*"KUONDOA MIPAKA YA KIUCHUMI (KIFEDHA) KWA DAMU YA YESU"*
✝️
*"KUONDOA MIPAKA YA KIUCHUMI (KIFEDHA) KWA DAMU YA YESU"*
Bwana Yesu Asifiwe!
Isaya 54 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako.
³ Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.
✍🏽 Nilipokuwa Katika jukumu langu la kulisha mtu wa ndani chakula!!Nikakutana na hili Andiko! Linasema IPanua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako;usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako;vikaze vigingi vya hema yako.Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.KISHA NIKAJIULIZA NAENEA UPANDE WA KUUME?!NAENEA UPANDE WA KUSHOTO!NIKAJIULIZA HEMA YANGU INAKUWA AU INAPUNGUA?!AU IMEBAKI PALEPALE!NIKAJIULIZA HEMA YANGU INATANUKA AU HAITANUKI?! Biblia inasema hivi!Kila neno la Mungu lina uhai tena lafaa kwa mafundisho!ni kupitia neno la Mungu ndipo tunapata Ufunuo!ni kupitia neno la Mungu ndipo tunapata ufahamu!kisha nikaanza kumuomba Roho Mtakatifu anifundishe zaidi.
💡Akaanza kusema nami! Akisema mimi sijazuia nyie msiongezeke! akaniambia asilimia kubwa sana vipato vyao ni kuanzia 10,000-90,000 yani (5 figures)!alafu Kuna lile kundi la 100,000-900,000 (6 figures) hili ni kundi la katikati.Alafu lipo kundi linalofuatia 1,000,000-9,000,000 (7 figures) hawa ni wachache si wengi na pengine ni 10% tuu! Kisha kundi linalofuatia ni 10,000,000-90,000,0000 (8 figures) hapa idadi inazidi kupungua sana! Inawezekana ni asilimia 5% tuu.kisha Kuna kundi la juu kabisa 100,000,000-900,000,000 (9 figures) Hawa inawezekana ni kati ya asilimia 2%-4% ya kundi lote!kundi la mwisho ni wale wa 10 figures!nao labla ni asilimia 1% tuu.
*➡️ ROHO MTAKATIFU NDIE MWENYE PASSWORD (SIRI) YA KUTOKA KUNDI MOJA! KUELEKEA KUNDI LINGINE!*
*— Isaya 48:17 (Biblia Takatifu)a*
“Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
”
✍🏽Sasa kama Roho Mtakatifu ndiye ongezeko lenyewe sasa kwanini hatuongezeki?! Kwanini hatutoki kundi Moja kwenda kundi ?lingine?!Kwanini mtu anakaa kwenye kundi Moja zaidi ya miaka 10! Kwanini mtu akitaka kuvuka anarudi nyuma?!Biblia iko wazi hapo juu! Isaya 48:17 anasema hivi mimi ni Bwana Mungu wako nikufundishaye upate faida! Ukishasikia neno kufundishwa jua hapo panapatikana maarifa! Panapatikana hekima!💡Unajua hauwezi kufanikiwa nje ya maarifa uliyonayo!hauwezi kufanikiwa nje ya taarifa ulizonazo!Hapo ulipo ni sababu ya kiwango cha Elimu ya Mungu uliyonayo.Iwe Elimu kuhusu uchumi!iwe Elimu kuhusu Imani.Jina la Bwana libarikiwe!Mfano kupitia Isaya 54:2-3! Ndipo nikapata Ufunuo na kutambua kuwa kumbe Kuna zuio au mpaka wa mtu kuongezeka kikipato.Cha pili tulichokiona kwenye Isaya 48:17! Anasema nikufundishaye njia ikupasayo kuifuata!Kumbe si tuu kuwa na Elimu ya uchumi!kumbe si tuu kuhudhuria training!kumbe si tuu kuhudhuria seminar mbalimbali!bali Kuna kuongozwa na kukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu! Nazungumzia kumsikia Roho Mtakatifu Kila anachosema na wewe! Nazungumzia kumtii Roho Mtakatifu Kila anachosema na wewe!Kuna wakati Elimu tunayopata inaweza sababisha kiburi cha uzima cha kutokufundishika!kutokuongezeka!Wakati mwingine njia ya Mungu hatuitaki bali tunatamani tupitie njia yetu tunayotaka!tunatamani tupitie njia ya watu wengine ya mafanikio.KUMBE KILA MTU KAANDALIWA NJIA YAKE.Halleluyaaah! Bwana Yesu Asifiwe.
✍🏽Roho Mtakatifu ndiye anayejua ufanye nini ili fedha yako ikae!Roho Mtakatifu ndiye anayejua ufanye nini ili fedha iongezeke!Roho Mtakatifu ndiye anayejua kwanini fedha yako haiongezeki! kwanini fedha yako inapotea!kwanini fedha yako haikuwi! Ni kitu gani kinakula fedha yako!ni kitu gani kinachozuia fedha yako isikuwe!Roho Mtakatifu ndiye mwenye siri!Roho Mtakatifu ndiye mwenye Ufunuo!➡️Huku duniani tunasema "mtoto aliye karibu na baba huyo ndie anayezijua siri za baba yake!yule mtoto mwenye mahusiano mazuri na baba yake huyo ndiye atakayefundishwa siri za kufanikiwa!Na yule mtoto mwenye kumsikia baba yake! Na kumtii baba na kufuata vile baba yake anavyotaka huyo ndiye baba yake humpenda na kumpa Kila kitu.Tena humpendelea Halleluyaaaah!IKO HIVYO HIVYO KWAKO WEWE NA MUNGU ALIYEHAI!Wengi hatuna mahusiano mazuri na Mungu aliyehai.Mahusiano mazuri huletwa na mawasiliano mazuri! *Nini maana ya mawasiliano!* Mawasiliano maana yake mimi naongea unanisikiliza.Wewe unaongea nakusikiliza!tunafikia sehemu ya kukubaliana la kukubaliana.Then yale tusiyokubaliana tunafikia sehemu ya kukubali kutokukubaliana.JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
*➡️FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA MUNGU SI MALI YA SHETANI:*
*— Hagai 2:8 (Biblia Takatifu)*
“Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.
”
✍🏽Ikiwa fedha ni Mali ya Mungu?!Si Mali ya shetani!!Na sisi tulio okoka tulio ndani ya Kristo tuu watoto wa Mungu!💡Sasa ni kwanini hatuna maongezeko?!kwanini tunakwama wakati fedha ni Mali ya Baba yetu?!kwanini wanaoisujudia miungu hata kwa kuuza nafsi zao na uhai wao kwa shetani wanapata Maongezeko!kwanini sisi hatuongezeki!WHY?!
*➡️MUNGU ANATAKA VITU VIWILI VIKUBWA ILI ROHO WAKE MTAKATIFU AKUHUDUMIE*
1.Mahusiano ya kweli ya Baba na mtoto.
*Kumbukumbu la Torati 6:5 (Biblia Takatifu)*
“Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
”
✍🏽Unampendaje Mungu?! Unampenda kwa kulishika neno lake na kulitii.Hauweki mipaka ya kusikia na kutii.Hauchagui cha kusikia na kutii.
2.Kuyafanya mapenzi ya Mungu.
*— Yohana 6:38 (Biblia Takatifu)*
“Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
”
✍🏽Wengi kwenye maamuzi na uchaguzi huwa hujikuta kwenye majaribu!wanashindwa kufanya mapenzi ya Mungu na hukimbilia kufanya mapenzi ya adui au mapenzi ya nafsi zao.
💡BAADA YA MAHUSIANO MAZURI NA UTII KWA MUNGU NDIPOSA SASA UKIMGEUKIA SHETANI UKIMNGOA ANANGOKA!UKIAMURU ARDHI NA MBINGU ZAKO ZIACHILIE ONGEZEKO ZITAACHILIA.SHIDA SI SHETANI!SHIDA SI WATESI NA ADUI ZAKO!SHIDA SI WACHAWI!NO! Shida ni kufanya mapenzi ya Mungu!Shida ni mahusiano yako mabaya uliyonayo na Mungu wako.Maana wengi tunampenda Mungu si kwa sababu alivyo kwetu! No! Ni kwa sababu ya vitu vyake!Wengi tunampenda Mungu sababu ya baraka zake!Si kwa sababu ana huruma!Si kwa sababu amejaa Rehema!Si kwa sababu yeye ni mwaminifu!Si kwa sababu ana upendo!Jina la Bwana libarikiwe!Badala ya kutengeneza mahusiano na yeye!Tunajenga mahusiano na baraka zake naye tunamweka pembeni.*Tutaenda kumlingana Mungu! Naye atasikia naye ataturejeshea roho ya mafanikio na maongezeko ambayo iliondolewa kwetu*.JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
💥part B inakuja na maombi Endelea kutafakari
#.Wanamaombi Online Ministry
#.Mtumishi Joseph Ntandu
#.0765 377506 0713 297066
*©W.O.M-2023*
Comments
Post a Comment