NAFSI ISIPO PATA UPONYAJI HUWEZA KUUWA MAFANIKIO YA KIROHO NA KIMWILI
Bwana Yesu asifiwe!
Nafsi ikikamatwa mtu hata hawezi omba tena.Nafsi ikishashikwa na kuvurugwa unaweza hisi kuchanganyikiwa.Kuna watu wengi wanahitaji uponyaji wa moyo nafsi zao zina makovu. Na majeraha.Binadamu hawezi ponya nafsi ya mtu. Seminar haziwezi ponya nafsi ya mtu. Mungu ndo anayeweza ponya kwa neno lake. Kuna tofauti ya kupooza na kuponya. Lipo neno la uponyaji kabisa kuhusu nafsi. Nirahisi kuwashangaa wana wa Israeli au kuwahukumu wana wa Israeli kuwa
waalikuwa wabishi, walikuwa wenye kiburi, hawakumuamini Mungu. Ukichunguza yaliyokuwa yanaendelea utajua kuwa wewe umepata Neema kipindi cha agano jipya. Ni raisi kuwalaumu kuwa hawakufika kaanani ukawaona Wao wamekosea Sana lakini kumbe nawe unapitia hayohayo.Nafsi ya mtu iki vurugwa inaweza vuruga imani, inaweza vuruga kupokea. Nafsi inaweza vuruga kila kitu kwenye maisha yako. Dalili ya mtu aliyevurugwa nafsi. Au utajuaje mtu kavurugwa nafsi
☑ana hasira mda wote
☑anataka malipizi mda wote
☑ni mtu wa kisasi mda wote
☑hawezi kusamehe kirahisi
☑hulaumu kila kitu na kila mtu
☑ni mbishi hata mambo yaliyo ya kweli
☑hukosoa neno la Mungu, hukosoa watumishi wa Mungu, huwadharau watumishi wa Mungu
☑huwadharau watu wengine
☑Hajali watu wengine
☑Hakuna huruma ndani yake
☑ Hawezi kukubali wala kutambua kazi ya mwingine. Wala kuidhamini
☑hubeba chuki juu ya kila mtu na kila kitu
☑anaweza kumkasirikia hata Mungu
☑kutokujali katika lolote. Maneno yake potelea mbali....
☑saa ingine watu au mtu akishindwa yeye hufuraia
☑roho ya wivu mpaka inageuka chuki
☑Hana Amani na watu wote, hujitenga na kutaka kukaa mwenyewe
☑ni mtu asiyeshaurika. Hataki ushauri wa mtu. Ana misimamo yake anayoisimamia hata Kama ni negative.
☑Humwambii kitu wala humsogelei. Yani Hana ule urafiki
hallelujah
Tuangalie jinsi nafsi ilivyovurugwa kwa wana wa Israeli hata ikawafanya kuyakataa maelekezo ya Mungu. Na kutaka hata kumuua Musa na Joshua.Na kutokuisikia sauti ya Mungu
Hesabu 14:1
. Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.
Hesabu 14:2
. Kisha wana wa Israeli wote wakamnung'unikia Musa na Haruni; mkutano wote wakawaambia, Ingekuwa heri kama tungalikufa katika nchi ya Misri, au, ingekuwa heri kama tungalikufa katika jangwa hili.
Hesabu 14:3
. Mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka; je! Si afadhali turudi Misri?
Hesabu 14:6
. Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;
Hesabu 14:7
. wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu.
Hesabu 14:9
. Lakini msimwasi Bwana, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye Bwana yu pamoja nasi; msiwaogope.
Hesabu 14:10
. Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa Bwana ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.
Hesabu 14:11
. Bwana akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hata lini? Wasiniamini hata lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.
Wana wa Israeli walimnungunikia Mungu, walimuonea Mungu hasira. Kila Mara Mungu alipotoka kujifunua kwa upya kutumia njia mpya wana wa Israeli waliona giza mbele Yao. Walichokuwa wanataka ni kufika kaanani! Hizi habari zingine hawakutaka kusikia. Ni sawa Na wewe unachotaka kusikia ni umepata Mme, umepeta mke, umepata nyumba, umepata gari, huduma yako imekuwa kubwa, huhitaji njia za Bwana. Kumbe safari ya kiroho ni hatua. Na kila hatua Ina njia yake.
Ulivyovuka January sivyo utavuka April. Kila Mara unahitaji maelekezo toka kwa Mungu. Wana wa Israel wakakasirika kuona uyu Mungu anatuzungusha kitu gani? Na tumeshatembea Sana jangwani? Wakamkasirikia Mungu. Wakamkasirikia Musa. Wakamkasiria Joshua. Hata kalebu wakataka wampige hata mawe wafe. Lakini ukichunguza iyo hasira ilitoka wap? Kutokumsikia Mungu kulitoka wap? Kumdharau Mungu kulitoka wap? Hallelujah
Kutoka 5:22
. Musa akarudi kwa Bwana, akasema, Bwana, mbona umewatenda mabaya watu hawa? Kwani kunituma mimi?
Kutoka 5:23
. Kwa maana tangu nilipokwenda kwa Farao, kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa; wala hukuwaokoa watu wako hata kidogo.
Kutoka 6:1
. Bwana akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.
Kutoka 6:2
. Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
Kutoka 6:3
. nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Kutoka 6:4
. Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya kukaa kwao hali ya ugeni.
Kutoka 6:5
. Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu.
Kutoka 6:6
. Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
Kutoka 6:7
. nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.
Kutoka 6:8
. Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.
Kutoka 6:9
. Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
Biblia inasema.....
hawakumsikiza Musa kwa sababu ya uchungu wa moyo na utumwa mgumu
Yani historia iliwafunga wana wa Israeli. Kule walikotoka walihitaji uponyaji kwanza wa mioyo Yao ndipo waendelee mbele.Kumbuka waliteswa. Walikuwa watumwa. Walitumikishwa. Ni sawa na wewe history yako kuhusu maisha yako imekuachia vidonda. Imekuachia makovu moyoni. Iyo hali ndo inayoleta nafsi kuvurugwa na adui. Shetani anapitia kwenye vidonda vya moyoni. Kwenye makovu ya moyoni. Kukuvuruga na kuifunga nafsi yako. Nafsi ikishafungwa ni vigumu kumtii Mungu. Sababu ya kupokea maelekezo mapya ya Mungu unafikiria malalamiko.Wana wa Israeli walikwamishwa na nafsi.Nafsi ilikuwa na makovu ya utumwa mgumu, na moyo wenye uchungu Wewe pia nafsi yako isipopata uponyaji inaweza kukukwanisha.Hallelujah!nachokufundisha hapa ukifuatilia na kuyafuata maelekezo yote na kuomba hapana shaka nafsi yako itawekwa huru Kwa jina la Yesu.
Utafiti unaonyesha magonjwa Mengi siku hizi yanatokana na uchungu moyoni.
⚪vidonda vya tumbo
⚪cancer
⚪pressure
⚪mifupa
Yanatokana na sumu zilizojirundika kwa mda mrefu. Ina maana mtu akiponyeka nafsi na hayo magonjwa yanaondoka na kumwachia.Katika jina la Yesu
Zaburi 103:1
. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu.
Zaburi 103:2
. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
Zaburi 103:3
. Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
Zaburi 103:4
. Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,
Haya maombi yalikuwa maalumu kwa ajili ya nafsi. Utagundua! Kuwa nafsi yake mwandishi ilikuwa haimuhimidi Bwana Kuhimidi ni zaidi ya kutii. Kunyenyekea. Kusujudia. Sasa mwandishi aligundua kuwa nafsi yake ilifika sehemu ikaacha kumuhimidi Bwana. Ilikuwa inahimidi vitu vingine. Inawezekana na wewe nafsi yako imeacha kumuhimidi Bwana
☑unahimidi pesa
☑unahimidi ndoa
☑unahimidi biashara
☑unahimidi uchumba
☑unahimidi kazi
☑unahimidi gari
☑unahimidi nyumba
☑unahimidi biashara
☑unahimidi cheo
☑unahimidi mafanikio uliyo nayo
☑unamhimidi Mme, unamhimidi mke
☑yani nafsi yako imeacha kumuhimidi Bwana.
Ndo mana akamalizia "na vitu vyote vilivyo ndani yangu vihimidi jina lake takatifu". Hallelujah!
Kwa iyo utagundua sababu ya kuhimidi vitu vingine umefungua milango kwa adui. Milango kwa adui ya kupanda vitu vingine ndani ya nafsi yako. Na adui kapanda
☑tamaa inayowaka ndani yako
☑kapanda kukata tamaa
☑kapanda hasira
☑kapanda kuchoka ndani yako
☑kapanda negatives za kila aina ndani yako. Hallelujah
Mwandishi anaendelea kuzungumza na nafsi anasema wala usizisahau fadhili zake zote .Manake nafsi yako imefika sehemu
⚪imesahau wema wa Bwana.
⚪Imesahau Bwana alipokutoa
⚪nafsi imesahau fadhili za Bwana
⚪nafsi imesahau jinsi Bwana alivyowahi kukupigania
⚪nafsi imesahau Bwana alivyokushindia
⚪nafsi imesahau Bwana alivyokuepusha na aibu
⚪nafsi imesahau alivyokufanyia mpenyo ukajikuta Una hiko cheo
⚪Mara hii nafsi imesahau matendo makuu ya Bwana aliyokutendea
✅ndo mana
☑nafsi inalalamika
☑nafsi inanungunika
☑nafsi inasikitika
☑nafsi inahuzunika
☑nafsi Ina majuto
☑nafsi inahasira
☑nafsi imekwazika
☑nafsi imechukia
✅MARA HII TUU KIPINDI KIFUPI TUU NAFSI TAYARI IMESAHAU FADHILI ZA BWANA, WEMA WA BWANA. hallelujah!
Mwandishi anaendelea "akusamehe maovu yako yote". Akuponya na magonjwa yako yote.Yani pamoja na hayo yote.Yani "Mimi Mungu nimeisamehe nafsi yako". Na nitaiponya nafsi yako.. Nafsi yako imepata ugonjwa wa
☑ hasira
☑kukata tamaa
☑chuki
☑malipizi
☑visasi
☑dharau
☑kujihesabia haki
☑kutokuwa na huruma
☑kutokujali wengine
☑kutokudhamini wengine
☑kutokushaurika
☑kuwa Na misimamo negatives
NAFSI YAKO INAHITAJI UPONYAJI. NA MUNGU ANASEMA USIHOFU! NIMESAMEHE YOOTE! HAYO HAPO JUU. NA NITAIPONYA NAFSI YAKO NA HAYO YOOTE HAPO JUU. HATA AMBAYO SIJAYAANDIKA. HALLELUJAH
Nafsi yako inamakovu. Nafsi yako inavidonda. Vya
☑ kusalitiwa
☑kuonewa
☑kuumizwa
☑kudharauliwa
☑kunyimwa haki
☑kushushwa
☑imejeruhika nafsi yako
MUNGU ANASEMA HATA IYO MILANGO ILIYOSABABISHA HAYO NIMESAMEHE. NA NITAIPONYA NAFSI YAKO. USIYAWEKE TENA MOYONI. USIYABEBE TENA SABABU MIMI NIKO TAYARI KUSAMEHE HAO WALIOSABABISHA. NA KUKUSAMEHE WEWE. NA KUKUPONYA WEWE. NA KUPONYA MAGONJWA YAKO. hallelujah!
ndo mana biblia inasema....

ugonjwa wa kiroho katika nafsi waweza kukusababishia kifo. Cha kiroho. Kifo cha kimwili. Kifo cha kiroho ni sababu huwezi piga hatua nafsi haiwezi kukuruusu. Huwezi msikiza tena Mungu na kuyafuata maagizo yake huku Una uchungu moyoni. Kifo cha mwili anazungumzia magonjwa ya mwili. Kuwa unangangania kunywa madawa ya pressure. Unakunywa madawa ya vidonda vya tumbo kila siku. Unapigwa mionzi kwa ajili ya cancer kumbe magonjwa hayo yangepata uponyaji wa kiroho ungeshapona kimwili na kiroho. Hallelujah!. Bwana Yesu asifiwe!
Magonjwa Mengi yakudumu husababishwa na uchungu moyoni. Uchungu katika nafsi. Hallelujah
Mungu Leo anasema usihofu nitakuponya nayo yote.
Ukifika hapa baada ya kuelewa vizuri
MAOMBI:
Sema katika jina la Yesu, Baba nakushukuru kwa uaminifu wako. Sifa utukufu na heshima nakurudishia wewe Bwana Yesu. Baba ni kweli nafsi yangu iliacha kukuhimidi wewe. Imehimidi biashara, imehimidi kazi, imehimidi ndoa, imehimidi pesa, imehimidi gari, nyumba, viwanja, mashamba, imehimidi uchumba, nafsi yangu imehimidi mafanikio imeacha kukuhimidi wewe, nafsi yangu imesahau fadhili za Bwana imesahau wema wa Bwana, imesahau huruma za Bwana,
imesahau kuvushwa na Bwana, imesahau wema wa Bwana Mara hii tuu. Leo ninatubu na kuomba Rehema. Bwana Yesu Asante kwa kunisamehe maovu yangu yote, maovu niliyoyafanya Mimi. Maovu yaliyofanywa na baba zangu, na waliotangulia hata kusababisha nafsi yangu kujehurika, hata kusababisha makovu, hata kusababisha vidonda katika nafsi Asante Bwana Yesu kwa kuisamehe
nafsi yangu Leo inawekwa huru kwa damu ya Yesu. Ninaachilia damu Ya Yesu juu ya nafsi yangu, kuta za nafsi yangu, misingi ya nafsi yangu itakaswe kwa damu ya Yesu. Bwana Yesu nakushukuru kwa kuiponya nafsi yangu. Asante kwa kuponya magonjwa yote yaliyo ndani ya nafsi yangu. Yapo magonjwa ya lawama, majuto, malalamiko, masikitiko, hasira, kiburi, kujihesabia haki,
manunguniko, Asante pia kwa kuniponya magonjwa yote yasababishwayo na uchungu wa moyo. Magonjwa ya pressure, magonjwa ya vidonda vya tumbo, kuchanganyikiwa, usaulifu, cancer na yote hayo. Ninaachilia damu ya Yesu juu ya magonjwa hayo sasa ninaamuru uponyaji kwa damu ya Yesu. Ninaamuru uzima kwa damu ya Yesu. Asante Bwana Yesu kwa kuwa halitasalia gonjwa la rohoni au
mwilini ambalo lililo letwa na nafsi bila kuponywa kwa damu Yesu. Asante kwa uponyaji sasa. Uchungu unaondoka sasa kwa damu ya Yesu. Hasira inaondoka sasa kwa damu ya Yesu. Wivu unaondoka sasa kwa damu ya Yesu. Chuki inaondoka sasa kwa damu Ya Yesu, majuto, manunguniko, masikitiko,kutokusamehe Na yote yafananayo na hayo yanaondoka sasa kwa damu ya Yesu. Uzito
unaondoka sasa kwa damu ya Yesu. Damu ya Yesu inaenda kuponya hata makovu na vidonda vyoote vya zamani kwa damu ya Yesu. Asante Bwana Yesu kwa kuukomboa uhai Wangu na kaburi. Uhai wa afya yangu. Uhai wa ndoa . Uhai wa uchumi. Uhai wa kazi. Uhai wa biashara. Uhai wa mwili wangu. Uhai wa hatua zangu. Uhai wa vibali vyangu kwa damu ya Yesu unakombolewa sasa. Kwa
damu ya Yesu kila mlango wa mauti uliopitia nafsi naufunga sasa kwa damu ya Yesu. Mauti ya afya. Mauti ya biashara. Mauti ya ndoa. Mauti ya kazi.mauti ya miradi. Mauti ya vibali.mauti ya nafasi, mauti ya mpenyo, Kila mauti iliyo ingia mlango wa nafsi nakukutanisha na damu ya Yesu. Nakuharibu ewe mauti. Nakuharibu ewe kaburi kwa damu ya Yesu. Kwa jina la Yesu.Asante Bwana
Yesu kwa ukombozi kamili wa nafsi yangu. Natangaza iko huru sasa, na kuta zake, na malango yake na misingi yake katika jina la Yesu. Sifa utukufu na heshima nakurudishia wewe katika jina la Yesu nimeomba. Amen
*endelea kuomba haya maombi kwa mda mrefu hadi amani ya moyo imerudi.
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu.Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0765377506/0713297066
Mwl Joseph Ntandu
Mwz 1-3 Mungu akasema iwe Nuru ikawa Nuru

Mungu akubariki mtumishi
ReplyDeleteAsnt mtumishi
ReplyDeleteAmen barikiwa Sana Mtumishi wa MUNGU
ReplyDeleteNimeelewa sana, nashukuru kwa ufafanuzi mzuri wako🙏🙏
ReplyDeleteAmina barikiwa mtumishi wa Mungu.
ReplyDeleteAmina Utukufu kwa Bwana YESU
ReplyDelete