HARIBU ROHO YA MAUTI INAYO KATISHA TAMAA ILI UWEZE KUPIGA HATUA


Bwana Yesu asifiwe!

Mauti ikiatamia ndoa itaenda kuuwa upendo, itauwa uvumilivu. Itauwa kusamehe.Mauti ikaatamia uchumi wako. Itauwa vibali vyote, na mipenyo yote,mauti ikahatamia biashara. Inaenda kuuwa kibali chako moyoni mwa watu, machoni mwa watu. Inaenda kuuwa wateja wako,ikihatamia miguuni mwako inauwa

hatua zako. Inauwa uwezo wako wa kumiliki na kutawala.Mauti ikiatamia mikono yako. Inauwa kila unachokishika na kukianzisha. Hata upewe mil 100 utazitapanya tuu. Mauti ikiatamia akili, fikra na ufahamu wako. Itauwa maarifa, itauwa hekima, inauwa misimamo, inauwa nia, inauwa uchaguzi.

Matokeo yake unafanya kama pepo anavyotaka.Mauti ikiatamia macho yako ya Rohoni. Unakuwa huwezi ona tena vitu vya rohoni. Unajua kuna tofauti ya kutazama na kuona. Kuona ni zaidi ya kutazama. Mauti ikihatamia masikio yako. Inauwa usikivu wako wa Rohoni wa kuisikia sauti ya Mungu.

Mauti ikikaa malangoni hakuna litakaloingia hakuna litakalo toka. Yote yatakufa mauti ikikaa kipengele cha ajira. Utatafuta kazi lakini huonekani manake vibali vya kuonekana na kukubalika vimekufa. Vibali vya kuchaguliwa vimekufa.mauti ikiatamia kitu huwa iko kitu hakibaki salama ni mpaka kife.

Mauti inaweza atamia jicho na ilo jicho likampeleka mtu kaburini. Jicho tuu. Mauti inaweza atamia damu uyo mtu akaonekana ana cancer, au damu yake si salama. Na ikangangania hapo. Halleluyah! Lakini lipo neno kabisa la mojakwamoja la kutangua mauti. halleluyah Watu  wengi wanachukulia mauti ni kitu rahisi tuu. Kuwa utasema tuu kwa jina la Yesu toka. Au ishindwe kwa jina la Yesu. Alafu itatoka kirahisi rahisi. Mauti imeingia kwa sheria. Mauti itatoka kwa sheria halleluyah

Leo tunaenda kuachilia damu ya Yesu ipambane na roho ya mauti. Maana shetani kaachilia roho ya mauti

kwenye biashara zetu
ndoa zetu
uchumba wetu
mahusiano yetu
kazi zetu
hatua zetu
vibali vyetu
ajira zetu
afya zetu
malangoni mwetu
mitaji yetu
miradi yetu
ndoa zetu
maono yetu
mashamba yetu
mipango yetu
........

Anatafuta kuuwa kila kitu. Lakini katika jina la Yesu leo ataharibiwa yeye na mauti yake. Na atafutika kabisa. Na kama ilo eneo liliuliwa na roho ya mauti utaona linaanza kuchipuka tena. Yani wewe mwenyewe utajua. Shetani anaweza jua kabisa imebaki hatua moja huyu apenyeze afanikiwe anakimbilia mbele kuachia mauti. Anauwa hatua inayofuata.....

Adui huwakatisha watu tamaa kwa roho ya mauti. Kila wanalolianza linakufa. Likaanza kuinuka linakufa. Likitaka kuchanua linakufa. Na wanafikiri Mungu ndo anaruusu hayo. Kumbe ni hila za adui. Matokeo yake mtu anakata tamaa

kufanya biashara
kutafuta kazi
kuomba
kufanya huduma
kujenga
kufanya miradi

Anafikiri Mungu karuusu hayo kumbe ni hila za yule mwovu. Na wengine wamejikalia tuu chini kushika “tama” wakijua ni mpango wa Mungu. Wakisema labla ni majaribu ya Mungu. Kumbe ni hila za adui. Kwa iyo watu wengi wanakata tamaa

wanafunga biashara
wanaacha kazi
wanaacha kumtafuta Mungu

KUMBE HAWAJUI roho ya mauti. Ipo mlangoni mwao. Imefunika hiko kitu na sasa kila kitu kinakufa. Bwana Yesu asifiwe! Wengi  wanasema hili neno la Roho Mtakatifu ni kweli kabisa iyo hali hata mimi imenikuta .Kila anachofanya kinakwama. Kila anachojaribu kufanya kinakwama.

 Akifanikiwa hatua ya kwanza inayofuata inakwama.  Shetani anapoona umechachamaa kumtafuta Mungu amejaribu kukushawishi hushawishiki. Amejaribu kukutisha na vitisho hutishiki. Anachofanya anakukatisha tamaa. Kwenda kuuwa vitu vyako kwa kuachilia roho ya mauti. Na anajificha katika sura ambayo huwezi mtambua. Mpaka hapa navyozungumza utakuwa tayari umeanza kugundua na kukumbuka ni maeneo gani shetani alikukatisha tamaa.

Kwa kuachilia roho ya mauti. Hiyo ni silaha ya mwisho ya kukukatisha tamaa ili uiache imani yako. Ili uache kuomba. Kumbuka shetani alijaribu kila njia ya kumwangusha Ayubu akashindwa matokeo yake akaenda kumshitaki kwa Mungu. Ili apate kibali cha kumkatisha tamaa. Yale yote aliyokuwa anatafanya kwa AYUBU ni kumkatisha tamaa

Ayubu 1
13 Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa, 
14 mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao; 
15 mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. 
16 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. 
17 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. 
18 Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; 
19 mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. 
20 Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; 
21 akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe. 

 Shetani aliuwa watoto wa Ayubu, aliuwa mifugo ya ayubu, aliuwa afya ya ayubu, aliuwa heshima ya ayubu, aliuwa ndoa ya ayubu, mke wake alianza kumgeuka ayubu. Nia ilikuwa ni nini kumkatisha tamaa. Shetani atakukatisha tamaa kwa kuuwa vitu vyako. Hawezi kukuuwa wewe ila atakimbilia kwenye

ndoa yako
biashara yako
kazi yako
hatua zako
vibali vyako
miradi yako

Atatafuta uhalali wa kuviuwa. Atanyemelea ili auwe kila ulichopewa na Bwana. Halleluyah haribu kila ambacho unakifanya. Unategemea kukifanya. Ataharibu kwa roho ya mauti. Shetani alimu mharibia  ayubu hata kwa kutumia marafiki zake. Marafiki zako, au watu waliokuzunguka wanaweza bebeshwa roho ya mauti. Halleluyah!

Wakati wewe umekazana. Wakati wewe unafunga na kuomba na kutamka na kungoa. Na kupanda. Shetani anajisemea nitamsubiri hatua inayofuata. Nitaachilia  mauti hatua inayofuata. Si kapata mtaji uyu? Nitafungulia matatizo yamalize huo mtaji. 
Nitamfunga akili zake asiweze fanya lolote halleluyah! Anajisemea adui si ashafungua duka.

 Nitazuia wateja. Nitamwinulia maadui kila kona kila upande alafu tuone. AKITAFUTA KUKUKATISHA TAMAA. AKITAFUTA URUDI NYUMA. AKITAFUTA UACHE WOKOVU. AKITAFUTA UACHE KUOMBA. AKITAFUTA UACHE KUMUAMINI MUNGU.

 Anaweza jisemea uyu ashakuwa mwanamaombi. Uyu ameanza kulijua neno. Uyu ameanza  na kufunga. Uyu ukimpelekea mapepo anayabamiza yote. Juzi kaninyongea mapepo yangu 71 😄. Akayachinja! Akayalipua kwa moto. Tena uyu ukimchokoza uyu vita yake ni zaidi ya Joshua yani huwa hakubali Yuko radhi asimamishe jua mpaka auuwe wote.

Tena ukimkimbia uyu bado anakufuata huko uendako. Na upanga na moto na mkuki. Huyu usije ukamchokoza kabisa....Tutamsimamishaje uyu.. Tuuwe vitu vyake. Tuachilie roho ya mauti. Ivyo adui anavyokuwazia mabaya anavyokungatia vidole.
Ukisoma kitabu cha ayubu utagundua kuwa shetani alitafuta jinsi ya kumzuia au kumfanya ayubu amwache Mungu akashindwa. Shetani alitumia roho yake ya mauti

akauwa heshima ya ayubu
akauwa utajiri wa ayubu
akauwa afya ya ayubu
akauwa familia ya ayubu
akauwa ndoa ya ayubu
akauwa urafiki na marafiki wa ayubu
akauwa mifugo ya ayubu

roho ya mauti ilimzunguka ayubu na kuuwa kila kitu kilichomzunguka. Shetani alichokuwa anataka ni ayubu amwache Mungu. Usifikiri ayubu alikuwa halalamiki alikuwa mpaka akilaani kila kitu. Ila hajawahi kumuacha Mungu.

Leo hii shetani anapokuona umesimama Kama ayubu anafanya vilevile alivyofanya kwa ayubu ili urudi nyuma. Anaona huyu hakuna jinsi atamwacha Mungu. Nimkatishe tamaa amchukie Mungu kwa iyo anaenda kuuwa kila unachofanya kila unachogusa kinakufa. Hallelujah

Sijui wewe shetani ameshauwa vitu vyako vingap? Kukukatisha tamaa. Hallelujah! Hizi ni zama za agano jipya Si zama za ayubu tena. Hallelujah. Yaliyotokea kwa ayubu ni ili Mimi Na wewe tujifunze tuchukue. Hatua! Hallelujah


Ufunuo 3:1
. Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
Ufunuo 3:2
. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
Kwenye hiki kitabu cha ufunuo tunaona Yesu akampa hayo maono Yohana. Akisema “najua matendo yako”. Kuwa Una jina lililohai lakini umekufa. Yani uko vizuri kila mahali. Mtu akikuona anaweza sema uyu Yuko vizuri. Lakini kiukweli umekufa. Yani mambo yako yamekufa. Hakuna linaloendelea katika maisha yako. Shetani kayauwa mambo yako. Mtu akikuona anaweza sema natamani maisha ya uyu mtu lakini hajui tuu.

biashara imekufa
ndoa imekufa
furaha ndani yako imekufa
kazi imekufa

Yani kwa nje unaonekana uko vizuri ila kwa ndani shetani kakuuwa. Ni Kama vile mtu mwenye cancer. Asipokuambia anachoumwa huwezi jua unaweza yatamani maisha yake. Lakini yeye anaweza jiona ni Kama tayari amekufa. Hallelujah
Yesu anasema uwe mwenye kukesha ukayaimarishe mambo yako yaliyo salia yanayotaka kufa. yani uwe mwangalifu usipochukua hatua atauwa hata hayo mengine.Kukesha manake Si kutokulala yani uwe macho. Uamke kiroho! Shetani atauwa kila kitu kilichokuzunguka. Hallelujah! Anaposema ninayajua matendo yako Una jina lililohai lakini umekufa Ana maana gani? Manake najua uko hai kiroho

unaomba
unafunga
unatoa fungu la 10
unasaidia wahitaji
unasoma neno
una imani

Lakini UMEKUFA

sasa ninakufa kivipi?

Unakufa sababu hakuna Kinachoendelea katika maisha yako uko vizuri kiroho lakini
umekufa kiuchumi
umekufa kindoa
umekufa kiafya
umekufa kimaono
umekufa kimahusiano
mambo mengine shetani kayauwa

Kwa iyo uwe mwangalifu. Amka! ukayaimarishe. Yani uombe. Shetani asije kukuuwa zaidi ya hapo. Hallelujah

Ninapoongea hivi tayari utakuwa unaanza kukumbuka

miradi iliyokufa
duka lililokufa
kazi iliyokufa
biashara iliyokufa
mipango iliyokufa
hatua ulizokufa

utaanza kukumbuka vitu ulivyovianzisha kwa moto gafla vikafa. Ulikuwa na mipango ya kubariki ndoa ikafa. Ulikuwa na mipango ya kujenga ikafa. Ulikuwa na mipango ya kuoa/kuolewa ikafa. Mipango mingiii lakini yote inakufa. Yote inakufa. 

Kila unachoanza kinakufa. Unafikiri kabla ni mipango ya Mungu. Si mipango ya Mungu ife. Mungu anasema ni Mimi Mungu nikufundishaye kupata faida. Shetani ndiyo anaiuwa ili ukate tamaa . Alijaribu kumkatisha tamaa Ayubu. Hashindwi kukukatisha tamaa wewe. Kazi hutafuti tena umekata tamaa.

Ulitaka kufungua kiwanda umekata tamaa. Ulitaka kufungua kampuni umekata tamaa. Ulitaka kwenda kusoma umekata tamaa. Kila unachokipanga unakata tamaa. Unachoka. Alafu unaona huu wokovu hauna maana Mungu mwenyewe
hanisaidii.. Kumbe shetani anauwa mwanzo wako. Anauwa hatua zako uchoke ukate tamaa. Hallelujah. Una maono mazuri. Mawazo mazuri lakini unakata tamaa. 

Unamuombea mtu abadilike shetani ndo anazidisha maudhi na makwazo unakata tamaa. Kabisa unatamani uanze upya maisha ya ndoa. Au utoke katika ndoa. Kumbe shetani anakatisha watu tamaa. Hallelujah

Kuondoa roho ya mauti inayopelekea wewe kukata tamaa kwa damu ya Yesu na jina la Yesu

Waebrania 2:14
. Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,

 Neno la Mungu linasema basi kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili. Anaposema watoto Ana maana wale ambao Yesu ni Bwana kwao. Kunatofauti ya kuwa mtoto wa Mungu na mtu wa Mungu. Watoto manake ni wale waliozaliwa kwa damu na maji. Yaliyotoka mwilini ubavuni kwa Yesu. Alipokufa. Walizaliwa kwa imani. Hallelujah! Yani wameokoka. Yesu ni Bwana na mwokozi wa maisha Yao. 

Kwamba siku ile ulipoongozwa sala Toba na kumpokea Yesu moyoni mwako.
nawe pia umeshiriki kufa na kufufuka kwa Yesu. Biblia inasema wewe ulishiriki mwili na damu. Na Yesu naye alishiriki ivyo hivyo. Ili kwa njia ya mauti aweze kumharibu kwenye nguvu ya mauti. Yaani ibilisi. Nitaelezea kidogo hapa. Kabla ya shetani
kuuuwa kazi yako. Biashara yako. Ndoa yako. Lazima atahitaji damu. Iwe damu ya kuku, ngombe, kondoo, binadamu, yoyote ile shetani atumie mauti ya hiko kiumbe kilichokufa  kuachilia mauti kwako.

Nitaelezea tena! kitendo cha kitu kufa inamaana hapo Kuna  mauti. Ndo mana ikatokea kifo. Iyo damu iliyomwagiga ya hiko kiumbe imebeba kifo na mauti ya hiko kiumbe. Kwa iyo shetani hutafuta mauti kupitia kifo na hutumia damu. Ili mauti iyo akaitumie kuuwa vitu vyako. Halleluyah! Ndo mana waganga wa kienyeji na wachawi 

wanapenda Sana kwenda makaburini. Wewe unafikiri ni kwanini? Ni sababu kule wanaenda tafuta mauti. Kwenye kifo Kuna mauti. Ndo mana hata wakristo baada ya mtu kufa makuburi huwa tunayaweka wakfu makuburi kwa jina la Yesu.

 unajua  ni kwanini? Ni ili wachawi wasije chukua mauti ya uyo mtu kwenda kutumia kichawi kuuwa vitu vingine. Mchawi akipata iyo mauti sababu mauti inanguvu ya kifo basi hutumia iyo kuuwa vitu au watu. Huuwa biashara. Ndoa. Kazi. Mahusiano chochote kile. Mungu baada ya kuliona Hilo ndipo hapo akaamua kumtoa mwanawe 

Yesu Kristo ili baada ya Yesu kufa mauti yake iweze kuharibu mauti ya kuku,Mbwa,Kondoo, Mbuzi,Binadamu. Yani mauti anayoitumia shetani. Sababu damu ya Yesu imebeba vitu viwili. Imebena mauti ya Yesu.Hapohapo imebeba uhai wa Yesu. Mauti ni kwa ajili ya kuharibu mauti ya shetani. Yani ibilisi. Uhai ni kwa ajili ya kuachilia uhai kwenye kitu kilichokufa. Hapo ndipo shetani aliposhindwa. Yeye hana

uzima Yesu anauzima. Hakuna damu sehemu yoyote yenye mauti na uhai hapohapo ila damu ya Yesu pekee.Kwa iyo anaposema ili kwa mauti yake amharibu mwenye nguvu ya mauti hapo utaelewa Sasa. Kwa kuwa wewe umeshiriki mwili na damu. Na Yesu kashiriki ivyo ivyo. Kama Yesu Ana nguvu ya kuharibu mauti na mwenye nguvu ya 

mauti basi hata wewe pia kutumia damu ya Yesu pia unauwezo wa kuharibu nguvu ya mauti na mwenye nguvu ya mauti.

Ninaposema nguvu ya mauti inaweza kuwa mapoza,Utasa,Uharibifu,Kifo. Hallelujah! ninaposema mwenye nguvu ya mauti nina maana anaweza kuwa waganga wa kienyeji. Wachawi. Washirikina.wasoma nyota,majini, Mapepo wote wanaotumia nguvu ya mauti kuuwa vitu vyako.

Sasa ukishaijua iyo siri...

Kumbe ahaaa damu ya Yesu imebeba mauti ya Yesu. Damu ya Yesu imebeba uhai wa Yesu. Na mauti ya ibilisi inaharibiwa kwa mauti ya Yesu. Ukishagundua ilo kazi yako ni ndogo Sana. Wewe ni kuachilia damu ya Yesu iliyobeba mauti ya Yesu kwenye kila mauti ya ibilisi. Unaweza kuwa na list yako ya vitu vilivyokufa, vitu ulivyo/unavyo vikatia tama, na mipango iliyokwama.Kama umefuatilia tokea mwanzo utakuwa imeiva vizuri


Hatua za kuomba:

1.Utatubu na kuomba Rehema kwa ajili ya mauti kuatamia vitu vyako (milango iliyofunguka) na mauti

kuatamia ndoa
kuatamia afya
kuatamia biashara
kuatamia nafasi za kazi
kuatamia hatua
utataja vyote

Kisha

2.Utaachilia damu ya  Yesu yenye mauti ya Yesu.

~ewe mauti uliyo atamia hatua zangu nakupambanisha  na damu ya Yesu yenye mauti ya Yesu
~ewe mauti uliye atamia

*hatua zangu
*kibali changu
*miradi yangu
*ndoa yangu
*miguu yangu
*mikono yangu
*fikra zangu
*nafsi yangu
*uchumi wangu
*ndo yangu

Wewe jini mauti. Pepo mauti. roho ya mauti nakukutanisha Na damu ya Yesu yenye mauti ya Yesu. Nakuharibu sasa kwa jina la la Yesu.Wewe mauti uliye uwa (taja vilivyokufa) naachilia mauti ya Yesu kwa damu ya Yesu nakuharibu sasa kwa jina la Yesu.Nakuharibu mauti. Kwa jina la Yesu. Kwa damu ya Yesu.Endelea kuachilia damu ya Yesu yenye mauti ya Yesu nakuharibu hizo mauti. Nazo zitaharibiwa kabisa. Hallelujah utaendelea fanya hivi utashangaa kila kitu kitaanza kuamka. Hata kukata tamaa kutaondoka. Hallelujah


kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu.Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0765377506/0713297066

Mwl Joseph Ntandu
Mwz 1-3 Mungu akasema iwe Nuru ikawa Nuru


Comments

  1. Nashukuru Sana mtumushi was Mungu.Barikiwa

    ReplyDelete
  2. Mungu akubariki mtumishi kwa somo zuri binafsi nimekuwa nikisumbuliwa sana na roho ya mauti sikujua niombeje na mshukuru Mungu nimepata kitu cha kunisaidia

    ReplyDelete
  3. Mtumishi wa Mungu, Mungu azidi kukubariki na maono na ufunuo wa kiroho ,fundisho hili nimeipokea na naamini kwa maombi haya tutafunguliwa na kuwekwa huru kutoka kwa maroho za mauti na maangamizi.

    ReplyDelete
  4. Mungu amekutumia mtumishi, vita tuneishinda na mauti ya shetani imekimbilia kuzimu ... ubarikiwe sana , YESU ni mwema

    ReplyDelete
  5. Me naombaa msaada maana kunamawazo yakufa kuna wakat nikikaa nahs kamaaa nimekufaaa hivi sielew

    ReplyDelete
  6. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA