UWEZO WA MUNGU UTOKAO JUU





Somo: Uwezo wa Mungu utakao juu.

Luka 24:49
49 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Matendo 1-8
 8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. 
 
Kumb 8-18
 18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo. 

Bwana Yesu asifiwe, Mungu Baba tunakushukuru kwa nafasi ingine ya kujifunza  neno lako. Neno lako ni taa neno lako mwanga tena ni njia ya maisha yetu. Roho mtakatifu tunakukaribisha tusaidie tuweze kuyaelewa maandiko.

Wapendwa Mungu alivyotuumba hakutuumba tujitegemee alituamba tuishi naye, alituumba tumtegemee yeye tuishi naye katika maisha yetu ya kila siku. Bahati mbaya sana tunachagua maeneo ya kumshirikisha Mungu. Ndio maana katika maeneo yale tusiomshirikisha tunapata wakati mgumu. Au tunaenda kwa tabu, tunafika huku tumechoka sababu ya vita. NINI MAANA YA UWEZO UTAKAO JUU? manake yake ni hii, ni nguvu 

za Kimungu special kukusaidia jambo flani liende kirahisi. Yani nguvu iyo inakutengenezea njia, nguvu iyo inaenda kumiliki nafasi kwa ajili yako, nguvu iyo inamsukuma adui  anayekuzuia usifike. Wapendwa tunapata wakati mgumu au shida kufika katika tunayoyafanya sababu adui anakusuma nyuma, adui anakuwekea vikwazo, yani kila kitu kinakupinga. Unapokuja uwezo huo huondoa upinzani wote, huondoa makwazo hapo ndipo utafanikiwa.

 Watu wengi wakisikia uwezo wa Mungu au nguvu za Mungu zitokazo juu picha inawajia kwenye huduma ya ki Mungu. Wanafikiria ule uwezo wa kuponya, uwezo wa kuhubiri injili, ule uwezo wa kumsaidia mtu kutabiri, ule uwezo wa ki Mungu kupitia mtumishi  kufungua watu kwenye vifungo, ule uwezo wa Mungu unaokaa kwenye maneno ya baraka, ule uwezo unaokaa katika mikono ya watumishi. Ule uwezo wa kutoa 

pepo, ule uwezo wa kuomba, uwezo wa kusoma neno, ni sawa kabisa uko sahihi, lakini leo nataka nikukumbushe kitu, na roho wa Mungu akufungue akili yako uweze kuelewa hili.  Kupata maono ni kitu kimoja, kukamilika maono ni kitu kingine, wengi wanapata maono, wengi wanaota maono, wengi wanaomba wanapata majibu yao, ila sasa hayo majibu kusudi yaonekane katika mwili, hayo maono yawe katika mwili huu wa  ulimwengu ndipo ambapo unahitaji huo uwezo, bila huo uwezo unaweza kuanza na ukapata upinzani mkubwa. Au ukarudi nyuma kabisa.

 Na hapa wengi  wanarudi tena kwa Mungu kutaka kujua kweli Mungu maono haya ni ya kwako kweli au akili zangu, maana anaona upinzani umezidi!? Na haelewi aendelee nao? Au aache? Au aanze kitu kipya? Nizungumze kwa mifano ili uelewe vizuri; unaweza pata maono ya kupata kazi biashara au ndoa na yakaanza kabisa lakini mbele ukakutana na upinzani mkubwa kiasi cha kuchanganyikiwa? Unaweza pata maono ya kufungua biashara flani au kufanya kilimo, kufuga au mtu atakayekuwa mwanandoa mwenzako lakini ile picha ya mwisho uliyoonyeshwa jinsi inavyotakiwa kuwa haiwi, instead inakuwa tofauti kama ni ndoa 

kunakuwa na mpasuko mkubwa,kama ni hatua ya kufikia ndoa kunainuka wimbi kubwa, kunakuwa hakuna amani tena,au urahisi picha inabadilika. Yale uliyotegemea yamekuwa ndivyo sivyo, kama ni biashara inabadilika kuwa madeni, kama ni kazi inakuwa mwiba mkubwa unamuuliza Mungu hii kazi ni yako kweli Mungu?. Kama ni kilimo au ufugaji unapata upinzani mkubwa kila kitu kimekufa, kila kitu kimatapanya, kimegeuka, na hapa ndipo watu wanaona wokovu ni mzigo ni kazi. Mpendwa sio kusudi la Mungu upitie unayopitia ila tuu hukujua kuanza na Mungu wakati wote, hukujua kuulizia uwezo wa Mungu katika ulichokianza, ulichokianzisha ndo mana umepata upinzani.


Bwana Yesu asifiwe sana. Uwezo wa Mungu si kanisani tuu bali katika biashara, katika ndoa, katika kazi, katika mipango, katika maono uliyoyaona, katika kutaka kujenga nyumba, katika kulea watoto, katika nafasi ya uongozi, katika kununua, katika kuuza, kila kitu mpendwa kinahitaji kinataka kipewe uwezo wa Mungu ndipo kitafanikiwa, wapendwa upinzani ni kila mahali, kila sehemu. Uwezo wa Mungu katika kuamua, 

uwezo wa Mungu unapokuja ndipo unakusaidia ufanye unayofanya na uwe star, fikiria kwa habari wa wachezaji mpira kiwanjani kwanini mmoja au wawili tuu ndio anakuwa star na si wote? Ipo nguvu inayomsaidia katika yeye kuwa kama alivyo. Sasa wana wa ulimwengu huu hutafuta uwezo wa nguvu za giza ambao unaexpire haudumu, ila uwezo utakao juu huu ukija kukusaidia hakuna wa kukupinga, kinachofanya huyu kafanikiwa mwenzake alichoshindwa ni huo uwezo utakao juu. Ngoja nikukumbushe kitu katika biblia.

*Yusuph aliyekuja kuwa Waziri mkuu wa misri mwana wa Yakobo alipewa uwezo wa kutawala ndio maana hakuzuilika. Pamoja na mazingira yote kumpinga.

*Daniel alipewa uwezo wa uongozi na kutawala ndio maana hakuzuilika, hata kuingizwa katika tundu la simba wenye njaa ule uwezo uliwazuia simba. Huo ni uwezo utakao juu.

*Yakobo alipewa uwezo wa kufuga kondoo ndio maana pamoja na hila zote za labani kutaka kumzulumu wale kondoo lakini pia ilishindikana.na akaondoka na wake zake wawili.

*Stephano alipewa uwezo wa kuhubiri injili ndio maana hata yale maumivu ya kupigwa mawe hakuyaona. Uwezo ulimfunika yeye alimtukuza Mungu tuu.

*Isaka alipewa uwezo wa kuzalisha kufyatua vitu akawa mtu tajiri sana. Alichimba visima visivyotoa maji navyo vikatoa maji, alipanda mazao naye alivuna sana. Huo ni uwezo.

*Petro aliporudi mara ya pili kuvua samaki akapata ni sababu zile nyavu ziliwekewa uwezo wa Mungu wa kuvuta samaki. Mwanzo hakuwa na uwezo wowote.

*Yesu alipewa uwezo wa kuukomboa ulimwengu ndo mana pamoja na mazingira yote mauti haikumtisha alidharau mauti na aibu. Huo uwezo utakao juu unapokuja hauzuiliki. Huo uwezo utakao juu unakushukia hakuna cha kukuzuia.

* Ester alipewa uwezo wa kuonekana ndio maana mabinti wote hawakuonekana. Ule ni uwezo utakao juu. Uliomfanya mfalme si kwa kutaka kwake, bali ile nguvu ilimsukuma Mfalme amchague Ester.

*Ayubu alipewa nguvu za utajiri ndio maana hata baada ya dhoruba yote na mapito yote utajiri ulirejea kwa Ayubu. Ayubu 42

BWANA Yesu asifiwe sana, kila kusudi la Mungu ulilopewa au kuambiwa katika maono upo uwezo utakao juu wa kukusaidia ufike kirahisi, usitumie nguvu, usipate shida usitumie akili zako za duniani. Kinachofanya uwezo huu usifanye kazi ni sababu baada ya kupata maono, au maono kuanza uliacha kuliombea au ulilianza bila uwezo utakao juu. Sasa imefika sehemu umeshindwa, na umechoka na umekata tamaa. Kule mwanzo nilisema Mungu anataka ushirika na wewe katika mambo yote, umshirikishe katika kila kitu, binadamu 

ameumbwa kuishi na Mungu hapa duniani ili binadamu uyu aweze kufanikiwa. Kwenye kila kitu hata mambo ambayo unaona unayaweza au unayamudu Mungu anataka umshirikishe alafu uruusu uwezo utakao juu ukusaidie. Mitego ni mingi ya shetani huwezi shinda mwenyewe. Kuna mahali ulitumia akili zako mwenyewe ndio maana umeshindwa, ndio maana unapitia wakati mgumu. Bwana Yesu asifiwe sana. Mungu anataka umtambue katika lolote unalolifanya si wakati wa kuomba na kuabudu tuu. Au kanisani. Anataka umtambue kila mahali na kila kitu kabla ya kufanya umshirikishe.....

NINI LA KUFANYA SASA!

1. Omba rehema kwa yale mambo yote uliyoyaanza kwa akili zako bila kumshirikisha , hata kama maono yalitoka kwake Mungu. Omba rehema katika asili yako, malangoni kama ipo dhambi ya aina hiyo achilia damu ya Yesu.

2. Baada ya rehema sasa uwezo wa Mungu utakao juu uje kukusaidia ili uweze kuvuka katika tatizo lako. Na tambua uwezo wa Mungu katika hilo lililokwama.

3. Omba uwezo katika kila kitu sasa ndoa, kazi zako, biashara yako, maamuzi, uongozi. Kila kitu kinachokuzunguka katika maisha yako omba uwezo sasa utakao juu maana kila kitu duniani cha ki Mungu kimeumbiwa uwezo wake ili kifanikiwe. maana umejua leo au umekumbuka ya kuwa uwezo huo si kwa ajili ya injili tuu bali ni katika maisha yako yote.katika mahusiano, kama watu wangetambua hili sisi wana Mungu tusingekuwa na taabu. Tungeishi kama wafalme. Hata kibali kinahitaji uwezo utakao juu. Pamoja na kujibiwa na Mungu au kuonyeshwa kinachokosekana hapo ni uwezo utako juu.


JINA LAKE MUNGU LIBARIKIWE!
 *kama hujaokoka ndugu chukua uamuzi leo umpe Yesu maisha yako. Kuokoka nikukubali Yesu atake control ya maisha yako ya kiuchumi,ndoa,kazi zako biashara zako, maisha yako ya kiroho, na mambo yote ya kiujumla, ni kumruusu Yesu atake charge ya maisha yako.kumruusu roho wa Mungu apige hatua na kuokoka si kubadili dini. Huwezi mshinda adui ukiwa upande wake,Hivyo chukua hatua leo ndugu, ukae upande salama kwa Yesu. Mimi ndugu yako Joseph Ntandu


josephntandu@gmail.com,0713297066

Comments

  1. Ubarikiwe Ila andika maandiko ya vifungu ambavyo watu walipata uwezo

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAOMBI HATARI YA KUVUNJA UCHAWI WA MAFUNDO

MAOMBI YA KUFUNGUA KIBALI CHA  NAFASI YA KAZI

MAOMBI YA KUHARIBU ROHO YA KUCHELEWESHA