IELEKEZE WAPI BARAKA IENDE UNAPOTOA SADAKA YA FUNGU LA 10

Somo fupi: *ielekeze wap baraka iende unapotoa sadaka ya fungu la 10*

Bwana Yesu asifiwe!

Unapotoa sadaka ya fungu la 10 usitoe kimya kimya, ingawa inajulikana na iko wazi ya kuwa Mungu hukubariki watu wanaotoa mafungu ya 10. Ila hupati baraka kwa kutoa pesa, au kutoa sehemu ya 10 ya Mungu

alichokupa kinachofanya Mungu akubariki au akupe dhawabu ni utii wa kusikia sauti ya Mungu, utii wa kutoa fungu la 10, baraka huja baada ya utii, na utii huu usiwe wa kulazimishwa, kutishwa, au kusukumwa

bali uwe automatic yani moyo unaopenda na kutaka kutaka kutoa kwa Mungu. Bwana Yesu asifiwe. Roho Mtakatifu akanifundisha jinsi ya kuombea sadaka ya fungu la 10, na jinsi ya kujiconnect na baraka kimaandiko

hicho ndicho nataka tupeane asubuhi hii ili tuongezeane ufahamu wa Mungu. Jinsi unavyolifungua neno na kuingia ndani jinsi unavyoingia deep ndivyo jinsi unatoka na madini. Halleluyah

Tuangalie histori ya sadaka ya fungu la 10

Mwanzo 14:18
. Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.

Mwanzo 14:19
. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.

Mwanzo 14:20
. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Neno fungu la 10 kwa Mara ya kwanza kabisa limetajwa hapo katika mwanzo 14:20, na ukisoma kitabu cha waebrania utaja kugundua Melkizedeki Mfalme wa mahali pa juu alikuwa Yesu katika agano la

kale. Kipindi hiko alikuja Kama malaika. Ila katika mwili wa binadamu. Malaika anauweza wa kuvaa mwili wowote ule. Bwana Yesu asifiwe. Sababu hakuna kuhani wa mahali pa juu zaidi ya Yesu. Na yupo

mmoja Tuu. Kwa iyo kwa Mara ya kwanza fungu la 10 linatolewa kwa Mungu mwenyewe. Kwa iyo fungu la 10 la kwanza lilitolewa kwa Mungu Si binadamu. Na Mungu alifanya hivi makusudi ili aweze

kumlindia Baraka binadamu Baraka. kumbuka binadamu wa kwanza Adamu na Hawa waliuza Baraka kwa dhambi. Hallelujah. Ikaingia laana. Ili kuhakikisha kwamba safari Baraka Haitui kwa shetani

ndo mana Mungu akashuka kwa binadamu. Kumtamkia mwenyewe Baraka na binadamu kumpa Mungu moyo wake. Kumbuka mke wa adamu uasi uliingia kwanza kwenye moyo ndipo wakatekeleza

uasi. Kwa Yesu kuchukua fungu la 10, katika mikono ya Ibrahimu hii manake alichukua moyo wa binadamu ili aweze kuucontrol na kumsaidia ili asije poteza Baraka. Maana huwezi utawala moyo wako mwenyewe

moyo wako umeumbwa kutawaliwa. Bwana Yesu asifiwe. Unapotoa sadaka ya fungu la 10, manake umemkabithi Mungu moyo wako. Ile 90% ya Baraka iliyobaki isije kukufanya ukamuacha Mungu. Yani Baraka

isije kukufanya ukamuasi Mungu. Tatizo Si kufanikiwa unaweza kufanikiwa kisha ukaangamia. Hallelujah! Kwa iyo sababu

huwezi kucontrol moyo wako mwenyewe na kujiongoza wenyewe hasa linapokuja swala la mafanikio ndio maana unatoa sadaka ya fungu la 10 ili Mungu akusaidie

#kufanya maamuzi sahihi
#kufanya uchaguzi sahihi
#Moyo wako usije muacha Mungu
#Moyo wako usije potoshwa kwa uongo wa shetani
#Moyo wako usije kukuongoza kwenye hasara au shimo
#Moyo wako usije tapanya Mali
#Moyo wako usije fungua milango kwa shetani na adui kupanda mapooza, uharibifu, utasa, mauti kwenye malango yako kwenye hatua zako

# sehemu ya 90% baada ya kutoa fungu la 10 Mungu huifuatilia, huibariki, huilinda maana umeshamkabithi

# Kwa kuwa moyo wako uko kwa Mungu ataleta mawazo mapya kwenye moyo wako, ataleta majibu ya maswali kwenye moyo wako,Mungu ataleta maelekezo kwenye moyo wako. Ili kuhakikisha unasonga mbele. Bwana Yesu asifiwe

#Mungu hutumia fungu la 10 kukufuatilia na kukufanikisha, wengi wanafikiri wakitoa pesa watapata pesa. Saa ingine ai pesa unayohitaji saa ingine unahitaji uhodari na ujasiri tuu wa kufanya kitu

# kwa iyo usimpangie Mungu jinsi ya kukufanikisha jinsi ya kukusaidia. Mungu atakutia nguvu, atakupa uhodari na ujasiri wa kufanya unayoshindwa kuyafanya.angalia hapo juu ngoja nirudie tena uone big picture.....

Mwanzo 14:18
. Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.

Mwanzo 14:19
. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.

Mwanzo 14:20
. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Ibrahim alitoa fungu la 10 lakini Melkizedeki alimpa neno. Na Si neno tuu Bali neno la Baraka, Ibrahim hakutoa vitu kisha Melkizedeki naye akampa vitu no!. Bali huyu katoa sadaka. Huyu katoa neno la Baraka. Kwa iyo kabla ya kitu lazima kuwepo neno la Baraka Hallelujah.

#Ibrahim alimbariki Melkizedeki naye akabarikiwa (uyu kabariki kwa kutoa vitu& uyu kabariki kwa kutoa neno la Baraka)
# Baraka unaweza ikwamishwa kwako au iteka kwako, angalia alichofanya Ibrahim alihitaji neno la Baraka akaenda iteka kwa kutoa vitu
#sheria ya ulimwengu wa Roho ukitaka kuchukua kitu lazima utoe kwa kukiweka kwanza. Miaka ya nyuma niliwahi sema huwezi kuchukua kitu usichokiweka katika ulimwengu wa Roho
#watu wengi wanapenda neno la Baraka neno la hekima la kuwavusha ili hawajui kujiungamanisha kiimani. Hawajui kuwa katika ulimwengu wa Roho unachukua ulichokiweka. Hallelujah
# angalia Ibrahim alichofanya! Swali ni nani alimuambia Ibrahim afanye vile? JIBU: ni Roho Mtakatifu alitaka kuachilia neno la Baraka kwa Ibrahim. Baada ya pale Baraka zikaflow hadi kwetu sisi. Hallelujah!

Kwa iyo sasa! Kwa wewe kutoa fungu la 10

✅unajiungaminisha na Baraka za Ibrahim alizotamkiwa na kuzipokea. Kipindi anatamkiwa wewe ilikuwa katika viuno vyake. Na kwa damu ya Yesu sisi pia ni kabila la lawi. Kwa damu ya Yesu sisi ni faida la Israeli. Bwana Yesu asifiwe sasa ninakuja kwenye jinsi ya kuiombea sadaka ya fungu la 10 kuiconnect na Baraka na kuielekeza wap sadaka iende usijiconnect na kuishia njiani tuu. Hallelujah! Melkizedeki wako anaweza akakutamkia neno la Baraka au asitamke. Lakini make sure wewe fungu lako 10 umeshalitamkia. Hallelujah nitakuonyesha mda Si mrefu. Jina la Bwana libarikiwe......

Utaiungamanisha sadaka yako na Baraka kwa kutamka maneno haya ya imani

*baba yangu wa imani Ibrahimu alikutolea sadaka mimi nikiwa kiunoni mwake, na wewe Bwana Yesu uliachilia baraka hizo kwa ibrahimu alipopokea ibrahimu na mimi nilipokea maana mimi kabila la lawi kwa

damu ya Yesu.ninapotoa fungu la 10 ninajiunganisha na baraka za ibrahimu kupitia damu ya Yesu na kujiconnect na agano jipya la damu ya Yesu. Na baraka zote za msalaba kwa damu ya Yesu.Na

baraka zote Mungu alizoziweka katika ardhi ya Israeli kwa damu ya Yesu* katika jina la Yesu.

Sasa angalia hapa kwa kuwa tayari umeshajiungamanisha na iyo Baraka usiishie hapo nenda mbele zaidi uieleleleze wap Baraka iende Hallelujah

Thank you Holly Spirit hizi ni siri za ajabu Sana za Ufalme

Kumbukumbu la Torati 28:2
. na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 28:3
. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.

Kumbukumbu la Torati 28:4
. Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.

Kumbukumbu la Torati 28:5
. Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.

Kumbukumbu la Torati 28:6
. Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.

Kumbukumbu la Torati 28:7
. Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

Kumbukumbu la Torati 28:8
. Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 28:10
. Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako.

Kumbukumbu la Torati 28:11
. Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.

Kumbukumbu la Torati 28:12
. Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.

Kumbukumbu la Torati 28:13
. Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;

Angalia hapo juu Mungu hakusema tuu Baraka hii itakujilia kisha akakaa kimya. No! Alizielekeza wapi Baraka ziende Hallelujah!

✅Baraka ilielekezewa mjini ilielekezewa kijijini
#ielekeze Baraka kwenye hiko kitega uchumi kilichopo mjini au kijijini. Kama ni mjini kabisa sema kabisa Baraka ya Ibrahim kupitia fungu la 10 kwa damu ya Yesu ninaielekezea kwenye duka. Ninaielekezea shambani

✅Baraka ilielekezewa kwa watoto na mifugo
# tamka kabisa naielekeza Baraka hii kupitia fungu la 10 kwa mwanangu Kelvin. Naielekezea Baraka hii kwenye mradi wa kuku

✅Baraka ilielekezewa kwenye kazi
#sema kabisa Baraka hii naielekezea kwenye kazi yangu cheo changu mshahara wangu biashara wangu

✅Baraka ilielekezewa kwenye malango ndo mana ya kubarikiwa uingiapo. Kubarikiwa utokapo
#ielekeze Baraka kwenye malango yako Kama ya ndoa, kazi, biashara, afya, huduma, ndoto na maono, afya na uzima na yote utakayoyakumbuka

✅Baraka ilielekezwa kwenye ulinzi. Ndo mana anasema adui zako watapigwa kwa njia saba
# tamka kabisa Baraka ya ulinzi iende wap? Kwenye ndoa, afya ya familia, kazi , biashara, nyumbani kwako, hapo unapotamka adui wakija watapigwa kwa njia saba

✅Baraka ilielekezwa kwa katika ghala zako, na ilielekezwa katika mikono yako
# ilelekeze Baraka kwenye account zako za bank, kwenye ghala zako za nyumbani, ielekeze kwenye kazi za mikono yako. Kama wewe unahubiri Kama Mimi kwa kuandika manake hii ni kazi mojawapo ya mikono yangu.

✅Baraka iliekezwa kwako ili mataifa wawe na hofu mbele zako

✅Baraka ilielekezwa kwenye mbingu zako na ardhi yako. Na kazi ya mikono yako. Na Mali zako ndo mana anasema utakopesha wewe hutakopa

#elekeza kote huko
✅Baraka ilielekezwa katika mafanikio ndio maana anasema utakuwa kichwa wala Si mkia Hallelujah

Kwa iyo kabla ya kutoa fungu la 10 embu fanya ibada kamili. Unaona hapo utagundua tulikuwa tukiomba na kuishia njiani omba kitu kikamilike. Ielekeze Baraka wap unataka iende. Bwana Yesu asifiwe.

Mtumishi anaweza ndio kukuombea lakini wewe mwenyewe unakuwa na ibada kabisa kabla ya kuachilia sadaka yako Hallelujah. Bwana Yesu asifiwe. Embu mshukuru Roho Mtakatifu kwa ufunuo huu maana utaanza

kuziona Baraka za Bwana na neno Hili halitampita Mungu bure. Hallelujah. Hii ni siri ya ajabu.sana. Kimbe tulikuwa tunaomba lakini hatumalizi. Lakini hatuingii ndani. Utaelewa kwanini Musa na haruni

kabla ya kutoa sadaka zao walikuwa wanafanya ibada kamili kuhusu sadaka Yao. Lakini sisi tunakimbia kimbia tuu sijui hata uwa tunawahi wapi au tunawahi nini?. Na matokea yake tuna short baraka. Hallelujah

Thank you Jesus

Malaki 3:10
. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

✅kutoa fungu la 10 kumbe ni njia ingine ya kujaribu uaminifu wa Mungu
✅Na ni njia ya Mungu kukujaribu uaminifu wako
✅ukiushinda huu mtihani ukatoa kwa moyo wa kupenda fungu la 10 kipo kiapo cha makubaliano Kati ya mtoa mafungu ya 10 na Mungu
✅kumbe unaweza kuwa unatoa mafungu ya 10 lakini kwa Mungu hiko kitendo huwa kinaenda jaribu uaminifu wa Mungu
✅Uaminifu wa Mungu upo katika kutimiza kile achoahidi
✅Mungu asipotimiza kila alichoahidi kwako, kwake linabaki deni
✅Ndo mana katika zaburi ya 15:4 inasema Mungu ameapa hata kwa hasara yake ayabadili maneno yake.
✅Yani inawezekana hiki Mungu alichoahidi kutamgharimu Mungu lakini sababu ameshasema basi Mungu anafungika kwa maneno yake mwenyewe
✅Ndo mana ilimgharimu kumtoa Yesu mwana wake wa pekee ingawa kwake ilikuwa gharama kubwa lakini Hana jinsi alishafungika na kiapo
Chake mwenyewe
✅sasa tuangalie Mungu alifungika na maneno gani
✅Mjue Kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni Baraka. HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA
✅Hilo neno hata isiwepo nafasi ya kutosha, inawezekana Mungu anakufanyia Baraka. Lakini je nafasi ya kupokea Baraka ya kutosha imejaa? Au bado ipo wazi?
✅Baraka zipo za aina nyingi. Baraka ndizo zinakidhi mahitaji. Ukiwa na shida ya Mil 1 Hilo Ni hitaji. Bwana Yesu asifiwe
✅Kwa iyo ipo ahadi ya Mungu ya kuachilia Baraka hadi isiwepo nafasi ya kutosha, Baraka ikatosheleze hata mahitaji yajitosheleze
✅zipo Baraka za Rohoni zipo Baraka za mwilini . Inawezekana Mungu anakushibisha Sana Baraka za Rohoni. Lakini za mwilini si Sana
✅Isikusumbue unachotakiwa ni kumkumbusha Mungu ili atimize uaminifu wake kwako kwa neno lake.
✅kabla ya yote yawezekana umeshajihesabia haki katika hili au umefanya kiburi cha uzima. Kwa iyo Toba na Rehema kwanza kabla ya jambo lolote. Kisha kwenda kuomba Mungu atimize uamnifu wake kwa kile alichokisema.

Baba katika jina la Yesu yawezekana madirisha haya ulishayafungua mbele yangu na nikayafunga Mimi mwenyewe au sikuyaona Kama ni madirisha ya mbinguni au niliyaona na sikuyafanyia kazi, na

inawezekana uaminifu wako ulishaonekana kwangu na Baraka ziliachiliwa lakini nilitapanya. Kuna mahali nimekorofisha Mungu wangu hata kwa kujihesabia haki, au kuwa na kiburi cha uzima baada ya kuona

dalili za Baraka na sikutaka kukusikiza tena, wala kufuata maagizo yako, katika hili nimekosa, neno lako Mungu ni kioo changu cha kujiangalia.ninatubu na kuomba Rehema jambo lolote lililofanya madirisha

ya mbinguni yasifunguke mbele yangu au yafunguke lakini sio kwa wingi wa kujaza nafasi za mahitaji Leo hii ninatubu na kuomba Rehema. Asante Bwana Yesu kwa kunisamehe sifa na utukufu na heshima

nakurudishia wewe Bwana Yesu kwa kuwa wewe ndiwe chakula cha kweli na wewe ndiwe kinywaji cha kweli. Kwako sioni kiu tena Kwako sisikii njaa. Sifa utukufu na heshima nakurudishia wewe, kwako Bwana

Yesu ile njaa ya mahitaji, ile kiu ya mahitaji inaenda kukomeshwa na wewe sasa. Kwa kuwa wewe ndio kila kitu kwangu na bila wewe Yesu siwezi jambo lolote. Nakushukuru BWANA YESU, kwa kuwa

wewe unayajua mahitaji yangu yote. Unayajua mahitaji yangu ya mwilini, unayajua mahitaji yangu ya rohoni na umesema nisijisumbue. Nami Bwana Yesu sitajisumbukia kwa habari la hitaji langu la

✅fedha
✅mtaji
✅kazi
✅taja mengine......

Bali Bwana nitakukumbusha kuhusu uaminifu wako "uliposema hata isiwepo nafasi ya kutosha ya kuweka hizo Baraka". Bwana Yesu kwangu bado ipo nafasi ya kuweka Baraka ninaomba Baraka zako

Bwana Yesu zifunguliwe sasa juu yangu kwa damu ya Yesu. Juu ya uchumi wangu, ili mahitaji yangu ya kiuchumi, yakutanishwe na Baraka zako katika jina la Yesu.

Ninakutanisha mahitaji yangu ya fedha na Baraka zako. Baraka zako Bwana Yesu kupitia damu yako ninakutanisha na mahitaji ya

✅Mtaji
✅biashara
✅kazi
✅Afya
✅Ndoa
✅mahusiano
✅kifedha
✅ya mwilini na Rohoni

Ninakutanisha na damu ya Yesu yeye Baraka. Wewe hitaji langu kutana na damu ya Yesu kwa mamlaka ya jina la Yesu.

Asante Bwana Yesu utukuzwe wewe pekee we ufanyaye mambo makubwa na ya ajabu na ya kutisha kuliko Yale niombayo kuliko Yale niyafikiriayo Asante kwa kufungua madirisha ya mbinguni. Asante kwa mvua za Baraka katika jina la Yesu nimeomba. Ameen.

kitu kinaitwa *meeting point*

Ukisoma maelekezo aliyokuwa anawapa Joshua wana wa Israeli na Musa hapo ndipo utaelewa vizuri.

Kitabu cha walawi

Nia ya sadaka Ni Mungu kukutana na mioyo ya watu wake kwa njia ya imani. Wapi inapoenda fungu la 10 Mungu ndo anajua liende wap? Yeye ndo distributor

Kusudi imegawanyika Mara mbili. Kule inakoenda lipo kusudi. Kule inakotoka lipo kusudi. Sasa tuzungumzie inakoelekea. Yani mtoaji. Mungu anaweza kuwa anataka

☑kufunga agano na mtu
☑kumsaidia mtu
☑kumbariki

Akatumia njia ya sadaka. Maandiko kuhusu fungu la 10 kwenye biblia Yapo Mengi. But common ni malaki 3:10

Malaki 3:10
. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Panapochanganya watu. *nyumba yangu* anaposema nyumba yangu Ana maana gani?

Agano la kale nyumba ni jengo
Agano jipya nyumba ni mwili wa mtu

Yesu alipokufa na kufufuka kanisa lilitoka kwenye sanduku la agano. Kwenda kwenye mwili wa mtu. Unasikia Yesu akanisa kubwa manake miili ya watu ndo jengo (kanisa) na mioyo ndo meeting point yani inatumika Kama madhabahu ya kukutana na watu wake au kuongea Na watu wake.

Hallelujah
Wana wa Israeli waliambiwa kabila la lawi ndio wanaopaswa kupokea fungu la 10

Kumbukumbu la Torati 10:8
. Na wakati huo Bwana aliitenga kabila ya Lawi ili walichukue lile sanduku la agano la Bwana, wasimame mbele ya Bwana kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.

Kumbukumbu la Torati 18:1
. Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za Bwana zifanywazo kwa moto, na urithi wake.

Kumbukumbu la Torati 18:2
. Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.

Kumbukumbu la Torati 18:3
. Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.

Kumbukumbu la Torati 18:4
. Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, umpe.

Kumbukumbu la Torati 18:5
. Kwani Bwana, Mungu wako, amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele.

Kabila la lawi Leo hii ni makuhani wa Yesu. Si makuhani tuu Bali ni wateule. Waliowekwa wakfu na BWANA kwa ajili ya kazi ya Mungu

Wapaka mafuta na Bwana.

Je Ni kila lawi wote unapaswa kumpelekea fungu la 10? Jibu ni hapana.

ni hapana sababu sehemu ambako Mungu anataka akutane nawe kwa njia ya sadaka. Hapo ndipo kaweka Baraka zako au kitu chako. Kwa iyo ukiweka sadaka ambako uyo mlawi hajapewa kitu chako sadaka itapokelewa lakini kusudi la Mungu hutakutana nalo.

Kumbukumbu la Torati 14:22
. Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

Kumbukumbu la Torati 14:23
. Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

Kumbukumbu la Torati 14:27
. na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

*Mahali atakapo pachagua BWANA apakalishe jina lake*

Nilisema kule juu! Agano la kale sanduku la agano lilikuwa linakaa kwenye jengo. Agano jipya ambalo ndo tupo sanduku la agano linakaa kwenye nyumba (miili) na hili Ni agano jipya la Bwana Yesu..

Na sii miili tuu Bali linakaa kwenye moyo. Na Si moyo wa nyama. Bali moyo wa Rohoni. Ndo mana unapookoka kinachookoka ni Roho na Si mwili. Lakini bila kusahau Roho inakaa ndani ya nyumba mwili.

Kitu gani kitakachokusaidia kujua je napopeleka fungu la 10 kwa mlawi uyu ni sawa au Si sawa?

Fungu la linatolewa

☑sehemu ambayo unakula Na kunywa kila siku chakula cha kiroho

☑Na si Kula tuu Bali unajiona unakuwa kiroho

☑sehemu ambayo Kuna wepesi wa uyo Mlawi kutumika na Mungu kukuhudumia

☑sehemu ambayo kila Mara Mungu huitumia kukupa neno la maarifa na kukupa neno hekima. Na ukitumia tuu Mungu hukuvusha

☑sehemu ambayo unapata urahisi na wepesi wa kumshirikisha uyo Mlawi mambo yako na Mungu humtumia kila Mara akisimama kwenye nafasi yake Kuna kitu chako kitapiga hatua kutoka hapo

☑sehemu ambayo unapata Amani kupeleka fungu lako la 10,yani unapata Amani na furaha baada ya kutoa fungu la 10,Mungu alimuambia Musa uchugue sadaka kwa wale moyo wao wawapa

kutoa.Musa hakuchukua kwa kila mtu. Yani kitendo cha kutaka kwako kutoa kiwe kinaamani ndani mwako, kuwe kuna uhuru, usijisikie kama unalazimishwa au kusukumwa. Yani ukifikiria kutoa tuu upate

amani na uhuru wa kutoa Ivyo Ni viashiria vya kukusaidia wapi upeleke. Muhimu Ni kukutana na Mungu kwa njia ya sadaka. Mungu akikuambia tukutane morogoro wewe ukaenda Dar hutamkuta. Ikiwa Kuna

maelekezo tofauti ya Mungu kuhusu pakupeleka fungu la 10. Mungu ataongea nawe, atakupa neno, na Amani moyoni na uhuru moyoni. Na wepesi wa kufanya hivyo. Baada kufanya hivyo utasikia Raha nafsini

mwako. Na uhuru wa Kristo. Na Amani ya Kristo. Moyoni hutakuwa na mashaka. Ukiona unapotaka kutoa hupati uhuru wa kutoa, hupati amani basi funga na kuomba kumuomba Roho Mtakatifu. Akuonyeshe

mlawi wako. Ili ukutane na baraka zako na ulinzi wa baraka kupitia uyo mlawi. Ili usije pishana na baraka zako. Ili ukutane na Mungu kwa njia ya fungu 10 mahali anapotaka mkutane.

Jina la Bwana libarikiwe.

✅nimesema hivi Roho Mtakatifu ndiye anayejua sadaka aipeleke wapi na kwa ajili ya nini. Mahali ambako amekuambia upeleke hapo ndipo utakutana naye, na hapo ndipo ameweka baraka zako. Sisi

watumishi kazi yetu ni kukuongoza ili uweze msikiza Roho Mtakatifu na kufuata maagizo yake. Kwa iyo Roho Mtakatifu ndiye atakayekuambia wapi upeleke sadaka yako iwe ni fungu la 10, iwe ni sadaka ya aina

yoyote. Kwanini tunakuongoza ni ili uweze msikia Mungu na kumtii Mungu. Ni ili shetani asije jigeuza yeye kama malaika wa nuru na kukupotosha. Nia ya kukufundisha ni ili Roho Mtakatifu atakapo ongea na

wewe basi uweze msikia na kumtii. Ndo mana nikakupa viashiria. Katika sauti ya mtumishi nyuma yake kuna sauti ya Mungu. Katika neno la Mungu nyuma yake kuna sauti ya Mungu. Mfano ninachoandika hapa

sicho hicho wewe unakisikia unaposoma. Nikitaka kupata unachosikia ukisoma inabidi nimalize kuandika kisha sasa na mimi nianze kusoma kama wewe. Swala la sadaka linategemea maelekezo ya Roho

Mtakatifu zaidi. Na sauti ya Roho Mtakatifu inapokuja ndani mwako hakutakuwa na , mashaka, hakutakuwa na uzito, hakutakuwa na kufungika kuhusu kutoa sadaka. Bali utafunguka kuhusu kutoa,utapata uhuru.

Utapata amani ya kutoa. Lakini fuata maelekezo ya Roho Mtakatifu. Unapotoa sadaka mahali Mungu ametaka utoe hapo mahali utakutana na

✅neno la hekima
✅neno la maarifa
✅neno la ulinzi

Kupitia madhabahu inayotumika na Mungu kupitia uyo mlawi.

Mwisho wa siku Swala la sadaka ni la ROHO MTAKATIFU ZAIDI. Muulize atakuongoza kama huna uhakika.

kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu.Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


Muhimu: 

Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia  tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo 



Mwl Joseph Ntandu
Mwz 1-3 Mungu akasema iwe Nuru ikawa Nuru

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA