VITA KATIKA MALANGO YA NDOTO

Somo: Vita katika lango la ndoto

Halleluyaaaah!

Bwana Yesu asifiwe!

Ndoto ni lugha katika picha juu ya mambo yaliyopita, mambo yanayoendelea katika maisha yako. au mambo yanayokuja katika maisha yako. Bwana Yesu asifiwe. Watu wengi sana huwa wanaota, wengine

wanakumbuka walichoota, lakini wengine hawakumbuki walichoota, wanaokumbuka wengine hawajui jinsi ya kuomba, sababu wanashindwa kupata tafsiri na ujumbe ulio katika ndoto, kuna namna rahisi ambayo kila

mtu anaifahamu, unapotoka kwenye ndoto kuna mambo unaweza yacheki, je nilipo amka, nilishitukaje toka usingizini, je nilikuwa nina amani? ama nilikuwa sina amani? moyo ulidunda?je umepata hofu

na kuogopa, je mwili umeamkaje? umeamka na mavamizi? umeshambuliwa? umeamka na amani na furaha? wengine baada ya kuota tuu baada ya siku mbili tatu kuna kitu huwa kinawatokea, wengine wanaanza

kuumwa, wengine mambo yanaanza kuvurugiga, kuharibika, unapotoka usingizini tuu, jikague kwanza, Halleluyaaaah! njia rahisi kabla hata hujajua maana ya ndoto, au tafsiri yake, ni kujicheki jinsi ulivyoamka,

kama tokea ndotoni hajaamka vizuri yani huna amani na furaha basi jua adui alikuwa kazini yakupasa usiendelee kulala bali upangue mitego ya adui, mashimo ya adui aliokuchimbia, manuizo ya adui, laana za adui, mipango ya adui kinyume chako,

ngoa kila mapando adui aliyokupandia, haribu, bomoa, vunja batilisha, kwa damu ya Yesu, tamka kabisa mipango ya adui haitanipata, mabaya hayatanipata, uharibifu hautanipata mimi. amka kanusha kwa damu

ya Yesu. funga na haribu silaha zote zilizofanyika kinyume chako, Halleluyaaaah

Mathayo 13
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.

Kwa iyo adui hupanda magugu katikati ya ngano, ngano inaweza kuwa kazi, katika ulimwengu wa roho mda wako wa kupata kazi umefika, adui anapanda magugu, magugu hayo inaweza kuwa roho

inayotumwa kukutoa ili usipate kazi, yule aliyetakiwa Akupe kazi mara unasikia amefariki, kifo cha mtu muhimu kwako ni magugu kwako, Halleluyaaaah. Ndo mana tunasema pangua kwanza vunja kwanza

kabla hata ya kujua maana ya ndoto, jina la Bwana libarikiwe, Biblia inasema hivi nasi hatukosi kuzijua fikra za ibilisi....

2 Wakoritho 2
11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

kupitia Roho Mtakatifu huwa tunajua hila za ibilisi, tunajua fikra za ibilisi, mlango wa ndoto ni mlango mojawapo shetani hutumia kufanya vita na watakatifu, husababisha

i. kusahau ndoto
ii.kutokuona umbo halisi katika ndoto
iii.kuota ndoto nyingi kwa mara moja
iv.kukuzuia kuomba baada ya kushituka katika kuota

☆Hayo hapo juu ni mambo ambayo yanatengenezwa na wachawi, Halleluyaaaah
yanaundwa kwa kinywa, wanasema kabisa asahau ndoto akiamka, asione umbo halisi atakapo ota, asituone sisi aone ngombe,

aone nyani, aone mnyama wa porini, aone sura ya mtu mwingine, amuone flani asituone sisi, Halleluyaaaah, Bwana Yesu asifiwe.wakati mwingine wanasema tumletee ndoto nyingi achanganyikiwe,

ashindwe kuomba, asikumbuke ndoto anayotakiwa kukumbuka, Halleluyaaaah,
asijue tafsiri, alafu pia ashindwe kuomba, abaki kulalamika, abaki kuhuzunika tuu. asiombe, kisha unashangaa baada ya

kuamka tuu, gafla huna nguvu za kuomba tena,huwezi kusifu, huwezi kuabudu, Huwezi kunena kwa lugha, unashangaa uwepo wa Mungu umekatika wakati ukilala uwepo wa Mungu ulikuwepo wa kutosha Halleluyah,

baada ya kuota tuu uwepo umetoweka, bugujiko limekatika, sasa tukaangilie vita moja baada nyingine vilivyopo katika mlango wa ndoto

_Kusahau ndoto_

Kwanini kusahau ndoto?

1.Ndoto huwa zinaruka au zinapaa
Ayubu 20
8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane;Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,

Biblia inasema akaruka mfano wa ndoto, akafukuzwa Kama maono, hii inaonyesha kwamba ndoto huwa zinaruka, na maono huwa yanafukuzwa, ndio maana mtu wakati mwingine baada ya kushituka tuu usingizini

huwa anasahau ndoto, ni kwa sababu ndoto iyo imeruka, ni sababu maono hayo yamefukuzwa, Halleluyaaaah, kwa iyo kabla ya kulala unatakiwa utamke kabisa, ndoto nazoota hazitaruka kabla ya kuzikumbuka

katika jina La Yesu, nipatapo maono hayatafukuzwa katika jina la Yesu nazungushia maono yangu ukuta wa damu ya Yesu.

2. Shetani kuiba ndoto

Yohana 10
10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

shetani anajua kabisa hii ndoto huyu akipata siri zangu zitajulikana, akizijua anajua huyu mwombaji ataniangamiza , shetani hapendi siri zake zijulikane, maana anajua kabisa ukishajua nini utafanya, ndo mana anafanya

vita na wewe ili usikumbuke ndoto, ili ndoto zipae, ili ndoto ziruke, kwa iyo anaiba kile ulichokiota anakizuia, ndo mana ni muhimu kabla ya kulala upambane na wanaoiba ndoto, upambane na wanaozuia usiote,

upambane na wanaofanya usahau ndoto, huwa tunapambana nao kwa damu ya Yesu

3.Ukiamka katika ndoto huandiki ndoto uliyoota

Habakuki 2
2 BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.
3 Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.

wakati mwingine huwa unakumbuka, ulichoota, Ila badala ya kuamka kukiandika kwanza mahali, huwa tunarudi kulala tena mara ya pili, matokeo yake ukiamka mara ya pili hukumbuki, umesahau, na wakati

mwingine unaota ndoto nyingine, kwa iyo ile ya pili inafuta ndoto ya kwanza, kabla ya kulala ni muhimu kujitamkia kabisa mimi sitalala baada kuota ndoto nitaamka na kuiandika na kuomba, Sababu usipotamka

wachawi wanakutamkia matukio au mazingira wanasema kabisa akiamka ndotoni, asiandike bali aendelee kulala, kwa iyo haya ni matukio kabisa yanatamkwa na kutengezwa katika ulimwengu wako wa

roho na wewe unafuata, yalipandwa na kupangwa kutokea, huwa haitokei bahati mbaya tuu, wewe kuamka kusahau ndoto, wewe kushituka baada ya kuota ndoto kisha kurudi kulala, wewe kushituka kukumbuka

ndoto kisha kushindwa kuomba. ni matukio ya kichawi haya yamepandwa juu ya maisha yako. ili usivuke, na wamechija damu ya kondoo, Damu ya kuku, damu ya mbuzi, juu ya huo mchoro ili ukamilike kwako, bila

kuomba utakuwa ukifuata au ukiishi kwenye Ramani ya wachawi,futa ramani za wachawi kwa damu ya Yesu, wakisha kukuweka kwenye ramani yao , unashangaa inatokea kama vile walivyopanga, inatokea kama vile

walivyonuiza, Halleluyaaaah, Bwana Yesu asifiwe sana, ndio maana huwa tunafuta
matukio ya kichawi kwa damu ya Yesu tunapoamka, lakini bahati mbaya tunasahau kufuta matukio ya kichawi, ramani za

kichawi kabla ya kulala. Halleluyaaaah, ungelikuwa unafuta haya yasingekufika
Bwana Yesu asifiwe sana, Sasa embu tuangalie kwa undani kwa nini shetani awekeze nguvu zake kwenye mlango wa

ndoto na maono, na kwanini Mungu autumie mlango wa ndoto? mpaka sasa utakuwa umegundua katika Roho Mtakatifu kuwa ndoto ni chanzo cha;

i.baraka
ii.au laana

*laana.*

Mwanzo 40
16 Mkuu wa waokaji alipoona ya kwamba hiyo tafsiri ni ya mema, akamwambia Yusufu, Mimi kadhalika nilikuwa katika ndoto yangu, na tazama, ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa changu.
17 Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kazi za mwokaji; ndege wakavila katika ungo juu ya kichwa changu.
18 Yusufu akajibu, akasema, Tafsiri yake ndiyo hii Nyungo tatu ni siku tatu.
19 Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako.
20 Ikawa siku ya tatu, siku ya kuzaliwa kwake Farao, akawafanyia karamu watumwa wake wote; akakiinua kichwa cha mkuu wa wanyweshaji, na cha mkuu wa waokaji, miongoni mwa watumwa wake.
21 Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, naye akampa Farao kikombe mkononi mwake.
22 Bali akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyowafasiria.

unaweza kuona mkuu wa waokaji kifo chake kilianzia kwenye ndoto, laana ya kifo ilianzia kwenye ndoto. baada ya kuota ingawa aliota fumbo lakini manake ilikuwa kifo chake mwenyewe na baadaye alikufa. ila

kama angelikuwa na ufahamu wa leo hii angebatilisha kwa damu ya Yesu, lakini ilitokea ili tujifunze kizazi hiki. ukiisha elewa hapa hutashangaa,ukiona mtu kuumwa baada ya kuota ndoto, hutashangaa mtu

kufilisika baada ya kuota ndoto, pia hutashangaa magomvi kwenye ndoa kuamka baada tuu ya mtu kuota ndoto, hutashangaa mtu kukosa wateja baada ya kuota ndoto, ni sababu lango la ndoto

linaweza kupitisha laana, linaweza pia kupitisha baraka.Halleluyah, sasa tuangalie upande wa baraka, Sura iyoiyo ya 40.

Mwanzo 40
9 Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu.
10 Na katika mzabibu mlikuwa na matawi matatu, nao ulikuwa kana unamea, unachanua maua, vishada vyake vikatoa zabibu zilizoiva.
11 Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.
12 Yusufu akamwambia, Tafsiri yake ndiyo hii. Matawi matatu ni siku tatu.
13 Baada ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako, atakurudisha katika kazi yako; nawe utampa Farao kikombe mkononi mwake, kama desturi ya kwanza, ulipokuwa mnyweshaji wake.
14 Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.

Hapa tunaona ndoto *imemrejesha kazini mnyweshaji mkuu* hapa lango la ndoto limepitisha habari njema, kwa iyo uyu mnyweshaji mkuu, taarifa ya kurudishwa kazini kaipata kwenye ndoto, Halleluyaaaah

ukishaelewa haya mambo utajua kwanini shetani anafanya vita mlango wa ndoto na maono. Tuangalie mfano mwingine nini lango la ndoto linaweza pitisha.

Mwanzo 12
7 BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea

ona hilo neno Bwana akamtokea Ibrahimu akamwambia uzao wako nitawapa nchi hii. ahadi ya Mungu kwa Ibrahim ilikuja kupitia mlango wa ndoto. Halleluyaaaah, taifa la Israeli lilianza kwenye ndoto. Halleluyaaaah

2 Nyakati 1
6 Sulemani akaipandia huko madhabahu ya shaba mbele za BWANA, iliyokuwako hemani pa kukutania, akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
7 Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe.
8 Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake.
9 Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.
10 Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?
11 Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao;
12 basi hekima na maarifa umepewa; nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.

Suleimani alipewa utajari, hekima, na maarifa kupitia ndoto, angalia hapo juu mstari wa 7 inasema Usiku ule Bwana akamtokea Suleimani. kila kitu alichokuwa nacho Suleimani alikipata au alikipokea kwa

njia ya ndoto, Halleluyaaaah, sasa fikiria labla aliyemtokea Suleimani si Mungu, manake Suleimani angepokea vitu tofauti kabisa, ndo mana adui haji kwa sura yake ili umuone,anakuja na sura ya mtu mwingine,

anakuja kwa sura ya wanyama, anakuja kwa sura ya ndege, anakuja kwa sura ya mtu ambaye unamfahamu, na wewe pasipo kuomba unakuta huelewi. kumbe ndotoni umepokea balaa, umepokea kushindwa,

umepokea aibu, umepokea kufutwa kazi na hukuelewa, Halleluyaaaah, si Suleimani tuu wako wengi sana.

Mwanzo 28
10 Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani.
11 Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale.
12 Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.
13 Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.
14 Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.
15 Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia.
16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.

tunaweza kuona pia hapa Yakobo kupita ndoto kuna mambo mazuri alipokea toka kwa Bwana, alipokea ulinzi, alipokea utajiri, alipokea umiliki wa ardhi, alipokea baraka, alipokea ushindi. Halleluyaaaah..., Bwana

Yesu asifiwe, alifanya agano na Bwana kupitia ndoto, ndo mana wakati mwingine ukitoka ndotoni huwa tunavunja maagano yote ya giza Halleluyaaaah ili yasianze kutufuatilia, pia Mungu hutumia ndoto kuwaonya adui zetu...

Mwanzo 20
2 Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara.
3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.
4 Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki?
5 Je! Hakuniambia mwenyewe, Huyu ni ndugu yangu? Na mwanamke mwenyewe naye alisema, Huyu ni ndugu yangu. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kuwa safi mikono yangu, nimefanya hivi.
6 Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.
7 Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.

Ibrahim alitaka kunyanganywa mke Mungu akamtokea Abimaleki katika ndoto akamtishia utiisho mkuu, Abimaleki akamrudisha mke wa watu. Mungu hutumia ndoto kuwatisha adui zetu. Chukua ufunuo

huu ukiona mtu anaingilia ndoa yako omba Mungu ampelekee utisho kupitia ndoto. omba Mungu ampelekee adui yako utisho kupitia ndoto naye atakuwa mdogo zaidi ya piriton Halleluyaaaah. mifano ni mingi sana

hatuwezi kumaliza. lakini pia Mungu hutumia ndoto kukufunulia siri za adui, na kukupa tumaini,

Waamuzi 7
7 BWANA akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake.
9 Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako.
10 Lakini, ukiogopa kushuka, shuka pamoja na Pura mtumishi wako kambini;
11 nawe utasikia wanayoyasema, na baada ya haya mikono yako itatiwa nguvu; ushuke kambini. Ndipo akashuka pamoja na Pura mtumishi wake hata kufikilia mwisho wa watu wenye silaha waliokuwa kambini.

☆☆☆ Tunaona hapa Gidioni anapewa mbinu za kumshinda adui

Waamuzi 7
12 Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia zao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi.
13 Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, naliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hata ikaanguka, nao ukaipindua, hata ikalala chini.
14 Mwenzake akamjibu akasema, Habari hii haikosi kuwa upanga wa Gideoni, mwana wa Yoashi, mtu wa Israeli. Mungu amewatia Wamidiani na jeshi lote katika mkono wake.
15 Ikawa, aliposikia habari ya ile ndoto, na kufasiriwa kwake, akasujudu; akarudi katika jeshi la Israeli akasema, Inukeni, kwa maana BWANA amelitia jeshi la Midiani mikononi mwenu.

☆☆☆Gidion hapa baada sasa ya kutoka katika ndoto baada ya kufuatilia anajua kuwa kumbe adui zake hawana lolote hawana chochote, na kumbe wanamuogopa Halleluyaaaah. upande wa Gidioni Mungu

kampa ndoto ya matumaini, upande wa adui Mungu kawaletea ndoto ya utiisho Mkuu. Halleluyaaaah, Mungu akikupa ndoto ya matumaini utapata nguvu kuu, utapata ujasiri wa kuendelea mbele. wakati

mwingine unapopata hofu, mashaka, woga, wasiwasi Omba Mungu akuletee ndoto ya matumaini. Halleluyah Bwana Yesu asifiwe.

☆hilo ni somo la ndani kabisa, soma kwa kurudia usisome haraka haraka kuna vitu vikubwa Roho Mtakatifu atakufunulia. huku tukiendelea kusubiri maombi yanakuja....

Muhimu: 
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia  tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo 

josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506

#Mtumishi Joseph Ntandu
#Wanamaombi Group

Comments

  1. Nabarikiwa sana Mtumishi kwa masomo yako

    ReplyDelete
  2. Somo zuri sana hili mtumishi wa Mungu,barikiwa sana.

    ReplyDelete
  3. kama ungependa kuokoa uhusiano/ndoa yako basi nitakupendekeza kwa Dk Dawn. alinisaidia kurejesha nyumba yangu baada ya miezi 11 ya utengano mkali kati yangu na mume wangu. Nilielekezwa kwake na dada yangu mkubwa wakati ndoa imeisha, akarudisha amani na furaha katika ndoa yangu, pia amesaidia marafiki zangu wengine na wanaishi kwa furaha kwa msaada wa Dk Dawn,
    Wasiliana naye ikiwa unahitaji usaidizi wa kurejesha uhusiano/ndoa yako/ ikiwa unataka kupata mimba au kuponya aina yoyote ya ugonjwa:
    Dk Dawn hatawahi kukukatisha tamaa:
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
    WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete
  4. Ujumbe mzuri sana ukiusoma kwa makini ... Asante sana

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA