MAOMBI YA KUTEKETEZA MAVAZI YA ASILI YAKO ILI UWEZE KUPIGA HATUA
*Somo: Teketeza mavazi ya asili yako ili uweze kupiga hatua.(Kumiliki/kutawala)*
Bwana Yesu asifiwe!
Hakimu hawezi kuhukumu mpaka avae vazi na kofia ya hakimu akae kwenye kiti cha Hakimu kisha anatoa hukumu. trafiki barabarani hawezi simamisha gari
Likasimama isipokuwa kavaa nguo za trafiki za kumtambulisha na Dereva akimwona anamtambua huyu Ni trafiki ivyo akimsimamisha atatii. Kama jinsi ilivyo Katika mwili ipo ivyo ivyo katika
Roho. Haroon alipovuliwa vazi la Kuhani ndio ilikuwa mwisho wake alikufa wengine waliobaki waliendelea na kazi iyo.katika ulimwengu wa Roho kila cheo
Kina vazi lake. Yesu atakapo kaa kwenye kiti cha Rehema ni tofauti na atakapokaa kwenye kiti cha hukumu. Kila cheo katika ulimwengu wa Roho kina vazi(utambulisho) Lipo vazi la
Mwanajeshi pia hutambulishwa kwa njia ya vazi na vazi Hilo linakuwa na cheo Bwana Yesu asifiwe! Katika ulimwengu yapo mavazi yanayokutambulisha na yapo
kukuruusu kuingia sehemu flani. Tukiwa kanisani utakuta wahudumu wamevaa vazi maalumu manake ilo vazi linawatambulisha. Kwa iyo sababu ya vazi
lake tayari kila mtu anajua wajibu wake. Ukienda hotel wale wahudumu huwa wana vazi maalumu. Linawatambulisha. Na vazi Hilo linamfanya atumwe Na
mteja! Au amuhudumie mteja bila kuulizwa maswali. Kanisani vazi la mhudumu linamfanya aweze kukusanya sadaka na watu wasiwe na wasiwasi
maana wanajua kazi ya lile vazi. KWA IYO VAZI LINAWAKILISHA KAZI. VAZI LA HAKIMU LINAWAKILISHA HUKUMU. VAZI LA DR. LINAWAKILISHA HUDUMA YA
AFYA, VAZI YA WAKILI LINAWAKILISHA UTETEZI, VAZI LA MWANAFUNZI LINAWAKILISHA KUJIFUNZA, VAZI LA SPIKA WA TANZANIA LINAWAKILISHA
UONGOZI WA KITI BUNGENI, VAZI LA JESHI LINAWAKILISHA ULINZI NA MPIGANAJI WA VITA. LIPO VAZI LA NESI LINAWAKILISHA HUDUMA YA AFYA, kama
jinsi ilivyo Katika ulimwengu wa Mwili ndivyo ilivyo Katika ulimwengu wa Roho. Vazi Ni symbol ya kazi. Au ni Alama ya kazi. Watu wanaokuona watakutreat
kutokana vazi lako. Watakupa heshima kutokana Na vazi lako linawakilisha kitu gani kwako. Bwana Yesu asifiwe! Sasa tuangalie katika ulimwengu wa Roho ikoje!
Waefeso 4:
22 . mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
25. Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
Hapo juu amezungumzia vazi la utu wa kale! Utu wa zamani! Vazi la tamaa! Vazi la kudanganya! Vazi uongo hayo ni baadhi ya mavazi ya ulimwengu wa Roho Mtume Paulo anasema.
Waefeso 6
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Hapo juu anazungumzia vazi la mwanajeshi wa Kiroho! Anayepigana vita. Mavazi ya Mtu aliyeokoka. Ukiangalia kwa makini hapo mavazi ya mtu aliyookoka
Waefeso 6:12 ndiyo mavazi hayo hayo unaenda kupigana na waefeso 4:22,25 mavazi ya uongo! Utu wa kale! Mavazi ya tamaa! Kwa iyo hii inanipa picha ya vitu
viwili yapo mavazi ya Mungu na yapo mavazi ya shetani. Inategemea kazi unayoenda kufanya. Bwana Yesu asifiwe! Mungu atakuvalisha mavazi ya Ki Mungu
haki, utu wema, imani, upendo, kusamehe, utakatifu, hofu ya Mungu.(uzima wa milele) Shetani naye naye mavazi yake Ni yaleyale
yanayotumiza kazi yake Yohana 10:10, kuiba kuharibu na kuchinja. Bwana Yesu asifiwe! Shetani anawatenda kazi wake. Falme za Giza, Jeshi la pepo wabaya,
Wakuu wa Giza, Wafalme wa anga. Izo level nne za kipepo zinakuwa aidha kwenye kila kabila lugha au taifa. Kwa iyo kwenye ukoo wako! Au watu wa aina flani
au eneo fulani. Hawa ndio wamepewa viti Na shetani kupambana na watoto wa Mungu. Bwana Yesu asifiwe! Tuangalie jinsi haya mavazi ya shetani yanavyofanya
vita na watoto wa Mungu.
Zakaria 3
1 Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?
3 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.
4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.
5 Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa Bwana akasimama karibu.
6 Kisha malaika wa Bwana akamshuhudia Yoshua, akisema,
7 Bwana wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.
Angalia kwa makini ilo neno shetani alikuwa anshindana na Mtumishi wa Mungu Joshua! Manake alikuwa anampelekea Mungu mashitaka. Ndo
mana anamwambia mstari wa 2! Hiki si kinga kilichotoka motoni? Motoni manake kuzimu kinga manake mashitaka toka kwa shetani kumshitaki mtoto wa Mungu.
_Lakini Tuangalie kitu kimoja shetani alipata wap ujasiri wa kumshitaki Joshua? Biblia inasema Mstari wa 3! Joshua alikuwa amevaa mavazi machafu! Mavazi_
_machafu yani si msafi yani dhambi. Shetani alikuwa anamwinda Joshua ili amshitaki kwa Mungu. Mungu akaingilia juu anasema muondoleeni nguo chafu_
_manake nini muondolee dhambi zake hukumu zake ni Mimi Mungu nimesema. Kisha mumpige kilema kizuri, wakamvika na mavazi Safi sasa. Angalia mwenyewe_
_mstari wa 5. Bwana Yesu asifiwe. Kama shetani alimpeleka Joshua mbele ya Mungu kumshitaki hata wewe anaweza tumia mavazi ya asili yako kukushitaki._
_Sababu bado hujayavua. Umeokoka ndio. Lakini bado yapo mavazi ya kwenu yanakufuatilia Na huwezi jua ni mpaka uombe. Huwa tunashinda kwa kuomba_
_kwa maarifa. Shetani unapooanza kupiga hatua anatumia vazi ulilivalishwa aidha na wachawi washirikina au vazi la ukoo. Kuna watu wamevalishwa mavazi ya ugonjwa._
_Wakiombea wanasikia nafuu mambo baadaye yanarudi tena. Wengine vazi la ufukara na umasikini. Vazi la huzuni, vazi la kutokuwa na amani na furaha, vazi la_
_madeni, vazi la mikosi. Mavazi mengine yametokana na familia zenye mizimu, mavazi ya kutokuolewa, mavazi ya kutokuzaa, mavazi ya kufiwa na waume_
_au wake, mavazi ya kichawi wengine wanatumika kichawi hata Wao hawajui. Vazi la kufanikiwa kwa kiasi flani, vazi la uharibifu, vazi la mauti, vazi la utengenifu,_
_vazi la upweke, vazi la ukichaa, vazi la kuchanganyikiwa, vazi la ajali vazi la kujiuwa! Wewe huna lakini bado umeunganishwa na asili ya Baba yako na_
_Asili ya Mama yako kupitia ardhi. Roho za Familia na ukoo zinakufuatilia kupitia ilo vazi maana ni utambulisho kwao. Bwana Yesu asifiwe ni mpaka umevua ilo vazi _
_ndipo utakuwa huru. Ndipo utaanza kuona unapiga hatua. Bwana Yesu asifiwe! Mungu amesema tuombee jambo Hili ivyo_
_baadaye nitaleta maombi hayo na kama Kuna vazi lolote baada ya Maombi haya basi litateketea kabisa. Na Mungu atakuweka huru._
*JINA LA BWANA LIBARIKIWE*
MAOMBI:
*"Kuteketeza mavazi ya shetani"*
Waefeso 6
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Zakaria 3
3 Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.
4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.
5 Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa Bwana akasimama karibu.
Baba katika jina la Yesu Asante kwa maarifa ya Rohoni katika jina la Yesu nasogea mbele zako Mfalme nakuja kama jinsi nilivyo ninaomba rehema ninaomba
msamaha ninaomba unirehemu Baba Mungu wa Mbinguni katika jina la Yesu. Ninatubu kwa ajili ya makosa yangu uovu wangu dhambi zangu zote mbele zako
ninaomba rehema nisamehe Bwana katika jina la Yesu. Kuna mahali nilipanda mbegu mbaya katika maisha yangu sasa ninavuna nilichokipanda nisamehe
unitakase katika jina la Yesu. Ninaomba damu yako Bwana Yesu ikanene mema Kwa habari ya kuvuna huko nilikokupanda katika jina la Yesu. Damu yako Bwana
Yesu isimamishe kuvuna nilichokipanda katika jina la Yesu. Baba Kwa kile nilichokipanda ninastahili kupata yanayonipata sasa ninageukia kwako
Baba Nina tubu. Naomba damu yako Bwana Yesu inene rehema juu yangu na juu ya maisha yangu. Baba katika jina la Yesu ninaomba rehema kwa ajili ya asili
Yangu ardhi ya chimbuko langu, ninamwaga damu ya Yesu katika ardhi ya asili ya Baba yangu Na ardhi ya asili ya Mama yangu. Ninatubu uovu wowote
Uliofanyika juu ya ardhi za asili yangu ninaomba unisamehe katika jina la Yesu.ninaomba rehema kwa ajili ya maagano mikataba na laana ya aina
Yoyote iliyonipata kwa kumuabudu shetani kupitia ardhi ya asili yangu! Kupitia asili yangu, kupitia madhabahu zilizojengwa na sisi wenyewe Leo hii
Natubu najitoa katika maagano hayo Kwa damu ya Yesu. Najitoa katika mikataba iyo kwa Damu ya Yesu, najitoa katika laana hizo za ukoo Na familia kwa damu ya Yesu
Kila mitandao ya Giza tokea kwenye kizazi changu upande wa mama na upande wa Baba, mitandao ya mizimu, mitandao ya roho za familia najitoa katika mitandao
Iyo kwa Damu ya Yesu, natangaza tokea Leo hii Mimi si wa mizimu kwa damu ya Yesu. Mimi niko upande wa Yesu, nimenunuliwa kwa damu ya dhamani
Kama isemavyo ufunuo 5:9 katika jina la Yesu. Asili yangu ni ya Yesu. Kila muunganiko wowote Na madhabahu ya asili yangu vunjika kwa damu ya Yesu.
Kila muunganiko wowote Na Roho za Famili vunjika kwa Moto wa damu ya Yesu. Chochote kilichoniunganisha Mimi na asili yangu upande wa Giza aidha kwa
Kutumia nywele zangu, kitovu changu, meno yangu ya kwanza, kucha zangu au vitu vyovyote vilivyopo katika madhabahu za Giza vikatolewa sadaka najitenga kwa
Damu ya Yesu, matambiko, mikataba ya Damu za Giza, manuizo kila ambacho kimeniunganisha Na madhabahu za asili yangu wakuu wa Giza na falme za Giza za
Ukoo nateketeza kwa Moto wa damu ya Yesu. Kila manuizo yaliyoniunga na mtandao wa Giza wa kiukoo Na familia kupitia jina langu au tarehe ya kuzaliwa
Mwaka wa kuzaliwa, mwezi wa kuzaliwa naachilia damu ya Yesu juu ya jina langu nalitakasa kwa damu ya Yesu, naachilia damu ya Yesu juu ya tarehe mwezi na
Mwaka wa kuzaliwa natakasa kwa damu ya Yesu. Ninaamuru Muunganiko kuvunjika sasa kwa jina la Yesu. Nakubomoa sasa! Nakavunja sasa kwa
Jina na damu ya Yesu Kristo, Baba najitoa kwenye ukoo wa mizimu kwa damu ya Yesu, najitoa kwenye roho za Familia kwa Damu ya Yesu. Muunganiko wowote
Wa Giza tokea kwenye asili yangu Katika malango yangu naachilia damu ya Yesu, pepo wote wanaotoka kwenye Falme za Giza, wakuu wa Giza, za kiukoo na Familia
Nawateketekeza kwa Moto katika jina la Yesu ninaamuru Moto wa damu ya Yesu uwaangamize kabisa. Wageni wote kwenye malango yangu naachilia damu
Ya Yesu katika malango yangu Katika jina la Yesu. Baba katika jina la Yesu vazi la umasikini tokea kwenye asili yangu nalivua kwa damu ya Yesu naliteketeza
kwa Moto katika jina la Yesu. Vazi la kutumika kichawi, vazi la ufukara, vazi la magonjwa, vazi la mikosi, vazi la balaa, vazi la aibu, vazi la misukosuko kutokea
asili ya Baba yangu au Mama yangu nalivua kwa damu ya Yesu naliteketeza kwa Moto katika jina la Yesu, vazi kukataliwa, vazi la kutokupata watoto,
vazi la Babu, vazi la bibi, vazi la shangazi, vazi la watu waliokufa, vazi la mauti nalivua kwa damu ya Yesu naliteketeza kwa Moto katika jina la Yesu. Vazi la
kutokuolewa, vazi la kutokuoa, vazi la utumwa, vazi la kutokufanikiwa, vazi la kurudi nyuma, vazi la kucheleweshwa nalivua kwa damu ya Yesu naliteketeza
kwa Moto wa damu ya Yesu, vazi la jini mme, vazi la jini mke, vazi la kukosa kazi, vazi la madeni, vazi la kufilisika, mavazi yote ya kurithi, vazi la kutokuendelea
Nalivua kwa damu ya Yesu, naliteketeza Moto wa damu ya Yesu katika jina la Yesu, vazi la kukwama, vazi la kutokuendelea, vazi la kutokujenga au kumalizia nyumba,
Vazi la kutokununua kiwanja, vazi la kutokumiliki Mali, vazi la kupoteza, vazi la ulevi, vazi la umalaya, vazi la laana, vazi la kutokusoma, vazi la uwizi, vazi la
kuchanganyikiwa, vazi la ukichaa, vazi la kukata tamaa,Baba ninavua mavazi hayo Kwa damu ya Yesu! Kwa damu ya Yesu! Katika jina la Yesu nayachoma Moto
Wa Roho Mtakatifu yawe majivu kabisa katika jina la Yesu, vazi la kutokuheshimika, vazi la kudharaulika, vazi la kutokutambulika, vazi la
kutokuonekana, vazi la kutokuaminika, katika kila aina ya mavazi ya washirikina waganga, wa kienyeji, wachawi, falme za Giza au wakuu wa Giza kutokea kwa asili
Yangu, mavazi ya utambulisho katika Giza nayavua kwa damu ya Yesu. Nayateketeza na moto wa Roho Mtakatifu katika jina la Yesu, mavazi ya siri yote niliyoyavaa kwa
siri kwa kujua au kwa kutokujua kutokea kwenye asili yangu naachilia damu ya Yesu! Naachilia damu ya Yesu ninayavua ninayachoma Moto wa Roho Mtakatifu
Wenye mavazi hayo ninawafuata kwa damu ya Yesu, ninaachilia mishale ya Moto ninawaangamiza, ninaachilia upanga ukawafyeke katika jina la Yesu
Naachilia shoka, naachilia rungu la JEHOVA, naachilia nyundo nawapasuapasua kwa jina la Yesu, naachilia mvua ya Damu ya Yesu popote
walipo kwenye ardhi juu ya bahari chini ya bahari, kwenya anga, katika mbingu moto wa damu ya Yesu uwaangamize! Moto wa damu ya Yesu uwateketeze,
ninawahukumu kwa damu ya Yesu. Kuanzia viti vyao hata vifaa vyao vya kichawi teketea kwa Moto katika jina la Yesu. Vazi lolote lile nililolivaa
nakumwagia damu ya Yesu! Damu ya Yesu. Naamuru Moto wa kuteketeza uunguze kabisa vazi ilo liwe majivu liteketee kwa Moto wa damu ya Yesu.
Roho Mtakatifu maombi haya sasa nayarudisha kwako juu yangu naachilia Moto wako na naachilia damu ya Yesu naomba upite kwa damu ya Yesu kila vazi
uliharibu kwa Moto wako katika jina la Yesu. Asante Bwana Yesu maana imekuwa na Asante kwa kuwa Roho wako Mtakatifu ataenda fanya zaidi niombavyo na nifikiriavyo Amen.
*Rudia Mara 3 maombi haya Kwa siku fanya Kwa mda wa siku 7*
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
Comments
Post a Comment