje mpaka inakuwa hivyo?
Tuangalie Mwanzo 3-1-5
MLANGO 3
1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
ANGALIA ILO NENO MSTARI WA 3 MSIYALE WALA MSIYAGUSE MSIJE MKAFA.
SASA angalia shetani anapoingiza fikra potofu kinyume na maagizo ya Mungu kinyume na elimu ya Mungu! MSTARI WA 4- NYOKA ANASEMA HAKIKA HAMTAKUFA. MSTARI WA 6 MWANAMKE ALIPOONA YA KUWA MTI UNAFAA KWA CHAKULA NA NA WAPENDEZA MACHO YAO, NA MTI WA KUTAMANIKA KWA MAARIFA BASI AKALITWAA AKALA. Kuna
uhusiano gani wa Eva kabla na baada ya kula? Shetani alipofusha fikra za Eva Kwanza! Akaweka kuona
1. Kupendeza
2. Chakula
3. Kutamanika
4. Maarifa
5. Kuwa kama Mungu.
Hivi ndivyo vitu vilivyomsukuma Eva kula lile tunda. Kwa iyo fikra ilipofushwa kwa kile
alichokisikia! Na kila alichokiona katika ulimwengu wa Roho, Sasa baada ya yeye kula sababu yeye ni mwili mmoja na Adamu, na ametoka kwa adamu,adamu naye akawa ameshakula, Rohoni, ile kumpelekea Adamu tayari ni ukamilishaji wa Rohoni kuja mwilini! BWANA Yesu asifiwe Sana. My Lord
my God. Kwa iyo basi ndio maana ni Rahisi wanawake kuwatawala wanaume kifrika, sababu mwanamke ni sehemu ya mwili wa adamu! Miili hufanya kazi moja haipingani! Ndo mana Biblia kule juu inasema nyoka alikuwa mwerevu kupita wanyama wote, Bwana Yesu
asifiwe! Kwa mfumo huu katika ulimwengu wa Roho shetani hubadilisha Fikra original za Kimungu na kuweka Fikra zake. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Kwa iyo ibilisi hapigani kitoto anapigani na wewe katika fikra, yani Fikra zako mwenyewe zinakupinga, Kama aliweza kumsikizisha sauti ya Rohoni Eva, Kama aliweza kukuonyesha mambo ya Rohoni Eva, Eva baada ya hapo akala lile tunda basi jua kabisa mawakala wake ambao ni wakuu wa Giza, Falme za Giza, jeshi la pepo
wabaya, na wakuu wa anga hizo ngazi nne haziwezi pigana na wewe bila kufanya vita ya fikra kwanza ya kukuchanganya akili! Kama alivyomchanganya Eva na Eva akajikuta kayaasi maagizo ya Mungu. Ibilisi hufanya na binadamu wote kwa fikra kwanza kabla ya kuyatuma mapepo! Ibilisi uharibu
fikra zako, za maamuzi, Fikra za utatuzi wa tatizo, Fikra zako za kutambua yanayokuja, Fikra zako za jinsi ya kupanga matumizi ya pesa, Fikra zako jinsi unavyoona watu rohoni, Fikra zako za ndoa, Fikra zako kuhusu kufanikiwa, Fikra kuhusu wewe mwenyewe unavyojiona, unajionaje? Wewe ni
masikini? Huna lolote? Unajiona mapanzi mbele ya waliofanikiwa, unajionaje wewe mwenyewe je unajikubali? Unajiamini? Au unajiona huna dhamani, unajiona ushashindwa? Unajiina huna mwelekeo? Unajiona huwezi? Unajiona unaonewa? Unajionaje? KUMBUKA JINSI UNAVYOJIONA NDIVYO JINSI INAVYOKUSUKUMA KUFANYA MAAMUZI, kufanya
maamuzi kumbuka kule juu Fikra zilizomsukuma Eva kufanya maamuzi ya kufanya dhambi. Hii nitaongea ili kuweka uzito ndo mana wanawake wengi huamini Sana kwa kusikia. Angalia ile historia kwenye biblia wanawake ni wepesi kuamini
kwa kusikia! Wanaume si wepesi wa kusikia ni wepesi baada kuona ndipo wanaamini! Baada ya adamu kumuona Eva Kala naye akala! BWANA YESU ASIFIWE SANA! kwa iyo ibilisi kwa kubadiilisha fikra kila Mara anakuongoza katika shimo la matatizo. Bwana Yesu asifiwe Sana! KWA IYO UKISHATAMBUA KUWA KUFANIKIWA KWAKO
HAKUTEGEMEI kitu kingine chochote isipokiwa fikra basi utasukumwa Sana kuombea Fikra
Fikra huleta mauti Kuna watu kwenye biblia waliwahi kupoteza maisha au kufa, kwa kupata mapigo ya Mungu sababu ya Fikra zao ziligoma kufikiri zilifika mwisho na walipoona ivyo wakaona ni Bora warudi nyuma ya safari Yao, ni bora
kutokumsikiza Mungu, ni Bora wawauwe watumishi wa Mungu kwa Mawe Mungu akaaingilia Kati.... Tuangalie maandiko
Hesabu 13-32-33
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
ukisoma hii hadithi kuanzia kutoka, mpaka huku kitabu cha Hesabu! Ilikuwa imebaki point ndogo kabisa waingie kaanani! Wapelelezi walioenda kupeleleza wanaleta report lakini report inainamisha mioyo ya mkutano wana Israeli wanawambia kule tulikoenda ni kuzuri lakini hakuingiliki
wakifafanua ya kuwa hao watu iyo nchi imejaa mijitu mirefu inanguvu wakaongezea tumejiona mapanzi navyo ndivyo walivyotuona sisi! MANENO HAYA YOTE NDIYO WALIYOYASIKIA MIOYONI MWAO NA KUJIONA NAFSINI MWAO! KUMBUKA KULE JUU JINSI EVA ALIVYODANGANYWA ALISIKIA ALAFU AKAONA (ROHONI) WENGI
stori hii mnaijua kilichotokea baada ya hapo ni kutokuelewana, somo mwenyewe iyo sura ya 13 yote Na kupelekea like kundi kugawanyika. Haikutosha wakataka kumpiga Musa na Haroon! Wakimlalamikia Musa kuwa ni bora wangefia misri utumwani! Bora turudi utumwani, wasijue ya kwamba wale watu kule
walio waona ilikuwa ni watu wa kuwatumikia Wao! Bwana Yesu asifiwe Sana! Sasa ikaleta ugomvi mkubwa Sana. Wakataka kuwapiga mawe Mara utukufu wa Bwana ukawazukia yani Mwanga katikati Yao wakajikuta mawe yanadondoka mikononi mwao. Sasa angalia Hesabu 14-36-37 wale watu
walioleta habari mbaya wakafa kwa tauni. BWANA YESU ASIFIWE! KWA IYO usipocontrol fikra zako mwenyewe shetani atazicontrol hata kama hutaki. Hapa duniani hakuna neutral aidha uwe kwa Mungu. Kama hutaki ibilisi atakukamata. Ndio maana Tanzania tunarasilimali nyingi lakini fikra zimekamatwa. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Nataka uone hatari ya kutokukabithi Fikra zako Bwana Yesu tena si Mara moja inatakiwa kila siku. Tutakuja huko lakini hapa nataka nikionyeshe haijalishi wewe ni Proffessor au Una PHD au Masterz au Una nafasi kazini au ushafanikiwa according to fikra zako! Kama Fikra zako zipo kwa ibilisi humkabithi Yesu bado wewe
ni mtumwa. Bwana Yesu asifiwe. Uhuru wa juu kuliko wote ni uhuru wa Fikra. Kuwa original you. Jinsi Mungu alivyokuumba. 100% ya matatizo yoote ya binadamu yapo kwenye fikra! Sababu watu hufikiri elimu zao na pesa na kazi na biashara zitamaliza matatizo Yao! Kumbe wamesahau kitu kitakacho
maliza matatizo yako ni fikra akupazo Mungu. Baasi! Nenda juu Rudi chini! Hata shetani Hana fikra mambo yote anachukua kwenye biblia anayageuza chunguza chunguza utagundua! Anachofanya anakufunga usipate hayo maarifa. alafu anageuza fikra za Mungu mwako anaweka za ibilisi. Bwana
Yesu asifiwe Sana! Ni mpaka utakapojifunza kufanya kazi kwa fikra za Mungu ndipo hapo utakuwa salama. Kumbuka kule nyuma . Eva alisikia + kuonyeshwa mambo mazuri = Moyo wake ukaamini lakini ndani yake kulikuwa na MAUTI. angalia mwenyewe kule juu MUNGU ALISEMA HAKIKA MTAKUFA, MUNGU alikuwa si mauti tuu Bali
FIKRA. Jiulize Mara ngap umesikia na kuona vya rohoni ukafuata ukatenda baadae ukaja kugundua ni shimo la ibilisi? Mara ngap Fikra zako zimekudanganya? halleluyah! Halleluyah!
Wakorintho 10:3:5
3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;
4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Nataka uone kitu
1.ingawa tunaenenda katia mwili
2. Hatufanyi vita jinsi ya mwili
3. vita vyetu
4. Silaha ya vita vyetu
5. kuangusha ngome
6. Mawazo
7. Elimu ya Mungu
8. Tukiteka nyara kila Fikra
9. Zipate kumtii Kristo
Kwa lugha rahisi inasema vita tunavyopigana kila siku katika maisha yetu! Asili yake ni rohoni na sio mwilini, kwa iyo tunapopigana vita hivyo hatumii,ngumi, mateke, matukano maana vita vyetu si kwa ajili ya vile vinavyoonekana vita vyetu asili ni katika mambo
yasiyoonekana! Ambayo ni majeshi ya ibilisi Katika ulimwengu wa Roho! Ambayo ni Falme za Mamlaka, wakuu wa Giza hili, majeshi ya pepo wabaya, na makuhani wa ibilisi wa kibinadamu Katika ulimwengu wa roho maana hawa ndio wanaokuletea matatizo uliyonayo
ndio adui zako hawa. Akaendelea kuelezea silaha zetu sisi Wakristo ambalo ni neno la Mungu si kwa ajili ya kupambana mwilini no! But rohoni, kwa izo silaha zina uwezo wa kuangusha ngome za shetani! Ngome izo kazi yake ni kuletea mawazo mabaya, ngome izo kazi yake kuteka elimu kinyume na elimu
ya Mungu. Na kila fikra potofu. Ili akili yako iweze kuona ya rohoni! Kusikia ya rohoni, iweze kuelewa lugha ya Mungu. Sababu haya mawazo elimu na fikra zikiwa haziko huru zinazuia, proper communication na Mungu. Kama,communication itakuwa dhaifu hata utekelezaji
utakuwa,dhaifu. Sababu akili ya binadamu imetengenezwa kufanya kazi na mawazo Fikra Elimu ya Mungu. BWANA YESU ASIFIWE
Kwa iyo ugomvi wa ibilisi na Mungu upo katika binadamu kuondolewa ule uwezo wa kusikia na kufuata sheria na maagizo ya Mungu. Ibilisi hapo ndipo anapigana usiku na mchana, ndivyo vita vya ibilisi na Mungu. Kwa iyo sasa ili avuruge maisha ya mtu atakuja kufanya vita Katika Fikra akivuruga Fikra tayari
kavuruga mawazo yako! Na imani yako uliyoipata katika elimu ya Mungu. Mfano mtu akiwa Hana kazi tatizo si kazi,chache au tatizo si expirience tatizo, ni yeye anaona nini anapofikiria kazi! Icho anachokiona ndio ukuta huo katika fikra. Ndivyo,ibilisi anapigana na
sisi. Sasa basi ibilisi anajua wewe Una elimu ya Mungu kwa iyo,haji kwa jinsi ya wewe utamtambua kirahisi Bali huja Katika njia ambayo wewe utajikuta fikra zako tayari zimeshatekwa. Fikra zako zikishakuwa utumwani ujue ndio mwisho wako huo. Sababu mwisho wa siku utaishia kulaumu
kunungunika kukata tamaa, kumbe pale ambako fikra zako zimefikia,mwisho ndipo Mungu anatakiwa akupe maarifa mapya kwako au njia mpya sasa tatizo atakupaje wakati humwelewi wala humsikii, wala humuoni na wewe fikra zako zimejaa kushindwa, kukata tamaa, kuchoka. Na ibilisi
ameshauwa kipengele cha Communication Kati ya wewe na Mungu, kila akitaka kuja Mungu kukusaidia anakuta ngome ambayo ni fikra za malalamiko, kunungunika, kukata tamaa, kushindwa, kuchoka, kutokutaka kuendelea mbele, kutokutaka kumsikiza tena Mungu, kumlalamikia Mungu,
kutokumuamini. BWANA YESU ASIFIWE Haya ni baadhi ya maeneo fikra za watu zimekamatwa na zimeathiri kufikiri kwao~ Mungu alinifunilia nilipokuwa naomba kuhusu Fikra. zimekamatwa na nguvu za giza. na wamekwama katika maeneo yote kihuduma! biashara! kazi! ndoa! elimu! familia! ukoo!
1. Kutoa sadaka mahali ambako hakuna Mungu wa kweli
2. Kupitia mitandao ya internet ni hatari sana 98% ya website na Blogs na socio media zipo nyavu za ibilisi za kuteka fikra na inaadhiri kufikiri kwao.
3. kupitia nyayo za miguu fikra za mtu hufungwa
4.kupitia kula na kunywa
5. kula na kunywa ndotoni
6. Fikra za watu wengine zipo round about, majalalani, makaburini
7. fikra zimekamatwa kupitia uchawi wa kupigwa mafundo
8. Fikra zingine zimekamatwa maeneo ya biashara , unakofanya kazi au ulikowahi fanya kazi, au nyumba unayoishi, au uliyowahi kuishi
9. Fikra nyingine za watu zipo kwa waganga wa kienyeji zimekamatwa kupitia vitu vyako ulivyowahi kuibiwa, au kupoteza
10. fikra zinakamatwa kupitia picha videos movies unazoziangalia zisizo mtukuza Mungu fikra zako zinakamatwa huko na unakuwa mateka!
* Fikra zingine zimeshikiliwa katika ardhi! angani! chini ya bahari. yani ule uwezo wako unakamatwa na kuondolewa. Fikra zikishakamatwa mpendwa basi biashara yako imekwisha. nikupe mfano T.v huwa inaongozwa na Remote control uhuru wa T v upo katika maamuzi ya mtumiaji wa Remote control, kwa
iyo T v ni wewe Remote control ni Fikra! sasa swali anayetumia Remote ndio mwenye uwezo kukuweka huru, kukuturn on, kuku turn off, Kama remote control yako ameishika ibilisi basi jua zile kazi za Yohana 10:10 ndizo zitakazotekelezwa kwako, yani mauti kila eneo! lakini kama Yesu akishika remote control basi jua utakuwa na uzima wa milele kila mahali katika maisha yako. Bwana Yesu asifiwe!
KUMBUKA UKIKWAMA KIFRIKA UMEKWAMA MAISHA. UKIFANIKIWA KIFRIKA UMEFANIKIWA MAISHA. MAFANIKIO YA MTU YAMEFUNGWA KATIKA FIKRA. (MAARIFA) UTAFANIKIWA NA KUWA HURU KWELI KWELI KAMA TUU YESU ATAHUSIKA.
ALAFU TUTAFANYA MAOMBI.KUHUSU FIKRA. JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
mwakasege alifundisha akasema katikati ya Jangwa na kaanani kuna FIKRA. nilipokuwa napitia notice zangu. Roho wa Mungu akanizamisha ndani zaidi.
Kile Mungu alichonifundisha ndicho ambacho tutaenda kuangalia...
JANGWA NI KIPINDI AMBACHO MTU HUWA ANASUBIRI MUUJIZA WAKE UJE YOKA ROHONI UJE KATIKA MWILI AUONE KABISA
Kusudi Fikra ziweze kukusaidia ufike kaanani lazima kwanza uelewe maana ya JANGWA
JANGWA NI KIPINDI AMBACHO MTU HUWA ANASUBIRI MUUJIZA WAKE UJE TOKA ROHONI UJE KATIKA MWILI AUONE KABISA
Wakristo wengi tunaomba mpaka sehemu flani alafu tunamwachia Mungu kumsubiri Mungu. wasichokijua Mungu anachokusaidia wewe ni maarifa tuu. Baada ya kupata maarifa unatakiwa uendelee mbele mwenyewe...
Roho Mtakatifu kanifundisha hapa kaniambia JANGWA LINA maana ifuatayo
1. utupu
2. ukiwa
3. Giza
Mwanzo 1:2
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
UTUPU ni nini?
-kutokuwa na kitu ndani yake
-emptyness
UKIWA
-Abondoned
-unyonge wa kutokuwa na msaada
-kutokuwa na tegemeo
-kutokuwa na msaada
GIZA
-Kutokuona mbele
-kutokujua njia ya kufuata
-No vision
* Sasa Roho wa Mungu akaniambia huwezi pata maarifa kama hujajua maswali ya kujiuliza juu ya utupu, ukiwa, na giza
*Mungu anataka mfanye kazi wote sio wewe uombe alafu ukalale hapana lazima akili yako ijishughulishe
unapojishughulisha ulipokwama ndipo Mungu huja kukusaidia lakini si Mungu kukufanyia hata kazi yako ya kufikiri hapana.
Kuna jangwa uchumi mgumu, kuna jangwa kutokuolewa, kutokuoa, kuna jangwa kukaa sehemu moja mda mrefu bila kupiga hatua kila mtu anajangwa lake! kufanikiwa katika ilo jambo ndio kaanani yenyewe. sasa wengi wanafikiri bila kufikiri kaanani itakuja tuu haiendi ivyo.
SASA KATIKA UTUPU, UKIWA, GIZA MASWALI YA KUJIULIZA mfano kwenye uchumi mgumu!
* Mfano wa maswali ya janga la uchumi ngumu.
*kwanini uchumi wako ni ngumu?
SABABA HAUZALISHI
*kwanini hauzalishi?
SABABU HAUKO KATIKA MZUNGUKO WA KUZALISHA
*Kwanini hauko katika mfumo wa kuzalisha?
SABABU HAKUNA INPUT YA KUTOA OUTPUT KWA IYO UCHUMI WAKO HAUZALISHI SABABU NO INPUT YANI KISABABISHI KAMA KAZI NZURI AU BIASHARA YENYE FAIDA NZURI.
*Kwanini hauna input? SIBABU SIJAWEZESHWA
*Nani wa kukuwezesha?
MIMI MWENYEWE
*Wewe utawezeshaje au utaondoaje huo utupu? katika uchumi mgumu
KWA KUANZISHA CHANZO CHA KIPATO.
*kipi?
KAZI AU BIASHARA
*Kipi kimekukwamisha usiwe navyo?
KAZI SINA LINK YA KIMUNGU YA KUNI HOOK KUPATA KAZI
BIASHARA NATAFUTA IDEA NA MTAJI
*Unatafutaje?
KUMUOMBA MUNGU ANIKUTANISHE NA WATU SAHIHI NA KUWEPO MAZINGIRA SAHIHI ILI IFANYIKE NJIA
*watu sahihi toka kwa Mungu ndio watatoa utupu wa iyo gap ya kupata kazi. NDIO
KUUSU BIASHARA NAHITAJI KUFANYA RESEARCH. utaifanyaje? NITAMWOMBA MUNGU ANIKUTANISHE NA WATU SAHIHI WA KUNIONGOZA AU MUNGU MWENYEWE ANIONGOZE.
*Je baada ya kujua ndo utakuwa umefanikiwa kuanza biashara. HAPANA HAPO BADO KUNA UTUPU UKIWA NA GIZA LA MTAJI. sasa utafanyaje? HAPO NITAMWOMBA MUNGU ANIPE MAARIFA JINSI YA KUFANYA ILI NIKUTANE NA HUO MTAJI AU WATU ALIOWAANDAA MUNGU.
swali la Kwanza:
kwanini mtu aseme uchumi mgumu? au utupu katika uchumi mgumu uko wap?
JIBU: Ni sababu hauzalishi manake yake hauna INPUT
* Nia si kujibu maswali yote nia ni kutafuta wapi unakwama.
*Pia kama unashindwa kujiuliza maswali haya hapo pia ndipo pa kuanzia.
*Hapo unaposhindwa ndio pa kumpelekea Mungu kuomba na kuendelea mbele! hivyo ndivyo utafikia kaanani yako si kwa kusubiri Muujiza. Bwana Yesu asifiwe?
*Mungu anataka mfanye wote hatua kwa hatua. sasa wengi wakikwama wanaacha na kuanza kulalamika. kama wana wa israeli.
*Na unapofanya haya pia unamvutia Mungu kuanza kudeal na wewe
* Kwa iyo katika kila kikwazo utakachokipata kwa kujiuliza maswali aidha ni kimoja au viwili icho ndicho cha kwenda nacho kwa Mungu cha kumsihi ajifunue kuhusu iko kikwazo au aukupe maarifa.
lakini ile tabia ya kusambaratisha kuvunja ni wakati upo misri ila ukishavuka bahari ukianza safari ya jangwa hapo ni sehemu ya unyenyekevu, subira, utii, ili uweze kuuliza kutulia Mungu aseme unasogea mbele hatua kwa hatua.
lakini ukiona ndani yako hakuna subira, utulivu, utii havipo ndani yako basi jua bado upo misri unapambana na Farao. Nimeongea lugha ya ndani sana ya biblia sijui kama mmenipata. Nachotaka
kukuambia ni hiki! kwenda kaanani unaenda kwa kujua kikwazo kilichopo ndani ya ilo jangwa uliopo sasa baada ya kujua kikwazo unaenda kwa Yesu yeye anafunguo yake. unafungua hapo unaendelea mbele.... ndivyo utakavyovuka.
lakini ukisubiri muujiza utasubiri maisha yako yote. TUMEKUWA WATU WAZIMA KATIKA KRISTO LAZIMA TULE VYAKULA VIGUMU. aidha umepata unabii aidha muujiza umeanza! KUMBUKA SHUHUDA IYO AU MUUJIZA HUO KWENDA KAANANI YAKO KATIKATI KUNA FIKRA.
Yani
MAFANIKIO+ FIKRA= KAANANI
*Mafanikio tunayapata kwa ahadi za Mungu, unabii wa Mungu Kusudi ufike kaanani yako hapa katikati Kuna FIKRA. NA fikra hizi ndani yake nimesema Kuna ( ukiwa, utupu na Giza)
Kwa iyo Mungu akaniambia chukua kalamu na Diary yako kisha nikaandika.mfano
UCHUMI+ FIKRA= KAANANI
Nikaanza kujiuliza ni vitu vinanikwamisha uchumi wangu yani ukiwa giza na utupu? kwenda kaanani? baada ya kumaliza kuandika Roho Mtakatifu akaniambia Fungua ufunuo 5:9
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
# nikaaza kusoma hapo palipoandikwa ukamnunulia Mungu watu wa kila kabila, kila lugha kila taifa. WAOOH NIKAPATA KITU NDANI YANGU Yesu kumbe alishuka duniani kuninunua Mimi, unauliza kivipi? Alishuka kununua uchumi wangu, afya yangu, mwezi wa ndoa, ndoa yangu.biashara mtaji, Na yote yaliyoshindikana. halleluyah halleluyah
SABABU ibilisi Kuna mambo yetu haki zetu kazinunua kwa damu za kuku, damu za wanyama damu za watu. Kwa mikataba, kwa iyo akapata uhalali wa kumiliki kwa dhambi yako ndio maana wewe
unahangaika. Kwa iyo sehemu ambayo umeshindwa kuuliza maswali kule juu, sehemu ambayo huna majibu usipate shida nunua kwa damu ya Yesu. Sema kibali cha ndoa kazi biashara au kupata
mchumba nakununua kwa damu ya Yesu. Naachilia damu ya Yesu ya mwanakondoo ya kununua sawasawa na ufunuo 5:9, itafanyikaje sijui, itakuwaje sijui nachojua hii damu ya Yesu ni damu
ya kimbingu iliyokuja duniani kudondoka juu ya ardhi ili Yale yaliyoshindikana. Gafla nikaanza chukua hatua baada ya kuchukua hatua roho Wa Mungu akaniambia wafundishe watu. Waelekeze watu.
Fikra zako zilipokwama zinunue kwa damu ya Yesu. Zinunue kwa damu ya Yesu. Kama niuchumba umekwama kama unakataliwa nunua kukubalika kwa damu ya
Yesu. Kama wateja wanasumbua sema naachilia damu ya Yesu Katika nchi na mbingu, na mji huu wateja wa kununua hizi bidhaaa nunua kwa damu ya Yesu. HALLELUYAH HALLELUYAH
Angalia pale juu huwezi kutawala na kumiliki ni mpaka UMENUNUA UMENUNUA TATIZO TUNASOMA HATUELEWI. TATIZO HATUNUNUI KWA DAMU YA YESU. HATUNUNUI KWA DAMU YA YESU. NUNUA NDOA YAKO! NUNUA BIASHARA!
NUNUA MCHUMBA! NUNUA UCHUMI. UNAPONUNUA FIKRA ZIREJEE ZIKIREJEA MAARIFA YANARUDI YAKIRUDI UNAJUA CHA KUFANYA GAFLA UNAJIKUTA UNATAWALA NA KUMILIKI JUU YA NCHI. Bwana Yesu asifiwe!
MAOMBI:
Baba Katika jina la Yesu Kristo! Nazileta fikra zangu mbele zako ninaomba Rehema kwa ajili ya fikra zangu katika jina la Yesu.
Ninaomba Rehema kwa jinsi yoyote nilifungua mlango kwa adui akakamata fikra zangu mawazo yangu akili yangu ufahamu katika jina la Yesu.
Ninaomba Rehema kwa ajili ya kutokiziombea fikra zangu, ninaomba Rehema kwa kufungua malango ya maneno malango ya macho kwa
kuangalia, malango ya kusikia, malango ya kula kunywa kila jinsi yoyote nilivyohusika kufanya mikataba, maagano, au kushiriki katika mazindiko, kafara pasipo kujua
hata ikawa ya kwamba fikra zangu zimekamatwa na shetani kupitia mawakala wake. Ninaomba Rehema kwa kutosimama Katika nafasi yangu ataikawa
ya kwamba nimebanwa fikra zangu hatua za fikra zangu kupitia nyayo za miguu. EE Mungu Baba naomba unirehemu maaana adui ameweka mitego kila mahali
kuwinda fikra zangu kuziwekea uvivu wa kufikiri, kuweka malalamiko, kuweka kunungunika, kuweka kukata tamaa, kuweka kuchoka, kuweka kutokufikiri na
kutokuchukua hatua. Naomba Rehema kwa ajili ya macho yangu yaliyoangalia videos mbalimbali ambazo hazina utukufu wako, ninaomba Rehema kwa ajili ya
picha nilizoangalia na movies pia nilizoangalia na nyimbo nilizosikiliza ambavyo zimekata fikra zangu maongezi niliyoshiriki, maneno niliyokiri, ambavyo
havina utukufu kwako ambazo ni mtego wa ibilisi eee Mungu Baba unisamehe unirehemu katika jina la Yesu. Saa ingine ninangangana kuomba kwa nguvu kumbe
fikra zangu zimefungwa ndio maana Ninapiga maritime, ndio maana kunamapooza kwangu Kuna utasa kwangu, Na nimekwama Bwana Leo
narejea kwako kwa rehema kwa ajili ya utakaso Kamili. Ili wewe Mungu mwenye uwezo wa kufungua fikra zangu zilipofungwa, ili wewe Mungu mwenye
fikra na maarifa ya kunitoa hapa unisaidie kwa damu ya Yesu kwa damu ya YESU. Ninaomba Rehema kwa ajili ya kila mahali nilipokanyaga na kwenda ambako
kulikuwa hakuna utukufu wako na fikra zangu na hatua zangu kupitia miguu zikanaswa hapo! LEO nimegundua pasipo wewe Bwana siwezi kusogea hapa
nilipokwama, pasipo wewe Mungu siwezi kujinasua ila ni wewe pekee uliyeniumba ukaniumba na fikra na mawazo ya kufakisha njia yangu. Kwa damu ya Yesu,
kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu Kristo ni rehemu Bwana kwa kutegemea akili yangu mwenyewe, nirehemu kwa kutokukupa nafasi nirehemu kwa kukataa
maneno yako. Nirehemu kwa kuwadharau watumishi wako, nirehemu kwa kuwacheka maana imeandikwa wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
sababu ya kukataa njia zako, na sababu wamekataa njia zako wewe Mungu umeniacha niende katika maanguko yangu, nirehemu kwa kiburi nirehemu
kwa ujuaji, naomba Rehema kwa ajili ya laana iliyonipa sababu ya kutoshika sheria zako. Na kufuata maagizo yako sawasawa na kumb 28: 15 niondolee laana zote kwa
damu ya Yesu kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu Kristo. Naja kama jinsi nilivyo Bwana nioshe nitakase kwa damu yako Bwana Kwa damu yako nirehemu katika
jina la Yesu Kristo.Baba neno lako linasema Pando lolote asilolipanda Baba Mungu wa mbinguni litangolewa sawasawa na Mathayo 15:13 nami sasa
katika jina la Yesu Leo ninaleta fikra zangu kwako nazikabithi kwako kwa damu ya Yesu. Kwa damu ya Yesu. Kama neno la Mungu lisemavyo kila Pando asilolipanda
Baba yangu aliyembinguni litangolewa Ee Bwana chochote kilichounganishwa na fikra zangu nakingoa sasa kwa damu ya Yesu, ninangoa matambiko, ninangoa
nguvu ya kafara eneo ninaloishi, mtaa ninao ishi, Kwa damu ya Yesu, Kwa damu Ya Yesu, ninangoa nguvu ya kafara kwenye fikra zangu mahali pa biashara,
nakofanya kazi, Kama zilishikwa kupitia ndoto kula na kunywa, kama zilishikwa Kukamatwa kupitia vyakula na vinywaji na manuizo yote ya kichawi,
sumu katika ndoto, manuizo katika chakula na vinywaji kwenye akili yangu nakungoa kwa damu ya Yesu! Kama fikra zangu zimeshikwa kupitia uchawi wa
mafundo uchawi manuizo katika akili yangu nakungoa kwa damu ya Yesu, kila ambacho kimepandwa katika fikra zangu nguvu ya dhambi, utumwa wa dhambi,
giza katika fikra, kukata tamaa, kuchoka, kujiona mnyonge ninapitisha sasa damu ya Yesu Damu ya Yesu katika fikra zangu. Kila pando la kipepo, la majini, mapando
kupitia malango yangu ya mwili, mapando kupitia malango yangu ya rohoni nanyunyiza damu ya Yesu! Damu ya Yesu ya kungoa mapando! Mapando ya roho
chafu katika fikra zangu. Mapando ya uchawi, uganga ushirikina, wingu jeusi, mapando ya maneno mabaya ya wachawi washirikina marafiki, mapando yote ya
ibilisi yaliyopandwa katika fikra zangu napitisha damu ya Yesu! Napitisha damu ya Yesu! Ninangoa kwa damu ya Yesu, ninangoa kwa damu ya Yesu ya kungoa
mapando katika jina la Yesu, mapando yote ya kufunga fikra, mapando yote ya kuzuia kusikia sauti ya Mungu, mapando yote ya kuzuia kufuata maagizo ya
Mungu, mapando yote ya kuzuia kuelewa neno la Mungu, mapando yote ya kuzuia kusoma neno la Mungu, kusikia sauti ya Mungu, Kwa damu ya Yesu, kwa damu ya
Yesu! Katika jina la Yesu! Kwa damu ya Yesu!Kwa damu ya Yesu.katika jina la Yesu fikra zangu sasa popote ziliposhikwa au kupandwa kama zimepandwa kupitia
sadaka za nilizowahi kutoa ambalo si kwa Mungu, Kama zilipandwa katika mitandao ya internet, Kama zimeshikwa kupitia nyayo za miguu na kumekuwa na uvivu,
utayari umeondoka, kuhairisha mambo, kutokupiga hatua, kurudi nyuma, kuzunguka mbuyu kwa damu ya Yesu! Kwa damu ya Yesu Baba wa Mbinguni
ninangoa fikra zangu huko, ninangoa fikra zangu huko kwa damu ya Yesu! Katika jina la Yesu! Bwana Yesu fikra zangu ziliposhikwa kupitia saloon kutengeneza
nywele, zilipokamatwa kupitia chakula na vinywaji nilivyokunywa, kupitia kula ndotoni au kunywa, fikra zangu zilizokamatwa kwa ushirikina, mazindiko,
matambiko, uchawi wa kupiga mafundo Bwana Yesu ninamwaga damu ya Yesu huko aidha ni ardhini baharini chini ya bahari, au angani ninangoa fikra zangu
huko ninangoa fikra zangu huko nazirejesha kwa damu ya Yesu,nanyunyiza eneo lililonishita mateka damu ya Yesu ipo juu yako ewe mateka wa akili yangu,
kwa damu ya Yesu! Ninaharibu nguvu zako mateka, ninaharibu kazi zako, nakuharibu mwenyewe kwa damu ya Kimbingu kwa damu ya Yesu katika jina la
Yesu, Baba Mungu kama fikra zangu zimekamatwa kupitia ndoto, au maono, kupitia manuizo, kupitia falme za giza, za ukoo/ familia/ eneo naloishi au mtaa
Kama zimekamatwa na wakuu wa Giza wa ukoo,familia,eneo naloishi au mtaa, Kama fikra zangu zimekamatwa kupitia madhabahu yoyote ile, iwe ardhini angani
baharini au chini ya bahari, Baba kama fikra zangu zipo Kwa malkia wa kuzimu, malkia wa bahari, malkia wa anga, Kwa damu ya Yesu ninaachilia damu ya Yesu
huko naachilia damu ya Yesu huko! Kwa mamlaka ya jina la Yesu ninangoa fikra zangu huko kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu. Eee Mungu Baba kama fikra
zangu zimekamatwa kwa wakuu wa anga, Jeshi la pepo wabaya wa ukoo/ familia, eneo au mtaa! Kama fikra zangu ziliwahi peperusha kwa upepo wa baharini, au
zimedakwa na waganga wa kienyeji, au zimedakwa katika kazi niliyowahi kufanya au ninanayofanya, biashara, nyumba nayoishi, sehemu ya ibilisi niliyowahi
abudu kwa kutokujua au kujua, mitandao ya kijamii, kwa damu ya Yesu ninanyunyiza hii damu ambayo asili yake ni MUNGU katika damu ya Yesu wewe
fikra zangu ninakungoa sasa ninakungoa sasa kwa damu ya Yesu katika jina la Yesu Kristo. Fikra zangu zilipokamatwa kwenye roho za familia, zilizokamatwa kwa
kupokea zawadi, zilizokamatwa mahali nilipowahi kutoa msaada, au fedha kwa mtu, au popote zilipo fikra zangu zilipotekwa nazinasua sasa kwa damu ya
Yesu, kwa damu ya Yesu Kwa damu ya Yesu Kristo katika jina la Yesu popote Bwana fikra zangu zilipopandwa nazingoa kwa damu ya Yesu. Damu ya Kimbingu,
Damu inenayo mema juu yangu inene mema sasa juu ya fikra zangu, navunja mafundo yote, navunja Giza, navunja vifungo vyote katika fikra. Navunja tanzi,
navunjwa kongwa, navunja viambaza, navunja mashataka, navunja hukumu, navunja magereza, katika fikra zamu kwa damu ya Yesu kwa damu ya Yesu kwa
damu ya Yesu. Baba wa mbinguni katika jina la Yesu na kwa damu ya Yesu sawasawa na ufunuo 5:9 Baba ninanunua fikra zangu kwa damu ya Yesu pale
zilipokwama hayo maarifa yaliyoondolewa na ibilisi yakasabisha Mimi kukwama nanunua kwa damu ya Yesu. Fikra za kazi, fikra za biashara, fikra
za mambo ya uchumba, fikra za miradi, fikra ya jinsi ya kupanga matumizi ya pesa, Fikra zangu mahali zilipokwama zikaleta matatizo Leo nanunua kwa damu Yesu.
Fikra katika ndoa, fikra katika Uwekezaji, fikra za kujenga, fikra za za kumiliki Mali, fikra za utajiri, fikra za huduma, fikra za ibada, fikra za kumtumikia Mungu. Bwana
ninakukabithi fikra zangu uziamshe, uzitembeze, uzinasue mahali zilipokwama, nianze kuona mwanga, nianze kuona nuru. Kwa damu ya Yesu,
kwa damu ya Yesu! Kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu Kristo. ROHO MTAKATIFU nakukabithi fikra zangu kwa damu ya Yesu ukatende zaidi ninavyoomba
au zaidi ninavyovifikiri unipe maarifa ya kunisaidia kwa ajili ya ufalme wa Mungu, na maisha Yangu binafsi kwa damu ya Yesu, Kwa damu ya Yesu, Kwa damu ya
Yesu. Mungu Baba nakushukuru kwa kuwa utaenda kufanya zaidi niombavyo na zaidi nifikiriavyo kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu Kristo nimeomba Amen.
*Rudia Mara 7 kila siku, fanya maombi haya kwa mda wa siku 7. UTAONA MABADILIKO MAKUBWA.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Hakika hii blog ni kwa ajili yangu. Usiache mwalim endelea Kutufundisha kwa njia hii hii nzur sana zaid ya video au audio napenda kusoma ili niwe narudia Rudia mpaka naelewa
ReplyDeleteUbarikiwe sana kwa mafundisho nimeyapenda na nimejifunza
ReplyDeleteAmina
ReplyDelete