UFANYAJE UNAPOPATA KITISHO/HOFU YA KUKUONDOLEA UJASIRI/KUKUFANYA KUTOKUJIAMINI TENA
Swali: Ufanyaje unapopata kitisho/hofu au taarifa za kukuondolea ujasiri/kukufanya kutokujiamini tena?
* labla niliwekee uzito au nitoe mfano! Umeokoka vizuri SHETANI ANATABIA YA KUTISHA, kuna vitisho vingine bila Roho Mtakatifu
haijalishi unajua neno kiasi gani vitakutikisa tuu! Haijalishi wewe ni mwamba kiasi gani bila Roho Mtakatifu vitakushake! Just
imagining umeombea ulinzi familia yako alafu kesho yake asubuhi unasikia mtu amekufa. Umeombea ulinzi duka lako kwenda kufungua
unakuta wamevusha wameiba. Unamwombea mtoto wako afaulu vizuri mitihani gafla anarudi nyumbani kafukuzwa shule kwa
utovu wa nidhamu. Au anarudi mjazito! Mungu amekupa gari umeliombea vizuri ile unaanza kuliendesha tuu unapata nalo ajali
linakuwa written off! Unaomba Mungu akupe kodi ya nyumba ili usije fukuzwa ukadhalilika ukaaibishwa linaibuka tatizo kubwa
la kodi linanafuu. Katika situation kama hizi au mifano kama hiyo UNAFANYAJE?
# wengi huwa tunapanic na tunasahau hata mistari ya biblia, au tunasahau kwamba tunaweza ya fix! HAPA DUNIANI MAJI YAKISHA MWAGIGA HAYAZOLEKI. KWA
MUNGU MAJI YAKISHAMWAGIGA YANAZOLEKA NA YANABEBEKA. je unazoeaje maji yaliyomwagiga katika ulimwengu wa Roho?
2 Mambo ya Nyakati 20:
1 . Ikawa baadaye, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni,
2 . Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi).
3 . Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.
4 . Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta Bwana.
5 . Yehoshafati akasimama kati ya kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, nyumbani mwa Bwana, mbele ya ua mpya;
6 . akasema, Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako.
7 . Si wewe, Ee Mungu wetu, uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele?
8 . Nao walikaa humo, wamekujengea patakatifu pa jina lako humo, wakisema,
9 . Yakitujia mabaya, upanga, hukumu, au tauni, au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako, (maana jina lako limo katika nyumba hii), na kukulilia katika shida yetu, nawe utasikia na kuokoa.
10 . Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;
11 . tazama, jinsi wanavyotulipa, wakija kututupa toka milki yako, uliyoturithisha.
12 . Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yatazama kwako.
13 . Wakasimama Yuda wote mbele za Bwana, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.
14 . Ndipo Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi, wa wana wa Asafu, akajiliwa na roho ya Bwana, katikati ya kusanyiko;
15 . akasema, Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya Mungu.
16 . Kesho shukeni juu yao; tazameni, wanakwea kwa kupandia Sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli.
17 . Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni, simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope, wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao; kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi.
18 . Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana.
# HAPO MUNGU ALINIPA MAMBO 10 AMBAYO NATAKA TUYAANGALIE. YAKUFANYA
1. YEHOSHEFATI alipata kitisho. Alipata taarifa mbaya ya kutisha kama jinsi Mimi na wewe tunaweza jikuta katika hali iyo. Taarifa mbaya
inaweza kuwa ugonjwa toka kwa dk. Taarifa mbaya inaweza kuwa kuibiwa, taarifa mbaya inaweza kuwa kutengana kwa ndoa, taarifa
mbaya inaweza kuwa kufukuzwa kazi, kupata ajali, msiba kwa namna moja au nyingine kila mtu aliwahi pata taarifa mbaya! Kila mtu
anakutana na taarifa mbaya. Tunatofautiana kwenye mda tuu.
2. AKAOGOPA , mstari wa 3! Kwa iyo kuogopa ni hali ya kawaida. Lakini si hali ya kawaida kama utaogopa mpaka ushindwe kuomba,
hofu inatakiwa ipite tuu sio ikae. Sasa Kuna watu wakipata vitu vya kuwatisha wanatetemeka mpaka wanamsahau Mungu Wao, ujasiri
unawatoka wanashindwa kuomba mbaya zaidi wanasahau Wao ni nani? Na wanasahau wanauwezo wa kusimamisha hiyo hofu,
wanauwezo wa kutuliza mawimbi ya bahari! Tatizo si kuogopa tatizo iyo hofu au woga unakaa na wewe kwa mda gani? Je unakudisturb
kiasi cha kushindwa hata kuomba? Je baada ya kushitushwa au kupoteza ujasiri au kuwa mdogo wanasema mjini je huwa unafanyaje kuinua nafsi yako?
3. AKATANGAZA MBIU YA KUFUNGA NA KUMTAFUTA BWANA, unajua nirahisi kusema aaah iyo naijua nitafanya! Nirahisi
sasa kama hauko kwenye tatizo. Ni rahisi kukiri maneno ya Mungu kama hauna tatizo lakini kama uko kwenye tatizo ndo utajua hiki kitu
naongea hapa! Ni Raisi kuwa jasiri wakati haupo kwenye tatizo wengi tukiwa kwenye tatizo huwa tunamkana Mungu. Kivipi
tunamkana Mungu kwa kukimbilia kwa binadamu kwanza. Utaanza kupigia simu watu, utalalamika kwanza! Kisha baada ya jitihada
zote kufaili ndipo tunamtafuta Mungu. Wachache wakipata tatizo kimya kimya kwenda kwa Mungu mojakwamoja. Mara nyingi tatizo
likitokea huwa tunajaribu kusolve sisi wenyewe kwa akili zetu tukishashindwa sasa huwa ndio tunampelekea Mungu. Angalia
Yehoshofati baada ya kupanic na kuogopa! Hakutafuta mtu alichofanya aliuelekeza uso wake kwa Mungu. Wengi tukipata
matatizo tunaanza sisi kwanza tukishafaili ndipo tunamtafuta Mungu. Hii inatufundisha unapopata tatizo cha kwanza kufanya elekezo
uso wako kwa Mungu. Manake nini acha kila kitu unachofanya mgeukie Mungu. kabla hata ya kujaribu kutatua mwenyewe. Kabla hata ya
kujaribu kuwashirikisha watu. Hata kama ilo jambo linapressure kiasi gani. Mpe MUNGU NAFASI YA KWANZA.
4. YEHOSHOFATI ANAISOMA C.V YA MUNGU, hapa ndipo kwenye point yangu! Angalia mtu wa Mungu uyu jinsi anavyomtafuta Mungu
anaisoma c.v ya Mungu anamuinua Mungu. Unajua Katika biblia Kuna watu wawili walikuwa na ushawishi mkubwa kwa Mungu walikuwa
wanaweza mshawishi Mungu mpaka Mungu akabadili mawazo yake. Alikuwa Musa na Daudi. Nikamuliza Roho Mtakatifu nini siri
yao ya ushawishi Wao! Ndipo akaniletea maombi haya ya Yehoshefati! Angalia kapata kitu cha kumuogopesha ndio kaogopa
lakini baada ya kuogopa kitu cha kwanza akautafuta uso wa Mungu. Baada ya kuutafuta uso wa Mungu siku hizi tunaweza sema kuuleta
uwepo wa Mungu. Yehoshefati hakuanza malalamiko kama sisi tunavyofanya. Utasikia mtu unamwambia Mungu "Mungu Mimi
siwezi kabisa" "nimefika mwisho" au kwanini Mungu inatokea kwangu? Au why me? Yehoshefati hakulalamika isipokuwa alichofanya
cha kwanza ni kusoma c.v ya Mungu anamkumbusha Mungu mambo aliyowahi wafanyia. Haya ndo maombi ya ushawishi mbele ya
Mungu na Maombi ya mtu aliyekomaa. Angalia Mstari wa 6 akamwambia Mungu si wewe Mungu wa Baba zetu?si wewe
Mfalme?Si wewe mwenye uweza? Mwenye nguvu angalia mtu wa Mungu anavyopeleka mada. Hasemi Mungu peke yangu siwezi no!
Anasema sifa za Mungu kabla hata ya kuleta mahitaji yake. Unajua hapa nimejifunza Sana. Unaweza tumia c.v ya Mungu maishani
mwako unaweza Muambia Mungu si wewe uliyenifanyia hivi! Si wewe uliyenisaidia pale! Si wewe Mungu wangu uliyenipa wokovu. Ongea c.v
matendo makuu Mungu aliyewa kukufanyia. Maana kwa Mungu hakuna kuvushwa kidogo. Kuvushwa ni kuvushwa tuu.
5. KISHA YEHOSHAFATI anamkumbusha Mungu ahadi zake! Kwa binadamu! Hapa sasa ni pale tunasoma maandiko tunam kumbusha Mungu maandiko ya
ahadi alizozitoa katika mazingira tofauti. Hii ni muhimu Sana kuwa na maandiko tofauti tofauti ya kuombea mambo mbalimbali
unaandika nyuma ya daftari yako ya Maombi. Wangap wanadaftari kwa ajili ya Maombi. Muombaji mzuri lazima uwe na daftari pekee kwa
ajili ya Maombi. hapa unamsomea kumkumbusha Mungu ahadi zake. Mstari wa 8
6. HAPA SASA YEHOSHAFATI anamuuliza Mungu je ahadi zako Mungu hutazitimiza! Mfano unaweza ukamwambia Mungu lile
andiko la Isaya 54:15 kuwa wanaokusanyika kwa ajili yako lakini si kwa shauri la BWANA kuwa wataanguka kwa ajili yako. hapa
unaweza muuliza Mungu je hutawaangusha. Haya ndo maombi ya ushawishi haya ndo maombi ya Musa na Daudi walikuwa
wanaomba kwa Mungu anaghairi ubaya kwa wana wa Israeli.
7. Baada ya yote haya sasa YEHOSHEFATI NDIPO ANAMSHITAKI ADUI YAKE AU ANAELEZEA TATIZO KWA MUNGU!
mstari wa 10 hakukurupuka kule juu hii Ina maana gani? MUNGU ANATAKA AU ANAPENDA KUONYESHWA KUWA YEYE NDIO
PEKEE NA YEYE PEKEE NDIO ANAWEZAYE KUTATUA SHIDA YAKO.
8. YEHOSHEFATI anajitoa katika tatizo kisha anamuweka Mungu. HAPA WATU WENGI SANA NDO HUWA TUNAKOSEA HATA MIMI
NILIKUWA NAKOSEA MPAKA ROHO MTAKATIFU ALIPONIFUNDISHA. JIFUNDISHE KUSEMA YESU NAOMBA UNISAIDIE BILA WEWE
SIWEZI. MWAMBIE MUNGU WEWE NDIO UNAYEWEZA. KUNA MANENO MAWILI SIKU HIZI NAYATUMIA NA YAMEBADILI SANA AU KUKUZA
HALI YA KIROHO. NENO LA KWANZA BWANA YESU NISAMEHE MIMI SIJAMILIKA MIMI NI DHAIFU. NENO LA PILI BWANA YESU MIMI
SIJUI LOLOTE NA SIWEZI LOLOTE WEWE NDIO UNAYEWEZA HATA KAMA UNAJUA KUFANYA MAOMBI YA VITA HATA KAMA KWA UZOEFU
UNAJUA ALWAYS JIWEKEE WEWE HUWEZI NA UNAOMBA MSAADA USAIDIWE. NAKUAMBIA UKIFANYA HIVI UTAMWONA MUNGU. WATU
WENGI WANASHINDWA VITU VINGI SABABU HAWATAKI KUKIRI WANAHITAJI MSAADA NA YESU ANAKUANGALIA TUU. sasa angalia
Yehoshafati mstari 12 anamwambia Mungu hatuna uwezo! Hatujui tufanyaje. Wengi tunaweza kujua tatizo alafu na kukurupuka.
kuanza kuvunja kubomoa bila kuomba msaada lazima uombe msaada. Kwanza ndipo maombi mengine yaendelee...
9. BAADA YA MAOMBI HAYO YEHOSHAFATI anatulia uweponi mwa Mungu. Wakristo wengi Sana hata Mimi nilikuwa mmoja Wao!
Tunaomba tukishaomba huwa hatusubiri majibu! UNATAKIWA UKISHAOMBA SIMAMA AU KAA AU KAMA UTALALA CHINI SAWA KAA
KIMYA USIONGEE KITU KWA DK. 5 MARA NYINGI SANA ROHO MTAKATIFU HUWA ANAJIBU WATU. HUKO KUNAITWA KUZAMA KATIKA
ROHO. AIDHA UMENENA KWA LUGHA AU USHAMALIZA KUOMBA MDA WOWOTE JIJENGEE IYO TABIA. KAA KIMYA KABISA SEMA
ROHO MTAKATIFU NIKO MAHALI HAPA NAKUSUBIRI WEWE SEMA NAMI BWANA YESU. ALAFU UNAKAA KIMYA ZIMA KILA KITU
T.V RADIO SIMU EVERYTHING KAA UWEPONI MWA MUNGU. UTAKUTA KIPINDI HIKI CHA KUTULIA UWEPONI MWA ROHO MTAKATIFU
NDIPO ROHO HUFUNGUA WATU, HUPONYA WATU HUBARIKI WATU. TATIZO HATUNA MDA SASA MIMI HII NAIFANYA ASUBUHI NIKIAMKA
NA JIONI KABLA YA KULALA LAZIMA NIOMBE ALAFU NITENGE DK. 10 ZA ROHO MTAKATIFU! NAKAA KIMYA NAMWAMBIA
BWANA YESU TALK TO ME NAKUSIKIZA. ROHO MTAKATIFU NIPO MBELE YAKO NAJISA
LIMISHA KWAKO PLS TALK TO ME!
MANENO HAYO UTAYAZUNGUMZIA MWANZONI. UTAKAA KIMYA KISHA WAKATI UMEKAA KIMYA SHETANI ANAWEZA JARIBU KUKUDISTURB
KWA KULETA MAWAZO MABAYA DONT WORRY USITOKE YAKIANZA KUJA TUU MAWAZO MABAYA RUDIA MANENO YALE YA MWANZO
UNAWEZA ONGEZEA SEMA YESU NAKUPENDA. YESU NAJUA UNANANIPENDA. HII ITAKUFANYA UVUKE SEHEMU NYINGI SANA. ndo
mana Yehoshefati hakuondoka uweponi mwa Mungu mpaka Mungu aliposema. Na Mungu aliongea Mstari wa 15
10. HII YA MWISHO NI YANGU HAIKO KWENYE NENO NI USHAURI WA KIROHO! USIWE NA HARAKA KUONDOKA! NA MUNGU ANAWEZA
ONGEA DAKIKA IYO AU BAADAYE. KAMA AKIONGEA AKIMALIZA KUONGEA CHUKUA DAFTARI YAKO UANDIKE YALE MUNGU
ALIYOYAONGEA. KAMA UNAJUA NINI CHA KUFANYA OMBA KAMA ROHO ANAVYOKUKUELEKEZA USISUBIRI UKASEMA HII
NITAOMBA KESHO NO! HAIENDI IVYO. LAZIMA UJIFUNZE TABIA ZA ROHO MTAKATIFU. KWANZA ROHO MTAKATIFU HANA HARAKA KAMA
WEWE YEYE NI MSTAARABU MNO LAZIMA UJIFUNZE KUMNGOJA KWA UNYENYEKEVU. ROHO MTAKATIFU AKIONGEA UNA ACT
HAPO HAPO USISUBIRI BAADAE MAANA BAADAE HUTAWEZA KUOMBA. ROHO MTAKATIFU ANAPOONGEA AU ANAPOTAKA
KUONGEA USIMKATISHE UKOTOKA UKAANZA KUFANYA SHUGHULI NYINGINE.
👆🏾 sasa nikuulize katika mtiririko huo wewe ulikuwa unakosea wap? Je Yehoshafati alifanya maombi ya vita?
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
Comments
Post a Comment