WEWE SI WA KWANZA KUMNUNGUNIKIA MUNGU

Bwana Yesu asifiwe!

Yapo maswali ya msingi!? ROHO MTAKATIFU aliruusu nimuulize nilipokuwa narudia kusoma vitabu vya Musa. Ambayo hayo maswali yananihusu Mimi wewe na kanisa! 🏽

#Maswali yenyewe

1. Kwanini kila saa wana wa Israeli walikuwa wanamngunikia na kumlalamikia Mungu?

2.Kwanini kitu kidogo wanatamka au wanataka kurudi misri. Utasikia ni "bora tungefia misri utumwani"? Nini kiliwasukuma kutamka maneno hayo?

3. Kwanini walikuwa wanafananisha shida yoyote mpya  na mateso ya misri?

4.Kwanini walikuwa tayari kurudi misri utumwani lakini si kuendelea mbele na changamoto mpya?

5. Kwanini walikuwa ni wepesi kukata tamaa na kuchoka wakati tayari walikuwa huru? Inakuwaje mtu yupo huru alafu anachoka na kukata tamaa?

6.Kwanini ni wepesi wa kumnungunikia Mungu zaidi ya kuuliza majibu au maswali? Nini kiliwasukuma kunungunika? Walipata madhara gani kumnungunikia Mungu?

7. Kwanini ilikuwa rahisi kwao kutamani kurudi utumwani kuliko kupita jangwani? Au Kuna tofauti gani mtu akiwa utumwani na mwingine akiwa jangwani?

Unajua its very very interesting story kiasi nilipokuwa nasoma nikawa ninacheka mwenyewe. Would like to hear!!! Alafu tuangalie kwa undani? Ni story ambayo Roho Mtakatifu akikupitisha utafurahi...

# Tuangalie baathi ya malalamiko na Manunguniko kwenye biblia...

🌴 TUANGALIE LALAMIKO NA SABABU YA KULALAMIKA. ALAFU BAADA YA KUPITA KATIKA BAADHI YA MALALAMIKO IM SURE ROHO MTAKATIFU ATAONGEZA KITU NDANI YAKO.

# LALAMIKO LA 1- MUSA

Kutoka 4-10
. Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.

Kutoka 4:11
. Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana?

Kutoka 4:12
. Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.

Kutoka 4:13
. Akasema, Ee Bwana, nakuomba, tuma kwa mkono wake huyo utakayemtuma.

# Mara nyingi Mungu anapootaka kuanza kutembea na wewe huwa hatuamini ile safari tunayooenda na BWANA, MUSA alitoa visingizio vyote alilalamika kote! Lakini Mungu hakumsikiza. Hii haina tofauti na Mimi na wewe tunayeomba usiku na mchana

Mungu akianza kushughulika na wewe kwa kutoa moyo wa jiwe na kuweka moyo wa nyama huwa tunaanza visingizio au malalamiko. Kama njia yenyewe ndio hii Mimi siwezi kabisa utasikia mtu akimwambia " Mungu siwezi tena haya majaribu nimefika mwisho" I

cant take it anymore! Yani Mungu nimefika mwisho wa kuvumilia hii haina tofauti na Musa alimwambia Mungu Mimi si msemaji toka zamani? 😊 Hapa nacheka jinsi Mungu alivyomjibu Musa unajua Mungu alikuwa anamajibu ya kufurahisha akamwambia Musa nani ametengeneza kinywa na

sauti? Si Mimi Mungu? Kama Mimi ndo niliyokupa kinywa na sauti kwanini unalalamika? Lakini Musa bado kikubwa HAPA MUSA
1. ALIKUWA SI JASIRI
2. HAKUMWAMINI MUNGU
na pengine ni kutokana na historia ya Musa maana kipindi kile alikuwa mchunga mifugo ya Baba mkwe

wake. Sasa akipiga picha anaona haiwezekani Pilato ataniuwa. Wasiwasi wake ni huu! Je vip kama Mungu asipo ni back up! Vip kama itakuwa ndivyo sivyo maana hata Mungu nayeongea naye hapa simuoni. Lakini Farao nimemuona na ninamjua wasiwasi wa kuanza safari ni huu vipi kama itaenda

ndivyo sivyo? Vip kama Mungu asiponiback up! Ninahakika gani Mungu hataniacha katika hii safari. Ni sawa na wewe Mungu amekuambia fanya kitu flani bado unawasiwasi je nitafanikiwa kweli?  Je Mungu atakuwa na Mimi kweli. Hii ndo sababu ya manunguniko. Kwa iyo learn to trust God sababu

always Mungu huja na kitu kipya kabisa kwako. Hawezi kuja katika njia unazofikiri wewe. Wengi badala ya kutake step tumekuwa na manunguniko Mengi na malalamiko. Na inazuia Mungu kufanya na wewe kazi katika hatua inayofuata. JINA LA BWANA LIBARIKIWE

# LALAMIKO LA 2 - WANA WA ISRAELI

Kutoka 5:20
. Wakakutana na Musa na Haruni, waliokuwa wanasimama njiani, hapo walipotoka kwa Farao;

Kutoka 5:21
. wakawaambia, Bwana awaangalie na kuamua; kwa kuwa mmefanya harufu yetu kuwa chukizo mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, mkatia upanga mikononi mwao, watuue.

Kutoka 5:22
. Musa akarudi kwa Bwana, akasema, Bwana, mbona umewatenda mabaya watu hawa? Kwani kunituma mimi?

Kutoka 5:23
. Kwa maana tangu nilipokwenda kwa Farao, kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa; wala hukuwaokoa watu wako hata kidogo.

# Sasa si Musa tuu hata wana wa Israeli inawachanganya! Nataka nikupe siri njia za Mungu ni nzito haziwezi kuja kibinadamu binadamu angalia maagizo ya Mungu yanamchanganya Musa yanawachanganya wana wa Israeli,

yanamchanganya na Farao, na yanawachanganya na manyapara wa wana wa Israeli. Ukiniuliza katika Roho hapa MUNGU alikuwa ana draw attention ya kila mtu. Kwa iyo usiogoe kuanza kitu alafu mwanzoni tuu ukakutana na vikwazo jua kuwa ni MUNGU

anataka akutambulishe, jua kuwa ni Mungu anataka ajitambulishe. Ivyo acha kulalamika unakutana na vikwazo mwanzoni. Mwingine anasema lakini Mungu ameongea na Mimi kabisa. Nimeota ndoto nimeonyeshwa hii biashara nimeonyeshwa hii kazi. Nilimuota uyu niliyeona naye lakini mbona

mambo yamebadilika? Sikiza mambo hayajabadilika isipokuwa Mungu alikuwa anasema msingi wake. Bwana Yesu asifiwe. Watu wengi baada ya kuomba na kupata walichooomba ile wanaanza tuu wanakutana na upinzani mkubwa matokeo yake wanaanza kumlalamikia Mungu. "Mungu

nilikuomba mtoto sikuomba haya mateso, Mungu nilikuomba biashara sikukuomba madeni, Mungu nilikuomba kazi lakini mbona sipati mda wa kukuabudu, Mungu hivyo sivyo nilivyokuomba why I'm I getting this! Wana wa Israeli wakamfuata Musa kwa hasira wakamwambia Mungu aamue Kati

yetu sisi na wewe. Maana wewe Musa umetuwashia Moto kwa Farao. Sasa angalia wana wa Israeli wanalalamika na Musa naye analalamika maana pressure ilikuwa kubwa Sana kwake. Ni kawaida kabisa Mungu akishakupa kitu unachotaka suprize ya kwanza

kukutana nayo ni mkwamo. Ni mkwamo! Sasa sikiza haukuwa mkwako Mungu alikuwa ana draw attention vichwani mwao!  Hii haina tofauti na kumuombe mtu Abadilike aache pombe unakuta siku iyo ndo kwanza harudi home analala bar! Kisha unarudi kwa Mungu kunungunika badala la kumshukuru

hajui ya kwamba Mungu ameweka introduction sasa miungu ya farao imechanganyikiwa haujui ni dalili ya kwamba Mungu anaenda na wewe. Sasa angalia Musa analalamika wana wa Israeli wanalalamika. Hii haina tofauti upate imani kuu kwenye neno alafu unaweka katika

matendo alafu ndo hali inakuwa ngumu Mara 2. Kila Mara akili ya Musa na wana wa Israeli ilipokuwa haimuelewi na Mungu ilikuwa inalalamika inanungunikia Mungu. Bwana Yesu asifiwe!

# LALAMIKO LA 3
WANA WA ISRAELI

Kutoka 14:11
. Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri?

Kutoka 14:12
. Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani.

# Nataka nikuonyeshe hakuna ambacho unapitia kutenda au kufikiri ambacho wana wa Israeli hawakupitia kuongea au kutenda Mungu anakujua ndo mana aliyaandika haya katika biblia ili kwa wakati unaofaa uje usome ujue. JINA LA BWANA LIBARIKIWE!

# angalia tena malalamiko ya wa Misri tena maneno mazito wakamwambia wewe Musa si tulikuambia tuache Misri? Tuwe watumwa wa Misri? MAANA afadhali kuwatumikia wamisri kuliko kufa jangwani! Au unafikiri Misri kulikuwa hakika makuburi ya

kutuzika? Daah kwa kweli haya yalikuwa ni maneno mazito Sana kwa Mungu. Sasa angalia hapa walianza na vikwazo safari Yao ya kwenda kaanani wakapitishwa ile tena wanataka kupita kikwazo kimoja Mungu tena anataka ajitwalie utukufu akaleta mkwamo

ambao akili zao ziligoma kabisa maana nyuma majeshi ya farao yanakuja! Mbele Kuna bahari! Wakifikiri aliyesababisha haya ni nani ni Musa! Maana Musa ndo aliyeanzisha ugomvi huu! Kumbe watu hawa miaka 400 akili zao zimezoezwa kutii to take order.

Hazijazoezwa kupambanua njia no! Hazina second option or alternative. Mtumwa manake ni kutii sheria, manake ni kufuata Njia adui aliyokudesign wewe kuifuata. Kwa zinapokuja njia mpya tofauti na akili ya Farao akili huwa haitaki maana haijazoea mapambano! Haijazoea

kujinasua katika tatizo ni sawa na wewe ukiwa utumwani wa mda mrefu huwa unakubali matokeo na kusema maisha ndivyo yalivyo ngoja nikubaliane nayo nitabisha mpaka lini? Ndivyo akili yake ilivyojitengeneza umezoea umasikini, umezoea mfumo dume wa kukaliwa, umezoea unyonge,

umezoea upweke, umezoea kukaa kimya, umezoea kuitikia wenye pesa , hata kama hutaki, sasa inapokuja njia ya kukutoa hapo akili inagoma maana haijazoea vita, haijazoea kuona mambo. Akili ishajiset na haitaki usumbufu. Na Mungu anataka sasa akili yako itoke utumwani. Lakini bado wewe

unangangania utumwani. Ushawi ona Mungu anamvusha mtu lakini uyo mtu bado anamlalamikia Mungu. Kuwa lakini nimeumia Sana! Miaka yote hii nimekusubiri Mungu. Ndio umenivusha lakini nimechakaa Mungu hivi Mungu hunioni? Miaka 8   ndo nakuja kuolewa kweli Mungu? Nina miaka 43 ndo napata

mtoto wa kwanza kweli Mungu. Hiki ndicho wana wa Israeli walikuwa wanamuambia Mungu. Mtumwa siku zote huwa anatafuta pa kulalamika hata sipo atalalamika tuu. Hata akiambiwa bwana yashaisha ataendelea kulalamika. Ndicho wana wa Israeli wanachomuambia Musa. Afadhali kule kuliko hapa. Na mwisho

nitakueleza kwanini ilikuwa hivi. Bwana Yesu asifiwe. Nafsi zao zilikuwa zimejaa malalamiko. Na zilimzuia Mungu wakati mwingine alikasirika na wakati mwingine Musa alikasirika.

# LALAMIKO LA 4 - WANA WA ISRAELI NA MUSA

Hesabu 11:4
. Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N'nani atakayetupa nyama tule?

Hesabu 11:5
. Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu;

Hesabu 11:6
. lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu.

Hesabu 11:11
. Musa akamwambia Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako? Kwa nini sikupata neema machoni pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu?

Hesabu 11:12
. Je! Ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye, uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao?

Hesabu 11:13
. Nipate wapi nyama ya kuwapa watu hawa wote? Kwani wanililia, wakisema Tupe nyama, tupate kula.

Hesabu 11:14
. Mimi siwezi kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni mzigo mzito sana wa kunishinda.

Hesabu 11:15
. Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie mbali, kwamba nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka yangu.

# wana wa Israeli walikuwa wanalalamika kwa kila kitu! Hawajawahi kuridhika na kitu Mungu anachofanya. Walikuwa na njaa wakamlalamikia Mungu. Mungu akashusha mana baada ya mda wanasema mana imewachosha imewakinai wanataka
nyama, sasa cha ajabu hawa walikuwa hawaombi walikuwa wanalalamika. Sasa kitu ambacho nilicheka ni jinsi Musa alivyoenda kwa Mungu aliongea maneno mazito kwa kweli ni vile tuu ni mtumishi mbele ya Mungu na ana neema ya Mungu. Ndio maana usije

muona mtumishi kaongea na wewe ukamwiga utajikuta kwenye matatizo na Mungu. Musa anamwambia Mungu mimi ndiyo niliyowatungisha mimba watu wote hawa wakazaliwa?  Anamwambia Mungu mbona umenitenda uovu? Je
sikupata neema machoni pako? Nipate wapi nyama ya kuwapa wote hawa! Mimi siwezi kuchukua mzigo huu peke yangu ni mzigo mzito sana, akamwambia Mungu kulikoni uendelee kunitenda hivi naomba uniulie mbali. Au nifadhili mbele ya macho yako nisiyaone mashaka

yangu. Malalamiko ya wana wa Israeli ilikuwa ni too Much, walikuwa wanalalamika mpaka wanamkwaza Musa wanasababisha Musa kumkasirikia Mungu. Je ni mara ngap kutokuridhika kwako umejikuta unamkasirikia Mungu. Na kuongea maneno ya ovyo? Wana wa
Israeli walikuwa wananungunika na kulalamika safari yao yote. Nakwambia wewe unalalamika na kunungunika lakini hujawafikia wana wa Israeli. Walikuwa hawana asante wala shukrani mbaya zaidi badala ya kuomba wananungunika? Mara ngap manunguniko yako yamemtia mtu katika dhambi au

yamemkwaza kama Musa. Nikawa najiuliza hivi akiwekwa huru anatakiwa awe mtu wa shukrani au malalamiko? Why kumlalamikia Mungu. Vitu vibaya unalalamika, vitu vizuri unalalamika Mungu hapa amekaa kimya tuu. Anawavumilia tuu. Nikawa najiuliza hivi Mungu alikuwa anajisikiaje? Moyoni

mwake? Kuona kwamba hawa watu nimewatoa misri kwa gharama kubwa, hawa watu nimetumia nguvu nyingi hawa watu nimewatendea mazuri yote bado wananilalamikia.

# sasa angalia Mungu alichokifanya WALE WALIOKUWA wanatoa malalamiko sababu ya TAMAA ya nyama. Kumbe tamaa ya nyama ilianza zamani haikuanza leo angalia hapo. Ili uepuke tamaa sabaabu itakusababishia kumlalamikia Mungu, na kumnungunikia Mungu.

Hesabu 11:31
. Kisha upepo ukavuma kutoka kwa Bwana, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, kuizunguka, nao wakafikilia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi.

Hesabu 11:32
. Watu wakaondoka mchana huo wote, na usiku huo wote, na siku ya pili yote, kuwakusanya hao kware; yeye aliyepata ya upungufu kuliko wenziwe alipata kiasi cha homeri kumi; nao wakawaanika wote kando-kando ya kambi kuizunguka pande zote.

Hesabu 11:33
. Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za Bwana ziliwaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno.

Hesabu 11:34
. Jina la mahali pale likaitwa Kibroth-hataava; maana, ni hapo walipowazika hao watu waliotamani.

# MUNGU alichofanya akawakomesha 😊 mtu aliyepata kware wa chini ilikuwa kware 10! Kwa iyo wakaaanika wakawachoma mwisho wake nyama zikawashinda matokeo yake Mungu akaachia mapigo na wale walafi wamero wa nyama wakafa pale kwa pigo la Mungu. Hii inatufundisha usiforce vitu! Subiri wakati wa Mungu utajikuta katika mauti usipokuwa mwangalifu

# LALAMIKO LA 5 - MARIAM NA HAROON

Hesabu 12:1
. Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

Hesabu 12:2
. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.

Hesabu 12:3
. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

Hesabu 12:4
. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.

Hesabu 12:5
. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.

Hesabu 12:6
. Kisha akawaambia,

Hesabu 12:7
. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;

Hesabu 12:8
. Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

Hesabu 12:9
. Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.

Hesabu 12:10
. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.

# Haya ni malalamiko yanasababishwa na wivu, au ni sawa na kumuambia Mungu kwanini umembariki uyu kwanini usinibariki mimi. Mungu kwanini yule anakaa sehemu nzuri jumba zuri, kwanini anatembea Landcruser

V8, kwanini anaenda safari ya nje, kwanini kwake kumuona Raisi ni kitu cha kawaida, kwanini anapendwa mimi sipendwi!? Kwanini anakibali? Kwanini ana mafanikio? Kwani Mungu tofauti yake na mimi ni nini? Ni sawa na

kumuambia Mungu wewe unaupendeleo ndiyo tafsiri yake. SO BE CAREFUL WITH JELOUS INAWEZA KUKUFANYA UMLALAMIKIE MUNGU AU MAOMBI YAKO YAWE NA MALALAMIKO! AU MANUNUNGUNIKO. ubaya wa

manunguniko na malalamiko wakati unayafanya si raisi kuyatambua . Wivu mbaya huleta manunguniko na malalamiko. Angalia Mungu aliachia ukoma kwa Mariam na Haroon! Sasa ukoma bado upo. Uko manake kutokupiga hatua. Bwana Yesu asifiwe sana

# LALAMIKO LA 6 WANA WA ISRAELI

Hesabu 14:1
. Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.

Hesabu 14:2
. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.

Hesabu 14:3
. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?

Hesabu 14:4
. Wakaambiana, Na tumweke mtu mmoja awe akida, tukarudi Misri.

Hesabu 14:10
. Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.

Hesabu 14:11
. Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.

Hesabu 14:12
. Nitawapiga kwa tauni, na kuwaondolea urithi wao, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, kisha yenye nguvu kuliko wao.

Hesabu 14:26
. Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

Hesabu 14:27
. Je! Nichukuane na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hata lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo.

Hesabu 14:28
. Waambieni, Kama niishivyo, asema Bwana, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;

Hesabu 14:29
. mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia,

Hesabu 14:30
. hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliinua mkono wangu ya kwamba nitawaketisha humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

Hesabu 14:31
. Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi ninyi mliyoikataa.

Hesabu 14:32
. Lakini katika habari zenu, mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili.

Hesabu 14:33
. Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arobaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hata mizoga yenu itakapoangamia jangwani.

# Hawa watu walikuwa wanalalamika sijawahi kuona angalia maneno yao! Yalikuwa mazito "ingekuwa ni heri kufa katika nchi ya misri" wangap washawahi kutamani kufa sababu ya changamoto✋🏾? Umetuleta mpaka nchi hii tuanguke kwa upanga?

Wake zetu watoto wetu watakuwa mateka? Wakaambiza tuchukue mawe tuwapige hawa haroon na Musa mara utukufu wa Bwana ukawazukia. MUNGU AKASEMA NA MUSA HAWA WATU WATANIDHARAU MPAKA LINI? HAWA WATU HAWATANIAMINI MIMI MUNGU MPAKA LINI?

nijapofanya ishara zote hizo bado wananidharau! HAPA MUNGU ALIKASIRIKA KWELIKWELI.  tuangale kilichotokea baada ya Mungu kuchoshwa na malalamiko na Manunguniko ya wana wa Israeli.

Hesabu 14:36
. Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung'unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi,

Hesabu 14:37
. watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya Bwana.

Hesabu 14:38
. Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.

# Mifano ni mingi sana hatuwezi kuimaliza kwa kifupi safari ya wana wa Israeli ilijaa manunguniko kwa Mungu. Sababu ya kutokuridhika, saa ingine kutokuwa na shukrani mbele za Mungu. Wivu, fikra kufika mwisho! LAKINI KUBWA KULIKO YOTE NILIPOMUULIZA MUNGU

KWANINI HAYA YALIKUWA HIVI ALINIPELEKA KATIKA HILI ANDIKO. HIVYO BAADA YA KULIANGALIA MUHIMU KUANGALIA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU JE NI YA MALALAMIKO, NA MANUNGUNIKO?

MAHUSIANO YAKO NA WATU WANAOKUZUNGUKA NA KUISHI NAO JE NI YA MANUNGUNIKO NA MALALAMIKO. manunguniko na malalamiko ni ukuta mkubwa sana. Wengi waliokufa jangwani ilikuwa ni sababu ya malalamiko na

manunguniko! Kweli safari ya jangwani si nyepesi but muhimu kuepuka manunguniko na malalamiko! Na wengi hawakufika kaanani sababu ya malalamiko na manunguniko. Ivyo angalia sana epuka sana manunguniko na malalamiko unapokuwa jangwani.

Ukiangalia hapo hawa watu walikuwa hawapambani na farao but MUNGU, NA WANA WA ISRAELI ILIWAGHARIMU SANA, ILIWAGHARIMU MNO!WENGI TUNATABIA YA KULALAMIKA BAADA YA KUOMBA AU KUTOKUONA MATOKEO! AU

KUMWADISIA MTU KAMA USHAMKABITHI MUNGU KITU KWANINI KUTAFUTA ushauri kwa binadamu? Hicho ndo Mungu alimuuliza Musa hawa watu watanidharau hata lini? Hawataniamini hata lini!? Kwa IYO SABABU KUU MUNGU ALIYONIONYESHA HII HAPA

Kutoka 6:9
. Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.

UCHUNGU WA MOYO NA UGUMU WA UTUMWA. unapopitia magumu moyo huwa unajenga uchungu ndani na kumbukumbu yake hukaa katika nafsi! Ugumu wa utumwa manake ni ile hali ngumu unayopitia mfano ile hali ngumu ya kutokuwa

na pesa za kuishi. Ule upweke wa kuwa lonely kuwa mpweke! Ule ugumu wa kulea watoto kwa shida na mateso, ule ugumu wa kukaa bila kupata kazi na una elimu. Kwa iyo inaumiza ndani ya mwili na nje ya mwili. Ni kitu ambacho kinaumiza

watu wengi sana kwa ndani manake moyoni. Kwa nje manake mwilini. Bwana Yesu asifiwe na ibilisi hutumia hii kuwaumiza watoto wa Mungu kwa makusudi. Sasa unapokuwa katika hali hii unahitaji healing ya Bwana Yesu. Hakuna

anayeweza kuitoa hali hii mpaka Yesu mwenyewe na  hiii inasababishaga watu kunywa pombe ili wasahau hawataki kukumbuka those days! Those tuff moment! Sasa unaweza kuja

naswali ninafanyaje sasa kutoka katika hali iyo ili nisilalamike au kunungunika! Ndio swali lako right?
🏾iyo ndo sababu kuu ya mtu kuwa na malalamiko na manunguniko ivyo vingine ni matawi tuu

# unapotumia dhambi ili kujisaulisha uchungu wa moyo na ugumu wa utumwa kumbuka unajipeleka motoni. Wengi hujikuta wakifanya mambo hata ambayo hawakuyapanga wamekuta wakinunua vitu ovyo, wamejikuta

wakienda katika starehe! Kama disco, casino, bar tena kwa siri! Wamejikuta wakifanya uzinzi na uasherati! Wakifanya dhambi kwa siri za kujificha ili wasionekane na waliokoka! Behind the doors! Unakuta mtu kaokoka then anajifungia chumbani anakunywa

wine, wiski, yani alimradi tuu ili kumbukumbu ya uchungu na utumwa wa moyo iondoke lakini bado. Sasa inapozidi ndani ya mtu ndipo kunakuwa na malalamiko na manunguniko. Malalamiko na manunguniko ni ishara ya kwamba

mtu wa ndani amejaa uchungu, mtu wa ndani amechoka sababu ya utumwa sababu ya matatizo Bwana Yesu asifiwe!

# KWA IYO USIISHI NA UCHUNGU WA MOYO, WALA USIISHI NA KUMBUKUMBU YA UGUMU ULIPOKUWA UTUMWANI. inaadhiri vitu vingi sana.
1.inaadhiri mahusiano yako na Mungu, mtu unayemlalamikia sana kibali mbele yake huwa kinakufa

2.inaleta kutomsikia Mungu anaposema Mungu husema kwa njia nyingi ikiwepo ndoto, maono, sauti,mawazo yako mwenyewe. Atakapokuwa anasema hutamsikia sababu ya uchungu wa moyo

3.inaleta wivu,hasira,kuwadharau wengine,inaleta saa ingine ubishi wa neno la Mungu au kuwadharau watumishi wa Mungu

4.inaondoa furaha na amani moyoni na nafsi yako kila mara inainama

5.inakufanya kutokuwa na mahusiano mazuri na watu sababu ya negative perception about everything.

Bwana Yesu asifiwe. Vipo vitu vingi ivyo ni baadhi tuu.

# Hatua za kujifungua katika uchungu na ugumu wa utumwa
1. Tambua kwamba huwezi mwenyewe ivyo jisalimishe kwa Bwana Yesu Mwambie siwezi naomba nisaidie! Yesu husaidia watu watiiifu wanyenyekevu, waliopondeka! Healing ya mtu wa

ndani ni ya Bwana Yesu! Shetani he dont akishaharibu anaondoka. Mwambie Bwana Yesu siwezi mwenyewe naomba unisaidie nahitaji kutoa uchungu ndani yangu but siwezi mwenyewe! Nahitaji kutoa kumbukumbu mbaya za ya magumu niliyopitia Halleluyah. Bwana Yesu asifiwe watu wa

Mungu. Omba rehema kwanza kwa kuwa umeenda kwa akili zako mwenyewe! Omba rehema kwa kuchukua nafasi ya roho Mtakatifu, omba rehema kwa kuamua kuchukua nafasi ya Mungu. Na kutaka kujiponya mwenyewe you

can not heal your self only God can. Ivyo just say Jesus im sorry kwa juhudi zangu nimeshindwa please help me.

# Hatua ya pili achilia damu ya Yesu ya ufunuo 5:9 ile damu ya kununua ilinunua mpaka uchungu wako wa moyo, ilinunua utumwa wako wa moyo. BWANA YESU ASIFIWE! Sema uchungu wa moyo naachilia damu ya Yesu ya kuninunua nakufita ndani yangu. Ni damu ya

Yesu pekee inayoweza fanya impossible's usiumize kichwa Damu ya mwanakondoo ilimwagiga kwa ajili ya mambo yaliyoshindikana unapoimwaga tuu tayari inaleta uponyaji! Inajua ifanye nini. Hii damu ilipomwagiga juu ya ardhi ilifuta laana zote za kaini, adamu na
laana zote ivyo chochote kinachokusumbua usiimize kichwa itakuwaje au ifanyikaje. Nenda madhabahuni kwa kuhani mkuu. Sema sema nachukua damu ya Yesu ya Ki Mungu iliyoninunua sawasawa na Ufunuo 5:9 naachilia iyo damu sasa katika uchungu wa

moyo! Kumbukumbu za ugumu au magumu niliyopitia nakuambia baada ya kufanya hayo utarudi hapa na ushuhuda. Maana ufunuo huu ni katika roho mtakatifu. Wewe

unayehitaji uponyaji wa moyo, nafsi au kumbukumbu za ugumu wa mambo do it right now, apply Blood of Jesus. Maombi mazuri ni ya kujiombea mwenyewe Jina la Bwana libarikiwe sana.

JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu

josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA