UWEZO WA MUNGU UTOKAO JUU
Somo: Uwezo
wa Mungu utakao juu.
Luka 24:49
49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Matendo 1-8
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha
kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Kumb 8-18
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu
wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara
agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Bwana Yesu
asifiwe, Mungu Baba tunakushukuru kwa nafasi ingine ya kujifunza neno lako. Neno lako ni taa neno lako mwanga
tena ni njia ya maisha yetu. Roho mtakatifu tunakukaribisha tusaidie tuweze
kuyaelewa maandiko.
Wapendwa
Mungu alivyotuumba hakutuumba tujitegemee alituamba tuishi naye, alituumba
tumtegemee yeye tuishi naye katika maisha yetu ya kila siku. Bahati mbaya sana
tunachagua maeneo ya kumshirikisha Mungu. Ndio maana katika maeneo yale
tusiomshirikisha tunapata wakati mgumu. Au tunaenda kwa tabu, tunafika huku
tumechoka sababu ya vita. NINI MAANA YA UWEZO UTAKAO JUU? manake yake ni hii,
ni nguvu
za Kimungu special kukusaidia jambo flani liende kirahisi. Yani nguvu
iyo inakutengenezea njia, nguvu iyo inaenda kumiliki nafasi kwa ajili yako,
nguvu iyo inamsukuma adui anayekuzuia
usifike. Wapendwa tunapata wakati mgumu au shida kufika katika tunayoyafanya
sababu adui anakusuma nyuma, adui anakuwekea vikwazo, yani kila kitu
kinakupinga. Unapokuja uwezo huo huondoa upinzani wote, huondoa makwazo hapo
ndipo utafanikiwa.
Watu wengi
wakisikia uwezo wa Mungu au nguvu za Mungu zitokazo juu picha inawajia kwenye
huduma ya ki Mungu. Wanafikiria ule uwezo wa kuponya, uwezo wa kuhubiri injili,
ule uwezo wa kumsaidia mtu kutabiri, ule uwezo wa ki Mungu kupitia
mtumishi kufungua watu kwenye vifungo,
ule uwezo wa Mungu unaokaa kwenye maneno ya baraka, ule uwezo unaokaa katika
mikono ya watumishi. Ule uwezo wa kutoa
pepo, ule uwezo wa kuomba, uwezo wa
kusoma neno, ni sawa kabisa uko sahihi, lakini leo nataka nikukumbushe kitu, na
roho wa Mungu akufungue akili yako uweze kuelewa hili. Kupata maono ni kitu kimoja, kukamilika maono
ni kitu kingine, wengi wanapata maono, wengi wanaota maono, wengi wanaomba
wanapata majibu yao, ila sasa hayo majibu kusudi yaonekane katika mwili, hayo
maono yawe katika mwili huu wa ulimwengu
ndipo ambapo unahitaji huo uwezo, bila huo uwezo unaweza kuanza na ukapata
upinzani mkubwa. Au ukarudi nyuma kabisa.
Na hapa
wengi wanarudi tena kwa Mungu kutaka
kujua kweli Mungu maono haya ni ya kwako kweli au akili zangu, maana anaona
upinzani umezidi!? Na haelewi aendelee nao? Au aache? Au aanze kitu kipya?
Nizungumze kwa mifano ili uelewe vizuri; unaweza pata maono ya kupata kazi
biashara au ndoa na yakaanza kabisa lakini mbele ukakutana na upinzani mkubwa
kiasi cha kuchanganyikiwa? Unaweza pata maono ya kufungua biashara flani au
kufanya kilimo, kufuga au mtu atakayekuwa mwanandoa mwenzako lakini ile picha
ya mwisho uliyoonyeshwa jinsi inavyotakiwa kuwa haiwi, instead inakuwa tofauti
kama ni ndoa
kunakuwa na mpasuko mkubwa,kama ni hatua ya kufikia ndoa kunainuka
wimbi kubwa, kunakuwa hakuna amani tena,au urahisi picha inabadilika. Yale
uliyotegemea yamekuwa ndivyo sivyo, kama ni biashara inabadilika kuwa madeni,
kama ni kazi inakuwa mwiba mkubwa unamuuliza Mungu hii kazi ni yako kweli
Mungu?. Kama ni kilimo au ufugaji unapata upinzani mkubwa kila kitu kimekufa,
kila kitu kimatapanya, kimegeuka, na hapa ndipo watu wanaona wokovu ni mzigo ni
kazi. Mpendwa sio kusudi la Mungu upitie unayopitia ila tuu hukujua kuanza na
Mungu wakati wote, hukujua kuulizia uwezo wa Mungu katika ulichokianza,
ulichokianzisha ndo mana umepata upinzani.
Bwana Yesu
asifiwe sana. Uwezo wa Mungu si kanisani tuu bali katika biashara, katika ndoa,
katika kazi, katika mipango, katika maono uliyoyaona, katika kutaka kujenga
nyumba, katika kulea watoto, katika nafasi ya uongozi, katika kununua, katika
kuuza, kila kitu mpendwa kinahitaji kinataka kipewe uwezo wa Mungu ndipo
kitafanikiwa, wapendwa upinzani ni kila mahali, kila sehemu. Uwezo wa Mungu
katika kuamua,
uwezo wa Mungu unapokuja ndipo unakusaidia ufanye unayofanya na
uwe star, fikiria kwa habari wa wachezaji mpira kiwanjani kwanini mmoja au
wawili tuu ndio anakuwa star na si wote? Ipo nguvu inayomsaidia katika yeye
kuwa kama alivyo. Sasa wana wa ulimwengu huu hutafuta uwezo wa nguvu za giza
ambao unaexpire haudumu, ila uwezo utakao juu huu ukija kukusaidia hakuna wa
kukupinga, kinachofanya huyu kafanikiwa mwenzake alichoshindwa ni huo uwezo
utakao juu. Ngoja nikukumbushe kitu katika biblia.
*Yusuph
aliyekuja kuwa Waziri mkuu wa misri mwana wa Yakobo alipewa uwezo wa kutawala
ndio maana hakuzuilika. Pamoja na mazingira yote kumpinga.
*Daniel
alipewa uwezo wa uongozi na kutawala ndio maana hakuzuilika, hata kuingizwa
katika tundu la simba wenye njaa ule uwezo uliwazuia simba. Huo ni uwezo utakao
juu.
*Yakobo
alipewa uwezo wa kufuga kondoo ndio maana pamoja na hila zote za labani kutaka
kumzulumu wale kondoo lakini pia ilishindikana.na akaondoka na wake zake
wawili.
*Stephano
alipewa uwezo wa kuhubiri injili ndio maana hata yale maumivu ya kupigwa mawe
hakuyaona. Uwezo ulimfunika yeye alimtukuza Mungu tuu.
*Isaka
alipewa uwezo wa kuzalisha kufyatua vitu akawa mtu tajiri sana. Alichimba
visima visivyotoa maji navyo vikatoa maji, alipanda mazao naye alivuna sana.
Huo ni uwezo.
*Petro
aliporudi mara ya pili kuvua samaki akapata ni sababu zile nyavu ziliwekewa uwezo
wa Mungu wa kuvuta samaki. Mwanzo hakuwa na uwezo wowote.
*Yesu
alipewa uwezo wa kuukomboa ulimwengu ndo mana pamoja na mazingira yote mauti
haikumtisha alidharau mauti na aibu. Huo uwezo utakao juu unapokuja hauzuiliki.
Huo uwezo utakao juu unakushukia hakuna cha kukuzuia.
* Ester
alipewa uwezo wa kuonekana ndio maana mabinti wote hawakuonekana. Ule ni uwezo
utakao juu. Uliomfanya mfalme si kwa kutaka kwake, bali ile nguvu ilimsukuma
Mfalme amchague Ester.
*Ayubu
alipewa nguvu za utajiri ndio maana hata baada ya dhoruba yote na mapito yote
utajiri ulirejea kwa Ayubu. Ayubu 42
BWANA Yesu
asifiwe sana, kila kusudi la Mungu ulilopewa au kuambiwa katika maono upo uwezo
utakao juu wa kukusaidia ufike kirahisi, usitumie nguvu, usipate shida usitumie
akili zako za duniani. Kinachofanya uwezo huu usifanye kazi ni sababu baada ya
kupata maono, au maono kuanza uliacha kuliombea au ulilianza bila uwezo utakao
juu. Sasa imefika sehemu umeshindwa, na umechoka na umekata tamaa. Kule mwanzo
nilisema Mungu anataka ushirika na wewe katika mambo yote, umshirikishe katika
kila kitu, binadamu
ameumbwa kuishi na Mungu hapa duniani ili binadamu uyu
aweze kufanikiwa. Kwenye kila kitu hata mambo ambayo unaona unayaweza au
unayamudu Mungu anataka umshirikishe alafu uruusu uwezo utakao juu ukusaidie.
Mitego ni mingi ya shetani huwezi shinda mwenyewe. Kuna mahali ulitumia akili
zako mwenyewe ndio maana umeshindwa, ndio maana unapitia wakati mgumu. Bwana
Yesu asifiwe sana. Mungu anataka umtambue katika lolote unalolifanya si wakati
wa kuomba na kuabudu tuu. Au kanisani. Anataka umtambue kila mahali na kila
kitu kabla ya kufanya umshirikishe.....
NINI LA
KUFANYA SASA!
1. Omba
rehema kwa yale mambo yote uliyoyaanza kwa akili zako bila kumshirikisha , hata
kama maono yalitoka kwake Mungu. Omba rehema katika asili yako, malangoni kama
ipo dhambi ya aina hiyo achilia damu ya Yesu.
2. Baada ya
rehema sasa uwezo wa Mungu utakao juu uje kukusaidia ili uweze kuvuka katika
tatizo lako. Na tambua uwezo wa Mungu katika hilo lililokwama.
3. Omba
uwezo katika kila kitu sasa ndoa, kazi zako, biashara yako, maamuzi, uongozi.
Kila kitu kinachokuzunguka katika maisha yako omba uwezo sasa utakao juu maana
kila kitu duniani cha ki Mungu kimeumbiwa uwezo wake ili kifanikiwe. maana
umejua leo au umekumbuka ya kuwa uwezo huo si kwa ajili ya injili tuu bali ni
katika maisha yako yote.katika mahusiano, kama watu wangetambua hili sisi wana
Mungu tusingekuwa na taabu. Tungeishi kama wafalme. Hata kibali kinahitaji
uwezo utakao juu. Pamoja na kujibiwa na Mungu au kuonyeshwa kinachokosekana
hapo ni uwezo utako juu.
JINA LAKE
MUNGU LIBARIKIWE!
*kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka
nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako
biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni
kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige
hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande
wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi
ndugu yako Joseph Ntandu
josephntandu@gmail.com,0713297066
josephntandu@gmail.com,0713297066
Ubarikiwe Ila andika maandiko ya vifungu ambavyo watu walipata uwezo
ReplyDelete