UPONYAJI WA UCHUMI

✝️

Day 3️⃣

*"KWA KUPIGWA KWAKE NIMEPONA TOKA KWENYE MADENI"*

Isaya 53 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

⁵ Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Baba katika jina la Yesu,Baba wa utukufu na Mungu Mtakatifu katika jina la Yesu Kristo,Baba kwa damu ya Yesu ninakuja kwako,kwa damu ya Yesu ninasogea kwako! Kwa jina la Yesu! unirehemu unisamehe!Neno lako linasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa!Ee Bwana lolote lisilo kupendeza naungama natubu na kuomba Rehema,Rehemu uovu wangu,dhambi zangu na makosa yangu kwa damu ya Yesu,na kwa jina la Yesu uyafute maovu yangu,dhambi zangu,na makosa yangu nakusihi!Rehemu mawazo yangu,matendo yangu na maneno yangu ambayo yamekuwa kinyume kabisa na mapenzi yako.Baba Mtakatifu uchumi wangu unaumwa,mikono yangu inaumwa,hatua zangu zinaumwa,nimekimbilia kwako kwa kuwa kwako kuna uponyaji,mikono yangu na fedha yangu inazaa mapooza,inazaa utasa,inazaa uharibifu,inazaa mauti!ninatubu na kuomba Rehema,yamkini nimerithi laana toka tumbo la uzazi la mama,nimerithi laana toka kiuno cha uzazi cha baba,na laana hizo zinaachilia mauti,laana hizo zinaachilia uharibifu,laana hizo zinaachilia mapooza,laana hizo zinaachilia utasa,laana hizo zinasukuma wachawi na washirikina kunuiza na kutamka mabaya matokeo yake,yale nilitakiwa niyafanye siyafanyi,Matokeo yake sifundishiki kwa habari ya uchumi na fedha,sikusikii kwa habari ya uchumi na fedha,sikuelewi Mungu kwa habari ya uchumi na fedha,sioni vizuri kwa habari ya uchumi na fedha,hauoni mabadiliko baada ya kunifundisha au kunionya linapokuja swala la uchumi na fedha sababu ya kufungwa na laana,laana imesababisha kukataa wito wako Mungu kama Yona na sababu hiyo nazuia uwepo wako kwa habari ya uchumi na fedha yangu,Ee Bwana hata ukinipa mafunuo siyaombei kwa msaada wa Roho Mtakatifu sababu ya laana iliyosimama kwenye uchumi na fedha imenifunga,Laana imejeruhi moyo wangu hata ninapotaka kuomba kwa habari ya uchumi na fedha ninashindwa Bwana Yesu,Laana inasababisha mimi kutokuwa na moyo wa shukrani na kutodhamini baada ya wewe Mungu kulituma neno lako kwa habari ya uchumi na fedha,Laana imeniletea kujihesabia haki hata nikiweka nadhiri naona ni sawa kutoitengua,hata baada ya Mungu kunivusha,laana imeuwa  bidii katika  kuomba hadi kuvuka! laana imefunga akili yangu na ufahamu wangu,utayari wangu,nguvu za kuomba laana imeharibu!hata nikiomba sifikii mwisho wa ushindi,Laana imenisukuma kuambatana na watu wasio sahihi kwenye kusudi uliloniitia Bwana Yesu,nao wamekuwa mwimba na uvuli mbaya kwangu na kwenye wito huu ulioniitia,Baba natubu na kuomba Rehema,Laana imenikosesha hata kwa habari ya utoaji wa sadaka,namna ya kutoa,jinsi ya kutoa,mahali pa kutoa akili na ufahamu umefungwa,Baba natubu na kuomba Rehema,unirehemu unisamehe,laana imefanya mbingu zangu kuwa shaba na ardhi yangu kuwa chuma na mambo ya uchumi yamezidi kuwa magumu,laana imefungua juu ya kichwa changu mvua ya mchanga na mavumbi juu yangu,laana imefunga mvua za vuli na za masika za baraka,Baba natubu na kuomba Rehema,Unirehemu unisamehe,laana imesababisha kuwa mkopaji badala ya mkopeshaji,laana imesababisha kupanda mbegu nyingi lakini kuvuna vichache,laana imesababisha nipigwe mbele ya adui zangu na watesi wangu linapokuja swala la uchumi na fedha,laana imesababisha mimi kuweke fedha yangu katika mifuko iliyotoboka,laana imesababisha yule alaye kula uchumi wangu,na kuharibu mazao ya shamba langu,na kupukutisha matunda kabla ya wakati wake,laana imesababisha kwa habari ya uchumi na fedha hatua zangu kwenda katika giza kama kipofu badala katika nuru,ninaenda kwa kupapasa papasa mchana kama vile usiku,na kuonewa na kutekwa nyara siku zote,na wala hakuna mtu kuniokoa wala kunisaidia,Baba natubu na kuomba Rehema,laana imesababisha akili yangu kuwa tegemezi na kuwatumainia wanadamu badala ya wewe Mungu,laana imeachilia bumbuwazi la moyo,laana imepiga ufahamu wangu,laana imempa adui uhalali wa kuninyanganya baraka yangu Mungu aliyonibariki,laana imesababisha matunda  ya kazi yangu,na taabu yangu kuliwa na mtu mwingine,na mimi kupondwa chini daima,laana imesababisha mimi kuwa mkia badala ya kichwa,laana imeniuza katika utumwa na imepelekea mimi kusukumwa kuitumikia miungu mingine hata si kwa hiari yangu,Ee Bwana Yesu!laana imepiga uchumi wangu na kuharibu,laana imepiga fedha yangu na kuharibu,laana imefunga vibali vyangu vya kimataifa,laana imefunga hatua zangu Bwana Yesu,laana imefunga akili yangu na kufunikwa na giza,laana imefunga ufahamu wangu Yesu ni mzito,hakuna ninachozaa kwenye uchumi isipokuwa ni hasara,mapooza,utasa,uharibifu,mauti,uchumi wangu umezikwa kaburini,uchumi wangu umefishwa kwa laana,Baba natubu na kuomba Rehema,kila laana ninayoijua na nisiyoijua,iliyojificha na iliyo waziwazi,Ee Bwana naomba sasa ruhusu damu yako,ikapite leo juu ya hizo laana,ikazivunje vunje kwa jina la Yesu,kwa kuwa imeandikwa Yesu Kristo alifanyika laana kwa ajili yangu,imeandikwa amelaaniwa mtu yule aangikwaye juu ya mti,na Yesu Kristo aliangikwa msalabani kwa ajili yangu,alifanyika laana ili mimi nisifanyike laana wala nisitembee chini ya laana,Baba Mtakatifu ninatubu kuomba Rehema,laana zote chanzo chake ni kuabudu miungu migeni,kuambatana na miungu migeni,kuifuata miungu migeni,kuifanyia ibada na kuitumikia na kuisujudia,nyumba ya baba yangu tumeyafanya hayo,nyumba ya mama yangu tumeyafanya hayo,nami nasimama mahali palipo bomoka kwa ajili yangu na walionitangulia ninatubu na kuomba Rehema,ninatubu na kuomba Rehema,ninaungama kwa ajili ya huo uovu,hiyo dhambi na hayo makosa Ee Mungu unirehemu unisamehe kwa ajili ya kila mashitaka yaliyo mbele yangu,kila hukumu na adhabu,Baba ninatubu na kuomba Rehema kwa kuwa imeandikwa baba zetu walitenda dhambi na sasa hawapo,nasi tumeyachukua maovu yao,Ee Mungu uyashikaye maagano ya Rehema kwa ajili ya watu wako,na kwa uaminifu wako ninatubu na kuomba Rehema,unirehemu na kunisamehe,unitakase kwa damu yako,unioshe kwa damu yako.Laana imenifunga katika minyororo ya madeni siwezi kutoka,na wamenitupa katika shimo la madeni na wameniingiza katika viapo na maagano ya freemanson kwa namna ya siri,kwa hila ya madeni,kwa mitego ya madeni,Lakini Wewe Mungu utupaye nguvu ya kupata utajiri kwa ajili ya kuimarisha agano la Ibrahim ndani ya Yesu Kristo,Wewe Mungu utufanyie kuwa matajiri kwa agano jipya la damu ya Yesu,Baba Mtakatifu ruhusu damu ya Yesu leo ikalipe kila madai ya makosa niliyofanya mimi na nyumba ya baba yangu na mama yangu,kila madeni ambayo ninadaiwa,damu ya Yesu ikanyamazishe kila sadaka iliyotolewa kinyume changu,iwe ni sadaka ya damu ya wanyama,damu ya ndege,damu ya wanadamu,Ee Bwana iwe ni kiapo cha uaminifu cha kuzimu,iwe ni agano la kipepo nililoingizwa kwa hila,Baba hakuna kiapo kikubwa ziada ya kile cha Yesu alichoapa kwa ajili yangu (Yohana 17:19),Baba hakuna agano bora na kubwa zaidi ya lile agano la damu ya Yesu,(Mathayo 26:28)! Hakuna mauti yenye nguvu zaidi ya mauti ya Yesu,yeye mwenyewe amesema nalikuwa nimekufa na sasa ni Hai,mimi ni Mwanzo na Mwisho maana yake yeye ni "umilele",Naye  Akasema ninazo funguo za mauti na kuzimu,Ee Bwana ninasema asante kwa kuwa funguo za mauti na kuzimu za uchumi na   fedha zangu hazipo tena mikononi mwa adui,Baba nakushukuru kwa kuwa mashitaka yote,na hukumu zote,na adhabu zote kwa habari ya uchumi na fedha zimefutwa na kugongomelewa msalabani,Baba nakushukuru kwa kifo cha Yesu kilicholipa fidia ya adhabu ya laana na mauti mimi nimekombolewa!niko huru mbali na laana!kwa kuwa imeandikwa Kristo amefanyika laana ili mimi nipokee ahadi ya Ibrahimu kwa njia ya imani,Baba nakushukuru kwa kuwa ndani ya Kristo tunaishi,tunaenenda na kuwa na uhai wetu,Asante kwa upendo wako Baba Mungu mbinguni,asante kwa damu ya Yesu,kupitia yeye tunakutana na nguvu ya msalaba,na huo msalaba wenye nguvu ya utajiri na baraka,Wenye agano bora la damu ya Yesu kupita maagano yote,Pokea sifa na utukufu Baba Mungu wa mbinguni.Nami sasa katika jina la Yesu ninanyunyiza damu ya Yesu juu ya lango la uchumi na fedha, ninaimwaga damu ya Yesu juu ya lango la uchumi na fedha, natakasa lango langu la uchumi na fedha kwa damu ya Yesu, natakasa lango la moyo wangu kwa damu ya Yesu,natakasa vibali vyangu vya uchumi na fedha kwa damu ya Yesu,natakasa hatua zangu za uchumi na fedha kwa damu ya Yesu,natakasa miguu yangu kwa damu ya Yesu,natakasa mikono yangu kwa damu ya Yesu,natakasa akili yangu kwa damu ya Yesu,natakasa chanzo cha mapato kwa damu ya Yesu,Baba Mtakatifu unirehemu sasa kila makosa,kila dhambi,kila uovu,adui anaotumia kunifunga katika madeni na hasara,Damu yako Bwana Yesu iruhusu ikalipe makosa yangu, ikalipe uovu wangu,ikalipe dhambi,inawezekana nilikopa kwa akili zangu,nilikopa kwa matamanio,nilikopa kwa mkumbo,nilikopa kwa kujihesabia haki, Baba natubu na kuomba Rehema, unirehemu unisamehe,nimejiingiza kwenye madeni, nimeingizwa na watu walionizunguka!Baba natubu na kuomba Rehema!Mungu wa Rehema wewe waweza kunirehemu na kunihurumia,na kunilipia hayo madeni,kama ulivyofanya kwa Petro,Bwana Yesu unirehemu na kunisamehe,Yamkini Ee Bwana nilipoona dalili ya madeni sikuomba inipasavyo,sikutafuta uso wako inipasavyo,sikutafuta maarifa yako inipasavyo,unirehemu unisamehe,unirehemu unisamehe,unitakase kwa damu yako,Ee Bwana waujua moyo wangu,mimi si mnyenyekevu vya kutosha mbele zako, nina madhaifu mangi, ninafanya makosa mengi,tena ni mtu mwenye kiburi na ninayejihesabia haki, ni mtu nisiyesikia sauti yako,mwenye madharau,mwenye mizaha,mara nyingi nalidharau neno lako silifanyii kazi,silishiki neno lako,siliheshimu neno lako,nisiye na moyo wa shukrani, mwenye tamaa, nisiyetosheka,nisiyeridhika,mwenye wivu wakati mwingine, mwenye manunguniko na malamiko,nisiye mwaminifu kwenye kazi yako,Baba Mtakatifu kama utahesabu makosa,siwezi kusimama mbele zako, nina makosa mengi, unirehemu unisamehe kwa damu ya Yesu, naomba unirehemu unisamehe kwa jina la Yesu,damu yako ya thamani inioshe,damu yako inisafishe,damu yako Yesu initakase!Ee Bwana iruhusu damu yako nakusihi,iruhusu inioshe,iruhusu damu yako initakase,iruhusu iniweke huru,iruhusu ilipe madeni yote, iruhusu ilipe hayo makosa,iruhusu ifute mashitaka,iruhusu ilipe kila madai shetani na ibilisi anayodai na kunishitaki nayo kwa jina la Yesu,Baba mashitaka yaliyo inuliwa kwa habari ya mimi ili nisipewe nguvu ya kuwa tajiri naachilia damu ya Yesu,ikafute hayo mashitaka, mashitaka yanayotoa uhalali wa roho ya madeni Baba napeleka damu ya Yesu ikafute mashitaka,Damu ya Yesu naipeleka kwenye kila madhabahu, kwenye kila sadaka iliyofunga uchumi wangu na fedha yangu,damu ya Yesu ikashughulikie kila agano la madeni na umasikini,kila kiapo cha madeni na umasikini,kila kifungo cha madeni na umasikini,kila laana ya madeni na umasikini,kila kamba,kila nira,kila mnyororo ya madeni na umasikini,damu ya Yesu ikashughulike sasa,kila sadaka iliyonishika katika madeni na umasikini damu ya Yesu ikashughulike sasa,kila ibada ya pombe,ibada ya vyakula,ibada ya uzinifu,kiapo cha majini mahaba,ibada ya wafu,Damu ya Yesu ikashughulike na ibada zote za matambiko,ibada za mazindiko,ibada za kiganga,ibada za kichawi,ibada za kishirikina zinazohusika mojakwamoja au kupitia wengine ili  kuharibu na kuuwa uchumi wangu na fedha yangu,ibada zote za kumwabudu joka damu ya Yesu ikashughulikie,hizo ibada katika jina la Yesu,popote nafsi yangu ilipowekwa,popote jina langu lilipo wekwa ili kufuatilia uchumi wangu na fedha yangu napeleka damu ya Yesu.Napeleka damu ya Yesu juu ya madhabahu zao.Vibali vyangu vilivyo chooni,hatua zangu popote zilipowekwa napeleka damu ya Yesu,popote akili yangu ilipo au ilipofungwa nanyunyiza damu ya Yesu juu ya akili yangu na ufahamu wangu,aliyeshikilia akili yangu,na ufahamu wangu kwa damu ya Yesu apigwe,kwa damu ya Yesu aangushwe,kwa damu ya Yesu ahukumiwe,kwa damu ya Yesu aondolewe kwenye akili na Ufahamu wangu katika jina la Yesu.Aliyeshikilia nyota yangu naachilia damu ya Yesu juu ya nyota yangu,naachilia damu ya Yesu juu ya nyota yangu,naachilia damu ya Yesu juu ya nyota yangu,Bwana Yesu ruhusu moto wa Roho Mtakatifu na radi ya damu ya Yesu, imhukumu yoyote anayetembelea nyota yangu,yoyote anayetumia nyota yangu,ahukumiwe na atenganishwe na mimi kwa jina la Yesu,ikiwa kuna chochote chake alichonipa kwa mtego,au nilichompa pasipo kujua cha mtego,anachotumia kujiunganisha na kujiambatanisha na mimi na kunifuatilia,natuma moto wa Roho Mtakatifu uteketeze vitu vyake,uteketeze mavazi yake,kwa jina la Yesu,rada yake,antena yake,receiver viungue na moto wa Roho Mtakatifu,viungue kwa moto wa Roho Mtakatifu!Kwa jina la Yesu Kristo,Kwa jina la Yesu Kristo,kwa jina la Yesu Kristo katika jina la Yesu,kila kifungo cha uchumi mgumu,kila kifungo cha utelezi,kila kifungo cha uharibifu,kifungo cha mauti nilichoingia kupitia agano la ndoa,kifungo cha laana,kifungo cha hasara,ninaachilia Damu ya Yesu,Damu ya Yesu!Naamuru funguka sasa,haribika sasa!kifungo cha madeni kupitia mikopo toka kwa freemanson,madeni yenye maagano ya uchawi,ushirikina,uganga,Baba naachilia damu ya Yesu yenye mauti ya Yesu,Yenye uhai wa Yesu!Ee Bwana  kila giza kwenye mikono yangu likatoweke sasa,kila giza kwenye uchumi wangu likatoweke sasa,kila nguvu ya giza ikaharibiwe sasa kwa damu ya Yesu,chochote walichotumia au wanachotumia kuunganisha nafsi yangu na nafsi zao,jina langu na jina lao,kibali changu na kibali chao,iwe ni picha,iwe ni video,Baba naachilia damu ya Yesu juu ya picha zangu zote,video zangu zote,popote zilipo nazigeuza kuwa moto wa Roho Mtakatifu,nageuza kuwa moto wa Roho Mtakatifu,anayetumia kibali changu chochote kile damu ya Yesu ikamshughulikie,damu ya Yesu ikamkemee kwa jina la Yesu Kristo.Wewe unayetumia kibali changu nakukemea kwa jina la Yesu,nakukemea kwa damu ya Yesu,Yesu akukemee!Kwa jina la Yesu naachilia damu ya Yesu juu ya kibali changu na moto wa Roho Mtakatifu,uunguzwe utengwe na mimi kwa jina la Yesu,Kwa damu ya Yesu,popote alipo post picha yangu naachilia damu ya Yesu kwenye profile yake,naachilia damu ya Yesu kwenye account yake,naachilia damu ya Yesu juu ya picha zangu na video zenye sura yangu nageuza kuwa moto wa Roho Mtakatifu.Bwana Yesu hata kama si kibali cha uchumi anatumia kibali cha ndoa,Bwana Yesu damu ya Yesu ikamhukumu huyo kuhani na mtandao wake wote kwa jina la Yesu Kristo.Kwa damu ya Yesu Kristo.Baba Mtakatifu uuponye uchumi wangu nakusihi,unifutie madeni yangu nakusihi,uponye akili yangu na ufahamu wangu nakusihi,uponye moyo wangu nakusihi,damu ya Yesu ikafute na kuondoa mipaka yote waliyoniwekea ili nisiwe tajiri!ninafuta kila mpaka wa laana,kila zuio la kupiga hatua ninafuta kwa damu ya Yesu,ruhusu Bwana Yesu nguvu zako kupitia damu ya Yesu ikanikomboe na kunifungua!Ruhusu damu ya Yesu kwa moto wa Roho Mtakatifu ikaharibu kila connection ya giza,Ee Bwana haijalishi amejiungaje au ameungamanishwaje na mimi!naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu.Naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,Naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu,naachilia damu ya Yesu Kwenye moyo wangu,Naachilia damu ya Yesu kwenye moyo wangu katika jina la Yesu!nakushukuru Baba Mungu wa mbinguni kwa kufanya kwa kutenda zaidi ya nilivyoomba kufikiri na kuwaza katika jina la Yesu ninaomba na kushukuru Amen.

✴️Endelea kuomba kama bado unao mzigo huo....

#.Wanamaombi Online Ministry
#.Mtumishi Joseph Ntandu
#.0765 377506 / 0713 297065

*©️WOM-2025*

Comments

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA