UPONYAJI WA UCHUMI
✝️
Day 1️⃣
*"KWA KUPIGWA KWAKE NIMEPONA TOKA KWENYE MADENI"*.
✔️Isaya 53 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
⁵ Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,*Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.*
(Kusudi usifanye makosa uliyoyafanya huko nyuma ulipokuwa unaombea madeni yako!✍🏽kubali kupokea maarifa toka kwa Roho Mtakatifu,neno la Mungu linaweza kuwa lilelile lakini *Roho Mtakatifu anapolihuhisha haliwi lilelile*,Mpe nafasi Roho Mtakatifu atamtukuza Yesu kupitia adeni yako.)
*➡️MASWALI MUHIMU SANA YA KUJIULIZA KABLA YA KUOMBA MSAADA WA MUNGU:*
✍🏽Kwa habari ya madeni!
*1️⃣Nimefikaje hapa katika hali ya madeni!kabla ya kuingia katika haya madeni nini kilinisukuma nikope?!*
✅Nimekopa ili kufuta madeni ya nyuma?!
✅Nimekopa ili kufanya maendeleo?!mf.kununua asset!!
✅Nimekopa ili kuwasaidia watu wa karibu?!
✅Nimekopa kwa kufuata mkumbo?!
✅Nimekopa ili kujitibia au wengine watibiwe (magonjwa)
✅Nimekopa kwa ajili ya kodi!ada!matumizi binafsi?!
✅Nimekopa ili kununua vitu vya starehe vya gharama?!
✅Nimekopa ili kupata mtaji au kuongeza mtaji wa biashara?!
✅Nimelazimika kukopa sababu ya kupungukiwa na kuishiwa!(sababu ya matumizi mabaya ya fedha).
*2️⃣Nini kimenisukuma niingie katika haya madeni,au wazo la kukopa limetoka wapi?!*
⏸️Kwa Roho Mtakatifu?!
⏸️kwenye nafsi yako (moyo)?!
⏸️miungu ya ukoo & familia inayokufuatilia?!
*🆗Kama ni Roho Mtakatifu! Je alikupa Ishara?!Je alithibitisha kuwa yupo pamoja na wewe katika kukopa kwako?!*
✔️alikupa ishara kuwa atakuwa pamoja na wewe?!
✔️alikupa neno kukuhakikishia kuwa atakuwa pamoja na wewe?!
✔️Alikupa amani na kukudhibitishia kuwa yupo pamoja na wewe?!
*✔️Je hukutumia akili zako katika kukopa?!hukushauriwa na watu?!*
▶️BAADA YA KUGUNDUA UNA MADENI HAYALIPIKI JE ULIFANYA NINI?! ILI UTOKE KATIKA MADENI!!
*️⃣Je Ulikopa zaidi ili ufute madeni?!
*️⃣Ulitafuta msaada kwa wanadamu ili wakusaidie kulipa madeni?!
*️⃣Ulitafuta msaada wa kiroho.mfano watumishi au wengine waganga?!
*️⃣Ulikimbia deni na kubadili namba ya simu au uli mblock anayekudai?!
*️⃣Ulijiongeza kwa kujiingiza kwenye uwizi na utapeli ili ufute deni ingawa haukufanikiwa?!
*✴️Case hii ya madeni je ni mara ya kwanza au imejirudia?!Kwenu kuna historia ya madeni?!*
💡Kama ni mara ya pili je mara ya kwanza ulivukaje?!
💡kama ilikuwa kiroho (maombi) uliomba deni lifutwe au roho ya madeni iondolewe?!
💡je ulishughulikia mzizi wa chanzo cha madeni hata ukapata amani kuwa roho hiyo imengoka?!
💡Baada ya ushindi wa mwisho kwa habari ya madeni ulifanya nini kwa Mungu aliyekusaidia?!
🆗Maswali haya utajiuliza na kujijibu mwenyewe! Nia yake *ni kuamsha fahamu zako ili uanze kujiuliza na kumuuliza Roho Mtakatifu nini chanzo cha madeni yako?!* Sababu watu wengi wanashindwa kuvuka sababu hawashughulikii chanzo inavyopaswa!na chanzo changu kwa mfano hakitafanana na chanzo chako.Na utajua chanzo kwa kuomba!Huwezi kuomba bila kujua unaomba nini?! na kwa sababu gani?! na Ili itokee nini.Lazima ujue unachokiomba ili ujue namna ya kuomba.*JINA LA BWANA LIBARIKIWE!*
MAOMBI:
Baba katika jina la Yesu,nasimama mbele yako kwa damu ya Yesu,na kwa jina la Yesu,katika jambo lolote ambalo halikupendezi ninatubu na kuomba Rehema,unirehemu dhambi yangu,uovu wangu na makosa yangu,Ee Bwana kila kitu kina chanzo,chanzo ya adhabu ya madeni ni mauti,iliyokuja kupitia dhambi,neno lako linasema nayo dhambi ikishachukua mimba huzaa mauti,Baba Mtakatifu ninaomba unifunulie ile dhambi iliyo malangoni,ule uovu na yale makosa ambayo kupitia hayo roho ya mauti na uharibifu "madeni" inapata uhalali,Ee Bwana umesema yaliyofichwa ni ya Mungu yaliyowazi ni ya mwanadamu,Roho wako Mtakatifu huyajua yote na huyatambua yote,hakuna lilijificha mbele yake,yeye huyachunguza yote,hata yaliyo mafumbo ya Mungu,katika jina la Yesu ninaomba sasa Ee Bwana kupitia Roho wako Mtakatifu yakachunguzwe,yakapelelezwe kwa Roho Mtakatifu nifunuliwe kwa damu ya Yesu,na kwa jina la Yesu,nikapate kuyaelewa! sababu ni ahadi yako Mungu,kuwa yaliyofichwa yatafunuliwa,yaliyositirika yatawekwa wazi.Bwana Yesu nakusihi ukafunue masikio yangu sasa na kuyatia mhuri,ukafunue macho yangu sasa na kuyatia mhuri,ukaondoe kifuniko cha giza kwenye moyo wangu katika jina la Yesu!ukayatie mhuri maneno yako kwenye moyo wangu!nikaelewe waziwazi katika jina la Yesu!ukanipe mafunuo yako Bwana Yesu ili nikapate kutubu na zije zile nyakati za kuburudishwa sawasawa na ahadi yako,Eee Bwana ukaongee kwa sauti,yenye mwangwi,na radi,na kwa kishindo na kwa waziwazi ili nikusikie na wala nisipuuzie tena wala kuyasahau hayo utakayo ongea nami.Neema yako Bwana ikapate kuwa pamoja nami,ikanifunike na kuniwezesha kuyapokea hata kama yatakuja kama upanga au moto unao yeyusha na kugawanya nafsi katika jina la Yesu,hata kama ni magumu!ee Bwana Yesu ongea nami ili nipone na kuvushwa na wewe!Maana nataka kuvuka katika jina la Yesu.Ukadhibitishe Bwana kwa ishara na miujiza na maajabu nikapate kuelewa na kuiamini sauti yako, kupitia Roho wako Mtakatifu,Neema yako Bwana isinipite!Ukanipe neema ya kupokea maelekezo na kuyafanyia kazi maagizo yako katika jina la Yesu.Katika jina la Yesu!Kwa damu ya thamani ya Yesu Kristo!Kwa damu ya agano jipya ya Yesu!Kwa damu ya mwanakondoo aliyeshinda katika jina la Yesu Kristo.Ameen
*✴️Endelea kutafakari na kuomba....*
#.Mtumishi Joseph Ntandu
#.Wanamaombi Online Ministry
#.0765 377506 / 0713 297066
*©️WOM-2025*
Comments
Post a Comment