MAOMBI: KUVAA MAMLAKA KUBATILISHA MASHAURI YA UHARIBIFU

MAOMBI: KUVAA MAMLAKA KUBATILISHA MASHAURI YA UHARIBIFU
Isaya 8:10
. Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Nehemiah 4:15
. Kisha ikawa, adui zetu waliposikia ya kuwa tumekwisha kupata habari, na ya kuwa Mungu amelibatilisha shauri lao, ndipo sisi sote tukarudi ukutani, kila mtu kwa kazi yake.
Zaburi 33
10 . Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.
11 . Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
Waebrania 10:22
. na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.

Baba katika jina la Yesu Kristo Asante kwa upendo wako kwangu. Bwana Yesu nakushukuru kwa Neema yako. Neema
yako Bwana Yesu yanitosha, Roho Mtakatifu ninatambua uwepo wako, ninatambua kazi yako kuu katika kumtumkuza Yesu Kristo. Mungu Baba
Uishie milele nakushukuru kwa ufunuo huu nami nimeelewa na kugundua sasa nini maana ya kuvaa mamlaka yako, nami nimetambua siri kuu ya shetani ya
kutumia jina langu kama lango. Mfalme wa Falme sawasawa na waebrania 10:22 naja kwako kwa ajili ya utakaso kamili Mungu wetu ninakiri na kutubu mbele
zako njia zangu zote zisizofaa mbele zako Baba ninaomba unisamehe Leo hii naomba unirehemu na unisamehe kila uovu, makosa na dhambi mbele zako
Baba katika jina la Yesu, ninaachilia sasa Damu ya thamani ya Yesu Kristo na ninaomba unitakase na unioshe nikapate kuwa Safi mbele zako kwa damu ya Yesu!
Naomba Bwana Yesu Unipatanishe sasa Roho yangu na wewe, nafsi yangu na wewe, mwili wangu na wewe, fikra zangu na wewe kwa damu yako Bwana Yesu.
Baba naachilia damu ya Yesu juu ya kila maagano niliyoyafanya kwa kujua au kutokujua, nayafuta na kuyavunja kwa damu ya Yesu. Baba naachilia damu ya
Yesu juu ya kila laana juu yangu naivunja na kuifuta kwa damu ya Yesu. Baba naachilia damu ya Yesu juu ya kila mkataba nilioufanya kwa kujua ama
Kutokujua nauvunja kwa damu ya Yesu, Baba nachilia damu ya Yesu juu ya mitandao yote ya Giza iliyonishikilia ikiwemo kwa njia ya ndoto,maono,
mawazo, ukiri wa maneno, Yale yote niliyoyaona , Yale yote niliyoyasikia kwa damu ya Yesu, najidisconnect na mitandao hiyo kwa damu ya Yesu.
Mungu Baba katika jina la Yesu iko mitandao ya kuzimu iliotunasa kupitia simu, picha,video,television kupitia kula ndotoni au kunywa ndotoni. Ninaharibu
Mitandao iyo kwa damu ya Yesu. Mungu Baba ninaachilia damu ya YESU ya utakaso juu ya ardhi niliyoikanyaga ikafunga maagano na Mimi pasipo kujua, ninaya
Vunja maagano hayo na kuyafuta kwa damu ya Yesu, kila mitandao iliyonikamata kupitia ardhi, kupitia anga, kupitia bahari hadi chini ya bahari
mitandao iyo ninaiharibu kwa damu ya Yesu. Ninajidisconnect na kila mtandao wa ibilisi uliokamata malango yangu ya rohoni malango ya Roho, malango ya
nafsi, malango ya mwili, malango ya nyayo za miguu, malango ya viganja vya mikono, malango ya fikra, malango ya macho na masikio ninajidisconnet kwa
damu ya Yesu.  Bwana Yesu kitu chochote cha shetani ambacho kimeunganishwa na Mimi kwa siri. Maagano ya siri, mikataba ya siri, Damu zilizomwagiga zinazofuatilia
maisha yangu Mungu Baba ninaachilia damu ya Yesu ya kujidisconnect, Baba katika jina la Yesu ninaomba Rehema kwa kumfungulia adui mlango. Ninaomba
Rehema kutokuwa mwaminifu wa moyo mbele zako, ninaomba Rehema kwa kusababisha matatizo Mimi mwenyewe, ninaomba Rehema kwa kutokufuata njia
zako , ninaomba Rehema kwa kutokukuamini, ninaomba Rehema kwa kukupa wewe nafsi ya pili, ninaomba Rehema kulidharau neno lako, ninaomba
Rehema kwa kuyakataa maagizo yako, ninaomba Rehema kwa kutosikiza sauti yako, ninaomba Rehema juu ya laana yoyote niliyoifungulia katika maisha
yangu, ninaomba Rehema kwa ajili ya jina nililolirithi, ninaomba Rehema kwa ajili ya kazi yangu ya mikono, ninaomba rehema kwa kutokuamini neno lako na
kulifanyia kazi, ninaomba Rehema kwa biashara zangu, ninaomba Rehema kwa ajili ya familia yangu, ninaomba Rehema kwa ajili ya ukoo wangu, ninaomba
Rehema kwa kutosimama katika zamu yangu, ninaomba Rehema kwa kutokusamehe! Ninaomba Rehema kwa ajili ya kuweka vitu moyoni. Ninaomba
Rehema kwa ajili ya afya yangu, ninaomba  rehema kwa ya uchumi wangu, ninaomba Rehema kwa ajili ya asili yangu, ninaomba rehema kwa ajili ya ardhi ya asili yangu
Ninaachilia damu ya Yesu,  ninaomba Rehema kwa ajili watu waliofungua madhabahu za shetani kutoka Katika familia yangu, ukoo wangu. Baba
ninaomba uwarehemu uwatakase kwa damu ya mwanao Yesu. Ninaomba Rehema kwa ajili ya ardhi napofanyia biashara, ardhi napoabudu, ardhi ninapo
Fanya kazi, ardhi ninapoishi Baba ninaomba uirehemu na uitakase kwa damu ya Yesu. Baba katika jina la Yesu ninaachilia damu ya Yesu maeneo hayo
Yote niliyoyataja ninaomba uyarehemu na uyatakase,Baba ninaomba uwarehemu watu wa karibu yangu wanaonisema vibaya, naomba uwasamehe uwatakase
kwa damu ya YESU, BABA naomba urehemu matendo yote yanayotendeka na familia yangu, ukoo wangu, mtaa wangu, ama nyumba nayoishi, na wilaya nayoishi, na mkoa niliopo, na nchi hii ya
Tanzania, Bwana Yesu naachilia damu ya Yesu ninakuomba upite ukitakasa sasa na Damu yako ya dhamani. Baba katika jina la Yesu ninaomba uirehemu Tanzania
kama Tanzania juu ya laana zote tulizojiletea sababu ya kutokushika sheria zako na kutofuata maagizo yako. Ninaimwaga damu ya Yesu ya Rehema juu
ya Tanzania. Baba ninaomba uwarehemu viongozi wote wa Tanzania ambao umewapa dhamana juu nchi hii, ninaachilia damu ya Yesu ya Rehema juu
ya Yao, Baba ninaomba unirehemu Mimi juu ya mizaha niliyoifanya kwa kila kinachoendelea Tanzania na serikali yake. Unirehemu kwa kuilaani Tanzania,
unirehemu kwa kutosimama katika nafasi yangu kama MKRISTO aliyeokoka. Baba Naomba ulirehemu kanisa la Tanzania
kwa kutosimama katika nafasi yake Katika ulimwengu wa Roho. Ninaachilia damu ya Yesu sasa ya Rehema Baba naomba ulitakase kwa Damu ya Yesu.
Baba katika jina la Yesu jambo lolote litakalokufanya usinisaidie katika maombi yanayofuata pia naomba Rehema natubu naomba unisamehe, kama Kuna hukumu,
mashitaka yoyote au viambaza au vizuizi vya kuzuia maombi yanayofuata natubu mbele zako Baba nimegundua uovu wangu na Leo hii nakuja kwako kwa ajili
ya utakaso kamili naomba unirehemu na unisamehe. ROHO MTAKATIFU ninatambua uwepo wako mahali hapa nakuomba unisaidie kuomba! Maombi
Haya nayakabithi kwako naomba utende kile nachoomba, kwa utukufu wa jina la Yesu, maana ninatambua wewe ndio kiungo mkuu bila wewe hakuna
Linalofanyika, hakuna hata moja litakalo fanikiwa kama wewe Roho Mtakatifu hutahusika katika maombi haya. Bwana nakukaribisha katika maombi haya
ninatambua neema yako Bwana Yesu katika kunibeba. Ninatambua Bwana Yesu wewe ndio kuhani mkuu, na damu yako ndio inayotupa neema pia naitambua
damu yako Bwana Yesu, pia natambua ndio ufunguo pekee wa kufungua kila mlango, pia natambua sistahili kusaidiwa na wewe ila ni neema yako tuu na
huruma zako tuu. Ivyo Bwana Yesu nakutegemea kila kitu katika maombi haya. Naomba unisaidie wewe wanijua zaidi ninavyojijua. Mungu Baba wa milele
asante kwa upendo wako. Upendo wako ni wa ajabu ndo mana ukasema walipokuwa wakitaka kuomba ulisikia na walipokuwa wakiomba ulitenda. Mungu
Baba ninatambua upendo wako wa ajabu mno uliokufanya ushuke duniani kama binadamu ujidhalilishe wakati wewe ni Mungu na ukabali aibu yote hayo
sababu ya upendo wako kwetu. Mungu Baba ninatambua niko hai ni sababu ya upendo wako na ya kwamba unanipenda sana. Na hauko tayari kunipoteza hata
kwa kitu chochote. Mungu Baba katika jina la Yesu asante kwa kuwa ninajua unanipenda kama jinsi nilivyo. Nami nakupenda ninakuomba sasa umtukuze
mwanao Bwana wetu Yesu wakati ninakuomba katika jina la Yesu. Roho
Mtakatifu ninaomba umtukuze Bwana wetu Yesu wakati ninaomba maombi haya yanayofuata. Sasa Bwana Yesu ninavaa mamlaka yako Kamili kwa damu yako
Ninaachilia damu ya Yesu ya mamlaka katika kinywa changu, ulimwengu wangu wa Roho na kila mahali sasa kwa jina lako  Asante kwa kunisaidia.
SASA TUNAINGIA MAOMBI YA KUBATILISHA MASHAURI YA UHARIBIFU

Kwa mamlaka ya jina la Yesu Kristo ewe adui uliyekaa kwenye jina langu uliyefanya jina langu ndio lango. Ninaiachilia damu ya Yesu Kristo
ninalitakasa jina langu kwa damu ya Yesu ewe jina langu (litaje) ninakutakasa kwa damu ya Yesu ninakuunganisha na damu ya Yesu, ninakuunga na nafsi ya KRISTO
iliyohai ewe jina langu. Baba ninaimwaga damu ya Yesu juu ya ardhi yoyote iliyoshikilia Jina langu. Ninaamuru sasa ardhi ya asili yangu, ardhi ya asili ya Baba
yangu, ardhi ya asili ya Mama yangu. Ardhi nilipokulia, ardhi nilipozaliwa, ardhi nilipopanga, ardhi napopamiliki, ardhi yoyote uliyounganishwa na jina langu na
adui akapitia hapo ewe shetani, ewe mzimu wa Babu na Bibi, enyi Roho za Familia, Majini yote mlionikamata kupitia jina langu mashetani yote yaliyonikamata
kupitia jina langu, maagano yote ya kuzimu yaliyonikamata kupitia jina langu ninaimwaga damu ya Yesu najitenga nawe sasa kwa damu ya Yesu. Kwa damu ya
Yesu. Ewe laana uliyepitia kwenye jina langu. Ewe matatizo yote, mikosi yote balaa zote. Shida taabu mateso chochote nilichorithi au kunifuatilia sababu ya jina
langu, sababu ya jina la ukoo ewe shetani, ewe urgent wa kuzimu nakuaondoa nakutenga nami kwa damu ya Yesu kwa damu ya Yesu. Ewe Jini Mme, wewe jini
mke, wewe jini mauti, wewe chuma ulete, wewe madeni, wewe mikosi balaa, wewe ugonjwa uliopitia kupitia jina nakusambaratisha kwa Moto
nawayeyusha kwa Moto naachilia mvua ya Damu ya Yesu naachilia mvua ya Moto wa Roho Mtakatifu naachilia mvua ya acid ya Mungu nawateketeza nawaharibu.
Nyie wachawi mnaonifuatilia kupitia jina langu, nyie waganga wa kienyeji, nyie washirikina nyie wakuu wa Giza nyie wafalme wagiza, jeshi la pepo wabaya,
wakuu wa anga, malkia wa kuzimu, malkia wa baharini, malkia wa anga mnaofuatilia mambo yangu kupitia jina langu naachilia Moto nawasambaratisha nawateketeza,
naachilia damu ya Yesu ya vita, damu ya Yesu ya hukumu, ewe madhabahu za kushirikina, madhabahu za wachawi, madhabahu za waganga wa kienyeji,
madhabahu za majirani, madhabahu za wakwe, madhabahu za kazini, madhabahu za ukoo na familia madhabahu zozote zile tokea sehemu yoyote maneneo ya kazi au
biashara wewe unaofanya vita na Mimi na unatumia jina langu kutolea sadaka za Giza, jina langu mmeliunganisha na matambiko mmeliunganisha na kafara za
Giza, jina langu mmeliunga na manuizo nawachilia damu ya Yesu ya hukumu damu ya Yesu ya hukumu juu ya wote wanaotumia jina langu. Wanafanya jina
langu kuwa mlango damu ya Yesu ipite na Moto,iteketeze kila uchawi uliounganishwa na jina langu, kila vifungo, vitanzi, nira, mizigo, uchafu, magereza,
hukumu, mashitaka nateketeza kwa Moto wa Roho Mtakatifu, ninaunguza kabisa kazi zozote za shetani, na mawakala wake na ma urgent wake ninawashambulia
kupitia moto wa  Yesu, ninaamuru vita hivyo vinyamaze sasa vita vinavyotokana na damu za kuku mbuzi kondoo ngombe, au damu ya Mtu
nakunyamazisha kwa mamlaka ya jina la Yesu. Kila Pando lililopandwa kupitia jina futika kwa jina la Yesu. Ninaamuru nyota ya jina langu urudi Kwangu kwa damu ya
Yesu. Ninamuru mafanikio, kutawala kumiliki kurudi sasa kwa damu ya Yesu. Wewe jini mauti uliyepita na jina langu wewe pepo mauti wewe Roho ya mauti
wewe uchawi wa kaburini, jalalani, ewe mauti uliyeungamanishwa na jina langu muda wako umeexpire nakumininia damu ya Yesu ya vita. Damu ya Yesu ya hukumu
yenye Moto ndani yake nakuteketeza sasa . Nakusambaratisha katika jina la Yesu. Bwana Yesu kila Pando ambalo halikupandwa na Baba Mungu wa
Mbinguni mapando ya ugomvi katika ndoa, mapando ya mafarakano, umasikini , magonjwa, ufukara, mapando
ya madeni, mapando ya kukosa kazi, mapando ya kufukuzwa kazi, mapando ya kufilisika, mapando ya kuuwa biashara, mapando ya kufukuzwa kazi. Mapando ya
cancer, mapando ya Hiv, mapando ya magonjwa ya aina yoyote, mapando yote kupitia jina ambayo yanasababisha ninaishi kama ninavyoishi. Baba neno lako
linasema kupitia zaburi 33:10 kuwa wewe uyabatilisha mashauri ya mataifa na ya kwamba shauri lako ndilo litakalosimama.nami sasa kwa damu ya
Yesu nabatilisha kila mashauri ya washirikina waganga wa kienyeji wachawi mashauri ya kwamba nife nayabatilisha kwa damu ya Yesu. Mashauri ya ajali
nayabatilisha kwa damu ya Yesu, mashauri ya kwamba nipate hasara nifunge duka nayabatilisha kwa damu ya Yesu.mashauri kwamba nikose kazi
nayabatilisha kwa damu ya Yesu, mashauri ya kwamba nifukuzwe kazi nayabatilisha kwa damu ya Yesu. Mashauri kwamba nisichomoke, nisipige
hatua, nisijenge, nisinunue kiwanja, nisiwe na maendeleo, ndoa ipasuke, nipatwe na mikosi, balaa,
nichanganyikiwe, nipatwe na mabaya, nirudi nyuma, nisiione Baraka, nisifunguliwe, nayabatilisha kwa damu ya Yesu. Nayabatilisha kwa damu ya Yesu.
Maana neno limesema Isaya 8-10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Kwa neno Hilo sasa kila ambalo lilikuwa likinipinga nalibatilisha sasa kwa damu ya Yesu, kila visiki njiani, mikwamo njiani, mipaka ya kutokuvuka kila ambacho
kilikuwa kinanizuia nakibatilisha sasa kwa damu ya Yesu. Nabatilisha kila mkwamo wa Giza kwa damu ya Yesu. Mambo yasiyoenda yataenda sasa kwa damu ya
Yesu. Ninafungua vibali vyangu kwa damu ya Yesu. Ninaitanguliza damu ya Yesu initangulie kila mahali sasa katika jina la Yesu. Roho Mtakatifu naomba upite na
Maombi haya yangu machache, ninakukabithi kila eneo la maisha langu lenye mashauri mabaya ya shetani kwa damu ya Yesu ninakuomba ukabatilishe
ukimtukuza Kristo kufanya zaidi nilivyoomba na ninavyofikiri. Asante Roho Mtakatifu kwa kunisaidia kupata ushindi
Kamili. Katika jina la Yesu ninaomba na kushukuru Amen.

*Rudia Mara 3, endelea Kuomba nayo mpaka uone mzigo umekuisha wa kuomba


JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
  *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066/0765377506

Comments

  1. Najaribu kutafuta archive ya masomo ya nyuma ili nisome yale niliyoyakosa sioni. Unaweza kunisaidia nikapata masomo ya nyuma?

    ReplyDelete
  2. Maombi yamenigusa nimelia mno asante mtumishi naamini nimefunguliwa

    ReplyDelete
  3. Maombi yamenigusa nimelia mno asante mtumishi naamini nimefunguliwa

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA