HARIBU ROHO YA MAUTI INAYO KATISHA TAMAA ILI UWEZE KUPIGA HATUA
Bwana Yesu
asifiwe!
Mauti
ikiatamia ndoa itaenda kuuwa upendo, itauwa uvumilivu. Itauwa kusamehe.Mauti ikaatamia uchumi wako. Itauwa
vibali vyote, na mipenyo yote,mauti ikahatamia biashara. Inaenda kuuwa kibali
chako moyoni mwa watu, machoni mwa watu. Inaenda kuuwa wateja wako,ikihatamia
miguuni mwako inauwa
hatua zako.
Inauwa uwezo wako wa kumiliki na kutawala.Mauti ikiatamia mikono yako. Inauwa
kila unachokishika na kukianzisha. Hata upewe mil 100 utazitapanya tuu. Mauti
ikiatamia akili, fikra na ufahamu wako. Itauwa maarifa, itauwa hekima, inauwa
misimamo, inauwa nia, inauwa uchaguzi.
Matokeo yake
unafanya kama pepo anavyotaka.Mauti ikiatamia macho yako ya Rohoni. Unakuwa
huwezi ona tena vitu vya rohoni. Unajua kuna tofauti ya kutazama na kuona.
Kuona ni zaidi ya kutazama. Mauti ikihatamia masikio yako. Inauwa usikivu wako
wa Rohoni wa kuisikia sauti ya Mungu.
Mauti ikikaa
malangoni hakuna litakaloingia hakuna litakalo toka. Yote yatakufa mauti ikikaa
kipengele cha ajira. Utatafuta kazi lakini huonekani manake vibali vya
kuonekana na kukubalika vimekufa. Vibali vya kuchaguliwa vimekufa.mauti
ikiatamia kitu huwa iko kitu hakibaki salama ni mpaka kife.
Mauti
inaweza atamia jicho na ilo jicho likampeleka mtu kaburini. Jicho tuu. Mauti
inaweza atamia damu uyo mtu akaonekana ana cancer, au damu yake si salama. Na
ikangangania hapo. Halleluyah! Lakini lipo neno kabisa la mojakwamoja la
kutangua mauti. halleluyah Watu wengi wanachukulia
mauti ni kitu rahisi tuu. Kuwa utasema tuu kwa jina la Yesu toka. Au ishindwe
kwa jina la Yesu. Alafu itatoka kirahisi rahisi. Mauti imeingia kwa sheria.
Mauti itatoka kwa sheria halleluyah
Leo tunaenda
kuachilia damu ya Yesu ipambane na roho ya mauti. Maana shetani kaachilia roho
ya mauti
☑kwenye biashara zetu
☑ndoa zetu
☑uchumba wetu
☑mahusiano yetu
☑kazi zetu
☑hatua zetu
☑vibali vyetu
☑ajira zetu
☑afya zetu
☑malangoni mwetu
☑mitaji yetu
☑miradi yetu
☑ndoa zetu
☑maono yetu
☑mashamba yetu
☑mipango yetu
☑........
Anatafuta
kuuwa kila kitu. Lakini katika jina la Yesu leo ataharibiwa yeye na mauti yake.
Na atafutika kabisa. Na kama ilo eneo liliuliwa na roho ya mauti utaona
linaanza kuchipuka tena. Yani wewe mwenyewe utajua. Shetani anaweza jua kabisa
imebaki hatua moja huyu apenyeze afanikiwe anakimbilia mbele kuachia mauti.
Anauwa hatua inayofuata.....
Adui
huwakatisha watu tamaa kwa roho ya mauti. Kila wanalolianza linakufa. Likaanza
kuinuka linakufa. Likitaka kuchanua linakufa. Na wanafikiri Mungu ndo anaruusu
hayo. Kumbe ni hila za adui. Matokeo yake mtu anakata tamaa
☑kufanya biashara
☑kutafuta kazi
☑kuomba
☑kufanya huduma
☑kujenga
☑kufanya miradi
Anafikiri
Mungu karuusu hayo kumbe ni hila za yule mwovu. Na wengine wamejikalia tuu
chini kushika “tama” wakijua ni mpango wa Mungu. Wakisema labla ni majaribu ya
Mungu. Kumbe ni hila za adui. Kwa iyo watu wengi wanakata tamaa
☑wanafunga biashara
☑wanaacha kazi
☑wanaacha kumtafuta Mungu
KUMBE
HAWAJUI roho ya mauti. Ipo mlangoni mwao. Imefunika hiko kitu na sasa kila kitu
kinakufa. Bwana Yesu asifiwe! Wengi wanasema hili neno la Roho Mtakatifu ni kweli
kabisa iyo hali hata mimi imenikuta .Kila anachofanya kinakwama. Kila
anachojaribu kufanya kinakwama.
Akifanikiwa hatua ya kwanza inayofuata
inakwama. Shetani anapoona umechachamaa
kumtafuta Mungu amejaribu kukushawishi hushawishiki. Amejaribu kukutisha na
vitisho hutishiki. Anachofanya anakukatisha tamaa. Kwenda kuuwa vitu vyako kwa
kuachilia roho ya mauti. Na anajificha katika sura ambayo huwezi mtambua. Mpaka
hapa navyozungumza utakuwa tayari umeanza kugundua na kukumbuka ni maeneo gani
shetani alikukatisha tamaa.
Kwa
kuachilia roho ya mauti. Hiyo ni silaha ya mwisho ya kukukatisha tamaa ili
uiache imani yako. Ili uache kuomba. Kumbuka shetani alijaribu kila njia ya
kumwangusha Ayubu akashindwa matokeo yake akaenda kumshitaki kwa Mungu. Ili
apate kibali cha kumkatisha tamaa. Yale yote aliyokuwa anatafanya kwa AYUBU ni
kumkatisha tamaa
Ayubu 1
13 Ilitukia siku moja
hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya
ndugu yao mkubwa,
14 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao;
15 mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
16 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
17 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
18 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa;
19 mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
20 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
14 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao;
15 mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
16 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
17 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
18 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa;
19 mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.
20 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia;
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
Shetani aliuwa watoto wa Ayubu, aliuwa mifugo
ya ayubu, aliuwa afya ya ayubu, aliuwa heshima ya ayubu, aliuwa ndoa ya ayubu,
mke wake alianza kumgeuka ayubu. Nia ilikuwa ni nini kumkatisha tamaa. Shetani
atakukatisha tamaa kwa kuuwa vitu vyako. Hawezi kukuuwa wewe ila atakimbilia
kwenye
☑ndoa yako
☑biashara yako
☑kazi yako
☑hatua zako
☑vibali vyako
☑miradi yako
Atatafuta
uhalali wa kuviuwa. Atanyemelea ili auwe kila ulichopewa na Bwana. Halleluyah haribu
kila ambacho unakifanya. Unategemea kukifanya. Ataharibu kwa roho ya mauti.
Shetani alimu mharibia ayubu hata kwa
kutumia marafiki zake. Marafiki zako, au watu waliokuzunguka wanaweza bebeshwa
roho ya mauti. Halleluyah!
Wakati wewe
umekazana. Wakati wewe unafunga na kuomba na kutamka na kungoa. Na kupanda. Shetani
anajisemea nitamsubiri hatua inayofuata. Nitaachilia mauti hatua inayofuata. Si kapata mtaji uyu?
Nitafungulia matatizo yamalize huo mtaji.
Nitamfunga akili zake asiweze fanya
lolote halleluyah! Anajisemea adui si ashafungua duka.
Nitazuia wateja. Nitamwinulia maadui kila kona
kila upande alafu tuone. AKITAFUTA KUKUKATISHA TAMAA. AKITAFUTA URUDI NYUMA.
AKITAFUTA UACHE WOKOVU. AKITAFUTA UACHE KUOMBA. AKITAFUTA UACHE KUMUAMINI
MUNGU.
Anaweza jisemea uyu ashakuwa mwanamaombi. Uyu
ameanza kulijua neno. Uyu ameanza na
kufunga. Uyu ukimpelekea mapepo anayabamiza yote. Juzi kaninyongea mapepo yangu
71 😄. Akayachinja! Akayalipua kwa moto.
Tena uyu ukimchokoza uyu vita yake ni zaidi ya Joshua yani huwa hakubali Yuko
radhi asimamishe jua mpaka auuwe wote.
Tena ukimkimbia
uyu bado anakufuata huko uendako. Na upanga na moto na mkuki. Huyu usije
ukamchokoza kabisa....Tutamsimamishaje uyu.. Tuuwe vitu vyake. Tuachilie roho
ya mauti. Ivyo adui anavyokuwazia mabaya anavyokungatia vidole.
Ukisoma
kitabu cha ayubu utagundua kuwa shetani alitafuta jinsi ya kumzuia au kumfanya
ayubu amwache Mungu akashindwa. Shetani alitumia roho yake ya mauti
☑akauwa heshima ya ayubu
☑akauwa utajiri wa ayubu
☑akauwa afya ya ayubu
☑akauwa familia ya ayubu
☑akauwa ndoa ya ayubu
☑akauwa urafiki na marafiki wa ayubu
☑akauwa mifugo ya ayubu
roho ya
mauti ilimzunguka ayubu na kuuwa kila kitu kilichomzunguka. Shetani alichokuwa
anataka ni ayubu amwache Mungu. Usifikiri ayubu alikuwa halalamiki alikuwa
mpaka akilaani kila kitu. Ila hajawahi kumuacha Mungu.
Leo hii
shetani anapokuona umesimama Kama ayubu anafanya vilevile alivyofanya kwa ayubu
ili urudi nyuma. Anaona huyu hakuna jinsi atamwacha Mungu. Nimkatishe tamaa
amchukie Mungu kwa iyo anaenda kuuwa kila unachofanya kila unachogusa kinakufa.
Hallelujah
Sijui wewe
shetani ameshauwa vitu vyako vingap? Kukukatisha tamaa. Hallelujah! Hizi ni
zama za agano jipya Si zama za ayubu tena. Hallelujah. Yaliyotokea kwa ayubu ni
ili Mimi Na wewe tujifunze tuchukue. Hatua! Hallelujah
Ufunuo 3:1
. Na kwa
malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo
Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina
la kuwa hai, nawe umekufa.
Ufunuo 3:2
. Uwe mwenye
kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona
matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Kwenye hiki
kitabu cha ufunuo tunaona Yesu akampa hayo maono Yohana. Akisema “najua matendo
yako”. Kuwa Una jina lililohai lakini umekufa. Yani uko vizuri kila mahali. Mtu
akikuona anaweza sema uyu Yuko vizuri. Lakini kiukweli umekufa. Yani mambo yako
yamekufa. Hakuna linaloendelea katika maisha yako. Shetani kayauwa mambo yako.
Mtu akikuona anaweza sema natamani maisha ya uyu mtu lakini hajui tuu.
☑biashara imekufa
☑ndoa imekufa
☑furaha ndani yako imekufa
☑kazi imekufa
Yani kwa nje
unaonekana uko vizuri ila kwa ndani shetani kakuuwa. Ni Kama vile mtu mwenye
cancer. Asipokuambia anachoumwa huwezi jua unaweza yatamani maisha yake. Lakini
yeye anaweza jiona ni Kama tayari amekufa. Hallelujah
Yesu anasema
uwe mwenye kukesha ukayaimarishe mambo yako yaliyo salia yanayotaka kufa. yani
uwe mwangalifu usipochukua hatua atauwa hata hayo mengine.Kukesha manake Si
kutokulala yani uwe macho. Uamke kiroho! Shetani atauwa kila kitu
kilichokuzunguka. Hallelujah! Anaposema ninayajua matendo yako Una jina
lililohai lakini umekufa Ana maana gani? Manake najua uko hai kiroho
☑unaomba
☑unafunga
☑unatoa fungu la 10
☑unasaidia wahitaji
☑unasoma neno
☑una imani
Lakini
UMEKUFA
sasa
ninakufa kivipi?
Unakufa
sababu hakuna Kinachoendelea katika maisha yako uko vizuri kiroho lakini
☑umekufa kiuchumi
☑umekufa kindoa
☑umekufa kiafya
☑umekufa kimaono
☑umekufa kimahusiano
☑mambo mengine shetani kayauwa
Kwa iyo uwe
mwangalifu. Amka! ukayaimarishe. Yani uombe. Shetani asije kukuuwa zaidi ya
hapo. Hallelujah
Ninapoongea
hivi tayari utakuwa unaanza kukumbuka
☑miradi iliyokufa
☑duka lililokufa
☑kazi iliyokufa
☑biashara iliyokufa
☑mipango iliyokufa
☑hatua ulizokufa
utaanza
kukumbuka vitu ulivyovianzisha kwa moto gafla vikafa. Ulikuwa na mipango ya
kubariki ndoa ikafa. Ulikuwa na mipango ya kujenga ikafa. Ulikuwa na mipango ya
kuoa/kuolewa ikafa. Mipango mingiii lakini yote inakufa. Yote inakufa.
Kila
unachoanza kinakufa. Unafikiri kabla ni mipango ya Mungu. Si
mipango ya Mungu ife. Mungu anasema ni Mimi Mungu nikufundishaye kupata faida.
Shetani ndiyo anaiuwa ili ukate tamaa . Alijaribu kumkatisha tamaa Ayubu.
Hashindwi kukukatisha tamaa wewe. Kazi hutafuti tena umekata tamaa.
Ulitaka
kufungua kiwanda umekata tamaa. Ulitaka kufungua kampuni umekata tamaa. Ulitaka
kwenda kusoma umekata tamaa. Kila unachokipanga unakata tamaa. Unachoka. Alafu
unaona huu wokovu hauna maana Mungu mwenyewe
hanisaidii..
Kumbe shetani anauwa mwanzo wako. Anauwa hatua zako uchoke ukate tamaa.
Hallelujah. Una maono mazuri. Mawazo mazuri lakini unakata tamaa.
Unamuombea
mtu abadilike shetani ndo anazidisha maudhi na makwazo unakata tamaa. Kabisa
unatamani uanze upya maisha ya ndoa. Au utoke katika ndoa. Kumbe shetani
anakatisha watu tamaa. Hallelujah
Kuondoa roho
ya mauti inayopelekea wewe kukata tamaa kwa damu ya Yesu na jina la Yesu
Waebrania
2:14
. Basi, kwa
kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo
hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani,
Ibilisi,
Neno la Mungu linasema basi kwa kuwa watoto
wameshiriki damu na mwili. Anaposema watoto Ana maana wale ambao Yesu ni Bwana
kwao. Kunatofauti ya kuwa mtoto wa Mungu na mtu wa Mungu. Watoto manake ni wale
waliozaliwa kwa damu na maji.
Yaliyotoka mwilini ubavuni kwa Yesu. Alipokufa. Walizaliwa kwa imani.
Hallelujah! Yani wameokoka. Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha Yao.
Kwamba siku
ile ulipoongozwa sala Toba na kumpokea Yesu moyoni mwako.
nawe pia
umeshiriki kufa na kufufuka kwa Yesu. Biblia inasema wewe ulishiriki mwili na
damu. Na Yesu naye alishiriki ivyo hivyo. Ili kwa njia ya mauti aweze kumharibu
kwenye nguvu ya mauti. Yaani ibilisi. Nitaelezea kidogo hapa. Kabla ya shetani
kuuuwa kazi
yako. Biashara yako. Ndoa yako. Lazima atahitaji damu. Iwe damu ya kuku, ngombe,
kondoo, binadamu, yoyote ile shetani atumie mauti ya hiko kiumbe kilichokufa kuachilia mauti kwako.
Nitaelezea
tena! kitendo cha kitu kufa inamaana hapo Kuna
mauti. Ndo mana ikatokea kifo. Iyo damu iliyomwagiga ya hiko kiumbe
imebeba kifo na mauti ya hiko kiumbe. Kwa iyo shetani hutafuta mauti kupitia
kifo na hutumia damu. Ili mauti iyo akaitumie
kuuwa vitu vyako. Halleluyah! Ndo mana waganga wa kienyeji na wachawi
wanapenda
Sana kwenda makaburini. Wewe unafikiri ni kwanini? Ni sababu kule wanaenda tafuta
mauti. Kwenye kifo Kuna mauti. Ndo mana hata wakristo baada ya mtu kufa
makuburi huwa tunayaweka wakfu makuburi kwa jina la Yesu.
unajua
ni kwanini? Ni ili wachawi wasije chukua mauti ya uyo mtu kwenda kutumia
kichawi kuuwa vitu vingine. Mchawi akipata iyo mauti sababu mauti inanguvu ya
kifo basi hutumia iyo kuuwa vitu au watu. Huuwa biashara. Ndoa. Kazi. Mahusiano
chochote kile. Mungu baada ya kuliona Hilo ndipo hapo akaamua
kumtoa mwanawe
Yesu Kristo ili baada ya Yesu kufa mauti yake iweze kuharibu mauti
ya kuku,Mbwa,Kondoo, Mbuzi,Binadamu. Yani mauti anayoitumia shetani. Sababu
damu ya Yesu imebeba vitu viwili. Imebena mauti ya Yesu.Hapohapo
imebeba uhai wa Yesu. Mauti ni kwa ajili ya kuharibu mauti ya shetani. Yani
ibilisi. Uhai ni kwa ajili ya kuachilia uhai kwenye kitu kilichokufa. Hapo
ndipo shetani aliposhindwa. Yeye hana
uzima Yesu anauzima. Hakuna damu sehemu
yoyote yenye mauti na uhai hapohapo ila damu ya Yesu pekee.Kwa iyo
anaposema ili kwa mauti yake amharibu mwenye nguvu ya mauti hapo utaelewa Sasa.
Kwa kuwa wewe umeshiriki mwili na damu. Na Yesu kashiriki ivyo ivyo. Kama Yesu
Ana nguvu ya kuharibu mauti na mwenye nguvu ya
mauti basi hata wewe pia kutumia
damu ya Yesu pia unauwezo wa kuharibu nguvu ya mauti na mwenye nguvu ya mauti.
Ninaposema
nguvu ya mauti inaweza kuwa mapoza,Utasa,Uharibifu,Kifo. Hallelujah! ninaposema
mwenye nguvu ya mauti nina maana anaweza kuwa waganga wa kienyeji. Wachawi. Washirikina.wasoma
nyota,majini, Mapepo wote wanaotumia nguvu ya mauti kuuwa vitu vyako.
Sasa
ukishaijua iyo siri...
Kumbe ahaaa
damu ya Yesu imebeba mauti ya Yesu. Damu ya Yesu imebeba uhai wa Yesu. Na mauti
ya ibilisi inaharibiwa kwa mauti ya Yesu. Ukishagundua ilo kazi yako ni ndogo
Sana. Wewe ni kuachilia damu ya Yesu iliyobeba mauti ya Yesu kwenye kila mauti
ya ibilisi. Unaweza kuwa na list yako ya vitu vilivyokufa, vitu ulivyo/unavyo
vikatia tama, na mipango iliyokwama.Kama umefuatilia tokea mwanzo utakuwa
imeiva vizuri
Hatua za
kuomba:
1.Utatubu na
kuomba Rehema kwa ajili ya mauti kuatamia vitu vyako (milango iliyofunguka) na
mauti
☑kuatamia ndoa
☑kuatamia afya
☑kuatamia biashara
☑kuatamia nafasi za kazi
☑kuatamia hatua
☑utataja vyote
Kisha
2.Utaachilia
damu ya Yesu yenye mauti ya Yesu.
~ewe mauti uliyo atamia hatua zangu nakupambanisha
na damu ya Yesu yenye mauti ya Yesu
~ewe mauti uliye atamia
*hatua zangu
*kibali
changu
*miradi
yangu
*ndoa yangu
*miguu yangu
*mikono
yangu
*fikra zangu
*nafsi yangu
*uchumi
wangu
*ndo yangu
Wewe jini
mauti. Pepo mauti. roho ya mauti nakukutanisha Na damu ya Yesu yenye mauti ya
Yesu. Nakuharibu sasa kwa jina la la Yesu.Wewe mauti uliye uwa (taja
vilivyokufa) naachilia mauti ya Yesu kwa damu ya Yesu nakuharibu sasa kwa jina
la Yesu.Nakuharibu
mauti. Kwa jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu.Endelea kuachilia damu ya Yesu yenye
mauti ya Yesu nakuharibu hizo mauti. Nazo zitaharibiwa kabisa. Hallelujah utaendelea
fanya hivi utashangaa kila kitu kitaanza kuamka. Hata kukata tamaa kutaondoka.
Hallelujah
kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu.Mimi ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0765377506/0713297066
Mwl Joseph Ntandu
Mwz 1-3 Mungu akasema iwe Nuru ikawa Nuru
josephntandu@gmail.com,0765377506/0713297066
Mwl Joseph Ntandu
Mwz 1-3 Mungu akasema iwe Nuru ikawa Nuru
Nashukuru Sana mtumushi was Mungu.Barikiwa
ReplyDeleteMungu akubariki mtumishi kwa somo zuri binafsi nimekuwa nikisumbuliwa sana na roho ya mauti sikujua niombeje na mshukuru Mungu nimepata kitu cha kunisaidia
ReplyDeleteMtumishi wa Mungu, Mungu azidi kukubariki na maono na ufunuo wa kiroho ,fundisho hili nimeipokea na naamini kwa maombi haya tutafunguliwa na kuwekwa huru kutoka kwa maroho za mauti na maangamizi.
ReplyDeleteMungu amekutumia mtumishi, vita tuneishinda na mauti ya shetani imekimbilia kuzimu ... ubarikiwe sana , YESU ni mwema
ReplyDeleteUbarikiwe sana
ReplyDeleteMe naombaa msaada maana kunamawazo yakufa kuna wakat nikikaa nahs kamaaa nimekufaaa hivi sielew
ReplyDeleteAsante Mungu akubariki
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete