MFAHAMU ROHO MTAKATIFU VIZURI ILI UPATE MSAADA KATIKA NJIA ZAKO ZOTE

BWANA YESU ASIFIWE SANA!

nilitamani tuzungumze habari za Roho Mtakatifu kwa undani tuangalie vitabu vinavyoelezea Roho Mtakatifu katika biblia

tuangalie watu waliowahi kujazwa roho Mtakatifu. Na kutembea na Roho Mtakatifu. Jinsi ya kusikia Roho Mtakatifu. Je unajua kikanuni

unaweza kuomba ujazo Roho Mtakatifu ukajazwa hata chumbani kwako? Hasara za kutoongozwa na Roho Mtakatifu! Faida za Roho

Mtakatifu. Wangapi wangependa tushirikiane? Kuna vitu viwili vinavyofanya wakristo washindwe vita moja kutokutumia damu ya

Yesu kwa usahihi, ya pili, kuomba bila roho Mtakatifu kumpa roho Mtakatifu asilimia chache ya maisha .

#Tuangalie kwanini kanisa la sasa linaomba sana kuliko kanisa la zamani. Lakini sasa hakuna matokeo makubwa kama ya

zamani! What is the different? Wao walikuwa na Roho Mtakatifu na sisi tunaye! Inakuwaje kuwaje? hayo ni mambo ya kuyangalia.

Jinsi unavyojifunza habari za Roho Mtakatifu ndivyo jinsi unamvutia aje kwako! Ndivyo jinsi atajifunua kwako zaidi.

# Kitabu cha Matendo ya mitume kimeelezea habari ya Roho Mtakatifu. HIVI UNAJUA KUNA TOFAUTI YA UJAZO WA ROHO

MTAKATIFU? NA UWEZO AU NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU. UNAJUA KUNA TOFAUTI KATI YA

ROHO YAKO NA ROHOMTAKATIFU?

#MASWALI MUHIMU YA KUJIULIZA; je Roho Mtakatifu yupo na mtu kila mahali kila saa? Inakuwaje mtu anajazwa Roho

Mtakatifu alafu bado anatenda dhambi? Ushawahi jiuliza haya maswali?!

# Roho Mtakatifu mwenyewe atusaidia atupe jicho la Tatu tusome maandiko alafu tujifunze! Kupitia watu au mazingira aliyofanya nao
kazi.

# Tuanze kwanza kuangalia mtu aliyekuwa kama wewe alikuwa na imani, alikuwa na utayari, yani kuusu Yesu ilikuwa umwambii lolote
alikuwa tayari kutembea hata juu ya maji alishuhudia matendo makuu yote ya Yesu aliyoyafanya. Alikuwa tayari hata kuuwa kwa ajili ya Yesu.

Alikuwa tayari kufanya lolote kuacha yote kwa ajili ya Yesu alijitoa kwa ajili ya Yesu alikuwa pembeni ya Yesu mda wote. Yani

kuhusu Yesu humwambii
kitu. Na Yesu alimfundisha tena katika wanafunzi ambao Yesu alikuwa akiwachukua pembeni

kudisscuss mambo mengine

pembeni yeye alikuwa mwanafunzi mmoja wapo. Lakini unajua kilichotokea pamoja na yote Petro alimkana Yesu. Nachotaka uone

tuangalie behind the scene nini kilimsabisha Petro kumkana Yesu? Why alimkana! Kwanini Yesu alijua kuwa atamkana? Je hizi habari

alizipata wap? Wakati naye alikuwa Kama sisi tuu binadamu. Tuangalie word-word translation.

Matayo 26:31
. Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.

33. Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe.

34. Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu.

35. Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe. Na wanafunzi wote wakasema vivyo hivyo.

47 . Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Thenashara akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.

51. Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

58. Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.

69. Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya.

70. Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo.

71. Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti.

72. Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.

73. Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.

74. Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.

75. Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

# Nataka umfuatilie Petro hapa kwa makini maneno ya Petro;

1.wajapochukizwa wote kwa ajili yako mimi sitachukizwa kamwe

2.ijaponipasa kufa nawe,sitakukana wote wakajibu hivyo hivyo

3.Petro alinyoosha  mkono wake akaufuta upanga akamkata mmoja wao sikio

4.Kijakazi akasema wewe ni mmoja Wao na Yesu Petro akakana

5.Mwanamke mwingine akamwambia ivyo ivyo Petro akakana vile vile

6.wengine walimfuata wakamwambia ivyo ivyo Petro akaendelea kukana tena hakukana tuu Bali alilaani kabisa.

# unaweza mcheka Petro lakini unaweza kuwa na imani ya kungoa milima! Unaweza kuwa ni jasiri but subiri jaribu lije la kukutingisha.

Petro alipigwa na roho ya ibilisi ndani yake Ile kuona kwamba uyu ni Yesu aliyefufua watu Leo hii anazalilishwa anapigwa namna hii!

Nilitembea juu ya maji kwa sababu yake Leo anapigwa unajua ile ndani yake iliyeyusha imani yake, iliyeyusha moyo wako, iliyeyusha

ujasiri wake, angalia maneno aliyoyasema kule juu. "Wajapokukana wote Mimi sitakukana, hata ikibidi kufa Mimi

nitakufa na wewe" lakini hata Yesu hajafa ile mwanzo tuu Petro kakana tena mpaka kalaani. Unajua huwa inatokea hata kwetu, unaweza kuwa

mjasiri. Unaweza kuwa na imani lakini subiri sasa jaribu lije "mioyo huwa inayeyuka"  kwanini huwa inayeyuka ni sababu vita vyetu sisi

si vya damu na nyama. Kwa iyo ili kupigana na roho zinazoleta hofu ya kufa lazima lazima na wewe usaidiwe na Roho Mtakatifu. Kwa

iyo bila Roho Mtakatifu haijalishi unajua biblia kiasi gani au unaweza kuomba masaa 3 bila hata kunywa maji. Au kufunga Tatu kavu. Wewe

subiri jaribu lije ndo utajua nini maana ya Roho Mtakatifu. Huwezi mwenyewe watu wengi wanashindwa vita vingi sababu

wanatumia akili zao wenyewe kuomba, hakuna ushirika Kati Yao na Roho Mtakatifu. Unakurupuka na kuanza kuvunja kupigana na

shetani. Kumbe shetani amekaa kwenye mguu wako. Sasa tuangalie Petro baada ya kujazwa uwezo utokao juu ilikuwaje?

Matendo ya Mitume 1

4. Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;

5 . ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.

6 . Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme?

7 . Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

8 . Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

# Sasa tuangalie nini kilitokea baada ya kujazwa ROHO MTAKATIFU, TUANGALIE YULE PETRO ALIYEMKANA YESU MARA TATU NA KULAANI.

Matendo ya Mitume 2

1. Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2 . Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.
3 . Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4 . Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Uyu ni Petro sasa aliyejaa Roho Mtakatifu angalia sasa hapa. 👇🏾

Matendo ya Mitume 3

1. Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa.

2 . Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.

3 . Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.

4 . Na Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, akasema, Tutazame sisi.

6 . Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.

7 . Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu.

8 . Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu Mungu.

9 . Watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu.

10 . Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.

12 . Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu  sisi?

#  Petro mwenye ujasiri wa Roho Mtakatifu ndani yake! Alivyokuwa anabishana na Masadukayo amekuwa jasiri sasa!

Matendo ya Mitume 4

1. Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na akida wa hekalu na Masadukayo wakawatokea,

2 . wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.

3 . Wakawakamata, wakawaweka gerezani hata asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni.

7 . Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya?

8 . Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli,

9 . kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa,

10 . jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.

11 . Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.

12 . Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

13 . Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.

# Masadukayo walipoona ujasiri wa Petro Wakatambua kuwa Yesu Yuko pomoja na Petro.

# SASA TUANGALIE ISHARA KUU NA MAAJABU ALIYOYAFANYA ROHO MTAKATIFU. KUPITIA WATU MBALIMBALI KATIKA BIBLIA.

#watu wengi wanaangalia matendo aliyoyafanya Yesu ila wanachosahau ni kwamba Yesu aliyafanya yote nayo baada ya

kujazwa Roho Mtakatifu. Miujiza yote hiyo ilifanywa na Roho Mtakatifu. Na Aliyemfufua Yesu kaburini ni Roho Mtakatifu. Ngoja

nikuonyeshe tukio moja la ajabu Sana la Roho Mtakatifu. Sababu Yesu kabla ya Roho Mtakatifu alikuwa wa kawaida tuu. Alikuwa

fundi seremala.  Watu walimjua tuu kama mtoto wa Yusuph. Lakini alipojazwa ndipo dunia sasa ikaanza kumjua Yesu ni nani.

Luka 3

21. Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;

22 . Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

23 . Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,

# sasa tuangalie matukio ya Yesu baada ya kujazwa Roho Mtakatifu

Luka 4

1. Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,

2 . akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa.

14 . Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.

# Hapa nakuonyesha mwenyewe uone kwa macho yako nini kilitokea ambacho si cha kawaida baada Yesu kujazwa Roho Mtakatifu

1.Alifunga siku arobaini bila kula na kunywa chunguza historia Yote agano la kale Musa naye aliwahi funga siku Arobaini for

sure aliongozwa na Roho Mtakatifu. Nabii Eliya naye alifunga siku arobaini. Kuna Mtu mmoja aliwahi nichallenge akaniambia wewe

umeokoka je waweza funga siku arobaini bila kula na kunywa kama Yesu?

Nikamwambia nikiongozwa na Roho Mtakatifu nitafunga. Maana
ataniongoza na kuniwezesha.

2.Habari zake zikaenea Galilaya na nchi za kandokando? Swali la kujiuliza nani alizihabarisha? Huo

umaarufu wa gafla ulitoka wapi? Yesu kafunga tuu halafu habari zake zikaenea nani kazieneza? Ushawaji .
jiuliza? Uyu ni Roho Mtakatifu ndio

alizieneza yani alimfanya Yesu kuwa maarufu.

# TUENDELEE NAKUPITISHA KATIKA MATUKIO YOTE MAKUU KATIKA BIBLIA ILI UJUE YA KWAMBA ROHO MTAKATIFU NDIO

KILA KITU. KUWA HUWEZI BILA UYO KAMA YESU ALIONGOZWA NAYE SEMBUSE WEWE!

Mwanzo 1

1. Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2 . Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

3 . Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

# Roho wa Mungu alikuwepo juu ya maji! Neno lilipotamkwa ROHO MTAKATIFU AKAFYATUA NURU. Roho Mtakatifu ndio mfyatuaji wa

vitu. Kwa iyo hii ikukumbushe ya kuwa Kila mara Roho Mtakatifu anapokuwa lazima uachilie neno la Mungu kimaombi unapoachilia

Ndipo Roho wa Mungu atafyatua. Kwa iyo haitoshi kuwa na neno la Mungu pekee au kuwa na damu ya Yesu pekee maana

mtendaji ni Roho Mtakatifu yeye ndio anayesababisha mambo yatokee.

# ROHO MTAKATIFU ALIVYOFANYA MAAJABU NA SAMSON

Waamuzi 13

3. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume.

5 . kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.

24 . Basi yule mwanamke akamzaa mtoto mwanamume akamwita jina lake Samsoni, mtoto huyu akakua, Bwana akambarikia.

25 . Roho ya Bwana ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.

# Samson alijazwa Roho Mtakatifu toka tumboni mwa mama yake. Samson alikuwa akiangusha miti alikuwa na uwezo wa kupigana na

wafilisti hata 1000- 2000 na akawauwa wote lakini cha kujiuliza alipata wapi izo nguvu? jibu ni raisi haikuwa yeye yule alikuwa Roho

Mtakatifu! Kila Mara hatari ilipokuwa inakuja roho Mtakatifu alikuwa anamjaza nguvu zake. Kuna mahali nilisikia shuhuda Mama

mmoja alipaki gari nyumbani kwake baada ya kupaki akaingia ndani kisha akaja mtoto akawa anacheza nyuma ya gari lile gari likaanza

kurudi nyuma alivyoona vile Kuna nguvu zikamuingia anaenda akashika gari kwa nyuma akaliinua akaliweka pembeni. Baada ya tukio

lile akashika mdomo akasema Hee! Nimeinua gari? MUNGU AKAMWAMBIA nilitaka nikuonyeshe uwezo wa Roho Mtakatifu! Kama

ukijifunza kumtegemea katika kila jambo. Leo hatuhitaji nguvu za kama Samson kupigana lakini tunamutaji Roho Mtakatifu. Mtu

mmoja kuuwa zaidi ya wafilisti 5000 tena kwa Mara moja au kwa lisaa tuu uyo hawezi kuwa binadamu wa kawaida. Ni Roho Mtakatifu

#TUANGALIE ROHO MTAKATIFU ALIVYOFANYA MAAJABU NA DAUDI

1 Samueli 16

13. Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

# Angalia baada ya tuu Roho wa Bwana kumjia ndipo akaanza kuuwa Simba na Dubu kule msituni. Ndipo akapata ujasiri wa kupigana na

Goliath watu wanaangalia Yale matukio tuu lakini hawangalii nini kilisababisha. Nini kilimsukuma Daudi. Ngoja tuangalie hayo matukio kidogo.

1 Samueli 17

32. Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.

34 . Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,

35 . mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.

36 . Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.

37 . Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe.

46 . Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

49 . Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.

#Unaona huo ujasiri aliokuwa nao Daudi baada ya Roho ya Bwana kumjilia kwa nguvu unaona nguvu hizo zilivyokuwa zikifanya kazi

ndani yake. Roho wa Mungu aliyetembea na Musa, Na Yesu, aliyetembea na Eliya aliyetembea na Samson aliyembea na Daudi ni

yuleyule kwenye mwanzo 1, ndo uyo uyo aliyefyatua Nuru, yeye hawezekaniki, hashindwi, yeye anaweza kila kitu. Na wala hayuko

mbali. Na ukimtaka ni kiasi cha wewe kukiri unamtaka. Tayari Yesu ashamtoa yupo tayari kwa yoyote aliye tayari. Na anayejaza watu

Roho Mtakatifu ni Yesu. Si Mtumishi hakuna mwenye uwezo wa kumjaza mtu roho Mtakatifu. Ivyo kiu yako ndio itakusababisha

Yesu akujaze na hawezi kukujaza kama hauko tayari au huna kiu. Na kiu utaipata utakapoendelea kusikia habari zake Roho Mtakatifu. Kuna

matukio zaidi ya 20 tutapita nayo kwa ufupi ili uwone nini Roho Mtakatifu alifanya na Daudi katika mazingira ya kawaida kabisa na

jinsi walivyoshirikiana katika maisha ya kawaida. Kabisa ya kila siku. Endelea Ku diggest huku tunaendelea.

#TUNAWEZA KUONA KAZI ZA ROHO MTAKATIFU JUU YA DAUDI NA JINSI ALIVYOPAMBANA NA VIKWAZO NA ROHO WA MUNGU

ALIVYOMSHINDIA. HAIJALISHI UNAJUA MAMBO MANGAPI UKO FITI KIASI GANI BILA ROHO MTAKATIFU KATIKA JAMBO

LOLOTE UTAANGUKA TUU!

# Naenda Weka matukio kwa ufupi na ref ya neno linapopatikana kwa ufupi utakuwa unapitia mwenyewe katika watu waliofanikiwa Sana ni

Mfalme Daudi lakini ni sababu mahusiano yake na Roho MTAKATIFU YALIKUWA YA HALI YA JUU.  tunaendelea na somo letu!

MATUKIO YENYEWE YA ROHO MTAKATIFU.

# 1. Roho Mtakatifu alitengeneza tukio la kumtambulisha Daudi Kwa Sauli na Wana wa Israeli. Kama jinsi alivyomtambulisha YESU bila hata

Yesu kujua. Roho Mtakatifu kazi yake kukufanya ufahamike uwe na kibali. Samweli 1, 16-17

#. 2 Roho Mtakatifu alimtengenezea Daudi mazingira ya kuishi nyumbani kwa Mfalme, ikamlazimu Mfalme Sauli amwombe Baba yake Daudi

Mzee Yese. ROHO MTAKATIFU NI MTENGENEZAJI MAZINGIRA alimtoa Daudi toka kwenye

kuchunga mifugo kwenye mapori mpaka nyumbani kwa Mfalme. Samweli 1, 16-22-23

#. 3 Roho Mtakatifu alimtengenezea Daudi kibali Katika mioyo ya watu! Na kwa Mfalme,Kwa kufanya tukio flani soma mwenyewe. Kwa iyo

kukubalika mioyoni mwa watu si kwa kujipendekeza mwombe Roho Mtakatifu akusaidie. Usitumie akili zako mwenyewe Samweli 1, 18-7-8

#.4 Roho Mtakatifu alimjengea Daudi ujasiri katika mazingira ya kule porini akawa jasiri, kuwa jasiri si lazima uwe Boss, au cheo au

ufanikiwe no! ukiwa na Roho Mtakatifu atakufanya jasiri! Kuna watu wanasema ukiwa Una pesa unakuwa unajiamini si kweli. Sauli

alikuwa Mfalme lakini alimwogopa Goliath, mpaka kuja kusaidiwa na Daudi. Samweli 1, 17-33-37

#.5 Roho Mtakatifu alimfundisha Daudi vita kwa iyo kama alimfundisha vita inamaana pia alimfundisha uvumilivu wakati wa

shida,alimfundisha kukokukata tamaa, alimfundisha kushinda na sio kushindwa. Ukiwa na Roho

Mtakatifu kabla hujakutana na vita tayari anakuwa alishakukuandaa. Samweli 1, 17-33-37

#. 6 Roho Mtakatifu alitumia mwili wa Daudi kufanya vita, jiulize inakuwaje kijiwe kidogo kitoboe paji la uso? Daudi alipata wapi ujasiri?

Unapokuwa na Roho Mtakatifu atakupigania vita atatumia mwili wako na Roho yako atafanya vita na mshindi utaonekana wewe na

utukufu utarudi kwa Yesu, mwili ukichoka anautia nguvu, anafanya kila kitu anakuwekea mazingira yote vizuri ili umpige adui. Ni Hatari Sana
kwenda vitani na huku unajua kabisa Roho Mtakatifu ilo eneo

hayupo. Hakikisha Unapoenda vitani Roho Mtakatifu yupo on tayari. Samweli 1, 17- 45-46, 49-51

#.7 Roho Mtakatifu alimsaidia na kumwezesha Daudi kutokukata tamaa! Mazingira ya Daudi yalikuwa ya upinzani Sana! Ingekuwa raisi

kukata tamaa na kurudi nyuma Kuna wakati mwingine alikuwa akimkimbia sauli kwenda kujificha aliishi kwa hofu lakini Roho

Mtakatifu alimsaidia always aliendelea mbele hakuangalia mazingira yanayomzunguka

aliangalia kule anakoelekea. Kwa iyo hakukata tamaa. Samweli 1, 17- 25-30

#. 9 Roho Mtakatifu hapa anamsaidia Daudi kufyatua mtego au kutegua mtego sauli aliomtegea alimtengenezea hila Daudi ili akafe

vitani! Lakini badala yake Roho Mtakatifu akaingia katika huo mtego na akautegua, aijalishi ushaingia katika shimo lakini kama

unaroho Mtakatifu yeye atakutoa huko salama. kazi yake yeye pia ni kutegua mitego.mitego ya ibilisi ni mingi mno bila Roho Mtakatifu

nakuambia utaiingia yote na itakuangamiza. Vipo vitu au mambo yaonekanayo mazuri lakini mwisho wake ni mauti ni mitego. Samweli 1, 18-25-29

#. 10 Roho Mtakatifu alimtengenezea Daudi sifa mbele za watu. Alitengeneza mazingira ya Daudi kupata sifa mbele ya Sauli. Ni Moja ya kazi yake pia. Samweli 1, 18-30

#. 11 Roho Mtakatifu hapa anamlazimisha adui ampe siri Daudi. Roho Mtakatifu alimbana Jonathan awe rafiki wa Daudi! Kana

kwamba haitoshi akambana mtoto wa kike wa Sauli akampenda Daudi badae tutakuona alimuoa uyo binti ya Sauli kwa iyo Dada Mtu na

Shemeji mtu wote hawajiwezi kwa Daudi. Roho Mtakatifu anaweza lazimisha adui yako akupende au rafiki wa adui yako akupende na

akupe siri. Nilisoma hapa nikacheka Sana. Soma mwenyewe. Samweli 1, 19- 1-5

#. 12 Roho Mtakatifu anamsaidia Daudi kufanya vita kitu ambacho Sauli-Mfalme kilimshinda! Roho Mtakatifu akitaka amfadhaishe adui
yako anakupa kitu ambacho yeye Hana, au hawezi kuvifanya wewe anakupa uwezo wa kufanya wengine anawaondolea uwezo wa kufanya. Samweli 1, 19-8

#. 13 Roho Mtakatifu hapa aliwageuza watu waliotumwa kumkamata Daudi kuwa manabii, badala ya kumkamata Daudi

wakifika sehemu Daudi yupo wale watu wakaanza kutabiri. Lilitumwa group la 1, roho ya utabiri ikawaingia wote nao wakaanza

kutabiri, group la pili, la tatu ivyo ivyo mwisho wake Sauli akaamua kwenda mwenyewe naye pia Roho ya kutabiri ikamkamata biblia

inasema alitabiri mpaka akavua nguo zote akalala uchi chini akiwa hajiwezi. Wote waliotumwa kumkamata Daudi wakifika huko

Roho ya unabii inawaingia. Unajua Roho Mtakatifu anaweza kucheza adui yako kumfanya kituko wala hatumii nguvu. Soma mwenyewe Samweli 1, 19-20-21,19-23-24

# NACHOTAKA KUKUONYESHA HAPA AS LONG AS MUNGU KAKUNYOOSHEA KIDOLE KAKUITA KATIKA NAFASI YAKO KAZINI,

BIASHARA, HUDUMA, FAMILIA, UKOO, NDOA lazima shetani atakupinga tofauti ya Mtu anayepigana vita na Roho

Mtakatifu. Na anayepigana kwa akili zake mwenyewe always anayepigana mwenyewe atashindwa atakata tamaa na

ataacha. Lakini uyu wa ROHO Mtakatifu kukata tamaa kupo na kuchoka kupo but haitachukua siku au wiki tayari atatiwa nguvu na

ataendelea. Usifikiri Daudi hakupata shida Daudi alipata shida Sana. Na hakika kama si Roho Mtakatifu kuwa pamoja naye angeweza

kusema MUNGU kama ni huo ufalme basi. Mimi siwezi tena. Nabii Eliya alipochoka alienda chini ya mti akamwambia Mungu Mimi si bora

kuliko hao wengine ni bora uchukue Roho yangu na alitishiwa na mwanamke tuu. Lakini ukichunguza vizuri Eliya mwili ulikuwa umechoka

maana aliwachinja Mabaali 400 kwa mkono wake usifikiri ni kitu raisi sasa ukishachoka huwa akili inaweza amua lolote shetani

alipoligundua ilo akatumia vitisho. Eliya alikuwa amechoka alafu ana njaa. Ndo mana yule malaika akaja akamwamsha akamwambia kula ,

na unywe maji kisha akalala tena. Kisha akamwamsha tena akamwambia kula kisha akalala tena alipoamka ndipo akakutana na

Mungu akamuuliza  unafanya nini hapa Eliya? Kwa iyo Daudi alikutana na mambo magumu Sana. Lakini kilichosababisha ashinde nisababu

Yale mafuta aliyowekwa kichwani kisha Roho wa Mungu akamjilia kwake kwa nguvu lakini kama si ivyo angalikufa kule msituni na wale
Simba. Kilichomsabisha aende mbali kiasi hiki ni Roho Mtakatifu.

# TUANGALIE MAZINGIRA MAGUMU YA DAUDI ALAFU UJIULIZE ALIVUKAJE KAMA SIO ROHO MTAKATIFU

1. Daudi alichukiwa na ndugu zake baada tuu ya kupakwa mafuta na Samweli.Hii inadhibitika Kaka yake

alipomfokea Daudi akamwambia Mimi nakujua wewe unakiburi samweli 1,17-28-30

2.Daudi alikoswakoswa kuwawa si chini ya Mara moja

3.Daudi alienda kujificha kwa kumuogopa Sauli aliishi msituni kama mkimbizi

4.Daudi alikuwa ni mtu wa kutegeshewa mitego tena ya mautini. Au kufanyiwa Hila ili afe

5.Daudi alitengwa na ndugu hata na Baba yake angalia baada ya kupakwa mafuta alirudi msituni kuchunga mifugo.

6. Kwa Sababu ya kuishi kwa hofu na kukimbia Daudi hakuwa huru. Kila wakati akili yake iliwaza vita.

7. Kuna sehemu Daudi alijifanya chizi ili akwepe kuuwawa. Hii tunasema ilimfosi aishi maisha ya maigizo yani siyo aliyoyataka yeye

8. Daudi alikuwa na wake wawili. Sababu ya maisha yake familia yake ilikuwa haina mda mzuri na Daudi

# HAKUNA MATESO KUISHI MAZINGIRA YA HOFU YA KUOGOPA KUWAWA, HUWEZI KULA UKASHIBA, WALA HUWEZI NENEPA,

HUNA AMANI, HUNA FURAHA, katika mazingira ya kawaida ni mazingira ya kukata tamaa Sana! Kuchoka vita, pengine hata

kutokuona umuhimu wa kuishi maana huoni raha ya maisha. Kusongwa na maadui namna hii! Kuanzia familia yako kutokukubali

kukuheshimu ni mazingira magumu. SIJUI WEWE UNAMAZINGIRA GANI BUT NACHOJUA BILA UYU ROHO MTAKATIFU HUWEZI SHINDA.

PETRO ALIAPA MWISHOWE AKAMKANA YESU NA KULAANI. wanafunzi wa Yesu waliapa kama Petro lakini Yesu alipoanza kupigwa

walikimbia wengine wakatoka uchi kabisa. Sijui ushajaribu vitu vingapi na ukashindwa. Jua ya kwamba bila uyu BWANA MKUBWA HUWEZI

SHINDA VITA YOYOTE UNAWEZA UKAMJUA LAKINI UKAWA HUNA USHIRIKA NAYE. WATU WENGI

HATUNA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU.

Na tunafikiri ukishanena kwa Lugha basi! Ushirika wa Roho Mtakatifu ni mpaka kwenye maamuzi madogo madogo. Na anapokushauri kitu

ukimpinga au ukidharau au usipofuata anakaa kimya matokeo yake ndo tunapata maanguko makubwa katika maisha. .

# KUSUDI USIANGUKE AU USISHINDWE JAMBO LOLOTE LILE LAZIMA ROHO MTAKATIFU AKUSHAURI, AU KUKUFUNDISHA

NA KUKUELEKEZA NA WEWE UFUATE KINYUME NA HAPO UTAANGUKA TUU. WEWE HAUPO ROHONI KAMA ROHO MTAKATIFU

YEYE ANAONA KESHO NA ANAONA ADUI YOTE ANAYOYAFANYA NA ALIYOKUPANGIA.

# PAMOJA NA YESU KUWA MWANA WA MUNGU HAKUANZA KAZI BILA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU, BIBLIA INATUAMBIA

BAADA TUU YA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU NDIPO YESU HABARI ZAKE ZIKAENEA SANA, NDIPO AKAANZA KAZI. Wanafunzi wa Yesu

walifundishwa na Yesu na wakapewa kufanya mazoezi, na wakafanikiwa kutoa pepo, na walishuhudia mambo mengine yani

walimjua Yesu vilivyo lakini akaawambia kaeni humu msitoke mpaka atakapo wajilia Roho Mtakatifu. Kwanini Yesu

asingewaruusu tuu waanze kazi na walikuwa wameiva? YESU ALIANGALIA UPINZANI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,

AKAWANGALIA WANAFUNZI WAKE AKAKUMBUKA HAWA WALINIKIMBIA NILIPOKAMATWA AKAJUA NISIPOTIA ROHO YANGU

NDANI YAO , hawa hawawezi watachoka! Hawawezi upinzani wa ibilisi pasipo uyu Roho Mtakatifu. Na ndio maana kanisa la leo tuna

matokea madogo ingawa tunaomba Sana na tunajifunza Sana ni Sababu tumemdharau Roho Mtakatifu, tumemzoea tunamchukulia

kawaida! Hatumchukulii ndio msaada wa pekee. Kama  Yesu alimueshimu na kumpisha ili aje

atusaidie basi ujue bila Roho Mtakatifu huwezi lolote.

# BAADAE TUTAANGALIA WATU WALIMFUATA ROHO MTAKATIFU WAKAFANIKIWA. NA WATU WASIOMTII WAKAANGUKA. KATIKA BIBLIA...

# Roho Mtakatifu anajua wakati mzuri wa wewe kufanikiwa, Roho Mtakatifu anajua safari uliyoanza kama itaishia vizuri au laah! Roho

Mtakatifu anajua hata kuuza na kununua, Roho Mtakatifu huwa anafundisha watu hata jinsi ya kuongea, Roho Mtakatifu

atakushauri hata jinsi ya kuvaa. ROHO MTAKATIFU kazi yake ni kutatua mambo yaliyoshindakana yote yeye anayo majibu yake tatizo

ushirika wetu na Roho Mtakatifu tumeuwekea mipaka! Tumemchukulia Roho Mtakatifu ni wa kunena kwa lugha tuu. Ni wa

kanisani tuu, ni wakutoa mapepo tuu, ni wakuhubiri tuu. Kitu ambacho kanisa la Leo limesahau hawajui kuwa Roho Mtakatifu yupo hata nje

ya kanisa, yupo chumbani yupo kwenye gari yupo sebleni yupo hata bafuni kwako. Roho Mtakatifu atakushauri hata ambayo hukuuliza.

Kiwango cha mafanikio yako na Roho Mtakatifu ndicho kiwango chako, cha kufanikiwa. Wengi Yale mambo tunayotaka ndiyo

tunamuuliza roho Mtakatifu lakini Yale ya hatarishi akitushauri huwa hatutaki. Roho Mtakatifu anatakiwa apewe 100% ya maisha yako. Ndipo

ahadi za Mungu utaziona. Mtu mwingine anakurupuka kufanya vitu bila kumuuliza Roho Mtakatifu matokeo yake anadumbukia kwenye
shimo. Unasema  Mtumishi mbona ninamshirikisha? Sikiza Paulo wakina Petro Mfalme Daudi wakina Musa wote walifanikiwa Sana

walimpa nafasi Roho Mtakatifu 100% sio 2% , huwezi taka mafanikio 100% ukapata wakati ushirika wako na Roho Mtakatifu ni 2%, ni kweli

uliumbwa na akili, uliumbwa kuwa huru na uliumbwa kufanya maamuzi uko huru. Lakini pia kufanya maamuzi sahihi huwezi mwenyewe

kuwa sahihi ni mpaka Roho Mtakatifu. Kiwango chako cha ushirika naye ndicho kiwango chako cha kufanikiwa. Ni mahusiano

yanajengwa kidogokidogo yanaendelea kukua atakufundisha yote. Asimilia 100% ya maanguko ya binadamu yametokana na

kutomsikiza Roho Mtakatifu. Huwezi Nenda popote pasipo huyu BWANA Mkubwa. Wengine wanaona Roho Mtakatifu hajui ivyo wanamua
mpaka kuhama makanisa wanaenda kwa Mtumishi hadi kwa Mtumishi uyu. Nataka nikuambie kitakacho fanya ufanikiwe ni sauti

ya ndani inayokupa maelekezo ya Roho Mtakatifu.

Isaya 63:10
. Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.

# NATAKA NIKUONYESHE KITU KIMOJA KIUKWELI KANISA LIMEMDHARAU SANA ROHO MTAKATIFU, LIMEMUONA NI

MSHAMBA, HAJUI, LIMEMUONA ANACHELEWA KUJIBU MAOMBI YAO, imefikia watu wamewaamini Sana watumishi wa Mungu kuliko

Roho Mtakatifu! Nataka nikuonyeshe kitu kimoja kwenye neno! Roho Mtakatifu akikishauri ukamdharau au usiposikia Roho

Mtakatifu hutoka upande wako alafu anakuwa upande wa adui! Anakupinga ili ukwame! Saa ingine si shetani anayekupinga ni Roho

Mtakatifu ndiye anayekupinga akishakupinga ukishaanguka utarudi nyuma utaanza msikiliza. Mwingine anataka akasome ila

anataka aache kazi. Roho Mtakatifu anamkataza anapiga kelele anamkataza lakini hasikii. Wala hataki anampuuza Roho Mtakatifu

mwisho wake Roho Mtakatifu anakuacha uende kisha anakupinga. Roho Mtakatifu ukimdharau na ukaamua kuendelea mbele na

msimamo wako anahuzunika kisha anageuka adui yako anakupinga. Angalia mwenyewe hayo. Maandiko kama watu wangejua hawawezi bila

uyu Bwana Mkubwa ahadi zote kwenye biblia huwezi zipata kama huna ushirika na utiifu wa Roho Mtakatifu. Mwingine ikifika saa 6

usiku anaanza kuvunja kubomoa kupambana na adui kila mahali ni fireeee fireeee bila kumuuliza Roho Mtakatifu adui kapitia wapi? Viko

vitu vingi tunafanya bila kumuuliza Roho Mtakatifu tumeanza biashara bila ROHO Mtakatifu Tumeingia katika ndoa bila Roho Mtakatifu,

tumeanza kazi bila Roho Mtakatifu, Sasa inatucost tumeanza safari bila Roho Mtakatifu, tumekurupuka kufanya vitu, kununua bila Roho

Mtakatifu. Na sasa ni vilio, tumekuwa wajuaji, saa ingine tumemshushua Roho Mtakatifu, tumemdharau! Kanisa la zamani

lilimuuliza Mungu. Kila kitu. Daudi alifanikiwa Sana Katika ufalme wake lakini alimuuliza Mungu Kila kitu. Ngoja tuangalie. Kidogo habari

za Daudi ushirika wake na Roho Mtakatifu na watu wengine wachache.

1 Samueli 23:2
. Basi Daudi akamwuliza Bwana, kusema, Je! Niende nikawapige hao Wafilisti? Naye Bwana akamwambia Daudi, Nenda ukawapige Wafilisti, na kuuokoa Keila.

# NATAKA UONE KITU HAPO, Daudi alikuwa na upako wa Roho Mtakatifu, alishawahi uwa Simba, Dubu, alishamuuwa Goliath, tena

ashapigana vita huko nyuma akashinda lakini hakukurupuka akamuuliza Mungu Je niende vitani? Sasa angalia baada ya kuuliza

hakwenda alisubiri Mungu ajibu ndipo akaenda, watu wengi wakishamuuliza Roho Mtakatifu Mara moja wasipopata majibu basi

ndo mwanzo na mwisho wa kuuliza. Saa ingine Roho Mtakatifu anataka muwe na mahusiano ya karibu. Sababu mtu unayewasiliana naye

Sana ndiye mnayekuwa na mahusiano mazuri. Anataka uendelee kuuliza keep more asking, wengi wakiuliza Mara Moja

wasipopata majibu wanazira , wanasusa, wanaacha, inatakiwa uendelee kumuuliza Roho Mtakatifu mpaka akujibu. Usianze safari

yoyote bila Roho Mtakatifu, usikubali pressure za kuanza kitu bila Roho Mtakatifu unakapoanza for sure utaanguka! Anayetia izo

pressure ni shetani! Ile point ya kujikuta nifanye au nimsubiri Roho Mtakatifu? hapo ndo wengi wanachanganyikiwa nami

nakuambia msubiri Roho Mtakatifu yeye achelewi. Yeye ndo kila kitu hata hicho unachokimbilia huwezi bila yeye.

1 Samueli 23:4
. Basi Daudi akamwuliza Bwana tena, Naye Bwana akamjibu, akasema, Ondoka, ukashukie Keila; kwa kuwa nitawatia hao Wafilisti mikononi mwako.

# Umeona hapo?👆🏾 Daudi aliuliza kila kitu hakufanya chochote bila kumuuliza Mungu. Huu ndio
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU NINAOUZUNGUMZIA HAPA.

1 Samueli 23:10

. Ndipo Daudi akasema, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, mimi mtumwa wako nimesikia hakika ya kuwa Sauli anataka kuja huku Keila, ili kuuharibu mji kwa ajili yangu.

11 . Je! Watu wa Keila watanitoa, nitiwe mkononi mwake? Je! Sauli atashuka, kama mtumwa wako alivyosikia? Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye Bwana akamjibu, Atashuka.

12 . Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? Bwana akasema, Watakutia.

# umeona hapo juu Daudi he was asking Everything sasa sio kuuliza tuu Bali na kutii aliyoambiwa. Maana kuuliza ni jambo la kwanza

alafu kutii ni jambo la pili. Bwana Wa Israeli nakusihi umwambie mtumwa wako! Daudi aliuliza kwa adabu zote kwa heshima! Kuna

wakati mwingine unajua unaweza mfuata Roho Mtakatifu kwa hasira, ukifanya hivyo usitegemee Roho Mtakatifu kukujibu! Daudi alikuwa

mtiifu mwenye subira alikuwa Hana haraka  na Mungu. Leo sisi haraka inatoka wap?  Unataka ukimuuliza Roho Mtakatifu akujibu sasa hivi.

Aiendi ivyo! Kumbuka Roho Mtakatifu ni Mungu. Kabisa. Ivyo usijisahau ukafikiri unaongea na binadamu mwenzako. Angalia

maongezi ya Daudi anajishusha anasema "Mimi mtumwa wako" Kuna jinsi pia ya kumfuata Roho Mtakatifu. Usimfuate Roho

Mtakatifu na hasira, usimfuate Roho Mtakatifu kwa kumlaumu, usimuharakishe Roho Mtakatifu, jishushe jua kuwa unaongea na

Mungu, usianze kuwauliza binadamu kisha ukishindwa ndo umfuate Roho Mtakatifu no! Hii ni dharau kwa Mungu manake

umemfanya Mungu wa pili, always unapomfuata Roho Mtakatifu mtambue Roho Mtakatifu na umwambie wewe hujui kitu na kuwa

unamtegemea na unamwamini. NA USIFANYE KWAMBA BAADA YA ILO SWALI UMUHITAJI TENA NO. weka mazingira ya kuwa unamuhitaji yeye
kila saa na kuliko kitu chochote. Alafu sio kila saa upeleke maswali saa ingine mwambie Roho Mtakatifu nataka tupige stori. Saa

inginee msifie muelezee kuwa unatambua uwepo wake. Na unajua pale na pale ni yeye alikusaidia.

# WATU WENGI WANA BAD COMMUNICATION NA ROHO MTAKATATIFU,ALAFU WANATEGEMEA GOOD

RELATIONSHIP! haiendi ivyo!

# GOOD COMMUNICATION BRINGS GOOD RELATIONSHIP WITH HOLLY SPIRIT, Muhimu kujua uyu ni MUNGU kabisa kama huna

mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu basi hakuna mwingine wa kumlaumu wa kwanza ni wewe wala si shetani. Sababu shetani

anashawishi tuu wewe ndio uliyeamua kutenda. Katika maombi yako ya Kila siku mwambie Roho Mtakatifu nataka kuwa na

mahusiano mazuri naomba nisaidie. Alafu mtu anayetaka msaada anaenda kiuhitaji si kiujuaji! Always mwambie Roho Mtakatifu I'm

nothing! Sijui kitu wala siwezi chochote naomba unisaidie tanguliza hayo maneno. Lazima unyenyekeze. Ni kweli ni ahadi ya

Mungu lakini wewe uko chini ya Mungu. Roho Mtakatifu ni Mungu. Wengi tunajisahau tunakosa heshima kwa Roho Mtakatifu. We

treating him like a toy. No UYU NI MUNGU. anastahili Heshima yote. NA HAPENDI UCHAFU! NA HAPENDI MOYO WENYE MAKWAZO
USIOSAMEHE AU UCHUNGU. kwa namna moja au nyingine sisi wenyewe tumekuwa kikwazo kikubwa Sana cha uyu BWANA

MKUBWA. kufanya kazi na sisi. Ni bora umwambie akusaidie. Jishushe pondeka kama mtu anahitaji msaada sio anayejua. Nenda kwake

kama hujui lolote na hujui njia. Tatizo ni hili naomba unisaidie! Usije sahau ilo neno naomba unisaidie. Mimi kila Mara

nilipotamka ilo neno Roho kwa kweli kawa mwaminifu Sana.

# ROHO MTAKATIFU ndiye anayeona chanzo cha tatizo, na anajua njia ya kutokea hapo! Ndio anayeona vitu wewe usivyoviona.

Na ndiyo mwenye maarifa yote binadamu anayohitaji ili aweze kufanikiwa. Ndio anayeona viumbe vyote Katika ulimwengu wa Roho

viumbe wa Mungu hata viumbe wa Shetani. Roho Mtakatifu ndiye anayeona siri zote za adui wanazozipanga juu yako. Roho

Mtakatifu anajua yote. Roho Mtakatifu ndio anayetoa nguvu, nguvu za utajiri, kuomba kuendelea mbele. Roho Mtakatifu akikupa

nguvu zake ndipo wewe unaweza kufanya uliyokuwa huyawezi, au kujikwamua uliponasa. Wachawi na waganga wa kienyeji wana operate

against kwa roho za shetani. Lakini wanapokuja kwako wakimkuta Roho Mtakatifu hawawezi fanya lolote. Roho Mtakatifu ni mkuu kuliko Roho

zote Katika ulimwengu wa Roho. Roho Mtakatifu ndio mfyatuaji toka rohoni kuja mwilini. Roho Mtakatifu anasiri zote za Mungu, anajua vyote

kuwa na Roho Mtakatifu manake ni kuwa na mtu ambaye yupo karibu Sana na Mungu manake ni hii kukifanyika kikao kule mbinguni

lazima Roho Mtakatifu awepo. Embu fikiria wewe unajuana na chief of staff very best Friend wa Magufuli. Manake wewe Kuna

Priorities nyingi utapata sababu tuu ya kujuana na mtu wa karibu wa Raisi. Sasa Roho Mtakatifu si tuu mtu wa karibu Bali amepewa

mamlaka yote ya kiungu. HIVI UNAKOSEJE KUWA KARIBU NA MTU KAMA UYU? YEYE NDO KIUNGANISHI CHAKO. ALIKUJA

KWA AJILI YAKO BAHATI MBAYA HATUJAMPA NAFASI. Vizuri tumempa asilimia chache Sana. Roho Mtakatifu atakushauri hata

mambo ya ndani ya ndoa. Yani ni mshauri wa ajabu. Yeye ndo anayeweza kukusaidia ukaishi na mtu mkorofi! Usione umefanikiwa

kuishi na mwezi wa ndoa jua ni Roho Mtakatifu uyu ni mshauri wa ajabu, mwalimu wa ajabu. Alafu pia anakusaidia na kutenda.

# KUNA WATU WALIOWAHI KUMKOROFISHA ROHO MTAKATIFU NA ILIWAGHARIMU KATIKA BIBLIA EMBU TUWAANGALIE.

Matendo ya Mitume 5

1. Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,

2. akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.

3. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?

4. Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.

5. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.

6 .Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika.

# Anania walikubaliana na Akina Petro auze kiwanja chake kwa ajili ya huduma, alivyofanya hivyo tuu, Roho Mtakatifu akakiboost kile

kiwanja. Tuseme kilikuwa na thamani ya Mil 5, Roho Mtakatifu akafanya thamani yake may be mil 25, anania kuona vile wakakubaliane
na mke wake tupeleke hizi mil 5 tuu ni mfano nakupa. Petro ndo akamuuliza akizungumza katika Roho Mtakatifu kwanini

kumdanganya Roho Mtakatifu? Ikamwingia hofu kuu bila shaka moyo ulisimama kwa kugundua nimejulikana. Akafa Anania hakujua

tokea mwanzo Roho Mtakatifu ndio aliohusika. Hii inakufundisha Roho Mtakatifu ndiyo anayehusika na kila kitu.

Matendo ya Mitume 5

7. Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.

8 .Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.

9 .Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.

10 . Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.

11 . Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya.

#Sasa si yeye tuu na mke wake.

Angalia hapa

# Angalia hapo juu kilichomuuwa Mkewe ni kosa la kupatana na Mme wake kumdanganya Roho Mtakatifu. Tena aliulizwa ndiyo bei

ya kiwanja pasipo kujua mme wake ashazikwa anakasema ndio. Ambacho alikuwa hajui wakati wanapatana ndani kwao chumbani

kwao Roho Mtakatifu alikuwepo na alikuwa anawasikiliza. Lakini pia kilichonifurahisha na hao vijana walikuwa sharp kuokota kwenda kuzika. 😊

# TUANGALIE MFANO WA MWISHO SIKU YA LEO! TUTAENDELEA KUJIFUNZA HABARI HIZI ZA ROHO MTAKATIFU JINSI UNAVYO

FUNGUA MOYO KUJUA HABARI ZAKE NDIVYO ATAZIDI KUJA KWAKO KWA NGUVU. Matokeo yake mtakuwa na strong bound na

unapata matokeo makubwa Sana na mambo mengine wala hutaombea Yeye atatenda maana umemtambua sasa.

Matendo ya Mitume 13

6. Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;

7 . mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.

8 . Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani.

9 . Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,

10 . akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?

11 . Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.

12 . Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.

# Enzi hizo kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akijiita baryesu yeye alikuwa akitumia pepo la utambuzi. Pepo la utambuzi kinaweza kujua

mambo yaliyopita na mambo yaliyokuja. Lakini hawezi kutoa msaada hii ndo inayofanya watu wengi kwenda kwa waganga wa

kienyeji. Kupiga ramli au kusoma bao kwa maneno mengine. Alifanya hivi akajipatia ela nyingi. Paulo na Barnaba walikuwa wanapita huo

mtaa. Liwali mmoja akawaona akawaita watumishi wa Mungu ili apate neno la Mungu. Lakini alikuwa amesimama na uyu baryesu yule

mchawi. Paulo alipoanza kumhubiria yule mchawi akawa  anapiga uchawi wa mafundo anamfunga akili yule liwali ili

asielewe. Na hii ni kawaida kabisa mtu aliyekufunga na nguvu za Giza atakufunga na ufahamu au maarifa ili usielewe. Ndo mana Mara nyingi

aliyefungwa hapendi neno la Mungu au hata kama analipata basi halielewi. Roho Mtakatifu ndani ya Paulo. Akamwona yule Bwana

pembeni ya liwali akamkazia Macho. Kisha yule mchawi gafla akawa kipofu. Ndo mana usicheze uyaone macho ya Roho Mtakatifu.

Sasa uyu Roho Mtakatifu ambaye tumemuona kuanzia mwanzo yupo hata wewe unaweza mpata na anafanya kazi ndani yako. Kazi zote

yeye anahusika na mambo yote hata Yale ya ndani kabisa. Kabla ya kuendelea na somo hili nitaweka maombi hapa kwa imani utayaomba

na Bwana Yesu atadhiririsha hiki nilichokuwa nazungumza hapa. Kwa iyo usikimbilie kuomba soma kwanza ili moyo wako ufunguke.

# MAOMBI HAYA NI KWA WOTE WALIOJAZWA NA WASIOJAZWA ROHO MTAKATIFU.WEWE AMBAYE UMEJAZWA ATAKUONGEZEA NGUVU ZA ROHO

WEWE AMBAYE HUJAWAHI KUJAZWA ATAKUJAZA VYOTE.  KUJAZWA NI KILA SIKU! YESU NDO ANAYEJUA UMEFURIKA AU VIP IVYO USIJIWEKEE MPAKA! YESU

KUKUJAZA NI MAHALI POPOTE ALIMRADI MOYO WAKO UMEFUNGUKA? JE UMEZISOMA HABARI ZA ROHO MTAKATIFU? UMEZIPENDA? UNGEPENDA

KUTEMBEA NA VIWANGO VIKUBWA VYA MAFANIKIO? UNGEPENDA UYU ROHO MTAKATIFU AWE PARTNER WAKO WA MAISHA? KAMA NDIYO BASI HAYA

MAOMBI HAPA CHINI NI YAKO.

PRECAUTION:
* Kama hujaokoka ni lazima uokoke umpokee Yesu! Huwezi pokea nguvu za Yesu na Huku hujamkubali. Lazima uwe upande wake 100%.

*Ukiomba ujazo huu wengine watajazwa sasa, wengine baadaye! Wengine taratibu ivyo kutokuona ishara haina maana huwa hujajazwa! Kwa mda huo!

* Lazima utambue Roho Mtakatifu ni ahadi toka kwa Mungu. Kwa iyo huna haja ya kuomba maana ushapewa la muhimu tunamjulisha kuwa Yesu tupo tayari!

Tunaomba atimize ahadi hiyo sasa. Ni ahadi kwa kila mtu aliyeokoka! Wala huna haja ya kufunga ili umpate Roho Mtakatifu no! YESU NDO ANAYEMTOA

ROHO MTAKATIFU KWA WATU WAKE! PILI AKILINI MWAKO UTAMBUE ANAYEJAZA NI YESU PEKEE SIO MTUMISHI. HAYA MAOMBI

Hapa chini utayarudia hata kama ushayarudia ili kama ulishajazwa alafu ukamuhuzunisha Roho Mtakatifu akakaa kimya basi utengeneze upya. Na wewe

Ambaye hujawahi kujazwa pia utaisema na wewe ambaye hujawahi ongozwa sala ya Toba pia utaomba kwa imani kwa sauti.tafuta sehemu unaweza kuwa huru

Kabisa ili usije kufanya kwa kuogopa watu au kujificha. Ni kitendo kizuri Sana ambacho kikija utatamani kisiondoke kwa iyo nikutoe wasiwasi ili uwe na amani

"Maombi ya kukupatanisha na Yesu"

Bwana Yesu Asante kwa kunisamehe dhambi, Leo nakuja mbele zako najisalimisha kwako kwa ajili ya wokovu wako ninaomba unisamehe dhambi makosa na uovu wowote katika maisha yangu yote. Ninatubu na kuanza upya kwa damu ya Yesu.Ninaomba unitakase Bwana Yesu kwa damu yako na  kunisamehe na kunisafisha. Leo kwa kinywa changu natamka kukubali na kuomba kuingizwa katika ufalme wako YESU. Ninamkataa shetani na dhambi zake zote Mimi siko tena upande wake katika jina la Yesu. Ninavunja maagano yote mikataba yote na laana zote za shetani kwa damu ya Yesu.Katika jina la Yesu. Bwana Yesu ninaomba sasa jina langu uliandike kwa damu yako ya dhamani katika kitabu cha uzima.BWANA Yesu tokea Leo hii wewe ni Bwana na mwokozi wa maisha yangu na Mimi ni mtoto wako katika jina la Yesu. Tokea Leo hii Mimi ni mwana wa Ufalme wa Mungu katika jina la Yesu. Nimelikataa Giza la shetani na kazi zake zote. Bwana Yesu naomba sasa uyatawale maisha yangu uniongoze unifundishe ili niendelee kukua imani hadi imaani hadi kuurithi uzima wa milele Amen.

"Maombi ya kumkumbusha Mungu kuhusu ahadi yake ya Roho Mtakatifu"

"Kama tayari unaweza nena kwa lugha basi nena kwa lugha (speaking in tongue) moja kwa moja. ila kama bado omba Maombi hapo chini"

Bwana Yesu niko mbele zako Leo kwa ajili ya ahadi yako uliyoitoa katika Luka 24:49
" Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu"  nimezisikia habari za Roho wako Mtakatifu na nimezipenda habari zake, siwezi kukaa tena hata dakika moja bila Roho Mtakatifu Bwana Yesu najisalimisha mwako naomba unijaze sasa! Nijaze Roho wako Mtakatifu Bwana Nijae! Niko tayari Bwana Yesu! Niko tayari sasa! Niko tayari kumpokea Roho wako mtakatifu! Bwana Yesu nimekufungulia moyo wangu  naomba uikamilishe ahadi yako Bwana Yesu! Sasa Bwana Yesu! Sasa Bwana Yesu! Sasa Bwana Yesu! Sasa Bwana Yesu! Sasa Bwana Yesu! Sasa Bwana Yesu! Ninaomba Nijaze sasa Bwana Yesu! Nijaze nifurike Bwana Yesu! Nakusubiri wewe Bwana Yesu! niko tayari achilia mafuta ya Roho Mtakatifu sasa katika jina la Yesu! Na kwa damu ya Yesu! Bwana Yesu Asante kwa ahadi yako! Asante kwa ahadi yako! Asante Bwana Yesu! Siwezi bila huyu Roho Mtakatifu! Leo nimemjua vizuri kabisa! Ndani yangu Kuna kiu Bwana Yesu ya Roho wako Mtakatifu! Asante kwa kunijaza Bwana Yesu! Asante kwa kunijaza Bwana Yesu! Asante kwa kunijaza Bwana Yesu! Niko tayari Bwana Yesu! Niko tayari sasa Bwana Yesu. Sio kesho sasa ivi Bwana Yesu! Timiza ahadi yako sasa Bwana Yesu. Now Jesus! Now Jesus! Now My Lord. Timiza ahadi yako sasa Bwana Yesu.
Asante Yesu! Asante Yesu!
Asante Yesu! Asante Yesu!
Asante Yesu! Asante Yesu!
Asante Yesu! Asante Yesu!
Asante Yesu!Asante Yesu!
Asante Yesu! Asante Yesu!
Asante Yesu! Asante Yesu!

Endelea kusema Asante Yesu usiache endelea kwa sauti na kwa spidi na huku ukiwa umefunga macho! Na umakini Mkubwa Kama lugha ikibadilika endelea nayo usiache mpaka ikatike yenyewe.....

Endelea na haya Maombi yarudie kila Mara na kila siku mpaka usikie kufurika. Kujaa.

*utaona mabadiliko makubwa.

ENDELEA KUFUATILIA SEHEMU YA PILI YA SOMO HILI......

Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

  1. Namshukuru Yesu kwa kuniongoza kuyasoma haya .mafundisho ya Roho Mtakatifu nimebarikiwa sana naomba Roho Mtakatifu azidi kunipa kiu ya kumtegemea kila wakati
    Roho wa Mungu azidi kukufunulia mafundisho zaidi ili tuyasome na kujengwa.
    Ubarikiwe sana!!!

    ReplyDelete
  2. Nimebarikiwa sana na umenitoa hatua moja kwenda hatua nyingine. Mungu wa mbinguni akutumie zaidi mteule

    ReplyDelete
  3. Mungu wa majeshi akubarik na kukufunulia zaidi mtumishi wake, nimepata nguvu na kiu ya kumtafuta roho mtakatifu

    ReplyDelete
  4. Nimebarikiwa sana mungu azidi kukujaza

    ReplyDelete
  5. Mimi nimeokoka na napenda Yesu kwa mda mrefu Sana.na nimekuwa sifahamu utendaji Wa Roho mtakatifu katika maisha yangu leo nakiri waziwazi kuwa nimepata kitu Cha tofauti katika maisha yangu. Rohomtakatifu nisaidie nikutii sauti yako

    ReplyDelete
  6. Sifa na utukufu zimwendee Mungu wetu aliye hai,anayetufundisha kwa uwezo wa Roho wake Mtakatifu.Pia akubariki wewe kwa kuitika wito wa kuandaa makala hii,imenifungua sana,kilichobakia kwangu ni kuweka ktk matendo tu.

    ReplyDelete
  7. Nimempomea Bwana Yesu tangu may 23 mwaka huu. Na tangu hapo sikuwa na ufahamu mkubwa kuhusu Roho Mtakatifu. Katik kutafuta tafut kwangu habari za Roho Mtakatifu leo nimekutana na huu ujumbe kwa hakika sichoki kuusoma tena na tena. Sasa nimepata kitu kipya ndani yangu, na nimesaidika sana katika kumjua Roho Mtakatifu. Mungu Roho Mtakatifu azidi kukupa nguvu na uwezo katika kufundisha neno lake. Amina

    ReplyDelete
  8. Yesu anisaidie nimefunguliwa kupitia ujumbe huu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA