VITA VYA MIUNGU KWENYE NAFSI
Somo: *Vita vya miungu kwenye nafsi*
Halleluyaaaah
Bwana Yesu asifiwe
Miungu wakati mwingi huwa inafanya kazi kinyume chako kwa njia ya siri sana, kwa hila sana, na wakati mwingine unaweza fikiri wewe ndo unamatatizo kumbe miungu imekukalia, katika jambo ambalo linawapa watu tabu basi ni hili, *mimi nimeokoka miungu itanikalia vipi?inapataje nguvu juu yangu na ikiwa nimeokoka?* , mpendwa mmoja alikuwa anamuomba Mungu amuondolee hasira, kila akiomba anaona katika ndoto anaongea na marehemu babu yake, kila akiomba baada ya wiki anapata hasira, kisha anamuuliza Mungu why? badaye Mungu akaja akafunua akambiwa babu yako alimwaga damu isiyokuwa na hatia,Kwa iyo adhabu ya kisasi malipizi hasira zipo juu ya ukoo wenu, hiyo damu iliyomwagiga damu, inanena kisasi malipizi na hasira juu Yenu, nikamwambia Mungu anapokuleta sura ya babu yako anataka ushughulikie chanzo, Jina la Bwana libarikiwe, iimeandikwa:
Maombolezo 5
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako;Na sisi tumeyachukua maovu yao.
☆unaweza kuona waliotangulia wametenda dhambi, wakafa baada ya kufa waliobaki wamechukua adhabu yao. iyo ni Mungu amesema si mimi.
Kutoka 20
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao.
☆anasema nawapatiliza yani nitalipiza kwa ajili ya baba zenu kunitenda uovu kuanzia kizazi cha kwanza hata cha nne, kama Karne moja ina miaka 100, kwa iyo ikiwa kuna babu zako au bibi zako. Walitenda uovu ndani ya miaka 400 kuanzia kwako kurudi nyuma.Uovu huo au adhabu iyo bado inaweza kukufuatilia ikiwa hukuchukua hatua. Halleluyaaaah! Sasa mapepo au mashetani ambayo yanakalia ukoo, familia, miungu inayomiliki ukoo yanatafuta huu ukoo una laana gani? kwenye d.n.a ya hawa huwa kuna kitu gani? kisha wanapatiliza laana iyo ifanye kazi kwako, ukitaka kujua huo ukoo au hiyo familia au ilo kabila lina laana gani?, wewe angalia kuna tabia gani kwenye huo ukoo, au nini kinawafuatilia kwenye huo ukoo?, usishangae kuona ukoo huo ni walevi sana, ukoo huo wanaugua wanasumbuliwa kisukari, h.i.v, blood pressure,cancer ndo magonjwa yanayochukua watu wakiwa bado wana nguvu au hufa na ajali ya gari sana,au huwa hawavuki miaka 40,wasomi wote wanakuwa vichaa,negative unayoiona kuhusu ukoo basi iyo ndo type ya mashetani yanayotawala huo ukoo, Bwana Yesu asifiwe.
Yohana 14
8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha.
9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
☆Yesu akasema aliyeniona mimi amemwona Baba, manake ukitaka kujua Baba yukoje mwangalie Yesu, ukitaka kujua Yesu atakuwaje mwangalie Baba.
Ezekiel 16
44 Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake.
☆Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake, ukitaka kujua binti akiwa mtu mzima atakuwaje basi muangalie mama yake yukoje sasa. ukitaka kujua maisha ya mtu ya badaye yatakuwaje mwangalie baba au mama yake hiyo itakupa picha halisi. kwa aliyeokoka ni zaidi ya hapo, imeandikwa hata mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya tazama ya kale yamepita nayo yamekuwa mapya. Kama jinsi tulivyoona baadhi ya matukio katika familia ya Ibrahim, hivyo hivyo kuna mambo ambayo wewe mwenyewe huyataki ila unashangaa unayafuatisha ingawa umeokoka, hiyo ndiyo inaitwa *vita vya miungu kwenye nafsi* miungu ya familia inasoma historia ya familia yako kisha iyo historia inairejesha kwako, unashangaa bibi aliachwa na mume, mme akaoa mke mwingine, mtoto aliachwa na mme akaoa mke mwingine, mjukuu naye hivyo hivyo, kitukuu naye vikao haviishi vya usululishi, na wote wameokoka, wapo mashetani ambao, wao wanafuatilia DNA ya ukoo, au gene ya familia au damu ya familia, kisha wanaleta mabaya. Embu tuangalie mfano mwingine....
Mwanzo 4
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
☆Damu ya Habili ilinena kisasi juu ya kizazi cha kaini, ilinena utasa na mapooza katika uchumi wa kizazi cha kaini. na unaposoma maandiko kitabu cha mwanzo utagundua ni kizazi cha kaini ndicho kilikuwa na maovu na kumuasi Mungu kilitoka kwenye kiuno cha kaini. wajukuu wa Nuhu kama unakumbuka walilaaniwa na Baba yao Hamu. Na Nuhu alitoka kwenye kizazi cha kaini. Najaribu kukuonyesha jinsi ambavyo mashetani ya ukoo, miungu ya ukoo inavyoweza kukuleta kitu kibaya inavyoweza kukuletea historia ya kwenu na kuitumia kukukwamisha kabisa.
Mwanzo 9
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
TUANGALIE JINSI HISTORIA ILIVYOMKWAMISHA MUSA KUINGIA KAANANI.
Mwanzo 49
5 Simeoni na Lawi ni ndugu;Panga zao ni silaha za jeuri.
6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao,Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao,Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu,Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ngombe;
7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali,Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.Nitawagawa katika Yakobo,
Nitawatawanya katika Israeli.
☆Ukisoma hii sura ya 49, Mzee Yakobo mjukuu wa Ibrahim alipokuwa mzee aliwaita watoto wake na kuwapa husia, alipofika kwa lawi aliwaelezea jinsi ambavyo hasira zitawagharimu, Yakobo alizungumza akisema katika ghadhabu yao walimuuwa mtu na kweli Musa alikuwa mlawi alimuuwa mtu na kukimbia ukisoma kutoka 3 yote na kuendelea,Pamoja kuwahusia akatamka maneno magumu ghadhabu yao akasema "Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana haina huruma". Mama yake na Musa alitokea kwenye hiko kizazi chenye hasira. Hata ukichunguza utumishi wa Musa, Musa alisumbuliwa na hasira. ikafika sehemu akashindwa hata kuyafanya mapenzi ya Mungu sababu ya hasira. Embu tuone.
Kutoka 15
24 Ndipo watu wakamnungunikia Musa, wakisema, Tunywe nini?
25 Naye akamlilia BWANA; BWANA akamwonyesha mti, naye akautia katika hayo maji, maji yakawa matamu. Basi akawawekea amri na hukumu huko, akawaonja huko;
26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
☆Hii ni mara ya kwanza wana Wa Israeli walimnungunikia Musa, Musa akawavumilia, tuangalie mara ingine ilikuwaje....
Hesabu 20
3 Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za BWANA!
5 Na mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya kunywa.
6 Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea.
7 BWANA akasema na Musa, akinena,
8 Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao.
10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?
11 Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.
12 BWANA akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa.
☆Mara ya pili Musa alikasirika kwa sababu ya manunguniko na malalamiko ya wana wa Israeli, Musa aliambiwa na Mungu uwambie mwamba huu utoe maji yeye kwa hasira akawaita wana wa Israeli waasi, kisha kwa hasira hakuwaambia mwamba utoe maji bali yeye akaupiga na ile fimbo yake,alifanya kinyume na maagizo ya Mungu kwa kuliheshimu jina lake Mungu akayatoa maji katika mwamba ule. Musa kwa hasira aliwahi kuvunja amri kumi za Mungu, Musa alitawaliwa na hasira, Musa kwa hasira aliwahi kuuwa mtu m'misri akakimbia kesi, Musa alitokea katika kizazi cha akina lawi, ambacho Yakobo alisema wamelaaniwa kwa hasira. ni watu wenye ghadhabu nyingi, mwisho wa siku Musa na Haroon hawakufika kaanani, Hasira ilimzuia Musa asifike kaanani, udhaifu wa Musa ulikuwa ni hasira, mimi na wewe tunajua udhaifu wetu, wengine wanaridhi kiburi, wengine wanarithi zarau, wengine wanarithi kujikweza, wengine wanarithi kujiinua, wapo wanaorithi ubishi,wengine wanarithi magomvi, wengine ulevi, wengine tabia ya umalaya, wengine magonjwa, wengine wanarithi umasikini, haijalishi sasa ukoje au una hali gani? jinsi alivyo mama yako au alivyokuwa ndivyo nawe utakuwa hivyo ivyo, jinsi alivyo baba yako nawe utakuwa ivyoivyo ikiwa hutakuwa ndani ya Yesu. Na ndo mana ukitaka kubadili historia lazima uingie ndani ya Yesu lazima uokoke, unapooka Yesu anapokuzaa rohoni basi hapo unazaliwa mara ya pili,anakuzaa kwa imani ya wokovu unaanza kuwa kiumbe kipya sasa na ya kale yamepita nayo yamekuwa mapya. miungu ina njia nyingi za kupambana na wapendwa kupitia nafsi
i.kujiinua kinyume na Elimu ya Mungu ndani ya nafsi
☆wakati mwingine mtumishi wa Bwana kwa mfano anaweza kuwa analeta ujumbe wa neno la Mungu. Huku moyoni miungu inaanza kuongea na wewe unasikia
~uyu mtumishi anakuchukia
~ana kuonea wivu
~anakufuatilia
~anakuchunguza
~hataki uvuke
~anakuombea vibaya
~anataka umtegemee
~hapendi uwe juu yake
~tatizo lake ni hasira
~anapenda kuhukumu watu
#moyoni yanakuja kama mawazo yako bila kuyachuja na wewe unayachukua, kumbe miungu inakuwekea hayo mawazo. akupangue usikutane na msaada wako,icho ndicho kinachotokea hata mtu ana left group wakati mwingine akisukumwa na miungu ya familia, kuna vile anasikia ndani yake. kumbe miungu inampiga vita. na kumpangua.
ii.Kupofusha fikra zako
☆ukishapofushwa fikra zako kinachofuata ni kufuata maagizo ya shetani, kutokuamini tena maandiko, kutoyaelewa tena maandiko,kutokuona tena mambo ya rohoni, kutokuona njia unaanza kusolve mambo mbalimbali kimwili si kiroho tena.
iii.kupotosha fikra zako
☆Kila lililo jema miungu inakutafsiria ni baya, inakupa wrong information about everything.
iv. kukutia uzito
☆uzito wa kumsikia Mungu
☆uzito wa kumtii Mungu
☆uzito wa kutokuchukua hatua
☆uzito wa kuamua
v.kupambana na imani yako ili usiamini
☆ile hali ya kukata tamaa
☆kukuyumbisha unachoamini ili uache kukiamini
Halleluyaaaah! miungu ya ukoo huwa inafuatilia d.n.a ya mtu, au gene ya mtu, au damu ya mtu! Halleluyaaaah! na kuleta yale mambo ambayo huwa yanatembea kwenye ukoo wenu, mashetani huwa yanatambua d.n.a katika ulimwengu wa roho, wakiona damu flani tuu wanajua hii damu ina d.n.a ya kichagga ni damu ya akina Urio wa kule uchagani rombo, kwa mfano, hawa d.n.a yao Inasoma
~damu ya magonjwa
~damu ya kuachwa katika ndoa
~damu ya umasikini
~damu ya kufilisika na kurudi nyuma
~damu ya hasira
~damu ya uwizi
~damu ya kutapanya mali
~...
☆mtoto yoyote akizaliwa ndani ya akina ukoo wa akina Urio kwa mfanobhuwezi mkosa na izo element,atakuwa na tabia izo tu... salama yake aokoke kisha avue mavazi ya miungu na mizimu avae asili yake Yesu. Ni damu ya Yesu pekee inayoweza kufuta maagano ya kwanza na kusimamisha ya pili, agano jipya la damu ya Yesu, si agano la mizimu, damu ya Yesu inanyamazisha damu za ajabu ajabu katika d.n.a ya ukoo wako. Halleluyaaaah!
2 Timotheo
5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
☆ Hapa mtume Paulo alimwandikia barua Timotheo akimwambia una imani lakini imetokea kwa bibi yako. Halleluyaaaah. just imagine sasa bibi yake Timotheo angekuwa na kitu kibaya cha uwizi kwa mfano ingekuwa timotheo ni Mtumishi wa Bwana lakini roho ya uwizi inamsumbua. hivyo ndivyo miungu inavyofanya vita wapendwa, na kuwafunga, na kuwatesa watu, au bibi yake timotheo angekuwa na damu ya uhuni, ile miungu ingechukua laana ya uhuni na kupambana na kumsukuma Timotheo ili awe muhuni unakuta ni mtumishi wa Bwana lakini ni muhuni unamsumbua.Halleluyaaah
*endelea kutafakari ujumbe huu
*maombi yatafuata
*endelea kuomba neema ya ushindi katika maombi haya
Muhimu:
Mungu amenipa maono ya kwenda live kupitia radio, na televison, ili masomo haya na maombi tuyapate live, yaani audio na video tutaanza na online radio, online tv, kupitia internet, Pia tutakuwa na live prayer line ya kuhudumia watu, Mungu amesema nami kwa habari ya studio kwa ajili ya huduma iyo. Nikupe nafasi ya kupanda mbegu yako kwa ajili ya studio hiyo. Na Mungu atakukumbuka sadaka yako injili itakapoenda duniani kote. kufungua, kuponya, kuokoa, kuinua. Kama unataka kushiriki baraka hizi uko ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania. basi tumia hizo namba hapo chini kutuma sadaka yako. kama uko nje ya Tanzania tumia izo namba nitakupa maelekezo
josephntandu@gmail.com,+255713297066, +255765377506
#Mtumishi Joseph Ntandu
#Wanamaombi Group
kama ungependa kuokoa uhusiano/ndoa yako basi nitakupendekeza kwa Dk Dawn. alinisaidia kurejesha nyumba yangu baada ya miezi 11 ya utengano mkali kati yangu na mume wangu. Nilielekezwa kwake na dada yangu mkubwa wakati ndoa imeisha, akarudisha amani na furaha katika ndoa yangu, pia amesaidia marafiki zangu wengine na wanaishi kwa furaha kwa msaada wa Dk Dawn,
ReplyDeleteWasiliana naye ikiwa unahitaji usaidizi wa kurejesha uhusiano/ndoa yako/ ikiwa unataka kupata mimba au kuponya aina yoyote ya ugonjwa:
Dk Dawn hatawahi kukukatisha tamaa:
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159