MAOMBI~ KUNYAMAZISHA MIUNGU KWENYE NAFSI KWA DAMU YA YESU
maombi~kunyamazisha miungu kwenye nafsi kwa damu ya Yesu
Maombolezo 5
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako;Na sisi tumeyachukua maovu yao.
Mungu uliyehai katika jina la Yesu na kwa damu ya Yesu nasimama sehemu iliyobomoka kwa ajili yangu ninatubu na kuomba Rehema kwa ajili yangu, ninatubu na kuomba Rehema kwa ajili ya mashitaka na hukumu, vinavyonishitaki katika ulimwengu wa Roho, Baba nasimama sehemu iliyobomoka kwa ajili ya malango ya familia yangu, lango la uzazi upande wa baba, lango la uzazi upande wa mama, ninatubu na kuomba Rehema kwa ajili ya uovu wowote usiotubiwa,Bwana Yesu unisamehe na utusamehe, Ee Bwana imeandikwa Baba zetu walitenda dhambi na sasa hawapo na sisi tumeyachukua maovu yao,Mungu uliye hai kinachonifuatilia kupitia misingi mibovu ya damu ya ukoo na familia ninatubu na kuomba Rehema kwa ajili ya misingi, nirehemu Bwana, utusamehe Baba Mungu wa mbinguni, Biblia inasema misingi ikiharibika mwenye haki wangu atasimama wapi, Baba uliye mbinguni ipo misingi ya kipepo, misingi ya mizimu, misingi ya mashetani yanayomiliki ukoo na kutawala familia na misingi iyo Bwana inatembea kupitia d.n.a ya ukoo na familia, Ee Bwana, Kama vile ambavyo misingi ya hasira ilivyomwadhiri Musa mtumishi wako ndivyo hivyo ivyo Bwana nasi tumeadhirika na misingi mibovu ya familia na ukoo, lakini leo tunashukuru kwa kuwa ipo neema kubwa juu yetu ya kutusaidia ipo damu ya Yesu, inayosimamisha misingi mipya ninaachilia damu ya Yesu juu ya misingi ya magonjwa ya miungu katika ukoo wangu, ninaachilia damu ya Yesu juu ya misingi ya miungu iliyojengwa katika fikra, iliyojengwa katika ndoa, iliyojengwa katika nafsi, iliyojengwa katika afya, iliyojengwa katika uchumi, iliyojengwa katika huduma yangu, iliyojengwa katika utumishi wangu, iliyojengwa katika mikono yangu, iliyojengwa katika miguu na hatua zangu, iliyojengwa katika hatua zangu,iliyojengwa katika kazi za mikono,iliyojengwa katika akili yangu, iliyojengwa katika ufahamu wangu, iliyojengwa katika kazi yangu, iliyojengwa katika biashara yangu, misingi ya miungu iliyojengwa katika uzee wangu,iliyojengwa katika umri wangu, iliyojengwa katika malango yangu, iliyojengwa katika nafsi yangu, iliyojengwa juu ya mwili wangu, iliyojengwa katika mawazo yangu, misingi ya miungu ya ukoo na familia iliyojengwa katika tabia, tabia ya ulevi, tabia ya uhuni, tabia ya magomvi, tabia ya ukatili, tabia ya uchoyo, tabia ya uwizi, tabia ya tamaa, tabia ya malalamiko na manunguniko, tabia ya uvivu, tabia ya mazoea, tabia ya ukorofi, tabia ya hasira, tabia ya malipizi, tabia ya kisasi, tabia ya kiburi na ujeuri, tabia ya dharau, tabia ya kujikweza,tabia ya kujitenga, tabia ya ubinafsi,tabia chafu, katika jina la Yesu,leo naibomoa kwa jina la Yesu, Baba Mungu wa mbinguni kila misingi ya miungu toka ukoo wa baba yangu na ukoo wa mama yangu, iliyopandwa kwenye moyo wangu, ninaimwaga damu ya Yesu na kunyunyiza damu ya Yesu naivunja vunja iyo misingi kwa jina la Yesu, Damu ya mwanakondoo ,ikavunje vunje iyo misingi katika jina la Yesu, ninaachilia damu ya Yesu juu ya misingi ya miungu au mashetani, mizimu ya ukoo na familia iliyopanda matukio ya kurithi juu yangu, matukio mabaya yakuipata familia yangu, matukio ya moto, matukio ya ajali, majanga kuangukiwa na nyumba,kila matukio mabaya yanayo iandama familia yangu, au mimi, ukoo wangu,yanayonifuatilia mimi na watoto wangu, na kizazi changu, ninayafunga kwa damu ya Yesu, Baba Mungu miungu iliyopanda kumbukumbu za ukoo kwenye akili na fikra zangu, ili wanitawale, miungu iliyonipandia akili ya ukoo kwenye fikra zangu ili nifanane na wanaukoo, ili nipite njia walizopitia wao,ninaachilia moto wa Roho Mtakatifu upite kwenye cell ya ukoo, upite kwenye tabia ya ukoo, upite kwenye matukio ya ukoo, upite kwenye akili ya ukoo, upite kwenye kumbukumbu ya ukoo enyi miungu msiyofanya nchi wala mbingu ninaongea na nyie kwa damu ya Yesu, mimi si wa kwenu, mimi nimeokoka nimenunuliwa na damu ya Yesu, imeandikwa hata mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita nayo yamekuwa mapya, niachilia miali ya moto, ipite kwenye damu ya ukoo, ninaachilia miali ya moto ipite kwenye d.n.a ya ukoo, ninawaamuru mashetani, ninawaamuru mapepo, ninawamuru majini, ninawaamuru mizimu ya ukoo na familia, enyi mizimu ya ukoo na familia ninawamuru kuchomoka sasa kwenye damu ya ukoo, ninawaamuru kufyatuka sasa kwenye damu ya ukoo, katika jina la Yesu, nyie miungu mnaorudisha ya kale mbele yangu, nyie mnaorudisha kumbukumbu za ukoo mbele yangu, mnaorudisha akili ya ukoo kwenye nafsi yangu, mnaorejesha matukio mabaya kwenye ukoo wangu, juu yangu, ili yanipate mnaorejesha tabia za ukoo kwenye nafsi yangu, wewe pepo unayefuatilia damu ya ukoo na uliyekalia nafsi yangu, umekalia maamuzi yangu, wewe unayejiinua kinyume na Elimu ya Mungu ndani ya nafsi yangu, wewe unayepotosha fikra zangu, wewe unayepofusha fikra zangu, wewe unayeniwekea uzito juu ya nafsi yangu, ili nisimsikie MUNGU, ili nisimtii MUNGU, ili nishindwe kuamua, ili nishindwe kuchukua hatua, wewe unayepambana na imani yangu ili nisiamini, au niache kuamini, wewe unayeleta mashindano kwenye nafsi yangu, wewe unayeitabisha nafsi yangu katika jina jina la Yesu leo ninakufunga kwa damu ya Yesu leo ninakusambaratisha kwa moto wa Roho Mtakatifu,nakusambaratisha, katika jina la Yesu ninaachilia damu ya Yesu ipasue madhabahu yako vipande vipande, katika jina la Yesu ninakutawanya kwa njia saba hutakaa tena kwenye nafsi yangu, hutaitawala tena nafsi yangu, hutaikalia tena nafsi yangu kwa damu ya mmwanakondoo katika jina la Yesu leo ninakufunga wewe na madhabahu iliyo nyuma yako na kuiharibu kabisa katika jina la Yesu, kila mapando uliyoyapanda juu ya nafsi yangu katika jina la Yesu, ninayangoa kwa damu ya Yesu, wewe pepo unaliyetumwa kupanda urithi mbaya tokea kwenye familia yangu, kupanda matukio mabaya, kupanda akili mbaya, kupanda kumbukumbu mbaya, kupanda tabia mbaya, kwa damu ya Yesu ninakufunga wewe pepo kwa jina la Yesu, ninakuteka kwa damu ya Yesu, naachilia moto ulao juu yako, nakusaga vipande vipande kwa moto wa Roho Mtakatifu, Hama kwangu kwa jina la Yesu, toweka kwangu kwa damu ya Yesu, toka katika jina la Yesu, Baba katika jina la Yesu, damu ya ukoo ya magonjwa inayonifuatilia nainyamazisha kwa jina la Yesu, damu ya kuachwa inayonifuatilia nainyamazisha kwa jina la Yesu, damu ya kukataliwa,mikosi, balaa, damu ya kuvunja ndoa, kutokuoa au kuolewa, damu ya umasikini, kufilisika,
kumaliza uzee vibaya,kutapanya mali, damu ya utasa, hasira, uhuni, ulevi, ujinga, damu ya ukoo na familia inayonifuatilia kwa damu ya Yesu ninanyamzisha kwa jina la Yesu, damu ya matukio maovu nainyamazisha katika jina la Yesu,mashetani wa ukoo na familia ninawatenga mbali na mimi kwa damu ya Yesu, napitisha moto wa Roho Mtakatifu kwenye damu yangu, napitisha moto wa Roho Mtakatifu kwenye d.n.a yangu, katika jina la Yesu napitisha miali ya moto ikawafyatue mashetani hao, watoke wakiwa wamefungwa katika jina la Yesu, damu ya Yesu ikawaponde majini hayo, ikawapasue mizimu iyo kwa moto wa Roho Mtakatifu katika jina la Yesu.
☆endelea kuomba huu ni mwanzo tuu nimekuanzishia
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
#Mtumishi Joseph Ntandu
#Wanamaombi Group
kama ungependa kuokoa uhusiano/ndoa yako basi nitakupendekeza kwa Dk Dawn. alinisaidia kurejesha nyumba yangu baada ya miezi 11 ya utengano mkali kati yangu na mume wangu. Nilielekezwa kwake na dada yangu mkubwa wakati ndoa imeisha, akarudisha amani na furaha katika ndoa yangu, pia amesaidia marafiki zangu wengine na wanaishi kwa furaha kwa msaada wa Dk Dawn,
ReplyDeleteWasiliana naye ikiwa unahitaji usaidizi wa kurejesha uhusiano/ndoa yako/ ikiwa unataka kupata mimba au kuponya aina yoyote ya ugonjwa:
Dk Dawn hatawahi kukukatisha tamaa:
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159