NI MPAKA UMEWEKA UPENDO KATIKA KATIKA MATENDO NDIPO UTAANZA ONA MAFANIKIO NA SI VINGINEVYO
SOMO: Upendo wa Mungu kwa binadamu/ love of God.
BWANA YESU ASIFIWE!
Katika masomo ambayo ni Muhimu Sana na ya lazima watu kufundishwa ni upendo wa Mungu. Somo hili lime over maeneo yote uponyaji, uchumi, kufunguliwa,
Neema ya Mungu, Baraka na kila kitu. uzuri wa somo hili linapofundishwa mtu/watu kujifunza basi Mungu Baba huwatuma malaika zake kwa utukufu
wake na lazima uwepo wa Mungu ukuzingire unapojufunza somo hili. Na kama Mungu atashuka expect FAVOUR into your life! Upendo wa Mungu ni somo
Pana Sana lakini Lina sehemu kuu nne! Tutaenda kuzitizama kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Huwa napenda kuanza
Na maswali sababu maswali yanakusaidia
Kukufikirisha! Yanakusaidia kutaka kujua zaidi. Kwanini wakristo wengi pamoja na kusoma neno! Kuimba kuhusu upendo bado wanafail hata kwa asilimia ndogo
Kupractise upendo? Kuna watu wengi wanalipiza mabaya pamoja na kuokoka? Je Mungu ananipenda? Je wewe unampenda Mungu? Mwingine
Anauliza kama Mungu ananipenda kwanini ninapitia hayo nayopitia? Kwanini maumivu mateso hayaishi kama Mungu ananipenda? Je nini HUKWAMISHA
Mkristo kuweka upendo katika matendo? Hakuna ambaye hapendi upendo, hakuna asiyependa kufanya mema lakini inatokea tuu mtu anashindwa practice upendo.
Nini huwa kinatokea?
Kabla ya kwenda huko kote Kuna jambo muhimu Sana nataka nikuonyeshe umelizoea ilo neno pengine unalijua lakini Leo nataka nikupitishe kwa jicho la Mwalimu
Marko 12
29 . Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 . nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.
31 . Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
Embu tuangalie hapo juu! Amri ya kwanza mpende Mungu wako kwa Moyo wako wote. Amri ya pili mpende jirani yako kama nafasi yako. Sasa nataka
nikuonyeshe kitu roho Mtakatifu amenionyesha. Kiti cha kwanza kabisa
1.WEWE <KUMPENDA > MUNGU (kwa moyo wako wote,akili yote,nguvu zote)
2.WEWE<KUMPENDA> JIRANI (kama nafasi yako)
KWA HIYO:
Wewe umehusishwa sehemu mbili ya kwanza ni wewe kumpenda Mungu. Ya pili ni wewe kumpenda jirani. Lakini MUNGU NDIO UPENDO WENYEWE!
KWA IYO SABABU MUNGU NDIYO UPENDO WENYEWE HAPO SHERIA NO .1 UNAWEZA KUSEMA NI MUNGU KUJIPENDA YEYE MWENYEWE. NDIO
MAANA KUMPENDA MUNGU NI LAZIMA UMPENDE JIRANI YAKO HAPO NDIPO UNAONYESHA UPENDO. SABABU MUNGU NI UPENDO WENYEWE SASA HUWEZI
Kuupenda upendo wakati wenyewe ni upendo ni sawa nakutafuta kitu au kujaribu kuunda kitu ambacho tayari ushapewa bure. Ndo maana kama
unataka kumpenda Mungu lazima umpende jirani yako. Bwana Yesu asifiwe Sana! Sasa lipo tatizo ANGALIA PALE JUU biblia inasema mpende jirani yako kama
Nafasi yako. KWA IYO INANIPA MAANA HII HUWEZI MPENDA JIRANI YAKO KAMA HUJAIPENDA NAFSI YAKO! AU hujajipenda mwenyewe. Sababu huwezi Toa kitu
ambacho hauna. Kusudi uweze kumpenda jirani yako! Lazima ujipende wewe mwenyewe kwanza. Ndipo uweze mpenda Mungu ndipo uwezo mpenda
jirani yako. Kwa iyo wengi tunafail kuwapenda wengine sababu
1. Hujipendi wewe mwenyewe
2.humpendi Mungu
3.Huwapendi wengine.
Kwa iyo KUSUDI UWEZE KUJIPENDA MWENYEWE LAZIMA UPOKEE HUO UPENDO KWA MUNGU. NIMESEMA HUWEZI TOA KITU HUNA. KWA IYO
circle yenu itakuwa hivi.
1.kuupokea upendo wa Mungu
2.kujipenda mwenyewe
3.kumpenda Mungu
4.kuwapenda wengine
Mpaka tukifikia mwisho wa step 4! Utakuwa umepata kitu kikubwa Sana kaa nami. BWANA YESU ASIFIWE SANA.
Upendo Una nguvu kuliko mauti ndo mana ukifa unafufuka! Na upendo ndio Mungu mwenyewe. Unampenda ndugu yako unapofanya mema bila kutaka
fadhila hapo tunasema MUNGU BABA YUKO MAHALI HAPO. SABABU HAPO UMEMWA APPLY MUNGU YANI UPENDO. YANI MUNGU YUPO HAPO. KITU
ULICHOKIFANYA MANAKE KUMUWEKA MUNGU KWENYE SCENE! KWENYE TUKIO.labla niongee lugha iyo ili upate kuelewa kutenda mema manake ni
kumweka Mungu katika tukio. Pengine hujui kwanini Agano jipya linazungumzia Sana upendo! Kutenda upendo. Unapotenda upendo manake
umemweka Mungu kwenye tukio! Sababu upendo ndio Mungu mwenyewe. Sasa upendo wa Mungu hauutafuti! Upendo wa Mungu huupati kwa kutoa sadaka
Upendo wa Mungu huupati kwa kufunga! Upendo wa Mungu huupati kwa kuomba! Upendo wa Mungu kwako ni tena bure inachokupasa ni kuupokea tuu. ITS THERE
For free tena usio na gharama yoyote. Wakati mwingine utaamka asubuhi kuwahi kazini na kukuta foleni kubwa au unawahi basi kusafiri kisha usafiri
unaokupeleka stand unaharibika unaanza kukasirika kuchukia. Kumbe ulikuwa hujui Mungu kakuepushia ajali kumbe ilishapangwa ufe wakati mwingine
unakosa tiketi unalaamu mpaka unachukia kumbe hujui Mungu alichokuepushia. Wakati mwingine utaenda hospital operation iliyotakiwa
kufanyika haifanyiki. Then unalaumu unachukia kumbe kulikuwa na wakala wa shetani pale anasubiri wanywendamu yako. Wakati mwingine Mungu
atakukwamisha kwa makusudi utachukia kumbe kakuepushia kitu kibaya. Wakati mwingine tunamkasirikia Mungu lakini hajawahi kuacha kututendea upendo.
Wakati mwingine utaingia kwenye public transport kisha Mara mtu anashuka anakupisha seat. Na wote waliokuwa wamesimama ile siti hawajaiona unaona
kawaida kumbe haujui ni upendo wa Mungu. Seminar ya mwisho ya Mwakasege Dar. Nilichelewa Sana. Kote kukawa kumeshajaa nikawa naenda
katikati ya watu gafla nikaona siti inakitabu direct nikaenda nikamuuliza yule dada panamtu akaniambia hakuna. Nikapata seat ya mbele kabisa. Upendo
wa Mungu ni mkuu Sana mkuu mno. Haijalishi wewe ni mdhambi au sio mdhambi Mungu hutenda upendo kila siku kila dk. Sema tuu hatuoni. Sababu
wewe umengangana na matatizo huoni. Hutambui. Unatafuta makosa. Unatafuta kasoro. Lakini kama ungekaa chini na kuanza kufikiria ni vitu vingap Mungu
kavitenda kwako ni vingi mno. Kuna sehemu alifanya kitu hukuaibika. Kuna jinsi ameshawahi kukuepusha na ajali hujui. Kuna jinsi ameshakuepusha usile
chakula chenye manuizo au sumu wewe hujui. Kuna sehemu alimlazimisha mtu awe msaada kwako wewe hujui. Mara nyingi Sana amekuepusha na
mashambulizi ya magonjwa wewe hujui. Amekuepusha usiolewe na mtu asiye sahihi hujui na unamnungunikia, Kuna vitu amekunyima sasa kwa ajili ya uhai wako
coz kama ungevipata sasa hakika ungekufa! Au ungeishia pabaya ww hujui unamlalamikia Mungu Kila siku. Huridhiki! Hutosheki! Hupendezwi. Sema wewe
hujui tuu Mungu anajua jinsi anavyokusaidia na kukulinda. Mawazo yako aaah yeye si Mungu kaniumba ni wajibu wake kama unawaza ivyo iko ni
kiburi Sababu Kuna sehemu alikuonya hukusikia ukaanguka na bado amekusaidia kukuinua na kuanza upya ila wewe hujui. BWANA YESU ASIFIWE!
SHETANI HUDANGANYA WATU SANA! ili waaamini wanayopitia ni sababu ya dhambi! Mungu anawapa adhabu. Nataka nikutoe wasiwasi Mungu ndiye
aliyekuumba anakujua toka siku mimba yako ilipotungwa hata siku unaingia kaburi na anajua Kila kitu kuhusu wewe anajua lini utaanguka katika dhambi
Anajua lini utamsikiza lini utaacha kumsikiza anajua kabisa kwamba unaudhaifu flani, na huwezi kuacha yani anakujua kuliko wewe unavyokujua kwa
Ivyo anakupenda kama jinsi ulivyo. Upendo wa MUNGU KWA BINADAMU CRITERIA YA KWANZA NI YEYE MWENYEWE! Mungu hatumii C.V yako ili akupende wewe,
Sababu Mungu anajua kabisa ni vigumu kuwa mtakatifu katika mwili huu wa damu na nyama. Na anajua huwezi enda katika njia iliyonyooka anajua usifikiri Mungu
hajui MUNGU ANAJUA KILA KITU, NDO MANA KUNA WATU WANAISHI KATIKA UTUMWA WA KUFIKIRI KWAMBA MUNGU ANAWACHUKIA. MUNGU
ANAWAPA ADHABU, MUNGU HAWAPENDI HUU NI UONGO MTUPU WA SHETANI KICHWANI MWA WATU. MTU ANAKUJUA NDIO MAANA
ALISHAKUSAMEHE KABLA YA KUTENDA DHAMBI YANI ANAJUA KABISA WEEKEND HII UTATENDA DHAMBI KWA IYO IPO DAMU YA YESU INAKUSUBIRI
UKISHAANGUKA UCHUKUE HATUA ZA KUPOKEA MSAMAHA. UNAFUTIWA DHAMBI KWA KUPOKEA MSAMAHA. unaweza enda sehemu unawakuta watu
wanaomba rehema mpaka wanajingata wanajipiga ukutani. Unajiuliza hawa wanajua maandiko kweli? Tayari Yesu alishatenda hayo ivyo wewe
unachopaswa ni kuomba Rehema na kupokea msamaha. Sema Baba napokea msamaba sasa katika jina la Yesu. Its free unachotakiwa wewe ni kupokea.
1 Yohane 4
16 . Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
17 . Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.
*NA MUNGU HUKAA NDANI YAKE! KAMA YEYE ALIVYO NDIVYO WEWE ULIVYO ULIMWENGUNI HUMU.UPENDO WA YESU
Unaupokea kwa kuutambua kwa shukrani
Je ni Mara ngap unachukua mda? Kusema MUNGU ASANTE! KUCHUKUA HATA DK. TANO KUFANYA REVIEW! YA SIKU YAKO NZIMA JINSI MUNGU ALIVYOKUSAIDIA?
au unafikiri ni nguvu zako mwenyewe? Kuamka ni nguvu za Mungu, kwenda kuoga kujiandaa ni nguvu za Mungu. Kitendo cha kupanga mambo yako
Na yakaenda sawasawa basi ujue Kuna upendo wa Mungu ulikufunika mahali. Upendo wa Mungu ni msaada wa Mungu wa kukuvusha sehemu au kukusaidia
sehemu ambayo hukustahili kusaidikika. Huo ndio upendo wa Mungu. Tena free kabisa. Tenga mda wako asubuhi au jioni mshukuru Mungu kwa upendo wake. Pia
Pokea upendo Wa Mungu. Sema Mungu Asante kwa upendo wako naupokea sasa naomba umimine upendo wako moyoni. Manake ni kumuambia Mungu leta uwepo
Wako moyoni. Na tunajua kabisa ukimuona mtu kafanikiwa ki Mungu ni lazima uwepo wa Mungu ulikuwepo mahali hapo. Vitu vitatu asubuhi namuo
mba Mungu. Moja namuomba Roho Mtakatifu anijaze cha pili naomba Neema ya Mungu inifunike! Tatu namuomba Mungu amimine pendo lake ndani yangu
Ukifanya ivyo nakwambia umecover maeneo yote muhimu ya kibiblia. Kwa IYO IWEKE KICHWANI KUWA UNAPOOMBA MUNGU AMIMINE PENDO LAKE KWAKO
Manake umemuambia amimine uwepo wake kwako. TATIZO LA SIKU HIZI NA MAKANISA YA SIKU HIZI HUTASIKIA WATUMISHI WAKIFUNDISHA UPENDO
KWA staili hii watagusa tuu kidogo. Watatumia mda mwingi kufundisha kuhusu mafanikio. Matokeo yake wakristo tunamfuata Mungu kwa ajili ya mahitaji
Na si Sababu tunampenda. Ni kitu kibaya Sana kutaka kitu cha mtu alafu yeye mwenyewe huna mda naye hutaki maongezi naye. Ndio maana Mungu
hakupi mpaka at least umeistablish mahusiano na yeye angalau akuone basi wewe humfuati sababu ya vitu Bali unamfuata Sababu unampenda. Kiukweli
Ndiyo mafundisho ya makanisa Mengi na yanasababisha watu wa MUNGU WASHINDWE KUPRACTISE UPENDO. UNAWEZA FANYA YOTE KAMA HUNA
Upendo wa Mungu. MUNGU HATAKUPA NJIA YAKO. UTAFANYA KILA KITU MUNGU ATAKUANGALIA TUU. NI MPAKA UMEJIFUNZA KUTENDA UPENDO KUISHI
upendo ndipo Mungu atakupa ivyo unavyotaka. Angalia watumishi wakubwa katika biblia Mungu aliowabariki MUNGU ALIWABARIKI SABABU WALIMPENDA
MUNGU. KAMA huwezi mpenda MUNGU SASA WAKATI HUNA KITU NI VIGUMU KUMPENDA UKIWA UNA KITU. NA PIA NI VIGUMU KUMPENDA JIRANI YAKO.
watu waliofanikiwa Sana Katika biblia au maisha ya wokovu wana sifa kuu UPENDO umejaa ndani Yao. WATU WANAOTEMBEA NA UPAKO MKUBWA
WA KUTINGISHA DUNIA KIMUNGU CHUNGUZA UTAKUTA UPENDO.UKIFANIKIWA KUPRACTISE UPENDO WA KIMUNGU YANI ULE
UPENDO SIO WA KIBINAFSI AU UPENDO WENYE LENGO LA KUFANIKISHA DHAMBI BASI HATA UMEFANIKIWA KUIISHI BIBLIA. HUWEZI FANIKIWA LOLOTE
Kama huna weka upendo wa MUNGU katika matendo! Sio swala la kusema iyo nishasikia iyo naijua nachozungumzia ni kuweka katika matendo kitu amacho
kinawashinda wangi. Pamoja na kusoma biblia yote! Pamoja na kusikia na kusikia na kusikia na kuimba but still watu tunashindwa kupractise upendo wa
Mungu. Hasa kwa majirani zetu. KWA IYO TUMESEMA HATUA YA KWANZA NI KUUPOKEA UPENDO WA MUNGU NA TUMESEMA UNA RECOGNISE MEMA YA
MUNGU NA KUMSHUKURU, HATUA YA PILI TUMESEMA UNA OMBA MUNGU AMIMINE PENDO LAKO NDANI YAKO. najua vita iliyopo lakini ukielewa ili somo
hata kidogo! ROHO MTAKATIFU ATAIONA KIU YAKO NA ATAKUSAIDIA HATUA KWA HATUA. NAJUA SI RAISI BUT ROHO MTAKATIFU NDIO KAZI YAKE KUFANYA
YALIYOSHINDIKANA. IKAFIKA SIKU YA KUPRACTISE UPENDO IN GOD WAY. NDO SIKU YA KARIBIA KILA TATIZO KUISHA. UPENDO NI MUNGU. PENYE MUNGU
hakukai vifungo, laana, maagano, shida , mapepo, uchawi, mateso, kuchanganyikiwa, kutokufanikiwa, wala hakuna kulia, hakukai cha shetani. Ndio
maana unaona vita kubwa katika kufanya upendo. KUMBUKA HILI KUTENDA UPENDO NI KUMLETA MUNGU KATIKA TUKIO. IYO USISAHAU. SABABU MUNGU
NDIO UPENDO WENYEWE.
NO.2 KUJIPENDA MWENYEWE! JE UNAJIPENDA MWENYEWE KIBIBLIA?
Asilimia 100% ya watu nikiwauliza je unajipenda watajibu ndio. Lakini ngoja tuanze kuchambua hapa utashangaa. Nazungumzia mahusiano Kati ya jina lako
na wewe je wewe mwenyewe unajipenda? Kama hujipendi nakuhakikishia huwezi mpenda Mungu wala huwezi penda jirani yako. Leo nataka
nikupe siri ya MASWALI MENGI AMBAYO WAKRISTRO WANAYO. ILI UNAPOMUONA MTU KAFANIKIWA KIMUNGU BASI IKUJIE PICHA MOJA KICHWANI UJUE MOYO
WAKE UNAUPENDO NA ANA PRACTISE UPENDO. kwanini wewe hujafanikiwa Leo hii ni sababu huna upendo! Kwanini unatamani Sana upako huna ni sababu
huna upendo, kwanini mwenzako analala usingizi wewe huwezi kulala mpaka uvunje uharibu upambane na mapepo ni Sababu huna upendo. Umeshindwa
kupractise upendo wala si Sababu huendi tuu kanisani kufanya ibada katika Roho na kweli Bali ni Sababu huna upendo. Mbinguni utaenda lakini ahadi za
Ibrahimu utazipata kwa upendo. Utazimiliki kwa upendo wa Mungu BABA HII NI SIRI NAKUPA NIMEPATA ASUBUHI HII NA ROHO MTAKATIFU. IVYO
UKIMUONA MTU KABARIKIWA ACHA KUMUONEA KIJICHO BALI TAMANI KILE KILICHOMFANYA ABARIKIWE NA WEWE UTENDE UTABARIKIWA. USITAMANI
ALICHO NACHO MTU INSTEAD TAMANI UPENDO NA HII NDO SABABU SHETANI ANAPIGA VITA USIKU NA MCHANA INJILI YA UPENDO ISIHUBIRIWE MAKANISANI.
WATU WAKO BIZE KUFUNDISHANA JINSI YA KUFANIKIWA PROSPERITY LAKINI SI UPENDO. KAMA HUNA UPENDO LAZIMA UTAKWAMA MAHALI TUU. SIJASEMA NI
KITU RAISI SIO RAHISI NI NGUMU NAKUAMBIA KWELI KABISA UJUE LAKINI ROHO MTAKATIFU YUPO KUKUSAIDIA HATUA KWA HATUA ATAKUSAIDIA. NI
KWELI UNAAHADI NYINGI SANA. NI KWELI YAPO MENGI SANA LAKINI KAMA HUNA UPENDO NAKUHAKIKISHIA HAYO MAMBO HUWEZI YAPATA! HUWEZI YAMILIKI. IPO
NEEMA SIKATAI YA KUKUBEBA LAKINI HATA NEEMA HUKUSAIDIA KAMA UNAJUHUDI, kama unajaribu! Biblia inasema walipotaka kuomba nalisikia. Na
walipoanza kuomba nalitenda. BWANA YESU ASIFIWE! Na hata Mungu akikubariki kigezo cha wewe kuendelea kuinuliwa kubarikiwa ni UPENDO, Baraka ya Mungu
Inatunzwa kwa upendo, matendo mengine ya imani unayofanya ni kwa ajili yako mwenyewe ili uwe na mahusiano mazuri na Mungu Bali MUNGU
anachotaka kwako ni upendo hataki kitu kingine. Sasa tuangalie je wewe unajipenda?
Marko 12:31
. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.
# NAWE MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO.
Kujipenda manake kujikubali jinsi ulivyo, jinsi Mungu alivyokuumba kuji appreciate kujipenda ni zaidi ya kujinunulia nguo mzuri! Ni zaidi ya kujijali na kujipenda
HAINA MAANA UWE MBINAFSI, huu sio upendo ninaozungumzia hapa. UPENDO HUU NAO ZUNGUMZIA HAPA SI WA KUKUFANYA UFANYE DHAMBI. mwingine
atasema Mimi napenda kutoka outing but mfukoni Hana ela ivyo matokeo yake anaingia kwenye dhambi ya tamaa. Huku siko kujipenda. HII INAITWA BIBLICAL
SELF -LOVE, ukitaka kujipenda acha kuji jugde mwenyewe Kiswahili chake acha kujihukumu. Jitadhimini lakini penye hukumu mwachie Mungu. Hukumu
inaweza kuwa Mimi mfupi Sana, Mimi mweusi Sana, Mimi mwembamba Sana, Mimi mnene Sana, Mimi sipendezi nikavaa nguo, Mimi hivi Mimi vile PLEASE
STOP THAT! ukifanya hivyo ni kujaribu kumkosoa MUNGU ALIYEKUUMBA NA KUKUPENDA SANA. JI APPRECIATE jinsi ulivyo jikubali jinsi ulivyo. MUNGU
AMEKUUMBA JINSI ULIVYO KWA MAKUSUDI ILI AKUBORESHE HATUA KWA HATUA MPAKA MUNGU AFIKIE VIWANGO ANAVYOTAKA YEYE. mtu anayejipenda
hatapasua kichwa kufanya mambo asiyo yaweza. Mfano si lazima uwe na simu ya bei ghali. Si lazima uwe na nguo ya laki tatu wakati zipo za elfu hamsini, si lazima
ukodi gari uonekana Una gari wakati uwezo huo huna na baada ya hapo utaishi kwa madeni. Fanya Yale yaliyo Katika uwezo wako Yale yasiyo katika uwezo
wako hayo ni ya MUNGU, usilazimishe mambo usilazimishe maisha ya aina flani while you can not afford, usijilazimishe kula samaki Sato wa mwanza while in
reality you can not afford. NIKUPE SIRI DALILI YA KUTOJIKUBALI JINSI ULIVYO MANAKE HUJIPENDI YANI hupendi uchumi wako! Hupendi maisha Mungu
aliyokupa! Hupendi kila kitu Mungu alichokupa ndio maana unajaribu unaforce kubadilisha, while you can not afford. Mtu wa namna hii hata ndoa yake itakuwa namatatizo kama hajikubali yeye
kama yeye kama yeye anajikosoa vip kuhusu her/his couple, mtu wa namna hii hawezi kukubali wengine maana yeye mwenyewe hajikubali. Mtu wa namna hii
hawezi kuwapenda wengine maaana yeye hajipendi. You can not give out something you dont have. Mtu anayejipenda hatufuti makosa kuhusu yeye au makosa kuhusu
watu wengine. SI KAZI YAKO KUTAFUTA MAKOSA KUTAFUTA MAKOSA NI KUINGILIA KAZI YA MUNGU YA KUHUKUMU. FANYA YAKO YA MUNGU
MWACHIE MUNGU. Saa ingine utamwona mtu akaingia ibadani badala ya kumtafuta MUNGU yeye anaanza kutafuta makosa anaanza angalia wahudumu anawatoa
makosa, anaanza angalia watu walivyo vaa anawatoa makosa. Anamuangalia Mtumishi anamtoa makosa. Mfano hata somo hili pengine huku unatafuta
makosa. Kama ipo hiyo hali iyo ndani yako nataka nikujulishe nikufahamishe unafanya kazi ya shetani bila kujijua. Kutoa makosa manake ni kuhukumu.
Kusengenya mtu ni kuhukumu. Kujikosoa mwenyewe kutafuta what is wrong with me ni kujihukumu. Kwa maana ingine unamkosoa MUNGU. unakosoa kazi ya Mungu hii itakisababishia usijipende! Ni
vizuri kufanya maboresho katika maisha yani IMPROVEMENT lakini isisababishe wewe kuchanganyikiwa. Na ndio maana unaishi huna furaha. Hupendi unavyo vaa,
hupendi unavyokula, hupendi unavyoongea, hupendi kupanda daladala humpendi Mme wako jinsi alivyo unatama ni mwanaume mwingine mwenye quality
zaidi yako. Humpendi mke wako unatamani mwanamke mwingine mwenye quality zaidi ya mkeo bila kuangalia SOURCE je uyo unayemtamani
hivo vitu unavyotamani kavipataje? 90% ya Wakristo hatujikubali wenyewe hatujipendi. Yani there is nothing good unachokiona kwako. Always unaona kwa
mwingine why? Na hii ndo inasababisha kuishi fake life. Hata sauti yako huipendi ndo unafake sauti tofauti! Yani hujipendi kila kitu na unajaribu kujibadilisha kila kitu
Mtu anayejipenda haishi fake life, anaishi real life! Na mtu anayetafuta mabaya kwa watu au kwake ni dalili za kutokujiamini. Hujiamini ndo mana kila Mara unatafuta
Makosa Ili ujirekebishe, au urekebishe na hio sio kazi yako Ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna mwingine hawezi toka ndani mpaka apake lipstick akikosa hatoki
Huo ni utumwa, mwingine hawezi kujichanganya na watu mpaka apate gari aliloazima, mpaka awe na ela nyingi huo Ni utumwa, kujaribu kuficha yaliyoyako
Mpaka ikakuingiza katika dhambi huko ni kutokujipenda. KWANINI HUJIKUBALI WEWE MWENYEWE? KWANINI UNAISHI ARTIFICIAL LIFE? JE MUNGU WAKO NI
Artificial? Au REAL? ACHA KUANGALIA mambo unayoyafanya kwa usahihi yani acha kujihesabia haki, Kuna watu tokea asubuhi anahesabu mema aliyoyafanya
Nimetoa lifti, nimempa yule masikini ela, nimemwelekeza mtu njia, nimemtumia mtu tigo pesa aliyenibom, nimesalimia watu. Unapofanya hivi utajiingiza katika
Kiburi cha kujihesabia haki. Na Mungu huchukia wenye kiburi, kiburi huleta ujeuri na ubinafsi, kiburi huleta kujiona
Bora zaidi ya wengine. Ukishafikia hatua.
Ya kumuona bora zaidi ya watu wengine tayari huwezi kuthamini mtu. Hapo ndipo utaanza kumkosoa kila mtu hata watumishi unawakosoa na iko Ni kiburi
Acha kuanza kuhofia kama umetenda sawa au hujatenda sawa, hii inakuweka kifungoni. Siku nzima unaanza kujilinda wap nimetenda haki wapi nimefanya
dhambi, don't worry about that Sababu Mungu anajua huwezi kuwa mkamilifu katika mwili huu wa damu na nyama kuanza kujichunguza kuwa wap Leo
Nimetenda haki wapi Leo nimekosea ni kumkosoa Mungu. by the way si kazi yako Ni ya roho Mtakatifu nasema hivi Sababu wapo watu ambao wana iko
Kifungo cha kuogopa kukosea wanajilinda kuanzia anavyowaza anavyoongea hata anavyosema. Huo ni utumwa wa fikra, na akili inakuletea kuchanganyikiwa kusiko
Na maana muachie hayo mambo Roho Mtakatifu. Acha kujichambua. Acha kutafuta makosa kwako, acha kujihukumu, acha kuwa na wasiwasi vip
Je kama nikitenda dhambi? Kuna vitu ambavyo shetani ametushikilia navyo na vimegeuka sheria katika kumtumikia Mungu. Na vinakufanya usiwe wewe Bali uishi maisha ya mtu mwingine. STOP
THAT.fanya unaloweza kufanya usiloliweza muachie Roho Mtakatifu kwa kumkabithi kisha umuamini kuwa atalifanya. Acha kutafuta vitu vya
kukuchanganya fanya unapoweza usipoweza mkabithi Mungu na muamini yeye atafanya. Usiogope kuwa na mapungufu, usiogope kuwa na madhaifu
Na usifiche madhaifu yako mbele ya Mungu. Kujaribu kuyaweka sawa mambo hayo sawa kwa akili zako ni kiburi. Mungu ndo aliyoyaruusu ili kupitia hayo akufanye
Mtu mwingine kutoyakubali, kutokutaka msaada kwa Mungu kuwa unamuomba akusaidie hiko kinaitwa self PRIDE, AU KIBURI, Musa alikiri kwa Mungu kuwa
Hawezi kuongea akasaidiwa na Mungu. Unakukumbuka visingizio vya Musa alivyotumwa na Mungu? Unakumbuka iyo story? Jeremiah pia alikiri madhaifu yake
Kwa Mungu.
Kutoka 4:10
. Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.
Jeremiah naye alikiri udhaifu wake kwa Mungu
Yeremia 1:6
. Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
Angalia mwenyewe sasa kwanini wewe hutataki kukubali umeshindwa huwezi mwenyewe kutokukubali kushindwa mbele ya Mungu Baba iko ni kiburi
Acha kuishi kwa kupendeza watu, kuwa unaweza kumbe huwezi. MUSA KUNA MAHALI KAZI ILIMSHINDA AKAMWAMBIA MUNGU MZIGO HUU NI MZITO SIWEZI
Na huko mbele nitashindwa kuliko nishindwe mbele ya hao au kazi iharibike bora uniuwe hapa. Na Mungu akainua maakida 70! Wakawa wasaidizi wa Musa
Mungu wale maakida akawagawia Roho ya Musa ya utumishi ivyo akawa wanasaidiana na Musa. Lakini ilifika sehemu Musa alishindwa aka kubali
kushindwa. Sasa kwanini wewe mambo yamekuelemea Na bado unakomaa. Hiko Ni kiburi. Saa ingine Mungu anayafanya yawe mazito ili uombe lakini bado ume
Komaa na unauchukua mzigo mwenyewe, Mungu hajali kama unakosea, au unamadhaifu, Mungu anajua unatamani Sana kufuata sheria zake na anajua
unajaribu na unashindwa kwa iyo hakuchukii hakuhukumu, wala hashangai wewe kushindwa ila anachoshangaa wewe kutokuomba msaada. Mungu
anakupenda jinsi ulivyo ivyo ivyo unavyojichukulia ndivyo anakupenda. Kwa iyo kwa kujua ilo
Acha kuishi kwa maneno ya watu
Acha kuigiza maisha flani
Acha kuogopa udhaifu wako
Acha kuogopa mapungufu yako
Acha kutafuta makosa
Acha kujihesabia haki
Acha kumpendeza Mungu kwa uwongo
Usijali mashutumu ya watu
Usijali kukoselewa
Usijali kutengwa
Usijali kukosea
Sababu hata YESU ALIPOCHAGUA MITUME 12 Aliwajua wote na alijua yoote na alijua mioyo Yao! Na aliwapenda kama jinsi walivyo. Kwa Sababu walijua hayo
Hawakufanya maigizo mbele ya YESU WALIISHI NA YESU KAMA JINSI WALIVYO.
Ni kitu cha kusikitisha wakristo tunafanya maigizo mbele ya Mungu. Na kujaribu
kumdanganya Mungu. Kumshawishi Mungu kwa maigizo wakati Mungu anakujua A-Z yeye si ndio aliyekuumba. Unanini cha kumficha. Tuache fake life.
Ishi kama Mungu alivyokuumba. IBRAHIMU ALIBARIKIWA SABABU ALIJIPENDA! ALIISHI KAMA JINSI ALIVYO. DAUDI ALIBARIKIWA SABABU ALIJIPENDA
ALIISHI KAMA JINSI ALIVYO! YOU CAN NOT FOUL GOD BUT YOUR FOULING YOURSELF BE REAL KWA MUNGU ILI AKUSAIDIE. okei sasa nirudi kule mwanzo
je mpendwa baada ya maelezo hayo nikuulize swali je unajipenda sawasawa na biblia?
KUMPENDA MUNGU/LOVING GOD
# Tunaendelea na somo letu, la upendo wa Mungu tayari tushaangalia jinsi ya kupokea upendo wa Mungu. Tayari tushaangalia jinsi ya kujipenda
mwenyewe kibiblia. Sasa tuangalie jinsi ya kumpenda Mungu. Somo la upendo Ni chakula kigumu lakini ukikipata ukadaka basi umevuka. BWANA YESU ASIFIWE!
Mungu hatumpendi baada tuu ya kutubariki! Mungu hatumpendi baada tuu ya kuwaangusha maadui zako no! Jinsi ndoa ya mke na Mme ilivyo ndivyo jinsi
mahusiano ya Mungu na binadamu yalivyo. Katika ndoa Mme hatakiwi tuu kumnunulia mke wake zawadi au kuuongea naye vizuri kwa kuwa anajua
atamhitaji ukifika mda wa wanandoa usiku! No!kama atamnunulia kanga! Kama atamnunulia kitenge! Kama atamletea zawadi isisukumwe na hitaji la kindoa
usiku. No! Iwe Ni natural uwe ni upendo halisi. Mke naye hata mtreat Mme wake vizuri, hatampikia vizuri, au kuwa naye karibu vizuri hata ule mda wa
wanandoa sababu Kuna hitaji anataka no! Atafanya ivyo kwa kuwa anampenda mme wake. Mwanaume asimpende mke tuu wakati anashida naye! Baada ya hapo
upendo unaisha. Na mwanamke asimpende au kuonyesha upendo sababu Kuna kitu anataka. No! Mahusiano yasiwe kwa ajili ya kitu flani. Yanatakiwa yawe
ya upendo halisi! Bila fadhila. Sio upendo wa kutegana uwe upendo wa kweli.Tena upendo usioangalia wakati mambo mazuri au wakati Kuna muddy mzuri. Mfano
Samahani nitaongea mambo ya ndoa ili tuelewe vizuri, mfano Mme akimtoa mke outing si lazima amwambie kitu usiku, No! Na mke naye asisubiri kupewa kitu ndipo
Atoe ushirikiano! Yani Mme anajua nikataka ndoa yangu lazima nitangulize zawadi. Mke naye anasema bila chochote hakuna ushirikiano wa ndoa.
Huu si upendo, Bali ni kulipana fadhila. Sasa nimeongea hivyo kwa makusudi. Kwa maana kanisa ni mke na Mungu ni Mme. Na mahusiano ya sisi mke kwa Mungu ni
Ya fadhila Mara nyingi hatuna true love. Mungu akikubariki. Utampa sifa zote "hakuna Mungu kama wewe" nitamtukuza Mungu wa Ibrahimu. Mungu
wa mahali hapa anatenda, nimemuona Mungu. Na maneno mazuri kama hayo yenye kumsifia Mungu. Sasa ngoja Mme amuonye mke kuwa tabia hizo sizipendi.
Yani Mungu amuonye Mpendwa tayari malalamiko. Na unaacha kutoa huduma za mke(kanisa) humuabudu vizuri, hutoi tena sadaka unapunguza muda na Mme
(Mungu)huongei naye vizuri unaongea naye kwa hasira, unamkasirikia Mme(Mungu) kisa tuu amekuonya, au amekunyima kitu unachotaka kwa mda
Kwa faida yako,wakati umesahau Mme(Mungu) alikupenda toka uko dhambini mpaka ukaokoka, ukaanza kutembea Katika ndoa(wokovu) kwa
Makosa Mengi Mme (Mungu) akawa anakuvumilia unafanya makosa anajidahi kama haoni vile, mwaka wa kwanza wa pili wa wokovu(ndoa) anajua kabisa sasa
Mke(Mkristo) kaanza kuzoea ndoa (wokovu) akianza kukurekebisha tatizo siku akitenda jambo zuri ndo unafanya mambo yote kumfurahisha mme(Mungu)
Asipotenda unakata huduma zote. Embu tuangalia katika neno hicho nachoongea hapo juu. Ili ukipate kwa uzuri zaidi....MAANA MUNGU SI BINADAMU
HATA TUMDANGANYE AU TUMLAGHAI ASIGUNDUE, na kama ukishindwa kumpenda Mungu automatic huwezi mpenda jirani yako. Jana nimesema
kutenda upendo manake ni kumuweka Mungu katika tukio. Nikasema asubuhi sababu ya uyu kubarikiwa Sana huyu kidogo, huyu kutembea na upako huyu
Hana. Pamoja na mambo yote ya imani unayoyafanya kama hutatenda upendo uwezi fanikiwa katika njia zako. Ingawa mbinguni utaenda. Upendo wa Mungu
hupati sababu umetoa sadaka. Au kwa kufunga Sana, au kwa kuomba Sana, no! Hupatikana kwa kutenda mema! Step four tutaangalia jinsi ya kutenda mema
ipasavyo kibiblia...
NATAKA NIKUONYESHE JINSI AMPLIFIED BIBLE ILIVYOELEZEA KWA UPANA.
3 In the same way, you wives, be [a]submissive to your own husbands [subordinate, not as inferior, but out of respect for the responsibilities entrusted to husbands and their accountability to God, and so partnering with them] so that even if some do not obey the word [of God], they may be won over [to Christ] without discussion by the godly lives of their wives,
1.Submissive
2.Adopt
Katika biblia jinsi inavyozungumzia ndoa, mwanamke anatakiwa a submeet kwa Mme wake. Na adopt responsibilities za Mme wake. Manake ni hii katika ndoa
Kuna vitu vitatu vikubwa. Migogoro yote ya ndoa inatokana na vitu vitatu vikubwa cha kwanza mwanamke kushindwa kumtii Mme wake, cha pili kushindwa
kukubaliana na Mme wake. Na kazi ya Mme ni kumpenda mke wake. Ukiona migogoro wowote duniani wa ndoa angalia hayo mambo matatu. Mke
kashindwa au hataki kumtii Mme wake, na hakubaliana na Mme wake. Au Mme kashindwa kumpenda mke wake. Mwanamke anaweza sema Mimi
hanipendi yanini kumtii na kumsikiza anavyotaka. Mwanaume anaweza sema Mimi hanieshimu kila Mara hanisikizi. Na kumtii mwanaume na kumsikiza
mwaname kunako ongelea biblia si kule kwa kitumwa kwa hofu au vitisho Bali kunatokana na upendo. Na kumpenda mwanamke haina maana kila Mara
mwanaume atake tendo la ndoa, no! Huu si upendo Bali Ni kutimiza haki ya ndoa kwa mwanamke kwa iyo Kuna wajibu wa wanandoa huo upo! Wajibu ukifanywa
kama sheria hapo hakuna upendo! Wajibu ukifanywa sababu ya kumpenda basi huo ndio upendo. Kwa iyo mwanaume atampenda mke wake si sababu ikifika
usiku atapata fadhila ya kumpenda No!. Na mwanamke Ata mpenda mmewe si sababu huduma imetangulia. Yani Kama hakuna huduma naye pia harudishi upendo.
Tuangalie Kiswahili nataka point hii ikuingie vizuri..
1 Petro 3:1
. Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
Sasa kama unavyoona migogoro ya wana ndoa ya kimahusiano! Ndivyo ilivyo exactly Kati ya kanisa na Mungu. Au wewe uliyookoka. Kazi yako wewe Mkristo(mke)
ni kusubmeet kwa mme(Mungu) na kumfuatisha Mungu anavyotaka. Na kazi ya Mungu ni kukupenda. Sasa angalia kama jinsi ndoa zilivyo na mgogoro wa
kimahusiano ndivyo jinsi Mungu ana migogoro na mahusiano na kanisa. Kusubmeet kwa maana ingine ni kumtii Mungu. Kingereza wanaita obedience Leo
hii wakristo tunamtii Mungu katika level flani. Na chunguza kiwango chako cha utii kwa Mungu ndicho kiwango chako cha mafanikio na ndicho kiwango chako cha
mahusiano na Mungu wako. Chunguza hata kwenye ndoa. Mwanamke mtii na anayefuatisha Mme wake anavyotaka ndio mwenye kupendwa zaidi. Hakuna
mwanaume ataacha kumpenda mke wake hasahasa kama uyo mwanamke ni mtii na anafuata njia za Mme wake. Kufuata njia ni huku Mme akisema please sipendi hiki
sipendi hiki basi atamuelewa mumewe na kuweka kichwani izo sehemu ili asimuuzi. Kwa iyo mume atajisikia kueshimiwa na atajisikia kupendwa maana mke kashika
Vile yeye anavyotaka ivyo nayeye
atakupenda tuu.sizungumzii mwanaume ambaye may be kafungwa anahitaji kufunguliwa hapana. Sasa ivyo ivyo Mungu na watu wake kama watu wakimtii
Mungu katika mambo yote sio nusu nusu. Yani katika mambo wanayoyapenda na wasio yapenda wakatii sababu tuu ya kumpenda Mungu. Basi huko ndiko
kumpenda Mungu.MUNGU ANASHINDWA JIZUIA. Mfano kiko kitu kizuri mbele yako na kinaushawishi mkubwa na hakuna mtu wa kukuangalia kukukemea lakini naturally! Unasema no! Hapana!
Nikifanya hivi Mungu ananiona. Ule uamuzi binafsi wa kukataa dhambi! Au kusimama na sheria ya Mungu, pasipo kuangaliwa na mtu basi huo ndio utii
Mungu anaupenda. Unajua Kiukweli upendo Una gharama. Na unapoanza kumpenda Mungu nikuambie tuu ukweli itakucost Kuna wakati Mungu atakula
mda wa program zako. Wakati mwingine utaingia gharama. Na mwili wako Mara nyingi haitakuwa comfortable maana vitu vingi mwili unavyovitamani Mungu ndo
anakukataza. Upendo kwa Mungu ni ile hali ya kumsikiza Roho Mtakatifu ndani yako anasema nini na kumtii. Biblia inasema hao wanaoshika amri zangu ndio
wanaonipenda. wakati mwingine utakuwa na Ela ya kununua gari Roho Mtakatifu atakukataza je utakuwa tayari kutii. Wakati mwingine utampenda Mtu na
unaona mda umeenda unataka nawe uanze maisha ya ndoa na Roho Mtakatifu atakukataza je utamsikiza? Wakati mwingine ndoa inaweza kuwa inawaka
Moto unasikia pressure ya kutengana kuondoka Roho Mtakatifu anakuambia ngoja kidogo uko tayari kumtii. Wakati mwingine Roho Mtakatifu hataongea
mwanzoni ila kama Ni safari ya jambo flani ushaianza kama ni uchumba kazi biashara mradi mahusiano au chochote alafu gafla anakuonyesha mwisho wake si
mzuri je utakuwa tayari kuacha kumsikiza Mungu. Wakati mwingine Mungu atakuhitaji na wewe mwili umechoka utakuwa tayari kumtii anachotaka?
UPENDO. UNA GHARAMA gharama yake ni MDA WAKO, SAA INGINE PESA, SAA INGINE MWILI HAUTAKI, LAKINI ROHO INATAKA! LAKINI NACHOJUA KWA
MUNGU HAKUNA MAJUTO, UNAPOCHUKUA HATUA ZA KUMTII MUNGU KATIKA KILA KITU, BASI WEWE UNAMPENDA MUNGU NAYE
ATALIMWAGA PENDO LAKE KWAKO AKALIMWAGA EXPECT MORE FAVORS! EXPECT BLESSINGS, UNAJUA KWANINI BWANA WETU YESU KRISTO KAPEWA
UTUKUFU MKUBWA KIASI IKO NA MUNGU YESU ALIKUWA MTII HATA ALIPOONEWA HAKURESPOND WALA KUJIBU UNAJUA KWANINI ALIKUWA
ANATII SHERIA ZA MUNGU BABA. SABABU KATIKA HALI YA KAWAIDA YA BINADAMU UNAWEZA MTII MUNGU KWA % FLANI ILA VITA VIKIENDELEA KWA MUDA MREFU
WACHACHE WATAKAA KIMYA WENGI TUTARESPOND TUU. sisemi ni raisi hata Yesu aliweza kwa msaada wa Roho Mtakatifu, bila yule Roho its obvious
angeshindwa maana alikuwa binadamu kama sisi, lakini Mungu siku zote hatafuti wewe kulishinda jaribu yeye anataka kujua Nia ya moyo. Anajua wewe ni
binadamu. Na ndio maana anakupa Roho Mtakatifu ukijidai unaweza mwenyewe Ni sawa nakuamuambia Roho Mtakatifu huwezi lolote.usimtii Mungu kwa Yale
Mambo mazuri tuu mwili unayoyataka na kuyapenda. Mtii Mungu hata akikuonya, mtii Mungu hata akiruusu hali usiyoitaka, unajua kwanini watu wengi Leo
hatufanikiwi? Ni sababu ya kile Musa alichowaambia wana wa Israeli mtakapoyashika maagizo Leo nikuagizayo na kuyatenda yote ee Israeli ndipo
utakapoifanikisha njia yako. Kuishika sheria ya MUNGU MANAKE NI HII UTAKAPOMPENDA MUNGU NDIPO UTAKAPOIFANIKISHA NJIA YAKO. NDIO
Maana hili somo ni muhimu Sana kuliko kitu chochote Sababu, tulisema kule mwanzo KUTENDA UPENDO NI KUMUWEMA MUNGU KWENYE SCENE
Kwa sababu umemleta Mungu lazima mambo yako Mengi yatafanikiwa maana Mungu yupo mahali hapo. Tukaangalia jinsi ya kujipenda tukaona kuwa Mungu
Anataka tuishi maisha original tusiwe fake. Leo tunaangalia kumpenda Mungu tumekuja kugundua kwamba ukitaka mpenda lazima utashika sheria yake.
Embu tuangalie...
Yohana 14:21
. Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Sasa TUANGALIE KUHUSU KUFANIKISHA NJIA YAKO:
Kumbukumbu la Torati 6
3 . Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali.
4 . Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
5 . Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
*Nimekuonyesha katika agano jipya na agano la kale kuwa huwezi kufanikiwa MPAKA UMPENDE MUNGU WAKO. SASA UNAMPENDA VIP NI KWA KUFUATA
SHERIA ZAKE. UNAZIFUATA VIP NIMESEMA KWA KUTII MAELEKEZO YA ROHO MTAKATIFU YOOTE. SI YALE UNAYOYATAKA. KWA MARA INGINE TENA
NENO UPENDO LIMEHUSISHWA NA MAFANIKIO YA MTU AU KUFANIKIWA KWA MTU HII INAZIDI KUSHINDILIA MSUMARI KUWA HUWEZI KUFANIKIWA
PASIPO UPENDO. angalia Musa hakusema mtakapo funga, mtakapo Toa sadaka, mtakapo omba na n.k Bali MUSA AMESISITIZIA UPENDO. YANI KUTI SHERIA YA MUNGU.UNATAKA YOTE HAYO
UNAYOMUOMBA MUNGU AKUPE BASI UKUMBUKE NENO HILI LA UPENDO. ROHO MTAKATIFU YUKO TAYARI KUKUSAIDIA HATA YESU HAKUWEZA
MWENYEWE HATA DAUDI HAKUWEZA MWENYEWE HATA YUSUPH MTOTO WA YAKOBO KUWATENDEA MEMA NDUGU
ZAKE WALIOTAKA KUMUUWA HAIKUWA KWA AKILI YAKE BALI ROHO MTAKATIFU ALIMSAUDIA. Hivi unajua kwanini watu wanahangaika na kufanikiwa
-kununua gari
-kujenga nyumba
-kuwa na ndoa
-kuwa na familia
-kufanya shopping
-kuweka ela bank
*je ushawahi jiuliza huwa watu wa aina iyo wanatafuta nini? Haijalishi wameokoka au hawajaokoka but hayo ndo maisha ya binadamu ushawahi jiuliza wanatafuta nini?
WANATAFUTA
-kukubalika
-kupendwa
-kuaminika
-kudhaminika
-kupongezwa
-kufarijiwa
-kutosheka
-kusikilizwa
-kuwa na utulivu
-kuwa na amani na Furaha
*KWA KIFUPI WANATAFUTA UPENDO. BINADAMU UNAKAMILIKA UNAPOPATA UPENDO! MWISHO WA SIKU HATA ANAYEUWA MWISHO WA SIKU ATATAKA
UPENDO. DUNIA INA NJAA YA UPENDO. ROHO ZA WATU ZINANJAA ZINAHAHA KUPATA UPENDO.SASA SIKIZA UFUNUO HUU, KULE JUU TUMESEMA KAZI YA
MKE(KANISA) NI KUSUBMEET KWA MME NA KUKUBALIANA NAYE. NA KAZI YA MME(MUNGU) NI KUMPENDA MKE(KANISA) YANI WEWE. KWA IYO BASI
NATAKA NIKUPE SABABU KUU MBILI ZITAKAZO KUKUSUKUMA KUMPENDA MUNGU. # 1. KUFANIKIWA NJIA ZAKO, KAMA ALIVYOSEMA MUSA. # 2. ILI NAFSI
YAKO IWEZE KUTOSHEKA! NAFSI YAKO ISIPOPATA UPENDO WA MUNGU NDIPO WEWE HUTOSHEKI NA UNAKUWA MTUMWA WA KILA KITU NA HUWEZI
KUWA HURU. Kwa iyo mtii Mungu katika mambo yote! Nyenyekea na mfuate anavyotaka! Mfanyie Mungu ibada katika Roho na Kweli si sababu your expecting
kitu toka kwa Mungu. BILA UPENDO HUJAKAMILIKA BILA UPENDO HUJAFANIKIWA. ANZA KUMPENDA
MUNGU UPENDO HALISI NA SI UPENDO FEKI WA VITU. Omba Roho Mtakatifu akusaidie uwe original uwe mtii katika mambo yote jina la Bwana libarikiwe.
# TUTAENDELA STAGE 4 YA MWISHO KABISA BAADAE....
[11/16, 13:00] Mtumishi Joseph: KUPENDA WENGINE/ LOVING OTHERS
kwa series toka tulipooanza utagundua kuwa pamoja na Maombi yako mazuri. Pamoja na Roho Mtakatifu kukusaidia kuwa Mtakatifu pamoja na kujitoa kwa
sadaka. Kufunga na kufanya matendo yote ya imani kwenda ibadani katikati ya week, jumapili. Kusoma biblia kwa bidii! Na kufanya kila kitu. LAITI KAMA
UNGEPRACTICE LOVING OTHERS UNGEKUWA MBALI SANA. WATU HUWA WANAMUULIZA MUNGU WAPI NINAKOSEA MUNGU MBONA NAJARIBU
KWA NEEMA YAKO KUWA MTII KWA NEEMA YAKO KATIKA MAMBO YOTE MBONA SIONI MABADILIKO LEO NAKUJIBU UKIBAKISHA UPENDO.
HUKUWAPENDI WENGINE IN GOD WAY. ULIWAPENDA KWA FADHILA. HIKI NDICHO KINAMTOFAUTISHA MTU NA MTU KWA MUNGU. UPENDO KWA WENGINE!
Nimesema kuanza kujipenda, kumpenda Mungu na kuwapenda wengine sio kitu raisi but ROHO MTAKATIFU YUPO KUFANYA RAHISI KAMA UTAKUWA
TAYARI. NIKUPONGEZE KWA KUENDELEA KUFUATILIA SOMO HILI. TAYARI NINAONA % ZA USHINDI KWAKO. Hakuna kitu kigumu kama kibinadamu kama
kumpenda mtu mwingine unless Roho Mtakatifu amekusaidia, uzuri nakuambia ukweli ili ukuweke huru. Binadamu hatuna shukrani, tunamaudhi, haturidhiki
Tunawakwaza wengine embu fikiria mtu ambaye humpendi unamchukia alafu ndo Mungu anakuambia mtendee mema! au pengine ni Mimi nimekuushi na Mungu
Anakuambia nitendee mema kiukweli kibinadamu ni ngumu sio?. Ila kwa Mungu yote yawezekana. Nataka nikupe siri hii mtu akikitendea uovu manake amemleta
Shetani Katika scene yani shetani yupo pale katika uovu. Sasa kwanini biblia inasema tusilipe baya kwa baya. Sababu kama mtu kamleta shetani wewe hutakiwi
Kumleta shetani unatakiwa umlete Mungu yani mtu akikutendea uovu wewe umtendee wema. Ushawahi jiuliza maana ya andiko hili pengine unalisoma kila siku
But Roho Mtakatifu hajakufunulia kitu kinaitwa behind the scene. Embu tuangalie ilo neno kisha tuendelee
Matayo 6:14
. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
*Ukitenda makosa manake umemuapply shetani. Ukilipa makosa manake umemuapply shetani kwa maana ingine umemsujudia shetani. Lakini
unaposamehe na kutenda mema manake umemuapply Mungu kwa ivyo umemleta Mungu katika tukio. Kwaiyo umemuabudu Mungu. Ndio maana ya ilo neno.
SASA TURUDI KULE MWANZO KUPOKEA UPENDO WA MUNGU NI RAHISI KAMA UTAUELEWA NI NGUMU KAMA HUTAUELEWA, SIJUI KWANINI WATU
WANA PICHA KICHWANI VITU VYA MUNGU NI RAHISI. VITU VYA MUNGU SI RAHISI PAMOJA NA KUJIFUNZA HAYA NA KUYAJUA ILA NAKUHAKIKISHIA HATA
KAMA YANAMPENDEZA MUNGU KAMA HUJAOMBA NEEMA HUTAWEZA. NDIO MAANA MTU ANATAKA KUACHA UBAYA NA ANASHINDWA INGAWA ANATAKA
Kwa iyo upendo nimesema unagharama lakini ndio ufunguo wa kila kitu lakini ukiharibu kwa nguvu zako utakuwia mgumu but ukimruusu Roho Mtakatifu
Ni Raisi Sana raisi mno. UNAANZA KUPOKEA UPENDO KWANZA KWA MUNGU, UKISHAUPOKEA NDIPO UTAWEZA KUJIPENDA MWENYEWE
UKISHAFANIKIWA KUJIPENDA MWENYEWE NDIPO UTAWEZA MPENDA MUNGU! UKIFANIKIWA KUMPENDA MUNGU BASI UMEFANIKIWA AU
ITAKUWA SANA KUWAPENDA WENGINE hii inamana gani? Kama hujipendi, manake hupendi jinsi ulivyo. Na jinsi ulivyo ni Mungu ndio kakuumba kwa
maana ingine humpendi Mungu. Kama humpendi Mungu Ni vigumu mno kumpenda jirani sababu siku zote huwezi Toa kitu ambacho huna. Mfano Mungu
Asingenijaza maneno yake ndani yangu nisingeweza kukuandikia yote haya. Kinaweza kukuandikia maana ndani yangu Mungu kajaza maneno ya kuyaandika
hapa.
KUMPENDA JIRANI YAKO SI KUMFANYIA WEMA KWA KUTAKA FADHILA NITATUMIA MFANO HUU ILI IELEWEKE VIZURI, ukimsomesha mtu kwa mema
akapata degree haina maana ya alipata kazi Ni lazima akupe ela huo sio upendo. Mwanaume akimsaidia mwanamke hata kama hawajuani haina maana kuwa aje
Stake kulipwa fadhila toka kwa mwanamke jinsi anavyotaka yeye huo sio upendo. Ukimsaidia kumtafutia mtu kazi usitake fadhila kwake, au kuanza
kumfuatilia au kumtawala huo sio upendo,ukimpa mtu mtaji mwache awe huru nao, usimtumikishe, na sijui kwanini watu wameweka kichwani ukimsaidia mtu
Lazima urejeshewe fadhila. Ukimsaidia mtu asipokuwa na shukrani haina maana uanze kumtangaza kwa watu. Na kumchafulia jina lake huo sio upendo...
KUNA MAMBO MENGI YANASABABISHA WATU WASHINDWE KUTOA UPENDO, MOJAWAPO MASHAKA, YA MAISHA KUWA ATAKULA NINI? JE VIP KAMA
ATAUMWA ITAKUWAJE? VIP KAMA ATAPOTEZA KAZI? VIP KAMA AKISALITIWA? SHIDA, UGUMU WA MAISHA, KUTOKUWA NA UTULIVU WA
AKILI, UBINAFSI, KUSHINDWA KUSAMEHE, WIVU, KUKOSOA WENGINE, AU WATU KUKUKOSOA, KUHUKUMU WENGINE AU WATU KUKUHUKUMU, KUDHARAULIKA,
KUTOHESHIMIKA, UCHUNGU WA MOYO, WASIWASI, KUTOKUJIAMINI, KUTAFUTA HABARI MBAYA, KUTAFUTA UMBEYA AU KUONGEA HABARI ZA WATU VIBAYA.
Kama Kuna haya mambo yanaendelea ndani mwako automatic huwezi mtendea mtu wema isipokuwa kwa fadhila. Kupitia maisha magumu au wakati mgumu haina
Maana uwe mkatili kwa wengine haina maana uwe huna huruma na wengine, haina maana uwe mbinafsi, haina maana uwe mchoyo, haina maana watu
wanatakiwa Ku suffer kama wewe ulivo suffer, please usimfanye mtu alipe uchungu ulio ndani yako, hasira iliyondani yako, alipe makosa yako mwenyewe au
Apitie unayopitia kisa wewe hukuwa na historia nzuri kisa umesoma kwa shida, kisa umepata kazi unayofanya kwa kujitoa hata wewe mwenyewe, kisa imekugharimu haina maana igharimu na
wengine huo sio ukristo. UKRISTO UPO NJE YA KANISA UKRISRO SI KANISANI KANISANI TUNAENDA KUJIFUNZA JINSI YA KUISHI NJE YA KANISA. Mtu anapopitia
magumu au shida moyo wako usifurahie sababu na wewe unapitia magumu, No! Moyo wako uhuzunike. Ujitoe kwa wema ili uyo mtu avuke. Kama mtu anatatizo na
wewe unajiibu lake ukakaa kimya sababu wewe hujatatua la kwako huo si upendo. Unajua kiukweli si rahisi nasema tena wewe uwe na mizigo alafu uchukue
mizigo ya wengine inahitaji MUNGU, lakini ukimruusu Roho Mtakatifu atakuwezesha atakusaidia, usimsaidie shetani kusambaza ushetani wake.
Bali msaidie Mungu kutangaza upendo wake. Hapo ndipo utaona dhawabu za Mungu. Kutenda wema in God way Ni kutangaza injili. Unajua kwanini
Ni vigumu kumfuata mtu kumweleza habari za Yesu akakusikiza. Ni sababu huna upendo badala ya kukimbilia kuanza kumueleza habari za Yesu tenda wema
kwanza mbariki kwanza tatua shida yake kwanza kisha wema wako utamvuta sasa automatically kwa MUNGU WAKO. ivyo ndivyo tutawapeleka watu kwa Mungu.
Na upendo kwa wengine watu wanautafsiri vibaya upendo ni kuwatreat watu kwa mema bila kutaka fadhila kwao, watu wanaokuzunguka, majirani, watu
Unaoishi nao nyumba moja, watu wa ofisi mwako, watu wa familia yako au ukoo wako bila kujali unamchukia au humchukii bila kujali uyo mtu ni mwema kwako au si
Mwema kwako,
Wakolosai 3
12 . Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
13 . mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
14 . Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
# Huo ndio upendo kwa watu wengine, sio upendo wa fadhila. Sio upendo nipe nikupe! Matatizo yako yasikufanye ushindwe kutenda wema kwa watu.
Kutendea wema kwa watu si lazima uwape pesa chakula au vitu. Kumtia Mtu moyo Katika Kristo huo ni upendo je nikikuuliza ni watu wangap umechukua jukumu la
kuwatia moyo kuendelea mbele au huoni umuhimu kwa kuwa unamambo yako shingoni? Ukiwa na uwezo kidogo ifanye siku ya mtu iwe na furaha ukiona mtu
kanuna Hana raha mnunulie soda na keki au chochote kile alimradi acheke! Muulize kunani mtie moyo aendelee mbele katika Bwana usijifanye kama humuoni. Kuna ile
hali ya kujiact kama huoni mwenye tatizo au hakuhusu ni wewe na nyumba yako, kwenye gari, kwenye gari ofisini, kanisani hutaki kujua jirani yako kaamkaje au
kashindaje najua unajiuliza sasa nikianza kufanya ivyo nitaonekanaje? JIBU RAHISI HUTAONEKANA WEWE ATAONEKANA MUNGU NDANI YAKO. NAJUA UGUMU
UNAWEZA ANZA SHETANI AKAKUWEKEA WATU WA KUKUCHEKA KUKUBEZA AU KUJIONA UNAJIPENDEKEZA NAKUHAKIKISHIA HATA YESU
WALIMCHUKULIA IVYO IVYO LAKINI KUMBUKA SHETANI HATAKI UMELETE MUNGU KATIKA TUKIO NDIO MAANA ATAKUZUIA. WATU WANAWEZA
KUKUCHEKA NDANI MWAKO UTAANZA KUSIKIA MANENO UNASUMBUKA NAYE WA NINI WAKATI WEWE MWENYEWE UNAMATATIZO? UTASIKIA UNAPOTEZA
MDA AU UNAWEZA MTENDEA MTU WEMA AKAWA NA BAD RESPONSE ! UKAJISIKIA VIBAYA. LAKINI KUMBUKA UNAFANYA KWA AJILI YA MUNGU. SI KWA
AJILI YAKO. NA KWA SABABU IYO MUNGU HUACHIA BARAKA ZAKE! USILIPE BAYA KWA BAYA MAANA UNAMSAIDIA SHETANI USHETANI. LIPA BAYA KWA ZURI
MAANA UNAMLETA MUNGU KATIKA TUKIO. NA DHAWABU YAKO NI KUBWA SANA SI HAPA DUNIANI TUU BALI MPAKA MBINGUNI. USIANGALIE BINADAMU BALI
WEWE ANGALIA MUNGU. Aya nayokuambia si kwamba yatachukua siku moja yanaweza chukua mwaka au hata miaka lakini kumbuka hakuna kitu
muhimu Sana kama kupractise upendo. Hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu ambacho watu wengi wameshindwa na wanajaribu hawawezi ila wewe kwa Roho
Mtakatifu atakusaidia upinzani utakuwepo. Lakini nakuhakikishia dhawabu yake ni kubwa kuliko maumivu yake. Ni kubwa kuliko unavyofikiri.
NACHOTAKA KUKUHAKIKISHIA UKICHUKUA HATUA ROHO MTAKATIFU NAYE ATACHUKUA HATUA. NA UTAWEZA KUJIPENDA. KUMPENDA MUNGU NA
KUWAPENDA WENGINE. KUNA WAKATI MWINGINE HUWA NACHUKUA JUKUMU LA KUWAOMBEA WATU NA HUWA SIWAMBII NINAWAOMBEA KWA MZIGO
NA MUNGU ANAMVUSHA NA HATA NIKIJUA WAMEVUKA SIWAMBII ILA ITATOKEA TUU NITAJUA. HUU NI USHUHUDA WANGU BINAFSI LABLA UTAKUJENGA NILIWAHI
OMBEA JAMBO MOJA KWA MDA WA MIAKA 2, BILA MAFANIKIO SIKU MOJA USIKU NIKAACHA KUOMBA NIKAMUULIZA BWANA YESU KWANINI UMEKAA KIMYA?
LEO SIACHI KUOMBA MPAKA UNIAMBIE KWANINI UMEKAA KIMYA NIKAOMBA SANA KISHA NIKACHOKA. ROHO MTAKATIFU AKAANZA KUONGEA NDANI
AKANIAMBIA KWA MDA MREFU SANA UMEKUWA UKIJIOMBEA WEWE NATAKA UACHE KUJIOMBEA NATAKA UOMBEE MTUMISHI WANGU AKAMTAJA OMBEA
HUDUMA YAKE. BASI NIKAANZA USIKU HUO NIKAACHA KABISA KWA IYO NIKAANZA KUMUOMBEA YULE MTUMISHI KWA MZIGO! MUNGU ALIJITUKUZA
NILIPOKUWA NAOMBA TUU ALIKUWA ANATENDA SASA MAMBO YAKAANZA KUBADILIKA KWENYE ILE HUDUMA. NA NINAONA KABISA MUNGU AKITENDA.
GAFLA YALE MAOMBI YAKAKATA NDANI YANGU! NIKAMUULIZA MUNGU WHAT NEXT? HAKUJIBU KITU LAKINI GAFLA! MAMBO KWANGU YALIANZA
KUBADILIKA. KUMWOMBEA MTU NI TENDO LA IMANI TENA MUNGU HULIPENDA SANA. TENGENEZA MAZINGIRA YA KUMTUKUZA MUNGU
WAKO KWA KUTENDA UPENDO KWA WATU. TENDA WEMA BILA FADHILA
UNAJUA BINADAMU UKITAKA AFANYE KITU MPE SABABU NAENDA KUFUNGA SASA SOMO LANGU.
Kwanini upractise upendo? Au why should you work in love?
1. KUTENDA UPENDO NI KUMLETA MUNGU KATIKA TUKIO. KUNAKUPA UHAKIKA WA KUFANIKIWA
2.HUWEZI KUFANIKIWA NJIA ZAKO NI LAZIMA UMPENDE MUNGU(kushika sheria za Mungu)
3. HUWEZI KUWA HURU AU KUWA NA FURAHA KAMILI KAMA HUJIPENDI.
4. ILI KUJIPENDA LAZIMA UPOKEE UPENDO KWA MUNGU
5.KISHA UMPENDE MUNGU, NDIPO UPENDE MWINGINE
6. VIWANGO VIKUBWA VYA BARAKA HULETWA NA UPENDO. YANI KUANZIA KWAKO KWA MUNGU NA WENGINE.
7.UKITENDA UPENDO KUNA MAMBO MENGI SANA HUTAYAOMBA NA YATAKUWA AUTOMATIC KAMA YESU ALIVYOKUWA JINSI ANAPATA AUTOMATIC KILA MAHALI.
*MUNGU NI PENDO. KWA HIYO KUPENDA NI KUMUABUDU MUNGU. USHAFANYA KILA KITU USHAJARIBU KILA MAOMBI KILICHOBAKI SASA TENDA UPENDO. YOU WILL HAVE YOUR WAY OUT.
# HAITOSHI KUELEWA SOMO HILI BALI UNATAKUWA UCHUKUE HATUA SASA! MUOMBE ROHO MTAKATIFU JIKABITHI
KWAKE . POKEA UPENDO KISHA HATUA ZINAZOFUATA MWOMBE ROHO MTAKATIFU AKUSAIDIE.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Barikiwa
ReplyDelete