MAOMBI YA KUWEKA HATUA ZAKO HURU KUPITIA NYAYO ZA MIGUU KUPITIA NAFSI KWENYE ARDHI
Zab 57
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nafsi yangu imeinama; Wamechimba shimo mbele yangu; Wametumbukia ndani yake.
Zaburi 56
6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.
Baba Mungu nakushukuru sababu ni wewe ndie utangazaye mwisho hata mwanzo. Naja mbele zako katika jina la Yesu. Asante kwa siri hii na
ufahamu kuhusu
miguu. Nami Bwana naja mbele zako kama jinsi nilivyo mfalme ninaomba rehema kwa ajili ya makosa yote, uovu wote, na dhambi nakuomba
Baba yangu
uliye mbinguni unitakase Kwa Damu ya mwanao Yesu. Kwa damu iyo sasa nipate uhali kuja patakatifu pako nikiwa ninahesabiwa haki kwa damu
ya Yesu. Ee
Mungu Baba Katika jina la Yesu ninaleta miguu yangu. Na malango ya miguu kupitia ardhi ya asili yangu. Asili Baba na asili ya mama ninaomba
rehema kwa ajili
ya asili yangu Ee Bwana. Ninaomba rehema kwa ajili ya tumbo la uzazi la mama yangu. Ninaomba rehema kwa ajili kiuno cha uzazi wa Baba yangu.
Ninaomba
unirehemu unisamehe. Makosa yoyote Dhambi Yoyote na uovu wowote uliopita kupitia vizazi vinne kwenda juu kwa adhabu iyo ikanipata hata Mimi Ee Mungu
Baba ninaomba rehema. Eee Mfalme yawezekana kabisa miguu yangu na nafsi yangu inaishi katika ufungwa wa gereza la ardhi ya asili yangu. Inaishi katika nyumba
ya utumwa. Baba mtakatifu na Mungu wa Israeli jambo lolote lililompa uhalali shetani yule ibilisi kukamata miguu yangu na kukamata nafsi yangu ninaomba
rehema Eee Bwana ninatubu katika jina la Yesu.Ninatangua na kubatilisha kama kuhani wa Bwana Yesu kila viapo vya uaminifu vya kipepo ambavyo shetani
anatumia kukamata miguu yangu kwa damu ya Yesu. Ninatangua na kubatilisha kila alama za uaminifu za kipepo ambazo zimempa uhalali shetani wa kukamata
nyayo za miguu yangu na nafsi katika jina la Yesu. Ninatangua na kubatilisha kila maneno yaliyonenewa juu ya ardhi yakampa shetani uhalali wa kukamata
nyayo zangu na nafsi kupitia ardhi Kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu ninaingia kwenye madhabahu ya Bwana Yesu. Ninachukua "stop order" warrant ya
damu ya Yesu ninaachilia Damu iyo juu ya ardhi yoyote niliyowahi kuikanyaga ikanikamata nyayo zangu na nafsi yangu. Iwe ni kwenye nyumba yoyote.
Iwe ni
sokoni. Iwe ni shambani. Iwe ni njia ya kupita kwa miguu. Iwe ni uchochoro, iwe ni kwenye kiwanja. Iwe kwenye nyumba nayoishi iwe ni sehemu nilienda nunua
vitu. Iwe ardhi ya shule ardhi ya hospital iwe ni ukumbi,iwe hotelini, iwe lodge,iwe guest house, iwe ni ardhi ya makaburini iwe ni ardhi ya pori au msitu ardhi yoyote
Mungu kupitia nafsi yangu naachilia damu ya Yesu ya kumuondolea shetani uhalali wa kukamata nyayo zangu Kwa jina la Yesu,naachilia
damu ya Yesu kupitia nafsi
yangu ishuke hadi kwenye nyayo zangu miguu yangu kwa damu iyo BWANA ishuke hadi kwenye ardhi yoyote iliyoshikilia maisha yangu,
yenye taarifa
zangu, kupitia maagano, kupitia mikataba, kutia uovu wa kupatiliza vizazi na vizazi naachilia damu ya Yesu Ishuke ee Mungu kwa jina la Yesu ikiwa pia nyayo zangu na
miguu alama yake ipo katika madhabu za wachawi, washirikina, waganga wa kienyeji ardhi
yoyote yenye data zangu na yenye uhalali wa kumsaidia pepo kufanya
anayotaka kuyafanya kupitia nafsi Bwana naachilia damu ya Yesu ishuke katika jina la Yesu. Damu ya Yesu ya kumuondolea shetani uhalali wa kufunga hatua zangu,
kumuondolea uhalali wa kumiliki na kuzitawala hatua zangu Katika jina la Yesu. Mashetani yote! Majini yote! Uchawi wa kukanyaga! Ushirikina! Nguvu
za giza! Tanzi! Kongwa! Mitego ya kipepo niliyoikanyaga kwa kujua au kutokujua Ee Bwana Mungu wa majeshi ninaondoa uhalali huo katika jina la Yesu. Ninaondoa
uhalali huo kwa damu ya Yesu. Katika jina la Yesu. Nakutangazia pepo toka kwenye ukoo wangu, pepo wa kunifuatilia hatua zangu, pepo wa ulinzi wa gereza la
ufungwa na nyumba ya utumwa ambao mmepewa assignment ya kufuatilia hatua zangu na kuzifunga hatua zangu na kuzikwamisha nabeba damu ya Yesu
iliyotoka miguuni ya stop order nasimamisha adui wote kabisa wanaohusika kuyafunga maisha yangu,
kuyaharibu maisha yangu, kuachilia mapooza, utasa, uharibifu, mauti katika hatua zangu Katika jina la Yesu. Sasa katika jina la Yesu Ee Mungu Mfalme
Kila pepo aliyefunga nafasi ya kazi kupitia miguu namteketeza kwa Moto wa damu ya Yesu katika jina la Yesu, naachilia Moto wa damu ya Yesu kwenye nafsi yangu kwa
Jina la Yesu Kristo ushuke kila mikwamo ya mitaji, mikwamo ya kuoa/kuolewa mikwamo ya Elimu, kila mikwamo ya kupata mikopo, kila mikwamo ya vibali
Nashusha Moto wa damu ya Yesu nateketeza kabisa kwa jina la Yesu. Kila mikwamo ya kupata haki yangu nashusha Moto wa damu ya Yesu nateketeza iyo
mikwamo katika jina la Yesu, kila mikwamo ya kufunguliwa,mikwapo ya kupata uponyaji, mikwamo ya maamuzi, mikwamo ya lango ya ibada, mikwamo ya
Huduma nashusha Moto wa damu ya Yesu, nateketeza kwa Moto wa damu ya Yesu katika jina la Yesu! Mikwamo ya Imani, mikwamo ya kuchukua hatua
nashusha Moto wa damu ya Yesu nateketeza katika jina la Yesu. Kila hofu iliyoachiliwa kupitia nyayo za miguu. Kila nguvu ya kutawala na kumiliki
niliyonyanganywa mashusha Moto wa damu ya Yesu nateketeza katika jina la Yesu. Kila kilichopandwa katika miguu yangu uzito wa hatua, magogo
waliyofunga ili kufanya miguu mizito nashusha Moto wa damu ya Yesu. Nyayo zangu walizozizika makaburini nashusha Moto wa damu ya Yesu katika jina la Yesu.
Nafsi yangu iliyokamatwa kupitia ardhi kupitia nyayo ikafunga uchumi wangu, ndoa yangu, elimu yangu, biashara yangu, kazi yangu, vibali vyangu nashusha Moto
wa damu ya Yesu. Hayo mapepo majini mizimu ya ukoo iliyopewa jukumu la kufuatilia hatua zangu Na kufunga hatua zangu nawateketeza na Moto wa damu ya
Yesu. Miguu yangu iliyopo Katika magereza miguu yangu iliyopo katika nyumba ya utumwa naikomboa kwa damu ya Yesu. Naitoa katika ufungwa kwa
damu ya Yesu. Naitoa katika utumwa kwa damu ya Yesu. Ee Bwana fikra zangu akili yangu na mawazo yangu yaliyofungwa kupitia nafsi kupitia nyayo za miguu
naachilia moto wa damu ya Yesu ishuke hadi kwenye ardhi yenye nyumba ya utumwa. Ishuke hadi kwenye gereza la ufungwa katika jina la Yesu. Ee Bwana
moyo wangu uliokamatwa kupitia nyayo za miguu kupitia ardhi naachilia Moto wa damu ya Yesu nawateketeza mapepo yote ya ulinzi wa utumwa huo. Na ufungwa
huo katika jina la Yesu. Ee Bwana naachilia damu ya Yesu ya miguuni kwenye nyayo za miguu yangu kufungua kila aina za vifungo katika jina la Yesu.
Baba naachilia damu ya Yesu ya miguuni kufungua hatua zangu zilizofungwa, kufungua vibali vyangu vilivyofungwa, kuondoa kila aina ya utumwa Na ufungwa
wa nafsi kupitia nyayo za miguu katika jina la Yesu. Naachilia damu ya Yesu ya miguuni juu ya miguu yangu nyayo zangu Na nafsi yangu kuondoa kila aina ya
mkwamo kwa jina la Yesu, Baba naachilia damu ya Yesu ya miguuni kuondoa kila mipaka niliyowekewa mipaka ya hatua mipaka ya kuamuwa mipaka ya mawazo
mipaka ya maono mipaka ya fikra/akili/mawazo katika jina la Yesu juu ya nafsi yangu na nyayo zangu za miguu.
Baba ninaunganisha nyayo zangu za miguu na damu ya Yesu ya miguuni natangaza ya kwamba kila
nitakapokanyaga nitapamiliki na kupatawala kwa jina la Yesu. Ninatangaza kwamba nyayo zangu hizi
zilizobeba damu ya Yesu ya miguuni kila nitakapoenda au kukanyaga giza litanikimbia kwa mamlaka ya jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu ya miguuni juu ya
nyayo zangu hakuna uchawi wala pepo alitegwa barabarani atakayefanikiwa kuniingia au kunifunga kwa jina la Yesu. Natangaza kufunguliwa Kwa mambo yote
yaliyokuwa Yamefungwa kupitia damu ya Yesu ya miguuni kwenye nyayo zangu Katika jina la Yesu. Ninaharibu kila aina ya utumwa na ufungwa wa aina yoyote juu
ya miguu yangu kupitia nafsi yangu kupitia ardhi yoyote Katika jina la Yesu. Asante Roho Mtakatifu kwa kuwa
unaenda kufanya zaidi niombavyo na zaidi nifikiriavyo.katika jina la Yesu ninaomba. Amen
*Yarudie maombi haya Mara 2, omba ukiamka, omba ukienda kulala! Omba mpaka upate mpenyo.
JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
Comments
Post a Comment