UPONYAJI WA UCHUMI

✝️

Day 2️⃣🅱️

*"KWA KUPIGWA KWAKE NIMEPONA TOKA KWENYE MADENI"*

💡Isaya 53 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.

⁵ Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

✍🏽Hiko ni kiapo cha Mungu kwa wale wote wamwaminio! Inakuwaje basi wengine wataomba kwa hilo andiko na bado hawatavuka?!

*➡️HIZI ZINAWEZA KUWA MOJA YA SABABU,INGAWA SI ZOTE...*

1️⃣Kukataa kufundishwa na kuelekezwa na Roho Mtakatifu.

✔️Isaya 48 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

¹⁸ Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari.

✍🏽Kila mtoto wa Mungu kusudi afanikiwe ni lazima aongozwe na Roho Mtakatifu,asiyeongozwa na Roho Mtakatifu lazima ataanguka kwenye hasara.(Piga picha kama ungejua huo mkopo haulipiki je ungekopa?!)

2️⃣Kukataa kubadilika hasa baada ya Mungu kukuonya.

✔️Ufunuo wa Yohana 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

✍🏽Mungu akigundua ni baraka ya uchumi mzuri ndio inayokufanya usimsikilize!anaondoa mkono wake wa ulinzi!"anajua ukishaanza kushambuliwa na watesi utarudi kwake na utamsikiliza kwa bidii".Ndo maana ni vizuri kujua chanzo cha tatizo lako kabla ya kuomba.

3️⃣Kukataa kazi ya Mungu kama alivyofanya Yona.

✔️Yona 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³ Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana.

⁴ Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.

✍🏽Mungu si Mungu wa hasara,hakuna aliyekataa kumtumikia Mungu aliyemuumba!kutumikia na mapenzi yake,kisha akawa salama.Kwa wengine adhabu ya madeni ni sababu wamekataa kukaa nafasi zao.Ingawa si kila aliye na madeni yuko chini ya adhabu.Napanua mawazo yako ili uweze kutafakari  chanzo.

4️⃣Kuombea tatizo la madeni pasipo mwongozo wa Roho Mtakatifu.

  ✔️Zaburi 32:8 (Biblia Takatifu)
“Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

✍🏽Maombi yenye majibu ya hapohapo,ni maombi ambayo agenda ya maombi inatoka kwa Roho Mtakatifu na sio kwako.Sababu agenda inayotoka kwa Mungu mwenyewe hiyo hutimiza mapenzi yake.Na Mungu huliangalia neno lake ili alitimize!si neno la mwanadamu  (Yeremia 1:12).

5️⃣Kuomba huku una majeraha moyoni sababu ya  kutokusamehe.

✔️Marko 11 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁵ Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

²⁶ Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]

✍🏽Na wengi maombi yao yanazuiliwa sababu wamegoma kuachilia na kusamehe!luka 6:37 inasema achilia nawe utaachiliwa!unajua uchungu,hasira,kisasi,malipizi chanzo chake ni KUTOKUSAMEHE.

6️⃣Kutokuwa na moyo wa shukrani baada ya Mungu kulituma neno lake.

✔️Zaburi 107 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁰ Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.

*²¹ Na wamshukuru Bwana kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu.*

✍🏽Ni wachache sana watakao mshukuru Mungu kwa ajili ya Mungu katuma neno lake kuponya na kuokoa,hata hapo "Daudi anasema na wamshukuru Mungu kwa fadhili zake".Wengi watataka wamshukuru Mungu! shuhuda ikisha kukamilika.Unapomshukuru Mungu kwa hatua moja,Mungu hufungua hatua ya pili.

7️⃣Kutoitengua nadhiri uliyo jiwekea baada ya Mungu kukuvusha.

✔️Mhubiri 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁴ Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.

⁵ Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.

✍🏽nadhiri kwa Mungu ni kiapo cha uaminifu!"Mungu ukifanya hivi nami nitafanya hivi"! Na Mungu alivyokuwa mwaminifu anafanya ila sababu ya udhaifu wetu hatufanyi sehemu yetu!nadhiri hugeuka deni kwa Mungu.Anaanza kukudai!njia mojawapo ya kukumbusha kuwa una deni kwa Mungu ni kudaiwa madeni na wanadamu na roho ya madeni inaanza kukuandama.

8️⃣Kutokuombea shida ya madeni kwa bidii hata umevuka kabisa.

✔️Yakobo 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.

¹⁸ Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.

✍🏽Ufalme wa Mungu unapatikana kwa wenye nguvu!haupatikani kwa uvivu na mazoea,unapatikana kwa majasiri!Kuna wakati mwingine Mungu atakushushia upako uombe na hutaomba.Atakuwekea mazingira ya ushindi na hutayatumia!Mungu ana sehemu yake na mwanadamu ana sehemu yake.Usipofanya sehemu yako kwa bidii itakuwa ngumu kuvuka.LAZIMA UMAANISHE UNAPOOMBA.

9️⃣Kuendelea kuambatana na watu wasio sahihi kwenye kusudi la Mungu alilokuitia.

✔️Waamuzi 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
*² nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?*

³ Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu;*lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.*

✍🏽madhara ya kuambata na mtu ambaye si wa kusudi la Mungu wala hakuletwa na Mungu isipokuwa ni wewe umejiambatanisha naye kwa akili zako au kushawishiwa,biblia inasema hao watu watakuwa miiba kwenu kwa maana ya kwamba,miungu nyuma yake itaanza kukufuatilia na kukusumbua sababu mmeambatana kiagano.Ukitaka kujua vizuri namna ambavyo mtu asiye wa kusudi la Mungu uliyeambatana naye anaweza kuwa mwiba kwako *chunguza na angalia jinsi ambavyo Lutu alivyomsumbua Ibrahimu kiroho hata kimwili ni mpaka pale walipotengana*.Ndipo Ibrahimu akaanza kumsikia Mungu tena.Na Mungu akaanza kutembea naye.(Soma sura yote👇🏾)

Mwanzo 13 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa kaskazini, na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi;

¹⁵ maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.

🔟 Makosa afanyayo mtu kwa habari ya utoaji wa sadaka (KUTOA KWA MAZOEA)

✍🏽Wengine ni waaminifu kwa habari ya kumtolea Mungu sadaka,ila wanatoa kwa mazoea...KABLA YA KUTOA NI MUHIMU

1️⃣Roho Mtakatifu akuongoze wapi upeleke sadaka yako.
2️⃣Roho Mtakatifu akuongoze ili ujue ni nani apokee sadaka yako.
3️⃣Je ni nani akuombee/ akuwekee mikono baada ya kutoa sadaka
4️⃣Ni nani akutamkie kwa habari ya uchumi wako ILI USTAWI
5️⃣Ni madhabahu gani inapaswa kupokea sadaka yako ya fungu la 10?!

✍🏽Sababu si kila mahali,si kila mtumishi,si kila kuhani,si kila madhabahu wamepewa kibali na Mungu Aliye Hai kukutamkia,kukuwekea mikono,kukuombea,ikiwa kweli unataka kumuona Mungu kupitoa sadaka yako.Basi Omba uongozi wa Roho Mtakatifu usitoe tuu.*(ikibidi funga omba kama huna hakika)*

*️⃣Maana yake! inakupasa uwe na ushirika na Roho Mtakatifu kwa habari ya ibada yako ya sadaka.Usitoe tuu kwa mazoea kama unataka kumuona Mungu kwa HABARI YA ULINZI WA BARAKA YAKO YA  KIUCHUMI,ili usiwe na madeni.Maana kubarikiwa ni kitu kingine,na ulinzi wa baraka ni kitu kingine kabisa.JINA LA BWANA LIBARIKIWE!Na wengi wanapokea baraka ila kwa sababu ya mazoea katika utoaji baraka zao zinakosa ulinzi.Adui anaanza kuzila na madeni.

✴️Baada ya maarifa haya kidogo yanayofungua ufahamu wako kwa msaada wa Roho Mtakatifu.Tutamlingana ILI APONYE UCHUMI WETU. *Endelea kutafakari maombi yanakuja....*

#.Wanamaombi Online Ministry
#.Mtumishi Joseph Ntandu
#.0765 377506 / 0713 297066

*©️WOM-2025*

Comments

  1. Ushuhuda

    Nilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
    Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
    Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.

    Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:

    ✅ Maneno ya mapenzi
    ✅ Tahadhari za Ujauzito
    ✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
    ✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.

    📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
    📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159

    Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA