WASHINDE WAKUU GIZA& FALME ZA GIZA ILI UWEZE KUMILIKI
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu, habari ya uzima wako?
Mungu alinionyesha sehemu nyingine muhimu ya kushughulikia katika ulimwengu wa Roho. Ni mpaka uishinde sehemu iyo ndipo utafanikiwa kumiliki chochote usiifahamu au kuishughulikia jua vita vitapigwa hapo kila siku na hutakaa umiliki au hata ukimiliki utakuwa na vita kila siku.
Mfano huwezi kuwa huru kiuchumi, huru katika ndoa, Huru kiafya, Huru kumfanyia Mungu ibada, Huru kifrika, Huru kifamilia, Huru katika biashara, Huru katika kazi, Huru katika vifungo vinavyokuzuia kuendelea mbele ni mpaka ili eneo umelishinda. Maana siku zote wewe unadili na Matawi ila hujaligusa
shina bado. Iyo ni mifano michache, mfano zipo tabia za mtu ambazo anazifanya hata yeye hataki kuzifanya alafu anajishangaa bila kushinda eneo ilo basi huwezi kuwa huru. Uhuru manake ni uzima wa milele. Yani iko kitu kinakuwa kizima na furaha milele si ya siku moja au mbili no ya mda wote.
Yohana 8:36
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli
Warumi 16:3
3 Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu;
1Kor 3:9
9 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Tuangalie Yohana 8:36 Vs 1kor 3:9, na Warumi 16:3 tulitafakari hilo neno kwa makini ndilo litatuingiza katika message ya Mungu. Na kumuelewa Mungu anataka tufanye nini.
Mungu kasema kule juu lakini mwana wa Mungu akikuweka huru utakuwa huru kweli kweli. Unajua kuna huru kisha kuna huru kwelikweli. Kuna watu wako huru kwenye uchumi lakini afya hawako huru. Wengine wako huru kiuchumi, afya, familia! Lakini maeneno
mengine ambayo ni siri yao hayako huru. Ndipo anasema When Jesus step in into your case utakuwa huru kweli kweli lakini swali linakuja? Lini nitakuwa huru kwelikweli? Wanafunzi wa Yesu waliwahi kumuuliza Yesu iyo habari ya jiwe kutokusalia juu ya jiwe, wakamuaambia tuambie habari izo zitakuwa lini je nini dalili ya kurudi kwako? Bwana Yesu asifiwe!
Soma hapo juu Inasema Basi Mwana akikuweka huru, akaweka koma kisha akarudia utakuwa huru kweli kweli. Umeona hapo ipo huru ya kwanza. Ipo huru ya pili yenye kwelikweli mbili. manake huru ya kwanza ni huru ya upande mmoja mfano upo huru kiuchumi Mungu kakuinua, upo huru una afya lakini ndoa yako haipo huru, au
umefungwa na vifungo vya giza. Sasa huru ya pili yenye kwelikweli ya pili hii ile inasema kabisa kabisa kwa maana mengine yani wewe kila maeneo uko huru ni ndoa uchumi afya kila lango lako lipo huru maeneo yote Yesu anayaweka huru. Iyo ndo tofauti ya huru. Na huru kwelikweli.ndo mana akatenganisha kwa koma na kurudia kutofautisha huru ya kwanza na huru ya pili yenye kwelikweli. Bwana Yesu asifiwe
Kwa iyo yakaja maswali ndani kwa msaada wa roho mtakatifu! Kwanini watu hawako huru kwelikweli kwanini tunatembea katika uhuru peke yake na maandiko yamesema tunatakiwa tuwe huru kwelikweli. Ndipo nikapelekwa katika Warumi 16:3, Na 1kor 3:9 zote inaelezea kutenda kazi na Kristo kutenda kazi
na Mungu. Akili ikazidi kufunguka kwani hatutendi kazi na Kristo? Mungu akaniambia katika vita ya mtu kuwa huru mara nyingi sana tunafanya vita tunachoka au tunaishia katikati . Mtu anaweza kufunga akaomba kwa bidii hata kwa wiki anakuwa moto kipindi hiko ulimwengu wake wa roho unawaka
green light yako uko on! Hata shetani akiangalia anaona moto unaowaka hakuoni wewe gafla baada ya kufunga au mda uliojiwekea kuomba tunapoa tena. Kwa kazi ya kujiweka na huru na ya wewe na Bwana Yesu. Lazima mshirikiane na Mungu sio kuomba then kukaa kimya haiendi ivyo. Wengi tunaomba alafu hatufuatilii
majibu kwa Mungu hata Mungu akianza kutembea na wewe iyo safari ya kufunguliwa hutaki unachotaka ni matokeo ya mwisho kumbe ilo jangwa lako siyo jangwa ni njia ya kaanani. Kwa iyo tumejikuta tukifanya kazi nusunusu na kumwachia Mungu. Hatuna tabia ya kufuatili mfano neno linaweza
kupita likakuweka huru. Na moyoni ukapokea Mungu anakupeleka darasa lingine tena tayari hutaki unachotaka ni kufika kaanani, kuiona kaanani lakini iyo njia ya Mungu huitaki. Bwana Yesu asifiwe. Sisi ni watenda kazi pamoja na Kristo, sisi tunafanya kazi pamoja na Mungu. Mungu kasema atakuweka huru kwelikweli lakini
lazima ufanye kazi uombe uchukue majibu uyafanyie kazi uendelee hatua inayofuata Mungu kazi yake ni kukuondolea ukuta. Ili upite lakini kufuata njia na kupita kufika ni kazi ya binadamu. Jina la Bwana libarikiwe.
Roho Mtakatifu hakuishia hapo akaendelea ndani kwangu lile swali likajirudia tena kwanini hatuko huru kwelikweli, nikashangaa maana nilijua tayari Nina majibu kumbe bado. Kwa iyo likaja andiko tena. Tuliangalie...
Waefeso 6:12-13
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
sasa hapa ndipo ufuatilie kwa makini ndipo Kuna siri nzito Mungu alinifunulia....
izo ngazi nne za ibilisi tumezizoea kuziimba hata usiku nikikukurupusha utaniambia iyo ni waefeso 6:12 kila mtu anaijua ila wasicho kijua au kujijua kukipuuzia ni hiki. Huwezi kufanikiwa sehemu yoyote mpaka umewashinda wafalme wa Giza na wakuu wa Giza wa eneo, mji, ukoo au Familia
usipomwangusha uyu kwa Maombi mkuu wa Giza huwezi pata uhuru wako. Sababu wachawi washirikina waganga wa kienyeji wasoma nyota madhabahu! Au viti vya enzi vya Shetani huwa vinapewa nguvu na wakuu wa Giza na wafalme wa Giza. Ibilisi hupigana juu angani na chini ardhini. Kisha kule kuzimu ndiko
kunachorwa master plan za uharibifu na kutoa nguvu nguvu hizi zinapewa mkuu wa Giza na Falme za Giza. Sasa uyu mkuu wa Giza na Falme za Giza zipo kwenye ukoo, kwenye familia, kwenye mtaa ulioko, zipo katika mji, zipo katika mkoa hata Tanzania mzima. Mfano wewe ukiwa na biashara hauuzi na umepambana Sana Katika maombi
jua yupo mkuu wa Giza mahali anakupiga vita. Ukiwa unapata vita Katika kuolewa au kupata kazi, au kwenye ndoa jua yupo mkuu wa Giza anafanya vita na wewe kwa kuwatumia wachawi, waganga wa kienyeji, washirikina, au anapanda uadui kwa watu waliokuzunguka. Sasa bila kumshinda uyu nakwambia utazunguka makanisa yote na nitakufundisha jinsi ya kumshinda.
Kwa iyo unapofanya vita na wachawi ukawauwa kwa Maombi au mapepo majini roho chafu mizimu au majoka au chochote uyu mkuu wa Giza huinua watu wengine. Kumbuka lile neno kuhusu yule mnyama aliyepewa nguvu juu ya kila kabila lugha na taifa katika kitabu cha ufunuo.
# nikupe shuhuda ili uweke uzito
# David Yonggi Cho wa Korea kusini Ni mhubiri mwenye kanisa kubwa wanaloabudu pamoja kuliko makanisa yote duniani. Alipoitwa na BWANA YESU ili amtumikie alianza kumtumikia. Lakini mwanzo tu wa huduma yake aliona mkuu wa giza anayelimiki eneo la Korea yote. Ilibidi Mchungaji Yonggi Cho
apambane kwa maombi na mkuu yule giza. alipomshinda kwa maombi kupitia jina la YESU ndipo huduma yake ilistawi na huduma hiyo imefikia hatua ya sadaka zinahesabiwa kwa zaidi ya siku 2 na sadaka hiyo kuipeleka bank ni kwa msafara mkubwa kukiwa na ulinzi mkubwa wa Polisi wengi.
Ndugu, ukishinda katika ulimwengu wa roho hata katika ulimwengu wa mwili utashinda pia.
#Askofu Moses Kulola kabla ya kuanza kuhubiri injili ya mafanikio makubwa katika Tanzania aliingia katika maombi ya kufunga siku 4 mlimani. Katika maombi hayo akiwa katika siku ya mwisho ya maombi aliona jitu kubwa la kutisha likija alipo na lilipokaribia lilimwambia kwanini anataka kulichukua eneo lake huyo mkuu wa giza, yaani
Tanganyika kwenye ulimwengu wa roho wa giza kulikuwa na mtawala wake ambaye ndiyo huyo roho ya kuzimu, kwa maombi Askofu Moses Kulola alimshinda yule mtoto wa shetani ndio maana akaanza kuhubiri injili ya mafanikio sana. Kila Eneo huwa lina utawala wa aina tatu. Kuna utawala wa kibinadamu, kuna utawala kutoka ulimwengu wa roho wa giza na utawala wa MUNGU hutawala pote na una mamlaka ya mwisho.
Kumbe ili ulipate eneo fulani kwa ajili ya kitu fulani chako chema inabidi kwa maombi umpige mkuu wa giza wa eneo husika.
Biblia inasema wateule watakapopakanyaka patakuwa pao maana yake watakuwa na mamlaka ya kupatiisha kwa jina la YESU waliyenaye, hata utawala wa shetani utasalimu amri maana wao wana BWANA YESU mwenye nguvu zote milele.
# izo ni shuhuda nilizofutilia mahali baada ya kuwa najifunza kuhusu vita vya wakuu wa Giza. But najua itakujenga na itakusukuna kuomba.
Shetani hawezi kufanya vita bila Giza manake uongo! Shetani hutumia Giza uongo kufanya mikataba ya siri na wapendwa! Hutumia Giza kuwaaingiza watu katika mikataba! Giza maana mingine ni kitu kisichoonekana! Sasa ni mafumbo ya giza ambayo
binadamu kwa tamaa zao, wanajikuta wameingia katika mitego ya ibilisi! Jana tumeangalia like somo la fikra shetani aliingia kwa Adamu kupitia fikra, shetani alimnyanganya Adamu Mamlaka na haki yake na uhuru wake kabla ya Yesu kwa giza. Kwa iyo lazima litangulie giza kwanza baada ya
giza ndipo wanapata access ya kufanya vita na wewe aya ni mambo ya ndani ndani mno! Naomba roho Mtakatifu aendelee kukufundisha hapa. Nitakupa mfano kuota ndoto inayokuonyesha hatari au watu wamekuja dukani mwako wamemwaga damu na wewe ukaona ukapuuzia hukuomba ilo ni
giza limekupiga. Likakufanya upuuzie mambo. Hawa wanapoleta giza wanazuia imani yako, wanaleta kumdaught Mungu. Kutoamini neno au watumishi wa Mungu hata msaada unapokuja hautakusaidia. Kabla ya uchawi, uganga, kabla ya madhabahu, kabla ya laana ya magonjwa huwa huanza giza kwanza.
Hata fikra za Eva kule bustani ya Eden zilifunikwa na giza kwanza ndipo binadamu wote tukajikuta kwenye matatizo. BWANA YESU ASIFIWE!
Halleluyaaaaaaah!
Kwa iyo ni kitu kizuri sana kufanya vita na ibilisi lakini utagundua ya kuwa tunafanya vita level ya chini yani vibaraka wa giza! Sasa unajiuliza kama mapepo wananisumbua vip hao wakuu wa giza? Usiogope ndio maana ya neno kule juu tunafanya kazi pamoja na Kristo.
Sisi tunatenda kazi pamoja na Mungu. Sisi mimi nimesema bali ni Mungu ndo mana ya 1kor 3:9, War 16:3 hauko mwenyewe vita hii unapigana na Mungu shetani kawafunika watu na giza kawawekea watu hofu eti ukifanya vita na wakuu wa giza au falme wa giza eti utapigwa eti utapoteza kazi
eti utakufa huu ni uwongo hili ni giza likatae katika jina la Yesu. Neno la Mungu linasema naye akamununulia watu wa kila lugha kila kabila kila taifa. Damu ya Yesu ilimwagiga ili wewe uwashinde wakuu wa giza ili wewe uwashinde wafalme wa giza. Unaposema mimi huko sigusi au huko ni level za juu kuna level za juu zaidi ya Yesu?
YESU AKAMWAMBIA YOHANA MIMI NALIKUWA NIMEKUFA TAZAMA NI HAI. NAMI NINAZO FUNGUO ZA MAUTI NA KUZIMU ANGALIA UFUNUO 1:17 BWANA YESU ASIFIWE! FUNGUO HIZO ANAZO YESU KILICHOBAKI NI WEWE KUFANYA KAZI NA YESU. KUPIGANA NA YESU KUKUBALI KUKETI PAMOJA NA YESU. Bila
kuwashinda hawa itapita mwaka hata mwaka hata mwaka utakuwa ukiona dalili tuu ya mwanga mara vita vinaanza tena. Lengo la kuandika hili somo ili upate hasira ya roho Mtakatifu ndani yako. Yakuomba mwenyewe! Kuwapangua hawa watesi walioyafunga maisha yako. Wanakufanya unafunga mpaka unapata vidonda vya tumbo.
Maana ukishinda vita moja mkuu wa giza analeta jeshi lingine unaanza upya tena. Mpaka lini? Ngoa shina na mizizi yake na matawi na matunda yatanyauka.
naenda kukupa neno hapa la kukuonyesha vita unavyopigana bila kuwangoa wakuu wa giza wawe chini yako huwezi kuwa huru kwelikweli na bila kupigana na damu ya Yesu na Yesu pia huwezi kushinda neno hili litakupa gurantee ya kushinda neno hili litakupa hakika au ni summary ya somo letu.
Tamani uwe huru kwelikweli. Kwanini uwe huru kwenye ibada unaomba unasifu&unaabudu. Unasoma neno kwanini usiwe huru katika afya. Kiuchumi, ndoa na mambo mengine biashara? Uwekezaji? Kwanini uwe huru nusunusu na una Yesu. Nijukumu ketu kuomba kwa neno hili tuangalie neno.
Ufunuo 13-3-7
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
Nataka uone jinsi wakuu wa Giza vitu walivyopewa nguvu kufanya vita kufanya vita na kuwashinda. Kule nyuma anasema Joka akampa nguvu zake yule mnyama na uwezo mwingi. Jana nilisema sio swala la kusema ilo najua nishawi kusikia
swala si kusikia swala ulilifanyia kazi na kazi ulimaliza? Sasa angalia neno linalofuatia linakuja kupinga yule joka. Limekuja kupinga uyo mnyama. Limekuja kupinga wakuu wa Giza wote. Bwana Yesu asifiwe Sana.
Ufunuo 5
4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama.
5 Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
7 Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi.
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
# angalia hapo juu alafu ufananishe kwa kufananisha hapo amezungumzia vifungo vigumu. Visivyo fungulika
Ndo mana kitabu chenye muuri zake! Angalia mwanakondoo naye alicholifanya amenununua watu wa kila kabila lugha na taifa. Angalia kule nyuma yule joka naye alipewa nguvu Kati ya kila kabila lugha taifa.. Lakini mwisho wa mwanakondoo wale wazee 24
wanasema wastahili wewe kukifungua hiko kitabu maana ulimnunulia Mungu watu kwa damu yako. Kununuliwa manake ni kuwa full paid. Vifungo vyote vinavyokutesa vimekuwa full paid. Kwa iyo damu haina mwisho imekulipia mbinguni duniani na hata kuzimu . Ukisoma mstari wa 2&3
Sura iyoiyo ya 5, inasema hapakuonekana mtu mbinguni juu ya chini wala chini ya nchi. Manake nini hapakuwa na mtu wa kushindana na yule mnyama alipewa nguvu na joka mbinguni duniani hata kuzimu isipokuwa mwanakondoo. Na ule ufunguo wa Mat 18:18 ambayo Yesu aliwapa
kanisa ni damu ya Yesu. Katika ufunuo 5:9 kwa iyo ukiapply iyo damu ya Yesu wakuu wa giza wafalme wa giza na wote lazima wakuacha na utakuwa huru kwelikweli. JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE.
NATAKA NIKUONYESHE UYU YESU AMBAYE ANAENDA KUKUPIGANIA VITA NI MUNGU WA AINA GANI? watu akili mwao hawana picha sahihi ya Yesu, Mara nyingi wanamfananisha Yesu na yule kwenye movie! picha ambayo si ya kweli kabisa.
Ufunuo 1
10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.
12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;
13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;
15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.
16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Hapa Yohana anaelezea Yesu alipomtokea ilikuwa alipochukuliwa mpaka mbingu ya tatu, katika Roho anasema nilisikia sauti kuu kama baragumu! Yani ni kama vile maji mengi yangukayo katika maporomoko hii ndo ilikuwa ndo sauti ya Yesu, anasema akaona vinara saba mfano wa binadamu unaona yeye alikuwa anafananisha
kila kitu na huku duniani manake karibia kikaribie cha duniani pengine alikosa mfano wake kwa iyo akasema nikaona vinara 7 vya dhahabu! Akaona mtu mfano wa binadamu amevaa vazi mpaka miguuni na kufungwa mshipi wa shahabu kifuani usawa wa matiti, anasema nywele zake ni nyeupe
kuliko theluji can you imagine lazima zilikuwa hazitizamiki ni nyeupe kuliko nyeupe lazima ilikuwa inaumiza macho mno! Anasema macho yake yalikuwa na miali ya moto. Kwa kweli Yohana aliona makuu mno! Miguu yake inangaa kama shaba iliyosuguliwa sana. Alikuwa na nyota saba mkono wa
kuume, na upanga mkali ukatao kuwili, ukitoka kwenye kinywa chake, uso wako wake unangaa kama jua can you imagine? Kama huwezi angalia jua je uso Wa Yesu unangaa zaidi ya jua je utaweza kweli kumuangalia? Anasema nilipomwona nalikuwa kama
nimekufa umeona nilikuambia huwezi stahimili. Yesu ni Mungu. Ule utukufu wake ukikusogelea tuu unaweza ukayeyuka he is God. Anasema nalikuwa kama nimekufa manake Yohana alikufa. Anasema nalikuwa nimekufa sasa ni hai. Nami ninazo funguo za mauti na
kuzimu. Sasa uyo ndo Yesu uyuuyu unayetembea naye. Ndo uyuuyu alishuka kuzima akampiga shetani. Ndio kiumbe cha kwanza kilichotoka juu sana na kushuka chini sana na kupanda juu uyu ndo Yesu si yule wa kwenye movies. Uyo ndo Yesu aliompiga baba yao na wakuu wa
giza, wafalme wa giza, yani hao wanaotumwa kukusumbua wewe boss alipigwa na uyu tunayemzungumzia hapa. You imagine Mungu unayemwabudu. Mahali alipo Yesu Jeshi lote la Mbinguni lipo ivyo usiogope katika jina la Yesu
Hakuna ambaye amewahi kumuona Mungu katika mwili akabaki mzima. Haiwezekani lazima utakufa . Ule utukufu its too Much. Ile nuru its too much! Holliness its too much to human being ndo mana watu lazima wafe ile wawe roho!
SAULI ulimtokea mwanga tuu ule mwanga uliingia machoni akapofuka macho. Uyo ndo Yesu tunayemzungumzia. Uwepo wa Mungu unao uonaga hapa duniani hao ni malaika wa Mungu tuu. Wanapewa huo utukufu wa Mungu na wakija unaweza kusema ni Mungu kumbe si Mungu. Unakumbuka Daniel alivyotokewa
na yule malaika Daniel alikufa biblia inasema malaika alimgusa Daniel akaamka yule malaika alibeba utukufu wa Mungu. Nakwambia haya mambo ya ufalme wa Mungu ukiwa unayafuatilia ni matamu.
Matendo 22
6 Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.
7 Nikaanguka nchi, nikasikia sauti ikiniambia, Sauli, Sauli, mbona unaniudhi?
8 Nikajibu, Wewe u nani, Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unaniudhi. 9 Na wale waliokuwa pamoja nami waliiona ile nuru, lakini hawakuisikia ile sauti ya yule aliyesema nami.
Sauli ambaye alibadili jina baadaye kuwa Paulo Yesu alipomtokea alipofuka macho! sababu ya ule utukufu wa Mungu.
MAOMBI YA KUHARIBU FALME ZA GIZA/ WAKUU WA GIZA
Baba katika jina la Yesu Kristo! Ninakuja mbele zako kwa damu ya Yesu Kristo ninakuja mbele zako katika jina la Yesu Kristo. Roho Mtakatifu naomba uniunge
mkono katika maombi haya ya kuangusha na kuporomosha Falme za giza, na Wakuu wa giza, wakuu wa Anga pamoja na Jeshi la mapepo wabaya. Ambao wamekuwa
wakizuia hatua zangu, wamekuwa wakiniletea vita usiku na mchana! Katika ngazi za ukoo na familia. Katika ngazi ya mtaa ninaoishi, katika ngazi ya mji au
mkoa Na Hata nchi. Na leo kwa damu ya Yesu. Leo hii kwa kiti cha Kristo! Leo kwa malaika wa vita wa Bwana, Leo kwa moto wa Roho Mtakatifu, Leo kwa tetemeko la
Mungu, Leo kwa mvua ya damu ya Yesu, Kwa mvua ya moto wa Roho Mtakatifu. Leo hii kwa mishale ya Moto wa Roho Mtakatifu nitaenda kuwasambaratisha
kabisa na hawataonekana tena mbele yangu kwa damu ya Yesu. BABA ninasogea mbele zako kwa ajili ya utakaso kamili, ninaomba rehema katika jambo
lolote nililolifanya ambalo limekuwa mashataka mbele yangu eee Mungu wangu katika jina la Yesu, ninaomba rehema kwa kutosimama katika zamu
yangu. Au kuomba kwa ulegevu, naomba MUNGU Baba wa Mbinguni unihurumie unirehemu unitakase ufute makosa maovu na dhambi mbele zako Baba,
ninaomba ile damu inanonena mema juu yangu ipite sasa katika makosa dhambi na uovu ikinitakasa kabisa ikiniosha kabisa ili kwa damu ya Yesu nihesabiwe mwenye
haki mbele zako Mungu katika jina la Yesu. Ninatubu kabisa na kujutia makosa uovu na dhambi zangu naomba Baba unisamehe kwa damu ya Yesu Kristo.
Bwana Yesu leo kwa akili zangu ninakubali kuketi na wewe katika ulimwengu wa Roho, Kwa damu ya Yesu Kristo, ninaketi na wewe katika kiti chako enzi Bwana
Yesu, ninaketi na nafsi yangu, roho yangu, mwili wangu, ninaketi na mali zangu, ninaketi katika ulimwengu wa Roho na ndoa yangu, ninaketi na kazi yangu, nina
Keti kwa damu ya Yesu Kristo na biashara yangu, ninaketi na familia yangu, ninaketi na ukoo wangu. Ninaketi kwa damu ya Yesu na watoto wangu katika jina la Yesu
Kwa damu ya Yesu ninakusanya mambo yangu yote katika mkono wangu kwa damu ya Yesu ninaketi nayo sasa katika duara la Yesu la ulimwengu wa roho,
Katika jina la Yesu ninatoka mimi na mambo yangu yote yaliyonizunguka Mungu aliyonipa yote kabisa ninayakusanya katika duara la mwilini
Kwa damu Ya Yesu ninaondoka na kuja hadi kwenye duara la rohoni la Bwana Yesu ninaketi nayo hapo. Katika jina la Yesu. Bwana Yesu ninakubali nafasi ya
Kikuhani na kifalme katika ulimwengu wa Roho kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu! Naipokea nafsi ya kikihani na kifalme kwa damu ya Yesu, katika jina
La Yesu. Bwana Yesu nakubali nafasi ya kikuhani na kifalme katika nafasi uliyoniitia ya kumiliki na kutawala katika kazi, ndoa, biashara, familia, ukoo,
Nyumba nayoishi, mtaa naoishi, mji naoishi, mkoa naoishi, hata nchi nayoishi iyo nafasi sasa naichukua na kuimiliki katika ulimwengu wa roho Kwa damu ya
YESU katika jina la Yesu natangaza katika ulimwengu wa roho kwa damu ya Yesu mimi ndio mfalme ninatawala katika ulimwengu wa Roho natawala nafasi
Ya ufalme na ukuu katika ndoa, katika familia, katika ukoo, katika kazi, katika biashara, katika eneo naloishi, mji naoishi, mkoa naoishi, nchi nayoishi katika jina la
Yesu Kristo, Naachilia damu ya Yesu sasa ya kumiliki maeneo yote niliyoyataja katika ulimwengu wa roho, sawasawa na ufunuo 5:9. Damu iyo ya kumiliki na
Kuchukua nafasi naimwaga juu ya ardhi naimwaga juu anga zote, naimwaga juu ya bahari zote, naimwaga juu ya nchi katika jina la Yesu, naimwaga damu ya Yesu ya
Kunitambulisha Mfalme na kuhani katika ulimwengu wa roho ngazi ya familia, ukoo ngazi ya mtaa ngazi ya mji, ngazi ya mkoa katika jina la Yesu iyo ni damu ya Yesu ya
Kumiliki na kutawala maeneo hayo yote niliyoyataja kwa damu ya Yesu. Wamiliki wote ambao hawamilikiwi na damu ya Yesu, ninaaanza kawanyanganya sasa ivyo
Viti vyao kwa damu ya YESU! KWA DAMU YA YESU! wamiliki wa izo nafsi Falme za Giza, Wakuu wa Giza, wakuu wa anga, na Jeshi la pepo wabaya naachilia damu ya
YESU ya kuwafuta kazi katika jina la Yesu. Kwa damu Ya Yesu wewe unaesimamia familia yetu, ukoo wetu, unaesimamia eneo ninaloishi, wewe inayesimamia mji
naoishi, wewe unayesimamia mkoa ninaoshi, wewe unayesimamia nchi na unanipanga katika nafasi yako ukitumia washirikina ukitumia wachawi, ukitumia
Waganga wa kienyeji, ukitumia wasoma nyota, ukitumia majini, ukitumia majoka ya baharini, ukitumia Malkia wa kuzimu, malkia wa anga, Malkia wa bahari kwa
Damu ya Yesu nakusambaratisha naachilia damu ya mwanakondoo juu yako sasa, ifanye vita na wewe katika jina la Yesu. Wewe unayetoa direction ya vita. Wewe
Unayenipinga katika level yako uliyepewa kiti na lile joka na nguvu juu ya kila kabila watu lugha na taifa, nakupinga kwa damu ya Yesu. Nakujia na Kiti cha Yesu kwa
damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu nakungoa sasa ewe Falme za Giza , ewe wakuu wa Giza, wakuu wa anga, na majeshi yenu ya pepo wabaya ambao
mnafanya vita na Mimi, mkinitengenezea maadui Leo ni mwisho kwa damu ya Yesu Kwa kiti cha Yesu, ninawangoa!
Ninawangoa! Ninawangoa! Kwa mamlaka ya jina la Yesu! Kwa damu ya Yesu! Ile damu ya kushindana vita ufunuo 12:11 naimwaga juu yako sasa nakungoa wewe
unayenipinga wewe mchawi uliyepewa kiti nakungoa kwa damu ya Yesu, wewe unayenifuatilia nakungoa na kiti cha Yesu kwa damu ya Yesu kwa damu ya Yesu!
Biblia inasema nikupinge nawe shetani utanikimbia nimkaribie Mungu naye atanikaribia,katika jina la Yesu Kristo unayezuia amani ya ndoa yangu, wewe
Uliyekalia biashara yangu, wewe wewe unayezuia nisioe/kuolewa, wewe unayezuia hatua zangu, wewe unayeleta kuchanganyikiwa, wewe unayezuia
Nisifanikiwe katika lolote, wewe unayenirudisha nyuma, wewe unayeniwekea ukuta, wewe unayefanya kazi ya kuwa chungu, wewe unayepiga
Uchumi wangu, wewe uliyekamata vibali vyangu wewe mkuu wa Giza tokea kwenye familia/ukoo wangu Leo nakuweka uchi kwa damu ya Yesu, wewe
Mfalme wa Giza tokea eneo la biashara au makazi au kazini, wewe mfalme wa Giza wa mji ninaoishi, mkoa ninaoishi, au Nchi ninaoishi shetani amekupa nguvu za
Kupambana na Mimi lakini kwa damu ya Yesu hutashinda, nakuponda kwa damu ya Yesu, ninakuja na kiti cha Yesu kwa damu ya Yesu ninakungoa nakutupa nje
Sasa katika jina la Yesu, nakunyanganya nafasi kwa damu ya Yesu, achilia kwa damu ya Yesu, ngoka kwa damu ya Yesu, nakutupa nje hadi shimo la Moto la
kuzimu Katika jina la Yesu, Falme za Giza za familia/ukoo wangu Mimi, Falme za Giza la eneo la makazi, biashara, kazi au eneo lolote la uzalishaji, Falme za Giza za
Mji, Falme za Giza za mkoa, falme za Giza za nchi ambao mmepewa na nguvu na yule mnyama wa ajabu! Mkawasukuma wachawi na washirikina na waganga wa
kienyeji wanifuatilie ambazo mnazuia njia zangu, mnaniwekea ukuta, mnaniletea mateso Mengi. Mnapinga kila kitu Mungu alichonipa mnapinga kuendelea kwangu
Leo kwa damu ya Yesu. Leo katika jina la Yesu ile damu ya mwanakondoo ya vita naachilia juu yenu sasa popote mlipo katika ardhi, anga, au baharini kwa damu
YESU, KWA DAMU YA YESU ninawaponda sasa kwa mkono wa Mungu, naachilia mishale ya Moto juu yenu, Kwa damu Ya Yesu nakuja na kiti cha Yesu ninawangoa
katika nafsi mlizo kuwa mmekaa na kuzimiliki katika jina la Yesu Kristo. Kwa kiti cha Yesu, Kwa damu ya Yesu ninawangoa na kuwatupa wote kwenye
Shimo la Moto kuzimu Falme zote zinazonifuatilia katika jina la Yesu Kristo! Naharibu network zao zote kwa damu ya Yesu Kristo! Naharibu kazi zao zote kwa
DAMU YA YESU KRISTO! ninawafuta kazi katika nafasi zao, ninawafuta kazi katika maeneo yote niliyoyataja kwa damu ya Yesu, maeneo hayo nayamiliki kwa damu
ya Yesu, ninawafukuza ninawafunga na
Kamba za Moto wa Roho Mtakatifu kuwatupa nje katika nafasi zao ninajiweka wakfu Mimi mwenyewe ndio mtawala
kuanzia Leo hii KWA DAMU YA YESU! KWA DAMU YA YESU, KATIKA JINA LA YESU KRISTO! Baba katika jina la Yesu Kristo katika eneo hili ninaloishi au
Kufanya kazi, au biashara au huu mji niliopo, na mkoa huu na nchi wako wakuu wa anga wanipingao kutumia kiti cha enzi cha ibilisi nami katika jina la Yesu Kristo
Enyi wakuu wa anga mkuu wa anga wa eneo ninaloishi, mkuu wa anga wa mji , mkuu wa anga wa eneo la biashara, mkuu wa anga wa eneo la kazi, mkuu wa anga
wa eneo la huduma wewe mkuu wa anga unayenipinga katika mambo yangu yote naachilia damu ya Yesu ya vita juu yako sasa! Ninakungoa katika nafasi yako kwa
damu ya Yesu. Ninaharibu network yako kwa damu ya Yesu, naharibu njia zako kwa damu ya Yesu, ninaamuru Moto wa roho mtakatifu ukuharibu na kukungoa
kwa damu ya Yesu! Ninakuja na kiti cha Yesu wewe mkuu wa anga popote ulipo katika ardhi, anga, bahari au chini ya bahari ninakungoa ninakungoa
ninakungoa kwa damu ya Yesu! Nafasi yako nakunyanganya kwa damu ya Yesu, kwa damu ya Yesu! Haijalishi umetokea katika familia yangu, ukoo
wangu, eneo ninaloishi au kufanya kazi, au kuabudu, au upo tokea kwenye mtaa, mji au mkoa hata nchi nakungoa wewe na kiti chako kwa damu ya Yesu,
nakuporomosha kwa damu Yesu. Katika jina la Yesu. EE Mungu Baba jeshi la pepo wabaya linalofanya kazi kupitia familia,ukoo,eneo nalokaa, kufanya kazi,
biashara, mji, mkoa hata nchi ambao Wapo kinyume nami, naachilia majeshi ya Jehova Bwana ya Malaika napambanisha na Jeshi la pepo wa baya
kwa damu ya Yesu Kwa damu ya Yesu, enyi jeshi la pepo wabaya mnaofanya vita na Mimi nawashushia mawe ya Mungu yawapige na kuwavunja katika jina la
Yesu,nawashushia mvua ya damu ya Yesu, na mvua ya Moto wa Roho Mtakatifu, na radi ya Mungu, katika jina la Yesu, nawashushia mishale ya Moto, Moto wa
Roho Mtalatifu, naachilia Damu ya Yesu ya vita popote mlipo Katika anga, baharini, au nchi kavu nawafuta kabisa msionekane kwa damu ya Yesu Kristo.
Katika jina la Yesu. Kila nguvu yoyote inayotokana na damu iliyomwaga ikinuiziwa jina langu ambayo inawapa mapepo nguvu ya kupigana na Mimi
naachilia damu ya Yesu, ninavunja maagano na mikataba ya damu za ndege, wanyama au watu katika jina la Yesu, naachilia damu ya Yesu inene mema juu
yangu sasa katika jina la Yesu Kristo. Katika jina la Yesu Kristo enyi Falme za Giza za shetani, enyi wakuu wa Giza wa shetani, enyi wakuu wa anga, na Jeshi
La pepo wabaya ambao mnafanya vita na Mimi kwa kupinga maombi, kwa kunikatisha tamaa, kwa kunichosha, kwa kufunga njia zangu, kufunga hatua zangu
Nyie mnaowapa nguvu mizimu, majoka, waganga wa kienyeji, wachawi, washirikina nyie mnaoniinulia maadui usiku na mchana, nyie mliofunga afya
Yangu, mkafunga na uchumi wangu. Biashara yangu, ndoa yangu mkaifanya iwe mateso, nyie mnaoniletea mateso machungu katika maisha yangu, mmefa
Nya kila aina ya hila kunichelewesha katika Baraka zangu, kuziharibu, kila jambo baya mlilolifanya juu ya maisha yangu, kunifunga na nguvu za Giza, vita
Vyote mishale yote mliyoielekeza kwangu, Leo ni mwisho ninawapinga kwa damu ya Yesu, nakuja na shoka la Mungu, nakuja na damu ya Yesu ya vita, ninakuja na kiti
Cha enzi cha Yesu kwa damu ya Yesu, ninakuja na hasira za Mungu, tetemeko la Mungu. Nakuja na nyundo ya Mungu, naachilia juu yenu mvua ya damu ya Yesu
Mvua ya Moto wa Roho Mtakatifu katika jina la Yesu. Popote mlipo sasa katika anga ardhini au baharini ninainua malaika wa vita, ninawaharibu kwa izo silaha sasa
Katika jina la Yesu ninashusha kipigo ninawavunja vunja na mawe ya Mungu kwa jina la Yesu ninawasambaratisha, ninawaharibu, ninawabomoa ninawangoa
Katika nafasi zenu, kwa jina la Yesu, hamtakaa tena kwenye izo nafasi ninawafuta kazi kwa damu ya Yesu, ninapigana na malaika wa jeshi la Bwana
kutumia ardhi, anga, au bahari kwa damu ya Yesu Kristo, katika jina la Yesu, Moto sasa wa Roho Mtakatifu usiovumilika uwasambaratishe kwa jina la Yesu.
Ninawaondolewa ufalme wenu na umiliki juu yangu, kwa damu ya Yesu, tokeo Leo hii mtakakuwa chini ya nyayo zangu kwa damu ya Yesu Kristo. Katika jina la Yesu.
Silaha yoyote itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa kwa jina la Yesu. Ninajifunika sasa kwa damu ya Yesu! Na kwa Moto wa Roho Mtakatifu. MUNGU
BABA ninaomba sasa malaika wako wa ulinzi aje kunilinda Mimi na watu na vitu vyangu vyote vinavyonizunguka. Nikijizungushia damu ya Yesu ya ulinzi na
wigo wa Moto wa roho Mtakatifu. Ninaomba nikishukuru. Roho Mtakatifu naomba utumie haya Maombi machache kufanya zaidi nilivyo omba na kufikiri katika jina la Yesu. Ameen
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Neno zuri...pia kuongezea hapo nyama juu ya MKUU WA GIZA soma hapa >>> https://wingulamashahidi.org/2019/02/28/mkuu-wa-giza/
ReplyDeleteSOMA HII UTAKUJA NISHUKURU
ReplyDeleteKATIKA SAFARI YA MAFANIKIO TUNAPITIA MENGI ILI TUWEZE KUFANIKIWA LAKINI WENGI WETU KUNA MAMBO MACHACHE SANA WENGI WETU TUNAYADHARAU NA KUMBE NDIO CHANZO CHA MAFNIKIO YETU.
N.B KWA WALE WAHITAJI WA PESA ZA NDAGU au MAJINI kwa mudamfupi nipigie DOKTA MDIRO +255 742162843
HAYA NI MAMBO 7 YAKUZINGATIA KATIKA SAFARI YAKO YA MAFNIKIO
i) Wazazi wako wakiwa wamekulea mpaka ukawa mkubwa wafumbua macho unawaona akikisha usiwafanye wakajuta kukuzaa asilimia kubwa wazazi wanakuwa na tabu sana ila zile tabu zao ndio zinazokufanya wewe una aminiwa na watu na unaeshimika na kujieshimu
Kwaiyo jitahidi sana kuwa nao vizuri kuna wengi maisha yao wanaishi kwa shida chanzo ni utofauti baina ya wazazi wao
Ukiona wazazi wako wanatabu sana usiwajibu vibaya wewe kaa nao mbali ila wape majukumu yao unacho fanya kuwaona nakurudi ulipo apo utaona mambo yako yatakuwa vizuri sana
ii) JAMBO LA PILI
Akikisha unatunza uzao wako yani ukijua ni mtoto ni wako basi jitahidi sana kutoa uduma ata kidogo ulicho nacho lakini udumia usiache uzao wako unateseka na njaa wewe una kula maisha aisee fahau
Kila mtoto wako anavyo kuwa ndio mambo yako yanaaribika usipo udumia kwaiyo ukiwa waitaji kufanikiwa zaidi jali uzao wako
iii) JAMBO LA TATU
ukiwa umeoa au umeolewa usitoe talaka au kuomba talaka kabla mwenzio ayupo tayari kwa muda huo fahamu ukiomba talaka au akikupa talaka bila bila sababu ya msingi yeye tu ana matamanio ya kidunia basi anamuda atapoteza muelekeo wa maisha yake
iv) UKIWA WAPATA PESA
ukiwa wapata pesa alafu utoi sadaka basi kufikia kwenye ukuu utachelewa sana mana mana pesa badala ya kutoa kwa iyari yako utatoa kwa matatizo kwaiyo jitahidi icho icho kidogo toa sadaka kwa wenye uitaji
v) USIMZULUMU MTU
kama wataka kufika mbali kwenye mafanikio yako usimzulumu mtu ata kwa uchache wa kitu usifanye ivyo itakugarimu kiasi kikubwa
vi) USIZARAH MILA
ukiwa kwenu kuna mambo ya mila mzimu tambiko jitahidi kufatilia sana aya mambo yanarudisha nyuma sana usipo yawahi mapema
vii)USIWE WA NAMNA
1)ikiwa ujafanikiwa jitahidi sana usiwe mvivu kufanya kazi usiwe muhuni usiwe mwenye chuki na asira zisizo za msingi usiwe na tamaa nyoa vizuri vaa nguo za eshima na usiige maisha ya watu TAWALA ZA MAJINI NA TIBA ZAKE NA NJISI YA KUWA TUMIA @highlight Following Everyone Products millard ayo TIBA ZA ASILI MAJINI NA UCHAWI 0715907487 TIBA ASILI NA NYOTA,PETE ZA MIVUTO NA MAJINI Follower sale KENYANS LIVING IN USA 🇺🇲🇬🇧
KWA MAWSILIANO ZAIDI KUHUSU MATATIZO MBALIMBALI YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA, PETE MALI ZA NDAGU NA MAJINI N.K
DOKTA MDIRO Call/whatsup +255 742162843.