UPONYAJI WA UCHUMI
✝️ Day 3️⃣ *"KWA KUPIGWA KWAKE NIMEPONA TOKA KWENYE MADENI"* Isaya 53 (Biblia Takatifu) ¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯ ⁴ Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. ⁵ Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Baba katika jina la Yesu,Baba wa utukufu na Mungu Mtakatifu katika jina la Yesu Kristo,Baba kwa damu ya Yesu ninakuja kwako,kwa damu ya Yesu ninasogea kwako! Kwa jina la Yesu! unirehemu unisamehe!Neno lako linasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa!Ee Bwana lolote lisilo kupendeza naungama natubu na kuomba Rehema,Rehemu uovu wangu,dhambi zangu na makosa yangu kwa damu ya Yesu,na kwa jina la Yesu uyafute maovu yangu,dhambi zangu,na makosa yangu nakusihi!Rehemu mawazo yangu,matendo yangu na maneno yangu ambayo yamekuwa kinyume kabisa na mapenzi yako.Baba Mtakatifu uchumi wangu unaumwa,mikono yangu inaumwa,...