TUMIA SABABU ZA KIBIBLIA KUOMBA BARAKA ZA MUNGU AKUBARIKI
#MTU AKIKUULIZA BARAKA NI NINI? AU WHAT IS BLESSING UTAMJIBU NINI? JE UNAWEZA TOA MIFANO?
# MUNGU HUJIFUNGUA KATIKA VITI VIDOGO SANA! SAA INGINE KUNA MTU MAHALI HAJUI BARAKA NI NINI? NA HAJUI KIBIBLIA KWANINI
#MUNGU AMBARIKI? KWA IYO SABABU HAJUI MUNGU NAYE ANASUBIRI AJUE. UNAJUA KAMA HUJUI KWANINI NI RAISI
#KUBARIKIWA ALAFU UKAPOTEZA IYO BARAKA MAANA HUJUI SABABU YA MUNGU WALA UMUHIMU WAKE.
au unapomwambia Mungu naomba nibariki huwa inamaanisha nini?
Je Baraka ni kuwa na nyumba? Kuwa na gari? Baraka ni kupata pesa ambayo kwako unaona ni kubwa? Baraka ni kupata kazi? Baraka ni kupata mtoto?
Kuna tofauti gani Kati ya Baraka na zawadi?
BAKARA ni zaidi ya zawadi Baraka ni mlango utoao ahadi za BWANA juu watoto wake usiopungua wala kukatika! Baraka haina kikomo,
Baraka Ina miguu popote uendapo inatembea na wewe! Baraka inafiti mazingira yote. Yenyewe Ina kusudi moja tuu. La kumuhudia mlengwa.
Kwa iyo Baraka ni ROHO WA KRISTO WA MAFANIKIO AMBAO HUMFUATA MTU KUMFANIKISHA MTU AIDHA KIPENGELE HUSIKA! AU VIPENGELE
VYOTE. ndio maana Esau aliuza Baraka akapewa zawadi.
IBRAHIMU alihaidiwa BARAKA sio zawadi. Ingawa katika kusubiri Baraka ya MUNGU anaweza kukupa zawadi kuku entertain. Ili kuifikia Baraka
yako. Nimegundua wakristo wengi tunakomaa na Mungu kumuomba Mungu zawadi na tunasahau kumuomba Mungu Baraka.
Tunasahau kumkumbusha MUNGU BARAKA. Mfano unapotoa FUNGU LA 10! MUNGU ANAKURUDISHIA BARAKA SIO ZAWADI INGAWA
KAMA NILIVYOSEMA MUNGU ANAWEZA KUKUPA ZAWADI ILI USICHOKE KUISUBIRI BARAKA INCASE KAMA MUNGU HATAKUPA
SASA. Mungu anaweza kukupa ZAWADI NA UKAFIKIRI NDO BARAKA YENYEWE.
MUHIMU kuyaelewa haya mambo ili akili yako isimfikirie Mungu katika kiwango cha zawadi. Akili yako imfikirie MUNGU katika kiwango cha
BARAKA, MUNGU hawezi kukupa kitu nje ya kiwango cha imani yako! Kama imani yako inafikiria vitu vidogo vidogo Mungu atakupa vitu vidogo
vidogo. Saa ingine imani yako inaweza kukukwamisha na ukakwama hapo hapo! Ni mpaka MFUMO WA AKILI YAKO UBADILIKE
KUHUSU MUNGU! YANI KICHWANI MWAKO UNAPOMUWAZA MUNGU je unamuona Mungu ni wa kukupa zawadi au Baraka?
AKILI YAKO INAPOKUBALI KUMFIKIRIA MUNGU KATIKA VIWANGO VIKUBWA BASI HIVI VITU VIDOGO NI RAISI KUWA NAVYO.
Mfano unaposikia Baraka za Mungu labla akili yako inawaza kazi. Alafu inawaza kazi ya mshahara wa mil 3! Hapo unasema hapo nimefika kabisa.
Sasa kinachotokea Mungu naye atakupa kazi inayolingana na iyo iyo au chini ya hapo. Tena hataanzia hapo ataanzia chini! Huku
akikukomaza mahusiano yenu mpaka atakufikisha kwenye huo mshahara wa mil 3! Hawezi kukupa mshahara nje ya imani yako! Akikupa ni raisi
kukuvuruga sababu moyo wako hakuuandaa kupokea mshahara zaidi ya mil 3. Kwa iyo Mungu atakupeleka kidogo kidogo mpaka unafikia pale kwenye imani yako.
NA HII NDO SABABU YA KUPOKEA KIDOGO NA KUBAKI KUMLALAMIKIA MUNGU. MUNGU ANAANGALIA MOYO WAKO UNASEMAJE NDIPO ANATENDA.
KWA IYO WENGI TUMEMFUNGA MUNGU KATIKA LEVEL YA ZAWADI. KISHA MUNGU AKIENDA KIDOGO KIDOGO ILI KUFIKIA IYO LEVEL YA
IMANI. TUNALALAMIKA KWANINI HATUPI BARAKA KWANINI ANATUPA ZAWADI IKO HIVI HATA KAMA MUNGU ANAKUPENDA KIASI GANI
KAMA HAJAKUANDAA HAWEZI KUKURUPUKA KUKUPA MIL 100, lazima tukue kiimani unless AMEKUANDAA! sisemi Hana uwezo
wa kukupa no! Nasema hawezi kukupa PESA KAMA MOYO WAKO HAKUANDALIWA KUPOKEA! UKIONA MIRACLE KUBWA BASI JUA MUNGU
ALISHAMUANDAA KWAHIYO IYO PESA HAIWEZI KUMVURUGA.SASA NAKUPA MBINU TENGENEZA MOYO WAKO UM'BEBE MUNGU
KATIKA VIWANGO VYA BARAKA ILI ANGALAU BASI ZAWADI USIKOSE.
SIKU MOJA NILIMWOMBA MUNGU ANIONYESHE BARAKA ALIZONIANDALIA MAISHANI HATA KAMA MUNGU HANA MPANGO
NIZITAWALE SASA. UNAJUA MUNGU NI MWAMINIFU ALINIONYESHA KWA KWELI NILIJISHANGAA. VITU AMBAVYO NILIKUWA NAMUOMBA
MUNGU NAWEZA KUSEMA VILIKUWA VYA MTOTO MCHANGA KABISA.
Isaya 65:
19. Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza.
20. Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.
21. Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.
22. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.
23. Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.
24. Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
#Hutajitaabisha na kazi yako bure! Hii ni guidance, proctection, support, na anamalizia kuwa itakuwa ya kwamba kabla hawajaomba nitajibu, wakiwa
katika kunena nitasikia. What a blessing! Unajua ukiwaza vizuri iyo unaweza cheka siku nzima. Manake nini? au kwa maneno mengine MUNGU
ANASEMA IVI NAYAJUA MAHITAJI YAKO! KWA IYO NACHOSIBIRI NI WEWE UOMBE TUU MAANA SHERIA LAZIMA UOMBE ILI NITENDE AU
UPEWE KWA KUWA NITAKUSIKIZA. UTAKAPOANZA KUOMBA. SABABU KABLA YA KUANZA KUOMBA NINAJUA UTAKACHOOMBA NA
NINAJUA NITAKUJIBU VIPI NA NITAKUSAIDIA KWA KUWA MIMI MUNGUNAKUSUBIRIA UOMBE TUU.
#SOMO HILI LINAKUONGEZEA MBINU ZA KUOMBA MBINU ZA KUMBANA MUNGU KWENYE KONA KUPITIA NENO LAKE MWENYEWE
sasa naenda kujibu lile swali kwanini Mungu akubariki. Nachomuomba Roho Mtakatifu akudakishe hata point moja tuu usimamie alafu uende
kwa Mungu kwa mada nzito. KWA KUELEWA TUU BARAKA NI NINI NA KWANINI MUNGU AKUBARIKI KUNA WATU MUNGU ATAENDA KUACHILIA BARAKA IZO JUU YAO.
1Samueli 1
11. Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.
1 Samueli 1:
20. Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.
MUNGU ALIZUIA UZAO WA HANA KWA MAKUSUDI ILI APITISHE NABII TUMBONI MWAKE! JE USHAWAHI KUWAZA KAMA HANA ANGEENDA
KAWAIDA AKAPATA MIMBA JE UYO MTOTO ANGEMTOA KWA BWANA!? jibu ni raisi asingemtoa! MUNGU alizuia tumbo la HANA MPAKA HANA
ALIPOJUA KWANINI APATE MTOTO. HANA ALIPOTAMBUA KUWA MTOTO WAKE ANATAKIWA NA BWANA. MUNGU AKIKUBARIKI AKAMPA MTOTO.
MUNGU AMEKUWEKA HAPA DUANI KWA KUSUDI KWA IYO KAMA HAUPO KWENYE KUSUDI MUNGU NAYE HAKUSAIDIII! MAANA UPO NJE
YA KUSUDI. MUNGU ANASABABU ZA KIBIBLIA ZA KUMBARIKI MTU LAZIMA AU MUHIMU UZITAMBUE. UKISHAZITAMBUA HATA AKIKUPA
UTAHESHIMU HUTAKENGEUKA. BWANA YESU ASIFIWE!
# 1. MOYO KUWA MWAMINIFU MBELE ZA MUNGU. Nehemia 9-7-8
Nehemiah 9:7
. Wewe ndiwe Bwana, Mungu, uliyemchagua Abramu, na kumtoa katika Uri wa Wakaldayo, na kumpa jina la Ibrahimu;
. Wewe ndiwe Bwana, Mungu, uliyemchagua Abramu, na kumtoa katika Uri wa Wakaldayo, na kumpa jina la Ibrahimu;
Nehemiah 9:8
. nawe ukauona moyo wake kuwa mwaminifu mbele zako, ukafanya agano naye, kumpa nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Myebusi, na Mgirgashi, naam, kuwapa wazao wake; nawe umeyafikiliza maneno yako, kwa kuwa ndiwe mwenye haki.
. nawe ukauona moyo wake kuwa mwaminifu mbele zako, ukafanya agano naye, kumpa nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Myebusi, na Mgirgashi, naam, kuwapa wazao wake; nawe umeyafikiliza maneno yako, kwa kuwa ndiwe mwenye haki.
# Hivi ushawahi jiuliza Mungu alitumia vigezo gani? Kumchagua Ibrahim! Au unafikiri Mungu alimchagua tuu? Biblia inasema Ibrahim alikuwa mwaminifu
alikuwa na moyo mwaminifu mbele za Bwana. Ni kama jinsi wewe ulivyokuwa mwaminifu mbele ya Mungu. Katika nyakati zote! Za furaha! Za shida! Za
kujaribiwa! Hujawahi mkana Mungu na kumuacha Mungu. Wala hujawahi sema basi wokovu nimeshindwa narudi
duniani. Huo uaminifu unapoendelea kwa mda mrefu Mungu Hana jinsi lazima akubariki
# . 2 KUTAKASA JINA LAKE LILILOTUKANWA/ KULIOSHA JINA LAKE LILILOZARAULIWA. Ezekiel 36-22
Ezekieli 36:22
. Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia
. Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia
unajisi katika mataifa mliyoyaendea.
Ni ukweli usiofichika sisi tuliokoka tunatukanwa tunadharaulika tunabezwa hasa na watu waliotuzunguka ingawa huwasikii but tunasemwa vibaya! Pia
wachawi waganga wa kienyeji wanaoharibu mambo yetu kila kukicha huwa wanafurahi kuona tunateseka na wanatucheka. Na wanamcheka Mungu
wetu. Shida inakuja pale unapopitia jangwani na unamsubiri Mungu atende utasikia anajifanya mlokole mbona anadaiwa mpaka anajificha! Yeye si
ameokoka aombe sasa Mungu wake amsaidie. Haya ni matusi makubwa kwa Mungu. Maana anayetukanwa siyo aliembeba Mungu no! But Mungu
inapofikia hapa mtu akianza kutukanwa sababu labla anapitishwa jangwani na mambo hayaendi vizuri pale mtu anapokuwa kwenye majaribu ya Mungu
na watu wasiomjua Mungu wakianza mcheka haya ni matusi kwa Mungu. Hapo ndipo Mungu anasema kwa ajili ya jina la langu nitatenda. Embu na wewe
mfuate Mungu mwambie Mungu maisha yangu hayaendani na jina lako nililolibeba jina lako Mungu linatukanwa sababu sina kazi, sababu Nina madeni,
sababu huu ugonjwa hauoponi. Sababu sina kodi, sababu nimepanga Mungu naomba ufanye kitu kwa ajili ya jina lako.
#. 3 KUWADHIBITISHIA WATESI WAKO KUWA MUNGU WAKO ANA NGUVU. zaburi 23-5
*wakati mwingine anapoona watesi wako wanajiinua Sana! Au wanakuonea Sana MUNGU HULAZIMIKA KUFANYA KITU ILI WATU WAMUOGOPE MUNGU
WAKO. mfano kama uko chini ya mtu na anatumia pesa au umaarufu chochote au uchawi kukukalia. MUNGU HUWA HUFANYA KITU KUKUINUA KWA JUU
YAKE. NA anapotenda kwako watesi wako lazima wakimbie huku wameweka mikono nyuma, kwa iyo wakati mwingine utamwambia Mungu tenda BWANA ILI
WAKUJUE WEWE NI MUNGU MWENYE NGUVU! TENDA BWANA ILI WAJUE NINAYE MUNGU MWENYE UWEZO.
Zaburi 23:5
. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
#.4 KUVUNJA NGUVU YA UPINZANI NA KUKUPA WEWE KIBALI. Yoshua 3
Yoshua 3
7 . Bwana akamwambia Yoshua, Hivi leo nitaanza kukutukuza mbele ya Israeli wote, wapate kujua ya kuvushwa uwa mimi nitakuwa pamoja na wewe, kama nilivyokuwa pamoja na Musa.
8 . Nawe uwaamuru hao makuhani walichukuao sanduku la agano, ukawaambie, Mtakapofika ukingo wa maji ya Yordani, simameni katika Yordani.
10 . Yoshua akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kuwa Mungu aliye hai yu kati yenu, na ya kuwa hatakosa kuwatoa mbele yenu Mkanaani, na Mhiti, na Mhivi, na Mperizi, na Mgirgashi, na Mwamori, na Myebusi.
13 . Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la Bwana, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yatatindika, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama chuguu.
14 . Hata ikawa, hao watu walipotoka katika hema zao, ili kuvuka Yordani, makuhani waliolichukua sanduku la agano wakatangulia mbele ya watu,
15 . basi hao waliolichukua hilo sanduku walipofika Yordani, na nyayo za makuhani waliolichukua sanduku zilipotiwa katika maji ya ukingoni, (maana Yordani hujaa hata kingo zake na kufurika wakati wote wa mavuno),
16 . ndipo hayo maji yaliyoshuka kutoka juu yakasimama, yakainuka, yakawa chuguu, mbali sana, huko Adamu, mji ule ulio karibu na Sarethani, na maji yale yaliyotelemkia bahari ya Araba, yaani Bahari ya Chumvi, yakatindika kabisa; watu wakavuka kukabili Yeriko.
17 . Na hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana wakasimama imara mahali pakavu katikati ya Yordani; Israeli wote wakavuka katika nchi kavu, hata taifa lile lote likaisha kuvuka Yordani.
#Wakati mwingine watu wanaweza kuwa wanakupinga au wanakujia juu au wako kinyume na wewe Mungu hulazimika kufanya kitu kwako. Ili kuvunja nguvu ya
upinzani! Kwa kukupa kibali iwe kwenye ndoa! Huduma! Kazini! Biashara popote Mungu alipokuita unajua unaweza kukaa na watu wa karibu kabisa na
wakakupinga au kukuzunguka. Na ni kawaida wanasema atleast 10% ya watu wanaweza kuwa wanakupinga na hawakukubali. Mungu hujitukuza kwako
kwa kufanya kitu ili upate kibali mbele yao. Hata wasipokubali ila wakikuangalia Kibali ulichonacho au baraka uliyonayo hawana jinsi watakubali tuu. MUNGU
ALIBIDI APASUA MTO JORDANI KAMA VILE ALIVYOFANYA KWA MUSA KATIKA BAHARI YA SHAMU NA MUSA ILI JOSHUA APATE KIBALI MBELE YA
WANA WA ISRAELI. wakati mwingine utamwambia Mungu naomba utende jambo naomba unibariki ili kuvunja nguvu ya adui zangu.
* unajua ninaposema Baraka za ndoa! Ni pana Sana huko ndani yake. Ninaposema Baraka za familia ni pana Sana ndani yake.
Ninaposema Baraka za Elimu ni pana Sana ndani yake. Ninaposema baraka za kazi ni pana Sana ndani yake. Baraka za biashara ni pana Sana ndani yake.
Unaposema Baraka za ulinzi ni pana Sana ndani yake. Unaposema Baraka za kumuiliki , kutawala kufanikiwa au Baraka za watoto au wajukuu ni pana
Sana ndani yake. Na watu hawatilii uzito ili swala sababu bado hawajui au hawajaelewa vizuri. Unaposema Baraka za kilimo ni pana Sana ndani yake.
Unaposema Baraka za huduma ni pana Sana ndani yake. Watu tunaomba tunadonoa donoa tuu. Hatuzami vizuri ndani kikanuni na kwa neno. Alafu picha
tuliyokuwa nayo kichwani ni ndogo ndo maana tunamatokeo madogo. Tunafanya maombi ya jumla Sana wakati mwingine tunalipua lipua na
hatuna mda na Mungu wakati mwingine kwa ajili ya kipengele kimoja ukimaliza uvuke ndipo uhamie kingine. Lazima tuombe kama hatuombi then we should
expect nothing. Miracle's zinatokea kwa ajili ya Mungu kujitukuza tena ni chache Sana. Usiishi kwa miracles ishu kwa neno na kusimamia imani yako katika neno.
#5. KUIBINGIRISHA AIBU YAKO ILIYOKUWA IMEKUKALIA Izaya 54:4
* Unajua Kuna matukio au majaribu hata kama yakiondoka bado yanaweza kuacha alama! Mfano mtu akiwa mlevi wa kutupa! Au mwanamke aliyekuwa
akitumia mwili wake kwa ajili ya pesa! Au mtu aliyepitia ufukara Sana! Au iliwahi mpata aibu au fedheha! MUNGU HULAZIMIKA KUKUINUA KIASI CHA
KWAMBA KITAWASAULISHA WATU LILE BAYA LILILOKUPATA. hapa unaweza msihi Mungu aondoe aibu yako kwa kufanya jambo jipya.
unajua unapopitia pito la mda mrefu alafu likakusumbua Mungu anapolitatua si Raisi Kumuacha Mungu au kumsahau Mungu. Kuna mambo yamekaa mda
mrefu! Na yanasumbua but finally ukilitua si raisi kumsahau Bwana Mungu wako.
Isaya 54:4
. Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.
# 6. UWEZE KUMWABUDUBU KWA AMANI NA FURAHA. zaburi 116-12-14
Zaburi 116:12
. Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Zaburi 116:13
. Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana;
. Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana;
Zaburi 116:14
. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.
. Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.
# 7. ILI USIMSAHAU MUNGU WAKO ALIYEKUTETEA KATIKA PITO LAKO kumbu 12-15-18
Kumbukumbu la Torati 8
12 . Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;
13 . na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;
14 . basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;
15 . aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,
16 . aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.
17 . Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
18 . Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
# katika strong point za kumuambia Mungu au kumshawishi Mungu. Kuwa Mungu naomba hiki Sababu kinasumbua moyo wangu kuwa na amani na uhuru
wa kukufanyia ibada katika Roho na Kweli! Unajua mtu mwenye matatizo anaweza kuabudu lakini moyo unaoenda kwa Mungu ni wa malalamiko. Mtu
aliyejibiwa na Mungu na Furaha akiabudu basi Moyo wake hutoa amani na Furaha. Unapomfuata MUNGU NA KUMWAMBIA NAOMBA UNIBARIKI ILI
NINAPOKUJA MBELE ZAKO NIKUABUDU KATIKA ROHO NA KWELI. NISIJE MBELE ZAKO KWA KUSUKUMWA NA MATATIZO BALI NIJE KWA KUWA
MOYO WANGU UNAKUPENDA NA KUKUFURAHIA.
pia katika Mungu hufanya ili kuimarisha agano Mungu aliofanya na akina
pia katika Mungu hufanya ili kuimarisha agano Mungu aliofanya na akina
Ibrahimu. Mfano Mungu akikupa vitu vingi ukala ukashiba na ukajenga. Ukabarikiwa hii inamaana utamwamini MUNGU kuliko kitu chochote. Ushawahi
kuwaza au kujiuliza kwanini shetani hataki watoto wa Mungu wabarikiwe! The moment umebarikiwa agano lako na Mungu litakuwa strong than before.
Chukulia ulikuwa huna kitu kabisa baada ya mda mrefu anakukumbuka anakupa miradi mikubwa na pesa inakuwa si tatizo tena je mahusiano yako na Mungu yatakuwaje?✋
# SABABU YA NANE (8) NA YA MWISHO
# 8. ILI UWAINUE WENGINE WALIO, CHINI Yohana 12:32,luka 22:31-32.
HII NI MUHIMU SANA, Mungu akikiinua ni ili uwainue wengine katika ukoo wako Katika familia yako. Mungu akitaka kuinua familia flani hainui wote.
Bali anamteua mmoja na anamuinua sasa kupitia hao ndo anategemea kama ni wewe watu wale watu wavae watu waende shule maisha yaendelee. Bahari
mbaya tukishabarikiwa huwa tunajilimbikizia Mali. Na kusahau wengine ndo mana Mungu akikupa ikawa unashindwa kuwainua wengine
atainua mtu mwingine na wewe atakupeleka chini. Hakunaga Baraka ya kuringishia watu, hakuna Baraka ya kutesa watu. Sababu pia inaweza Nenda
nayo kwa Mungu ni hii very strong. Kuwa Mungu nibariki ili niinue watu kwenye ukoo wangu. Kwenye familia yangu. Sasa ole wako uweke nadhiri alafu
upate ukae kimya ulicho ulicho kiahidi Mungu atakitaka mkononi mwako. Hizi ndizo hoja za msingi. Sasa haitoshi kusema aaah hizo nazijua Mungu h
aangalii mdomo wako au akilini mwako MUNGU HUANGALIA MOYO! JE MOYO WAKO UNATAKA KUBARIKIWA KWA SABABU HIZI NILIZOANDIKA? AU ZIKO
NJE YA HIZI? JE VOGUE UNALOMUOMBA MUNGU NI SABABU YA SABABU HIZI NANE (8) AU SHOE OFF? MOYO WAKO NDIO UNAOJUA.
# 8. ILI UWAINUE WENGINE WALIO CHINI. Yohana 12:32, Luka 22:31-32
* utachukua daftari yako! Utaandika zile Baraka unazozihitaji kwa Mungu kisha Mimi nitakusaidia
kuingia ndani ili uombe kwa undani. Kuhusu izo Baraka. Ili usiombe vitu vidogo vidogo. Omba Baraka usiombe zawadi! Tutafanya maombi haya kwa
mda wa siku 7 seriously utaombea Baraka hizo na kuleta hizi sababu (8) kwa Mungu Kila siku katika hizo siku 7! Na katika Baraka hizo zote ulizoziandika.
# Zipo baraka za ndoa. Ndoa ikiwa na baraka toka kwa Mungu misuguano itapungua, uchumi utakaa vizuri, watoto watapatikana, upendo utaongezeka,
matatizo yatakuwepo lakini hayatawapa presure yani utakuwa katika uwezo wa kuyahandle. Ndoa inahitaji sana baraka
# zipo baraka za Afya! Afya si lazima uumwe afya ni pamoja na furaha na amani! Afya ni pamoja na kula vizuri wewe na familia yako unapopata baraka
za afya ela yako haitaishia hospital. Unapokuwa na afya akili yako itafanya kazi vizuri kwa utulivu itakuwa na uwezo wa kutatua matatizo! Utamwabudu
Mungu katika Roho na Kweli kama una afya nzuri sasa si mtu wa nje tuu. Afya pia mtu wa ndani anahitaji afya mfano nafsi kuinama ni dalili ya kutokuwa na
afya. Kula chakula na kutokufurahia manake huna afya ya kula au kukosa appetite. Afya huombi unapoanza
kuumwa unaomba kabla ya kuumwa. afya kitu kipana sana. Iyo ni mifano tuu ya baraka kwa iyo nenda kwa Mungu kwa picha kubwa ya baraka.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Nimejifunza kitu, asante sana na ubatikiwe na Mungu wetu alie hai
ReplyDeleteNimejifunza kitu , Mungu akubariki sana, akutie nguvu uendelee kutoa hii Huduma, watu wengi tuna ihitaji, na akili zetu zimetekwa.
ReplyDeleteNimejifunza kitu , Mungu akubariki sana, akutie nguvu uendelee kutoa hii Huduma, watu wengi tuna ihitaji, na akili zetu zimetekwa.
ReplyDeleteNimijifunza Mungu akuvuvie mengi Sana .ubarikiwe Sana
ReplyDeleteJamani haya ndio mambo sasa yaani umenisaidia vzr #Ubarikiwe
ReplyDeleteMungu akubariki sana, nmebarikiwa sana, naamini sitakuwa nlivyokuwa.
ReplyDeleteMungu akubariki sana nimejifunza vitu
ReplyDeleteNmebarikiwa Sana na nmejifunza mengi, mungu akubariki
ReplyDeleteMwenyezi MUNGU akubariki sana nimejifunza kitu kikubwa sana.
ReplyDelete